Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,337
- 113,179
Naomi Kaihula ni mwanamke mwanaharakati wa kweli na mwanasiasa aliyelelewa na siasa tangu enzi za mfumo wa siasa za chama kimoja. Huyu Mama alinifundisha somo la siasa shule ya sekondari ya Tambaza miaka ya themanini. Nadhani alijiendeleza kielimu na ku upgrade toka mwalimu wa sekondari mpaka mhadiri wa chuo kikuu cha CBE.
Mama Kaihula ni muongeaji mzuri, ila mama Sofia Simba yeye ni muongeaji wa type ya pashkuna, misuto ni jadi yake kama walivyo mabinti wa Kizarazo, hivyo mdahalo kati yao moto wa kelele utawaka, mmoja akimwaga hoja, mwingine akimsuta!.
.
Ukimsikiliza-mama Simba, utagundua ni 'Debe Tupu' hata JK amempigia kampeni kiaina, nakumbuka baada ya Mama Kahama kuibua tuhuma za rushwa dhidi ya Mama Simba, nilisema hii ni kesi ya nyani kapeleka kwa ngedere, nikasisitiza JK hata akithibitisha uchafu huo wa Mama Simba, hawazi kukubali ukubaliwe na kuchafuua chama chake na serikali yake, bali ni rahisi zaidi kumdismiss Mama Kahama- na kumbeba Mama Simba.
Tatizo ni vyama vyao, kuuidahalisha UWT na BAWACHA ni sawa na Tembo na Sisimizi, japo sisimizi anaweza kumuua Tembo, UWT inajisikia kuwa ina hatimiliki ya issues za wanawake wote wa Tanzania chini ya mwamvuli wa CCM ambacho ni chama dola na ndio waliopelekea kupigwa marufuku kwa lile baraza la wanawake la Prof.Tibaijuka, BAWATA. Hivyo UWT hawawezi kukubali mdahalo na BAWACHA.
Wanawake wa CCM wamezoea kubebwa, hakuna asiyejua jinsi Sofia Simba alivyobebwa na kuukwaa uenyekiti UWT, akikubali mdahalo na Naomi Kaihula, nani atambeba?. Kuliko kugalagazwa, bora wakatae.