sooo disapointed | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

sooo disapointed

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by dagaa, Dec 10, 2011.

 1. dagaa

  dagaa JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 80
  habari zenu wapendwa! mume wangu alikwenda site tunako jenga, alikwenda tangu asubuhi, akarudi sa 8 usiku, na alipokuja nilimfungulia mimi na akalala tv room, ila anachonishanga akiwa site huwa tunawasiliana ila ikifka sa kumi atumi message wala kupiga sim,na ukimpgia anaongea kwa wasiwasi, mpaka siku hizi nimeacha kumpigia. na hii ni mara ya tatu jamani nifanyeje? na si mpenzi wa kutoka nje, ila akitoka kasumba yake ndo hiyo, nahisi nimechoka na tabia hii, mi uwa namnyamazia naishia zangu kulia.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  sasa usiposema atajuaje kama hupendi hiyo tabia? Wanamme wanakamua nje lakini mwambie ili ajue abadili trick maana hiyo kama umeishtukia atumie nyingine ambayo haitakuumiza.
  Acha kutumia antena tumia brain.
   
 3. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,454
  Likes Received: 7,220
  Trophy Points: 280
  Usimfuatilie,utakufa siku si zako,mwenzako wala hataumia kihivyo,na ataoa mwingine
   
 4. Prof Gamba

  Prof Gamba JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 390
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Nadhani bado hujamalizia. Ukweli wako kwa mumeo utakuweka kuwa huru. Muulize na umwambie kuwa tabia yake kwa sasa inakukera na inakufanya uwe unaishia zako kulia. Pole sana bi dada.
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  wakati mwingine wala mshkaji hafanyi kitu chochote, wanawake are good at imagining things hasa anapokuwa paranoid.

  Paranoia ni ugonjwa mbaya sana unaweza ukaona sisimizi ukamkuza akawa tembo ukaita na game rangers waje wamuue.
   
 6. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,515
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  unamawazo meeeeengi wakati mwenzako anajenga
   
 7. chriss brown

  chriss brown JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mumeo kimeo huyo,kwa nini asikupigie,au hatumi msg?muulize,ukishindwa,sepa zako dada,kwan wataka kufa mapema weye.
   
 8. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2011
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Pole sana dada......huyo jamaa (m sorry) ni msha--mba sana huyo hayo madudu wenzake huwa wanayafanya with a very high degree of respect kwa mke wa ndoa.....hope tutakutana naye huko street university tumpe lesson on "how to respect a wife"

  ILA; Sasa ukilia ndo nini na wewe ushakuwa mama ??? Anafanya huo unyambilis wake kwa kuwa anajua na wewe ni soft kama tissue paper.....nakuibia siri hapa (masela mnichunie ili kuimarisha ndoa ya huyu man mwenzetu) mamy sisi (responsible husbands) huwa tunatingishika khaswaa unapokuta mkeo hayuko na amani na anafanya responsibilities zake kama kawaida as la kwanza kwetu ni furaha ya familia then sarakasi za nje ndo zinanoga. kama family inayumba hata huko nje ni tasteless sasa chukia kweli na uoneshe umechukia kwa kauli na matendo tena dai hiyo haki ya kusikilizwa usiku na mchana...then umuwekee mabaya yake na kwanini wewe unayaona ni mabaya......safari za site kama uko free nawe nenda sio ukae tu unaangalia nigerian movies....mtafute pesa wote yeye akakae juani na mafundi we upumzike tuuu kama mama yake mzazi....waweza kuta kuna jirani hapo site anapika na kupakua we upo na remote tuu kubadilisha channels.............Get up....stand up...stand up for your rites (Bob Marley)
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Dec 10, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,231
  Trophy Points: 280
  vunja ukimya.

  Imeletwa kwenu kwa hisani ya marekani.
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Dec 10, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,468
  Trophy Points: 280
  sasa si umfuate site kuanzia saa tisa siku moja upate ukweli????????
   
 11. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #11
  Dec 10, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,043
  Likes Received: 3,235
  Trophy Points: 280
  Pole samaki pole.
   
 12. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #12
  Dec 10, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,115
  Likes Received: 24,197
  Trophy Points: 280
  Word!!!!!!:poa
   
 13. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #13
  Dec 10, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Huyo ni mume sio boifriend dada dagaa una mamlaka yakumuuliza kila unapohisi kuna chochote ambacho hakiendi sawaa...kulia sio solution wakati we unalia kama ana mambo yake ya kijinga afanya then kama kawaida atayaendeleza na mwisho wa siku yatakomaa..utakosa wa kumlaumu. Okoa ndoa hiyo mama!
   
 14. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #14
  Dec 10, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Tena majirani wa design hiyo wabayaaaaa.....maana atakuwa anajifanya ndo mwenyeji wa jamaa kila akienda,si anajua mwenyewe yupo busy sana.. Bonge la advice hapo umepata..Jiamini dagaa..au unaomuogopa sana jamaa? Usikute ukitia neno tu ataku-tyson...
   
 15. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #15
  Dec 10, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  Ngoja nikupe haka ka siri na mimi (wadada ipotezeeni kama hamjaona)

  Mwanamke au mkeo akikupenda sana nao ni msalaba maana huwa inapelekea kitu kinchoitwa paranoia. Mme alichelewa tu unaanza kumuona anamvua nguo mwajuma. Afu labda mama ako anakupigia simu anakuambia mmeo kapita hapa kutusalimia basi wewe tabasamu linarudi usoni lakini kama usingeambiwa chochote utaona na lipstick kwenye kiatu chake.

  Ndo mana mie husema kama mwanamke anaweza bora amwelewe tu mumewe.

  Hajamshika na mwanamke zaidi ya kuhisi tu, chunguze kwanza hasa ndo mnapokuwa na mtoto mmoja huwa ni kama adolescence ya ndoa kwa wadada
   
 16. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #16
  Dec 10, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,724
  Trophy Points: 280
  You said it all. Wanaume wengi wananogewa nje kwa sababu wake zao wanaugulia chini chini. Usimpe peace of mind uone kama huko nje itasimama. Jua position yako bidada :"you are the WIFE for Christ's sake!"

  Huyo mwanaume ni wewe mwenyewe unamharibu kwa kutokuwa muwazi. Ngoja awe sugu uone kama atabadilika.

  Mulika mwizi:director:

   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Dec 10, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hisia zinaua haraka kuliko facts,

  Tafuta kwanza facts badala ya kujitafutia kifo......!!

  Nitarudu baada ya lunch,

  Babu DC!!
   
 18. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #18
  Dec 10, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Duuuuu,

  Hapo umemaliza kila kitu...Hakuna mwizi anaiba penye mwanga mkali...Lazima atafute uchochoro wenye giza giza...

  Ni bora huyu dada azibe vichochoro kwanza badala ya kulia lia kama mtoto!!
   
 19. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #19
  Dec 10, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  Asante babu DC, haya mambo ya hisia bila jua ukweli mi wala huwa hayaniingii.

  Kuna mwingine mtu alisafiri wiki bila kuaga akadhani ni alshabab kumbe wala hata sio ila kuna coincidence ziliingiliana hapo akajua alshaba kabsa
   
 20. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #20
  Dec 10, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,724
  Trophy Points: 280
  Ushauri wangu mwingine (Plan B) ikifika siku ya kwenda site na wewe jiandae, usimwambie kuwa unaenda. Akiingia kwenye gari na wewe tia timu. Mwambie leo honey nimejisikia ghafla kuandamana na wewe.

  Afu mkifika huko mwambie naomba kutumia simu yako; hapo simu yako iache home sema umesahau. Hakikisha unakaa na simu ya Mr for as long as possible mwambie unachati na friend, ikibidi uwe unachati kweli hata na ndugu. Hapo ndo utaona huyo anayemzingua either anatuma message au anapiga. Utamjua mwizi wako. Kaba mama kaba mpaka penati.

  Otherwise baki ila badili sim card yake kwa siku hiyo na kuweka new sim card na kuweka simu card yake kwenye simu yako but you need to save all his numbers in his phone book to that new sim card ili akitaka kumpigia asikwame afu set simu yake kwenye private number ili anayempigia asijejibu tumia new number ila atumie namba ya simu card uloiba(hii trick niliisoma humu humu JF)
   
Loading...