Songea yetu, karibuni mji uliobarikiwa

Songea yetu, karibuni mji uliobarikiwa

yaani mkuu nimekusoma vilivyo we inaelekea ni wa miaka ya 198.... maana hiyo mechezo ya dombi dombi mmmh! nakumbuka sana hasa nikiwa shule ya msingi Majimaji
Majimaji kabla haijahamishwa? Mi nilikuwa kuburang'oma enzi hizo mlima ulifukia wanafunzi
 
Warning:wana Songea hadi Namtumbo watapata madhara makubwa na hasa cancer kutokana na uchimbaji wa madini ya uranium ambayo wana Ruvuma hawatapata kitu ila wataachiwa magonjwa ya kudumu.Hii ndio sera ya Magamba.Wana songea simameni hakikisheni hata kama mtaachiwa magonjwa angalu mpate faida.Ulizeni maswali kuhusu afya yetu kutokana na huyo mgodi.Angalia wenzenu wanalia huko katika nchi ya GABON.
 
Mkuu veve u mdesi(kwa kihehe uwongo) Songea gani hiyo? Uchawi kila sehemu ukienda utapewa story za wanga so usiseme uwongo
mkuu nakubaliana na wewe hakuna sehemu isiyokuwa na wachawi,ila kwa hapa topic ni SONGEA.
 
Ukipita pale Mfaranyaki nisalimie sana washkaji zangu waambie nitapita huko mwezi wa June nikajidai na ulanzi na mahindi ya kuchoma 🙂🙂
 
Warning:wana Songea hadi Namtumbo watapata madhara makubwa na hasa cancer kutokana na uchimbaji wa madini ya uranium ambayo wana Ruvuma hawatapata kitu ila wataachiwa magonjwa ya kudumu.Hii ndio sera ya Magamba.Wana songea simameni hakikisheni hata kama mtaachiwa magonjwa angalu mpate faida.Ulizeni maswali kuhusu afya yetu kutokana na huyo mgodi.Angalia wenzenu wanalia huko katika nchi ya GABON.
mkuu songea watu wamewaamini sana magamba.huko vijijini hususan namtumbo ndo usiseme!wakiona tu kofia na t.shirt za kijani wanachanganyikiwa kabisa.
 
mkuu songea watu wamewaamini sana magamba.huko vijijini hususan namtumbo ndo usiseme!wakiona tu kofia na t.shirt za kijani wanachanganyikiwa kabisa.

Mkuu pale town wameamka sana sasa hivi, kuna madiwani wa chadema, huyu nchimbi kwanza hakushinda pale town walichakachua matokeo ccm
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Matuta yanazidi yale ya barabara ya Mirambo huku Dar au yale ya barabara ya kwa bibi Nyau kule kwa mtogole... ?? Sana Huko Songea matuta ni pale Bombambili na shule ya msingi misufini basiii...
Matuta makubwa kuliko yote Afrika Mashariki yapo Arusha eneo la kwa Dr. Mohamed. Chanzo kilikuwa ni Radio One Stereo kipindi hicho.

Hayo matuta mpaka yashinde kwa ya Arusha yakoje?

Jamani hivi Box 2 imefanyiwa hata kaukarabati kidogo.

Na Tamsala napo??
 
...Kwa walioko Songea sasa Hivi: Nilimaliza darasa la saba mwaka 1974 hapo Mfaranyaki shule ya Msingi enzi za kina Mwalimu Lucanus Mbano, Kabiru Mbawala, Mrs Matembo, Mzee Tuka, Mzee Mande na wengineo.

Wakuu mlioko Songea mnaweza kunipa taarifa zozote za watu kama Ramadhani Alidina, Ahmed Daimu, Rashid Kauza, Petro Markusi, Hassan Fakiri, Misheck John, Edmund na kaka yake Timothy, Daawa Rabii, Mfaume Abdurabi, Fatuma Abdurabi, Mansard Ramadhani na nk. Wote hawa watakuwa watu wazima sasa hivi. bila shaka inawezekana hata watoto wao wako humu!

Baadhi ya vijana niliowataja hapa waliwakilisha mkoa wa Ruvuma kwenye michezo wa shule za msingi Ummishumta ambayo mwaka huo 1974 yalifanyika Singida. ninakumbuka baada ya kurejea kwenye michezo hiyo tajiri mmoja wakati huo akiitwa Mzee Matimila wakati huo akimiliki guest house mitaa ya Mfaranyaki aliwakusanya na vijana wengine wa mitaa hiyo na kuunda timu ya MWANGAZA SC ambayo baadae ndio ilikuwa chumbuko la timu iliyokuja kuwika ya Majimaji. Mwangaza ilikuwa ni jina la moja ya Guest house zake pale karibu na Uwanja wa Majimaji wakati huo ukiwa umezibwa tu na Matete!

Nilikuwa nikiishi na wazazi kulikokuwa kukiitwa Uzunguni mtaa wa Mpambalyoto mbele kidogo ya ofisi za iliyokuwa Posta na Simu na Gereza Kuu la Songea kwa wakti huo. sijui kama ndivyo ilivyo hadi sasa maana sijarejea tena huko tokea niondoke mwaka 1974!
Nakumbuka mikate ilikuwa kwa Booking pale Angoni Arms njia ya kwenda Matogoro ambako ndio ilikuwa sehemu ya wazito wa mji kustarehe mwishoni mwa wiki.

Nakumbuka miaka ile kutokana na hali ilivyokuwa, wanafunzi wote wa darasa la Saba wa shule za pale mjini ilikuwa ni lazima kwenda mafunzo ya mgambo kwa miezi mitatu kwenye kambi a jeshi iliyo pale karibu na makao makuu ya mkoa. Ah, Those were the days. Songea ilikuwa ya Amani kweli potelea mbali kwamba barabara ya Lami ilikuwa moja tu kutoka juu kule Regional Block hadi chini kuleee....njia ya kwenda Uwanja wa Ndege kwa wakati huo...!!!

Mimi ni Tanga-line lakini ninai-Miss sana Songea na moja ya ndoto zangu kubwa ni kurejea huko kuona mabadiliko ya tokea wakati huo!! Nitashukuru mno kama kuna mtu ataweza kutupia humu japo picha mbili tatu za eneo lolote la mji wa Songea hasa Shule ya Msingi ya Mfaranyaki ilivyo sasa.
 
Kumbe tavangoni tiyi tamahele apu ndayaki tibela kuunda umoja wa Wangoni JF?

Basi tijiyandikishai apa, ndo timanyai tivi ta valinga, ne ni wanza na vangi mbwelayi...

1.Ogah....nihuma ku Mfaranyaki
 
napakumbuka sana pale bombambili standi kwa wahuni.
 
Back
Top Bottom