Spika Job Ndugai alishindwa Kumlinda Sophia Simba na wenzie 12 walipofukuzwa na CCM, ubavu wa Kumlinda Halima Mdee na Wenzie 18 atautoa wapi?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,721
2,000
Salaam Wakuu.

Kama mnakumbuka mwezi March 2017 CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kiliwafukuza wanachama wake 12, akiwamo Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT), Sophia Simba.

Sophia alilazimika kupoteza ubunge kutokana na uamuzi huo, alifukuzwa baada ya kupatikana na makosa ya maadili kinyume na Katiba na kanuni za chama cha Mapinduzi (CCM).

Sophia Simba alikuwa katumikia Ubunge kwa takribani miaka 22, pia alipoteza nafasi yake ya uenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania(CCM) aliyokuwa ameitumikia kwa muda wa miaka 10.

Alipokuwa akitoa taarifa ya Mkutano wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa (NEC) kwa waandishi wa habari, Aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepele, pasipo kufafanua, alisema Sophia alipatikana na hatia ya makosa ya kiuadilifu ya chama cha CCM.

“Wajumbe wa NEC kwa sauti moja wameridhia kumfukuza uanachama Sophia Simba,” alisema Polepole.

Mbali na Sophia, pia alisema wenyeviti wa CCM wa mikoa minne nao wamefukuzwa kwa makosa kama hayo.

Aliwataja wenyeviti hao na mikoa yao katika mabano kuwa ni Jesca Msambatavangu (Iringa) Sasa hivi ni Mbunge wa Iringa(CCM), Erasto Kwilasa (Shinyanga), Ramadhan Madabiba (Dar es Salaam) na Christopher Sanya (Mara). Polepole aliwataja wanachama wengine waliofukuzwa kuwa ni Willfred ole Mollel ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini, mjumbe wa NEC wa Wilaya ya Babati Mjini, Ally Sumaye na Mathias Manga wa Wilaya ya Arumeru.

Katika orodha hiyo, pia walikuwemo wenyeviti wa wilaya wa chama hicho ambao ni Omari Awadhi (Gairo), Ally Msuya (Babati Mjini), Makolo Laizer (Longido) na Salumu Madenge (Kinondoni-Dar es Salaam).

Ingawa Polepole hakufafanua sababu za kumfukuza uanachama Sophia, kumpa onyo kali Nchimbi na kumsamehe Kimbisa, wanachama hao ndio waliojitokeza hadharani kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM iliyoketi kupitisha majina ya wagombea urais kupitia chama hicho mwaka 2015.

Itakumbukwa, Nchimbi, Kimbisa na Sophia walipinga kitendo cha kamati ya maadili chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wake Rais Mstaafu Jakaya Kikwete cha kukata majina ya wagombea urais likiwamo la aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na kupeleka majina matano tu yajadiliwe ndani ya kamati hiyo. Wanasiasa hao walidai kuwa kanuni za chama hicho zilikuwa zimepindishwa.

Hayo yote yakifanyika, Mheshimiwa Jon Ndugai hakunyanyua ulimi wake kusima amlinde au hata kumteteta Sophia Simba ambaye alikuwa Kamuapisha kuwa Mbunge. Tena ndani ya Bunge. Sikuona Anawakingia Kifua.

Hata Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) lilipofukuza Wabunge 8 wa viti Maalum, ambao walikuwa Wameapishwa, Sikusikia wala kuona anawakingia Kifua badala yake aligongelea Msumari. July 26, 2017 taarifa kutoka ofisi ya Bunge ilieleza kuwa Spika Job Ndugai ameridhia kufutwa uanachama kwa Wabunge hao na hivyo nafasi zao ziko wazi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Spika Ndugai amejiridhisha kuwa Wabunge hao wamefutiwa uanachama kulingana na taratibu za chama hicho na hivyo hawana sifa za kuendelea na Ubunge. Hivyo kwa mamlaka aliyonayo kwa kuzingatia kifungu cha 67(1)(b) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 kikisomwa pamoja na kifungu 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi Sura ya 343 kama ilivyojadidiwa Mwaka 2015, Spika alitangaza nafasi hizo kuwa wazi na kumuandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi aendelee na hatua zinazostahili kujaza nafasi hizo kwa mujibu wa Sheria.

Waliovuliwa ubunge ni Uongozi wa CUF walikuwa ni Mheshimiwa Severina Silvanus Mwijage, Mheshimiwa Saumu Heri Sakala, Mheshimiwa Salma Mohemed Mwassa, Mheshimiwa Riziki Shahari Mngwali, Mheshimiwa Raisa Abdallah Mussa, Mheshimiwa Miza Bakari Haji, Mheshimiwa Hadija Salum Ally al Kassmy na Mheshimiwa Halima Ali Mohamed.

SWALI:

Iweje leo Uongozi wa CHADEMA imefukuza Wanachama wake Spika ambaye ni Wanachama wa CCM anadai atawakingia kifua wakati alishindwa Wakingia Kifua CCM wenzie? Ujasili anautoa wapi?
 
Interested Observer

JF-Expert Member
Mar 27, 2006
2,076
2,000
CCM ni watekaji ina bidi washitakiwe mahakamani, tena ya kimataifa. They took these ladies hostage, mmewabambikia kesi, yaani hao ni victims wenu na mnawatumia kisiasa sasa; this is discrimination. Yaani hata hao kina Nd--ai, Bash--iru na serikali wanafanya vitendo vya ajabu sana.

WaMewanyanyasa kwenye kura, mmewaweka vidole (kuna video kabisa), mkawafunga; sasa mnawatumia, loooo, sijawahi kuona serikali kama hii duniani, Tanzania ni Nchi ya kwanza, na hii ikisikika duniani is going to be scandalous and will bring this country to its knees! We are ruled by hus---lers; halafu hao ni wanawake! Hata SA arpatheid hawakutesa wanawake, walitesa wanaume, walikuwa na limits.

CCM a gang of hustlers
 
CHARLES2016

Senior Member
Mar 22, 2016
151
250
Ukifuata sheria inavyotaka, baada ya wabunge hao wa viti maalum kufutwa uanachama wao, inatakiwa Spika apewe taarifa kwa maandishi (barua) kutoka kwa katibu mkuu wa Chadema akimtaarifu kuwa watu hao siyo wanachama wa Chadema.

Spika asipopata barua hiyo hana mamlaka ya kuwavua ubunge wao wa viti maalum.

Changamoto ni kwamba Chadema hawatambui viongozi wote waliopatikana kutokana na uchaguzi uliopita akiwemo spika, Sasa watamwandikiaje spika wasiyemtambua? Wakiandika barua kwa spika maana yake madai yao yote kuhusu uchaguzi yatakuwa ni batili.

Kwa hiyo usishangae ndugai anaposema atawalinda anafahamu Sheria inawalinda.
 
mwanateknolojia

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
834
1,000
Rejea alichofanya kwa mbunge Cecil Mwambe ambaye alijivua ubunge yeye mwenyewe, lakini bado akakataa kuitambua taarifa ya CHADEMA!

Rejea alichofanya kwa wabunge wasaliti wa covid kina Silinde, Lijualikali na wengine, Hawa wote kumi walivuliwa uanachama na CHADEMA lakini spika aligoma kuyatambua maamuzi ya chama, alafu hata CHADEMA walipojaribu kwenda mahkamani, bado mahakama ilitupilia mbali kesi! Hivyo hata kwa hao anaweza kutumia kigezo kwamba hawakupewa nafasi ya kusikilizwa na hivyo akaamua anavyojua yeye, usishangae hata mahakama ikaja kutupilia mbali kesi!

Njia ya pili wabunge wale wasaliti wanaweza kusukumwa kwenda mahakamani kupinga maamuzi ya chama kwa kutoa sababu yoyote ile na usishangae mahaka ikawasikiliza na kuwekea pingamizi la utekelezaji wa adhabu ya chama na issue ikabaki hivyo hadi miaka yote 5 bikakatika!

Kwa ufupi CCM imevuruga sana mifumo ya haki, wanaweza kuamuru kifanyike chochote ilimradi kudhoofisha upinzani!
 
osward mambo

Senior Member
Jul 31, 2020
125
225
CCM ni watekaji ina bidi washitakiwe mahakamani, tena ya kimataifa. They took these ladies hostage, mmewabambikia kesi, yaani hao ni victims wenu na mnawatumia kisiasa sasa; this is discrimination. Yaani hata hao kina Nd--ai, Bash--iru na serikali wanafanya vitendo vya ajabu sana...
Wakulaumiwa ni hao walipkubali kurubuniwa
 
LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
8,487
2,000
Ukifuata sheria inavyotaka, baada ya wabunge hao wa viti maalum kufutwa uanachama wao, inatakiwa Spika apewe taarifa kwa maandishi (barua) kutoka kwa katibu mkuu wa Chadema akimtaarifu kuwa watu hao siyo wanachama wa wachadema...
Kiutaratibu taarifa ya umma iliyotolewa na chadema kuwavua wanachama wake walioapa kiapo Cha ubunge, spika anapaswa kuifanyia kazi. Kina mdee wanapaswa kuondolewa bungeni.Hilo ni takwa la kikatiba.
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
10,236
2,000
Habari ya Sofia Simba haikua ya kisiasa peke yake. Alikua na madudu mengi sana yule bimkubwa

Kikubwa alirudi akatubu na kufanya malipizi
 
Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
13,992
2,000
Ukifuata sheria inavyotaka, baada ya wabunge hao wa viti maalum kufutwa uanachama wao, inatakiwa Spika apewe taarifa kwa maandishi (barua) kutoka kwa katibu mkuu wa Chadema akimtaarifu kuwa watu hao siyo wanachama wa wachadema...
Haya ya pili watajifanya hawaijui
 
Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
13,992
2,000
Kiutaratibu taarifa ya umma iliyotolewa na chadema kuwavua wanachama wake walioapa kiapo Cha ubunge, spika anapaswa kuifanyia kazi.Kina mdee wanapaswa kuondolewa bungeni.Hilo ni takwa la kikatiba
Ufanyie kazi taarifa ya Kwa vyombo vya habari
 
Usher-smith MD

JF-Expert Member
Jul 7, 2015
8,510
2,000
Kwa waliofukuzwa mwezi wa 3 Silinde na wenzake , na yule aliyejivua uanachama walibaki wabunge kwa nguvu ya nani
IMG_20201130_103932_639.JPG

Sent from my G-PADLITE using JamiiForums mobile app
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,778
2,000
Iweje leo Uongozi wa CHADEMA imefukuza Wanachama wake Spika ambaye ni Wanachama wa CCM anadai atawakingia kifua wakati alishindwa Wakingia Kifua CCM wenzie? Ujasili anautoa wapi?
CCM haifanyi mambo kienyeji
Hao kina Halima waliitwa wapi kujieleza?katiba ya chadema inataka mtuhumiwa apelekewe mashitaka siku 7 kabla ya kikao,ili apate muda wa utetezi,hilo lilifanyika?
 
Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,081
2,000
Salaam Wakuu.

Kama mnakumbuka mwezi March 2017 CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kiliwafukuza wanachama wake 12, akiwamo Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT), Sophia Simba.

Sophia alilazimika kupoteza ubunge kutokana na uamuzi huo, alifukuzwa baada ya kupatikana na makosa ya maadili kinyume na Katiba na kanuni za chama cha Mapinduzi (CCM).

Sophia Simba alikuwa katumikia Ubunge kwa takribani miaka 22, pia alipoteza nafasi yake ya uenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania(CCM) aliyokuwa ameitumikia kwa muda wa miaka 10.

Alipokuwa akitoa taarifa ya Mkutano wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa (NEC) kwa waandishi wa habari, Aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepele, pasipo kufafanua, alisema Sophia alipatikana na hatia ya makosa ya kiuadilifu ya chama cha CCM.

“Wajumbe wa NEC kwa sauti moja wameridhia kumfukuza uanachama Sophia Simba,” alisema Polepole.

Mbali na Sophia, pia alisema wenyeviti wa CCM wa mikoa minne nao wamefukuzwa kwa makosa kama hayo.

Aliwataja wenyeviti hao na mikoa yao katika mabano kuwa ni Jesca Msambatavangu (Iringa) Sasa hivi ni Mbunge wa Iringa(CCM), Erasto Kwilasa (Shinyanga), Ramadhan Madabiba (Dar es Salaam) na Christopher Sanya (Mara). Polepole aliwataja wanachama wengine waliofukuzwa kuwa ni Willfred ole Mollel ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini, mjumbe wa NEC wa Wilaya ya Babati Mjini, Ally Sumaye na Mathias Manga wa Wilaya ya Arumeru.

Katika orodha hiyo, pia walikuwemo wenyeviti wa wilaya wa chama hicho ambao ni Omari Awadhi (Gairo), Ally Msuya (Babati Mjini), Makolo Laizer (Longido) na Salumu Madenge (Kinondoni-Dar es Salaam).

Ingawa Polepole hakufafanua sababu za kumfukuza uanachama Sophia, kumpa onyo kali Nchimbi na kumsamehe Kimbisa, wanachama hao ndio waliojitokeza hadharani kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM iliyoketi kupitisha majina ya wagombea urais kupitia chama hicho mwaka 2015.

Itakumbukwa, Nchimbi, Kimbisa na Sophia walipinga kitendo cha kamati ya maadili chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wake Rais Mstaafu Jakaya Kikwete cha kukata majina ya wagombea urais likiwamo la aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na kupeleka majina matano tu yajadiliwe ndani ya kamati hiyo. Wanasiasa hao walidai kuwa kanuni za chama hicho zilikuwa zimepindishwa.

Hayo yote yakifanyika, Mheshimiwa Jon Ndugai hakunyanyua ulimi wake kusima amlinde au hata kumteteta Sophia Simba ambaye alikuwa Kamuapisha kuwa Mbunge. Tena ndani ya Bunge. Sikuona Anawakingia Kifua.

Hata Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) lilipofukuza Wabunge 8 wa viti Maalum, ambao walikuwa Wameapishwa, Sikusikia wala kuona anawakingia Kifua badala yake aligongelea Msumari. July 26, 2017 taarifa kutoka ofisi ya Bunge ilieleza kuwa Spika Job Ndugai ameridhia kufutwa uanachama kwa Wabunge hao na hivyo nafasi zao ziko wazi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Spika Ndugai amejiridhisha kuwa Wabunge hao wamefutiwa uanachama kulingana na taratibu za chama hicho na hivyo hawana sifa za kuendelea na Ubunge. Hivyo kwa mamlaka aliyonayo kwa kuzingatia kifungu cha 67(1)(b) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 kikisomwa pamoja na kifungu 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi Sura ya 343 kama ilivyojadidiwa Mwaka 2015, Spika alitangaza nafasi hizo kuwa wazi na kumuandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi aendelee na hatua zinazostahili kujaza nafasi hizo kwa mujibu wa Sheria.

Waliovuliwa ubunge ni Uongozi wa CUF walikuwa ni Mheshimiwa Severina Silvanus Mwijage, Mheshimiwa Saumu Heri Sakala, Mheshimiwa Salma Mohemed Mwassa, Mheshimiwa Riziki Shahari Mngwali, Mheshimiwa Raisa Abdallah Mussa, Mheshimiwa Miza Bakari Haji, Mheshimiwa Hadija Salum Ally al Kassmy na Mheshimiwa Halima Ali Mohamed.

SWALI:

Iweje leo Uongozi wa CHADEMA imefukuza Wanachama wake Spika ambaye ni Wanachama wa CCM anadai atawakingia kifua wakati alishindwa Wakingia Kifua CCM wenzie? Ujasili anautoa wapi?
Banana Republic
 
Msororo69

JF-Expert Member
Feb 27, 2016
2,728
2,000
Ukifuata sheria inavyotaka, baada ya wabunge hao wa viti maalum kufutwa uanachama wao, inatakiwa Spika apewe taarifa kwa maandishi (barua) kutoka kwa katibu mkuu wa Chadema akimtaarifu kuwa watu hao siyo wanachama wa Chadema.

Spika asipopata barua hiyo hana mamlaka ya kuwavua ubunge wao wa viti maalum.

Changamoto ni kwamba Chadema hawatambui viongozi wote waliopatikana kutokana na uchaguzi uliopita akiwemo spika, Sasa watamwandikiaje spika wasiyemtambua? Wakiandika barua kwa spika maana yake madai yao yote kuhusu uchaguzi yatakuwa ni batili.

Kwa hiyo usishangae ndugai anaposema atawalinda anafahamu Sheria inawalinda.
Nimekuwa nikiiona hoja ya kitoto ikitembea kama hii. Nani katika nchi hii asiyejua kama chadema haijapeleka majina ya viti maalumu kwa mujibu wa sheria, nani hajui kuwa spika kawakataza hao wabunge kwenda kwenye kamati kuu kusikilizwa, ni nani asiyefahamu kuwa serikali nzima inahusika kufanya huu mchakato haramu. Kwa mahovyovyo yote haya hakuna wabunge pale kwa mujibu wa katiba na sheria zetu
Tunachosubiri kukiona Je hawa watu wanaheshimu katiba walioapa kuilinda? Kushindwa kuheshimu viapo vyao wanakosa sifa za kuheshimiwa. Hata kuwapuuza na kuwadharau ni adhabu tosha historia yetu itaendelea kuwahukumu hata vizazi vyao.
Kwa kuwa umma umewaachia waisigine katiba wapendavyo hakuna wa kuwazuia kuapisha wabunge wawapendao kwa mujibu wa matakwa yao.
Sisi tutajiuliza ni halali hapana si hali kikatiba, kisheria, mila na destuli zetu si halali.
Nimalize kwa kukupongeza kufunga mkono uvunjaji wa katiba na shiria za nchi hii
 
Reykijaviki

JF-Expert Member
Aug 25, 2020
372
1,000
Sofia simba alifukuzwa na chama halali Lakini akina mdee wamefukuzwa na chama ambacho sio halali!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom