Songwe: Raia wampiga anayedaiwa kuwa mlinzi wa JKT aliyejificha kukamata magendo

Huko Mbeya inaelekea kuna ulaji sana ndio maana kila mtu anafanya shamba la bibi.

Wacha wamdunde tu maana njaa ni kitu mbaya sana.
 
Mtu anayedaiwa kuwa ni mlinzi wa Kampuni ya Suma JKT, Emmanuel Myela (35) mkazi wa Wilaya ya Mbozi, amelazwa katika hospitali teule ya rufaa mkoani hapa, baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira, alipokuwa akivizia watu wanaosafirisha bidhaa za magendo toka nchi jirani ya Malawi jana Oktoba 17.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Janeth Magomi alipoulizwa kwa simu kuhusu tukio hilo amesema kwa sasa hawezi kulizungumzia kwa kuwa hakuwa na taarifa iliyo kamili.

Mmoja wa shuhuda aliyekuwepo eneo la tukio, Mussa Mgode amedai kwamba askari hao ambao walikuwa watatu hawakuvalia sare za jeshi wakiwa na pikipiki mbili walifika eneo hilo majira ya saa 9 alasiri kisha walimkamata mtu mmoja waliyedai kuwa amebeba magendo hao.

Alisema baada ya kumkamata mtu huyo palitokea mabishano kati yao na ndipo walipojitokeza wenzao kadhaa ambao waliamua kupambana na ‘askari hao’.

Kama hiyo haitoshi, shuhuda huyo alisema lilijitokeza kundi la wananchi waliokuwa wakitokea kwenye msiba na kuanza kuwasaidia vijana hao na ndipo askari wawili walifanikiwa kukimbia kusikojulikana wakizitelekeza pikipiki zao mbili ambazo baadaye zilichomwa moto na wakazi hao.

Hata hivyo, mmoja wao aliyebaki alikimbilia iliyo jirani na kujifungia, lakini wananchi kwa hasira walivunja dirisha la nyumba hiyo na kumtoa nje na kuanza kumshushia kipigo kikali kabla ya Polisi kufika na kumuokoa.

Kaimu Mganga Mfawidhi, Dk Lighton Alex amethibitisha kumpokea majeruhi huyo akiwa hajitambui kutokana na kipigo.

Amesema askari huyo alifikishwa katika Hospitali hiyo kwa gari ya polisi baada ya kuokolewa kwenye kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.

Amesema baada kumfanyia vipimo vya mionzi ilibainika kuwa majeruhi huyo alipata mpasuko kwenye fuvu lake la kichwa.

Ameongeza kuwa, mtu huyo ana majeraha mbalimbali kwenye mikono yake yote miwili, pamoja na mguu wa kulia, hivyo kutokana na hali hiyo atapatiwa rufaa ili akapatiwe matibabu ya juu zaidi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpanda, George Mwambubha lilipotokea tukio hilo, amesema mara kadhaa watu hawa (askari) wamekuwa wakifika kijijini hapo na kukamata vijana wanaosafirisha magendo ya mafuta ya kula na pombe za viroba kutoka Malawi, lakini jana ilikuwa tofauti.

Mwananchi
 
JKT wanaruhusiwa kukamata?
Hawana akili hao, kuna siku nilienda stend ya magufuli mbezi sasa huyo suma jkt akawa anakagua tiketi pale getini, baada ya kumpa tiketi yangu akachelewa kunirudishia nikamwambia nipe tiketi yangu akanijibu nikiamua sikupi, nikabaki kushangaa sasa asinipe ili aifanyie nini?
 
Hao walikuwa wahuni tu wala si askali, hao waliotoroka hawawezi onekana kamwe,maana wanajua walichokiwa wanafanya ni uhalifu
 
Ni Jambo la heri kuona wananchi wanashirikiana vizur kiasi hcho!

Kama mikoa yote tungekuwa na ushirikiano wa namna hii, Basi tungeheshimiana Sana mitaani!
 
Back
Top Bottom