Sophia Simba (UWT) -Vs- Naomi Kaihula (BAWACHA)

Naomi Kaihula ni mwanamke mwanaharakati wa kweli na mwanasiasa aliyelelewa na siasa tangu enzi za mfumo wa siasa za chama kimoja. Huyu Mama alinifundisha somo la siasa shule ya sekondari ya Tambaza miaka ya themanini. Nadhani alijiendeleza kielimu na ku upgrade toka mwalimu wa sekondari mpaka mhadiri wa chuo kikuu cha CBE.

Mama Kaihula ni muongeaji mzuri, ila mama Sofia Simba yeye ni muongeaji wa type ya pashkuna, misuto ni jadi yake kama walivyo mabinti wa Kizarazo, hivyo mdahalo kati yao moto wa kelele utawaka, mmoja akimwaga hoja, mwingine akimsuta!.
.
Ukimsikiliza-mama Simba, utagundua ni 'Debe Tupu' hata JK amempigia kampeni kiaina, nakumbuka baada ya Mama Kahama kuibua tuhuma za rushwa dhidi ya Mama Simba, nilisema hii ni kesi ya nyani kapeleka kwa ngedere, nikasisitiza JK hata akithibitisha uchafu huo wa Mama Simba, hawazi kukubali ukubaliwe na kuchafuua chama chake na serikali yake, bali ni rahisi zaidi kumdismiss Mama Kahama- na kumbeba Mama Simba.

Tatizo ni vyama vyao, kuuidahalisha UWT na BAWACHA ni sawa na Tembo na Sisimizi, japo sisimizi anaweza kumuua Tembo, UWT inajisikia kuwa ina hatimiliki ya issues za wanawake wote wa Tanzania chini ya mwamvuli wa CCM ambacho ni chama dola na ndio waliopelekea kupigwa marufuku kwa lile baraza la wanawake la Prof.Tibaijuka, BAWATA. Hivyo UWT hawawezi kukubali mdahalo na BAWACHA.
Wanawake wa CCM wamezoea kubebwa, hakuna asiyejua jinsi Sofia Simba alivyobebwa na kuukwaa uenyekiti UWT, akikubali mdahalo na Naomi Kaihula, nani atambeba?. Kuliko kugalagazwa, bora wakatae.
 
...hata JK amempigia kampeni kiaina

"Kiaina" vipi wakati ile ilikuwa kampeni ya nje nje, kwenye mkutano wa wazi wa UWT?

Kulikuwa kuna wagombea watatu, mmoja amelenga kampeni yake kwenye ghanima aliyonayo dhidi ya mpinzani wake mkubwa kwamba yeye ana elimu, mwenzake hajasoma vizuri. Kikwete akaja kwenye mkutano wa UWT punde kabla ya kura akatangaza "chagueni msomi." Kungekuwa hakukuwa na swala la usomi katika kampeni hii, na Kikwete angesema toka awali kwamba CCM ikuze viongozi wasomi hapo tungekuwa wazushi tukisema Kikwete anamlenga mtu yeyote. Hapa Kikwete ni wazi alimpigia debe Mama Simba.

Sasa Kikwete huyu huyu mwezi jana katoka kuwakaripia wazee waliojiingiza kwenye kampeni za vijana. Kina Makamba, Kawawa, Kingunge kumbe hawakutumwa na CCM kuingilia uchaguzi wa vijana, maana Kikwete alikerwa na walichofanya, akasema:

"It's a crime (ni uhalifu), ni mbaya sana kujiingiza katika masuala ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wakati we si kijana wala mwanachama, hii ni mbaya. Ni lazima kujiuliza huyu Kikwete yuko nje ya uanachama, lakini anaweka mtu wake kwenye nafasi ya uongozi na anataka ashinde, anataka nini huyu?"

Baada ya hapo Kikwete anakuja kwenye uchaguzi wa UWT, anasema chagueni msomi, wakati tunamfahamu anaejiita msomi, aliye run campaign platform ya usomi, ni mmoja tu. Hiyo sio kampeni ya wazi hapo? Sio vizuri kuita watu majina, hususan kwa waheshimiwa kama Rais wetu, lakini jama, huu aliofanya Rais tuuiteje, sio unafiki huu? Sio unafiki?

Jakaya anampenda Sophia. Akashindwa kujizuia kwenda nusu nusu katika kum-sapoti maana dhambi nyingine bana ukishaianza ni heri tu uimalizie. Ukiamua kula nguruwe kula aliyenona. Tatizo ni kwamba nguruwe mwenyewe hajanona. Sophia Simba hana caliber ya uongozi ya kustahili Rais kutoa muhanga maadili yake kumpigia debe bila kujificha. She is simply not worth the candle.

Unam-kampeinia mtu anaesema kwamba wanawake wawezeshwe katika katika kazi zisizo za maofisini. Kwamba katika enzi hizi za mapinduzi ya teknolojia wanaume wamepoteza kazi za maofisini na ni wanawake ndio wanaweza kujiajiri. Yani, badala ya kusema wanawake inabidi wawezeshwe kushiriki katika uchumi na ajira mpya za mapinduzi ya technolojia anasema kazi za maofisini ni za wanaume! Sasa kazi za wanawake za kujiajiri ambazo sio za ofisini anazoziongelea Waziri wa Nchi ni zipi kama sio kufuma mikeka, kuhudumu kwenye majumba Oysterbay, kuuza la mnazi, kuhudumia order na mahitaji mengine ya walevi katika joints za nyama choma?

Kikwete anamu-endorse mtu anaefikiri hivyo. Kamteua ubunge, akampa wizara nyeti, kubwa kuliko. Anasimamia Usalama wa Taifa, na TAKUKURU. Wahisani wote wanaikodolea macho wizara ya utawala bora maana "good governance" ndio buzz words wanazotuimbia pay masters wetu kila kukicha. Wananchi wanaikodolea hii wizara macho tukitegemea itulindie amani, usalama na utulivu. Naombea isiwe huyu mama ndio anatoa uongozi katika mambo yote tata tata, na delicate delicate ya usalama wa nchi. Uhusiano wetu na nchi jirani ambako wakimbizi na majambazi huingilia kuua raia wa TZ, maamuzi ya kushitaki au kutoshitaki the Mkapas and the Wariobas of the world, na CCM financiers na deal cutters kama Rostam na Chenge, na maamuzi ya juzi kutuma ma spy Arusha ku-interview terror suspects kwenye misikiti, ku arrest secessionists wa Zanzibar kuhusiana na tensions za Bara na Zanzibar, maamuzi juu ya swala la mahakama ya Kadhi Mkuu. Very, very delicate issues chini ya huyu Mama Simba. Mtu anaefikiri kwamba wanawake kazi wanazoweza ni za mama ntilie.

Ndio visions za Jakaya na Sophia. Couple ya ajabu hii.
 
Heehee Kuhani usinichekeshe mie Asha, Eti tuna Waziri wa utawala bora mwenye utawala bomu UWT asiyejua wajibu wake kama mwenyekiti. Tuangalie asijegueza usalama wa taifa kuwa kama uwt ya ccm.

Halafu huyu ni Waziri wa TAKUKURU mwenye tuhuma ya kutoa rushwa yeye mwenyewe.

Ama kweli ni SIMBA kwelikweli

Asha
 
"Kiaina" vipi wakati ile ilikuwa kampeni ya nje nje, kwenye mkutano wa wazi wa UWT?

Kulikuwa kuna wagombea watatu, mmoja amelenga kampeni yake kwenye ghanima aliyonayo dhidi ya mpinzani wake mkubwa kwamba yeye ana elimu, mwenzake hajasoma vizuri. Kikwete akaja kwenye mkutano wa UWT punde kabla ya kura akatangaza chagueni msomi. Kungekuwa hakukuwa na swala la usomi katika kampeni hii, na Kikwete angesema toka awali kwamba CCM ikuze viongozi wasomi hapo tungekuwa wazushi tukisema Kikwete anamlenga mtu yeyote. Hapa Kikwete ni wazi alimpigia debe Mama Simba.

Sasa Kikwete huyu huyu mwezi jana katoka kuwakaripia wazee waliojiingiza kwenye kampeni za vijana. Kina Makamba, Kawawa, Kingunge kumbe hawakutumwa na CCM kuingilia uchaguzi wa vijana, maana Kikwete alikerwa na walichofanya, akasema:

Its a crime (ni uhalifu), ni mbaya sana kujiingiza katika masuala ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wakati we si kijana wala mwanachama, hii ni mbaya. Ni lazima kujiuliza huyu Kikwete yuko nje ya uanachama, lakini anaweka mtu wake kwenye nafasi ya uongozi na anataka ashinde, anataka nini huyu?

Baada ya hapo Kikwete anakuja kwenye uchaguzi wa UWT, anasema chagueni msomi, wakati tunamfahamu anaejiita msomi, aliye run campaign platform ya usomi, ni mmoja tu. Hiyo sio kampeni ya wazi hapo? Sio vizuri kuita watu majina, hususan kwa waheshimiwa kama Rais wetu, lakini jama, huu aliofanya Rais tuuiteje, sio unafiki huu? Sio unafiki?

Jakaya anampenda Sophia. Akashindwa kujizuia kwenda nusu nusu katika kum-sapoti maana makosa mengine bana ukiyashaanza ni heri tu uyamalizie. Ukiamua kula nguruwe kula aliyenona. Tatizo ni kwamba nguruwe mwenyewe hajanona. Sophia Simba hana caliber ya uongozi ya kustahili Rais kutoa muhanga maadili yake kumpigia debe bila kujificha. She is simply not worth the candle.

Unam-kampeinia mtu anaesema kwamba wanawake wawezeshwe katika katika kazi zisizo za maofisini. Kwamba katika enzi hizi za mapinduzi ya teknolojia wanaume wamepoteza kazi za maofisini na ni wanawake ndio wanaweza kujiajiri. Yani, badala ya kusema wanawake inabidi wawezeshwe kushiriki katika uchumi na ajira mpya za mapinduzi ya technolojia anasema kazi za maofisini ni za wanaume! Sasa kazi za wanawake za kujiajiri ambazo sio za ofisini anazoziongelea Waziri wa Nchi ni zipi kama sio kufuma mikeka, kuhudumu kwenye majumba Oysterbay, kuuza la mnazi, kuhudumia order na mahitaji mengine ya walevi katika joints za nyama choma?

Kikwete anamu-endorse mtu anaefikiri hivyo. Kamteua ubunge, akampa wizara nyeti, kubwa kuliko. Anasimamia Usalama wa Taifa, na TAKUKURU. Wahisani wote wanaikodolea macho wizara ya utawala bora maana good governance ndio buzz words wanazotuimbia pay masters wetu kila kukicha. Wananchi wanaikodolea hii wizara macho tukitegemea itulindie amani, usalama na utulivu. Naombea isiwe huyu mama ndio anatoa uongozi katika mambo yote tata tata, na delicate delicate ya usalama wa nchi. Uhusiano wetu na nchi jirani ambako wakimbizi na majambazi huingilia kuua raia wa TZ, maamuzi ya kushitaki au kutoshitaki the Mkapas and the Wariobas of the world, na CCM financiers na deal cutters kama Rostam na Chenge, na maamuzi ya juzi kutuma ma spy Arusha ku-interview terror suspects kwenye misikiti, ku arrest secessionists wa Zanzibar kuhusiana na tensions za Bara na Zanzibar, maamuzi juu ya swala la mahakama ya Kadhi Mkuu. Very, very delicate issues chini ya huyu Mama Simba. Mtu anaefikiri kwamba wanawake kazi wanazoweza ni za mama ntilie.

Ndio visions za Jakaya na Sophia hawa. Couple ya ajabu hii.
Asante Kuhani, hapo umenena na nimekupata vilivyo. Nadhani JK hajui anataka nini, wala hawezi kupambanua, nchi imetoka wapi, iko wapi na inakwenda wapi. In short hana vision.
Jambo moja naamini, ana washauri lakini hashauriki. Hii itamcost at the end of the day.
Hawezi kutofautisha pupularity na distinguishable, ndio maana kwa watu wake, hata waboronge vipi, atawakingia kifua, kuwalinda na kuwabeba kadri iwezekanavyo kisa eti ni wanamtandao.
Nilikuwepo alipofanya ziara za mwanzo. Nilitegemea anaporejea atakuwa anafuatilia mrejesho wa ile vision aliyoiseti mwanzo. Kumbe hakuna vision wala mission ni blah blah tupu.
Any way hebu tumwache isije onekana JF hatumfagilii.
 
Heehee Kuhani usinichekeshe mie Asha, Eti tuna Waziri wa utawala bora mwenye utawala bomu UWT asiyejua wajibu wake kama mwenyekiti. Tuangalie asijegueza usalama wa taifa kuwa kama uwt ya ccm.

Halafu huyu ni Waziri wa TAKUKURU mwenye tuhuma ya kutoa rushwa yeye mwenyewe.

Ama kweli ni SIMBA kwelikweli

Asha

Lord have mercy!!!!!!
Yaani huyu mama ndio WAZIRI wa UTAWALA bora????

Makubwa haya!...........I am speechless
 
Lord have mercy!!!!!!
Yaani huyu mama ndio WAZIRI wa UTAWALA bora????

Makubwa haya!...........I am speechless

Bimkubwa, kama una dakika 15, ishirini, msikilize anavyoongea. Mipasho mipasho kama sio Waziri, kama stori za uani wakati unakunywa Kilimanjaro mbele ya kideo. Kuna wakati akasema alivyoona wapinzani wake atakaogombea nao akajua atashinda, you know, mteremko. Anaemhoji akacheka, Sophia akasema kishankupe shankupe "I am telling you..."!
 
Bi Mkubwa, kama una dakika 15, ishirini, msikilize anavyoongea. Mipasho mipasho kama stori za uani wakati ukiwa unakunywa Kilimanjaro mbele ya kideo. Kuna wakati akasema alivyoona wapinzani wake atakaogombea nao akajua huo ni mteremko. Anaemuhoji akacheka, Sophia akasema kishankupe shankupe "I am telling you..."!

Ee bana nimesikiliza, yaani kama hawa ndio viongozi wetu, na visions zao ndio hizo...tuna njia ndefu sana ya kwenda huko tunakokusudia kisiasa.

Hivi katiba ya CCM haijaainisha majukumu ya Mwenyekiti wa hiyo jumuiya ya wanawake? Inakuwaje huyu Sofi hajataja majukumu yake kikatiba anakimbilia kusema kuwa Uenyekiti UWT ni ceremonial?
 
Hahahahahaaa....yote yanaanzia kwa aliye juu. Sasa msikikilize hata Kikwete mwenyewe anavyoongea. Najua sasa tuna dwell zaidi kwenye trivial lakini ndio hivyo tena
 
Back
Top Bottom