Mwaka 2017 CCM ilimfukuza M/kiti wa UWT Sophia Simba aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Ndugai hakusema ni unyanyasaji wa kijinsia

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,313
2,000
Machi 11, 2017 Kamati Kuu ya CCM iliwafukuza wanachama kadhaa wa chama hicho na wengine kupewa onyo kwa makosa mbalimbali ya maadili kinyume na Katiba na kanuni za uongozi na maadili za CCM.

Waliofukuzwa (kuvuliwa) uanachama ni pamoja na Sophia Simba, Mwenyekiti UWT ambaye pia alikuwa ni Mbunge wa Viti Maalum na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu. Kufuatia maamuzi hayo Sophia Simba alipoteza nafasi yake ya Ubunge wa Viti Maalum na Uenyekiti wa UWT.

Wakati Sophia Simba na wenzake wakifukuzwa Ndugai alikuwa Spika, hatukumsikia akisema CCM inanyanyasa Wanawake.
 

Ryaro wa Ryaro1233

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
353
1,000
Kitendo cha Kupatikana na Kura Ndani ya Mabegi Meusi Kule KAWE, Wakati walijua Halima Mdee ni Mwanamke hivyo wangaacha Uwanja sawa ili Ngwajima apite kwa haki lakini CCM kipindi hicho hawakumwona dada huyu kama ni Mwanamke wakamchakachua kura zile.

Kitendo cha Kumweka Police Upendo Peneza huku wakijua wakati Kura zinaenda Kupigwa CCM hawakujua alikuwa Mwanamke. Ndugu Yangu wewe acha tu Mungu Ndio anajua Zaidi, maana sisi Wanadamu wa Kawaida Maovu ya Sisiem Hayaesabiki.
 

Tigershark

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
7,055
2,000
Usisahau pia wabunge8 viti maalumu walitimuliwa na Lipumba na spika alikuwa India kwa matibabu, siku hiyo hiyo akaiandikia NEC barua kueleza kuwa nafasi ziko wazi!

Hakuwatetea wala kuwalinda wale viti maalumu!
 

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,568
2,000
Wakati Sophia Simba na wenzake wakifukuzwa Ndugai alikuwa Spika, hatukumsikia akisema CCM inanyanyasa Wanawake.
Sophia alipewa nafasi ya kujitetea,na alihukumiwa na vikaostahiki
katiba ya chadema inataka mtuhumiwa kupelekewa mashitaka yake kwa maandishi siku saba kabla ya kikao husika,je hilo lilifanyika?
Mdee ni kiongozi wa juu,hukumu yake inatoka baraza kuu,sio kwenye kamati kuu,ndio mana ndugai amekataa kubariki uhuni wenu
 

Reykijaviki

JF-Expert Member
Aug 25, 2020
353
1,000
CCM wanazitaka zile trillion 2 za mabeberu, hawana lolote!
Wangeacha kuiba haya majimbo la Hai, mbeya, Arusha, Iringa, na Kawe hayo majimbo matano yangewapa hizo pesa lakini kwa sababu wanatamaa wacha waisome namba, kwanza advertise imeanza kupewa milioni 50 badala ya 90, hahahaha PANGA KALI in kikwete voice!
 

Papy ndombe

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
3,192
2,000
Wakati wanaiba kura waliwaza ushindi wa kishindo na awakuwaza kuna pesa za mabeberu watazikosa wamekumbuka shuka
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom