Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Wakizungumza na EATV baadhi ya Wanawake kijijini hapa wamesema tayari wameshaanza kutumia njia za uzazi wa Mpango kwa lengo la kutopata ujauzito kutokana na changamoto wanazopata kwenye matibabu hasa huduma ya kujifungua pamoja na kwenda Kliniki za kila mwezi huduma ambayo wanaipata katika vijiji jirani ambavyo viko mbali na makazi yao hivyo huongeza gharama wawapo nje na makazi yao.
Licha kukamilika kwa ujenzi wa boma la Zahanati ya kijiji na Serikali kutoa fedha kiasi cha Shilingi Milioni 50 tangu Mwaka 2024 bado Zahanati hiyo haijakamilika.
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wanawake wakidai kunyanyaswa wanapofuata huduma katika vijiji vya jirani.