Songea yetu, karibuni mji uliobarikiwa

Songea yetu, karibuni mji uliobarikiwa

mji ambao ukiwa na not ya sh.10000 ukaenda sokoni kununua kitu, change itatafutwa saa nzima. yaani ukiwa na sh.elfu kumi wewe ndio tajiri. ukienda kusalimia wazee lazima uende na sukari usipobeba sukari ww huna maana tena utasikia wakilalamika "yaani anakuja bila hata kilo ya sukari, amekuja kufanya nini sasa" yaani kule kwetu sukari ni anasa.
Hapo kwenye kutafuta change ya elfu 10 saa nzima mh...!
Kuna walakini...
 
hakuna wajanja km watu wa songea. Dar wajinga wengi
 
hayo
nayatambua,kuwa waganga wengi wanatoka ktk hyo miji unayoizungumzia,ila
kwa sasa tunaizungumzia songea,kwani ishu ya matuta makubwa ya
barabarani yanayoongoza duniani ina uhakika kwa asilimia ngapi?HAPA
TUNAIZUNGUMZIA SONGEA,NA REFFERENCE ZOTE ZTOKE HUKO,SIO NIGERIA. Ngalikihinja
Matuta yanazidi yale ya barabara ya Mirambo huku Dar au yale ya barabara ya kwa bibi Nyau kule kwa mtogole... ?? Sana Huko Songea matuta ni pale Bombambili na shule ya msingi misufini basiii...
 
dombi ehh sidombi tena eh dombi sidombi tena! Kimolo, makambi, matogolo huko enzi hizo ikishafika jioni saa moja usiku miaka ile no TV tunajimwaga kwenye kambindi Fruit hujaitaja hii ngoma ni tamu ajabu. Vijana mnakusanyika hapo mnacheza wee. Mkuu Fruit Songea tamu ajabu hufi njaa kuna embe maji, embe bolibo embe sindano kila baada ya mita ishirini.

Viazi jeshi aka majeko kila shamba utakaloliona, ndizi katuli kila genge, mboga za majani za kumwaga. Ndugu yangu Fruit kuna samaki toka ziwa Nyasa wanaitwa mbelele na mbasa uwii delicious kinoma. Hahaa Fruit umesahau mbulika penye apa! aka kumbikumbi bwana wewe ukifika msimu wake watu wanatafuna km karanga.

Kambi za jeshi nazo zinaleta utamu wake, chandamali na ile nyingine. Kuna wakati nimemaliza frm 6 nikarudi zangu matogolo kuna jamaa nilisoma nao primary wapo chandamali pale kwa vile napiga ball km dinho jamaa akaja home kunichukua nikachezee timu yao, we bwana wa jeda noma afande alipigwa kanzu na kuvuliwa hajakaa sawa tobo raia si wakashangilia kwa nguvu, afande akachukua madaraka yake akasimamisha mazoezi akampa adhabu private Mbuzi ya kichurachura na lindo la siku 5. Kweli sikurudi tena chandamali jeshini nikahamia ttc matogoro.
 
Songea karibu kila nyumba uwani wanafuga mkuu wa meza aka kitimoto! Songea ni tajiri kwa madini kuna wakati mtu alikuwa anafua akaokota kipande kidogo cha gold pale chini ya daraja mto matalawe, raia nusura wachimbue daraja lote, bombambili nako nyumba ya mtu ilitaka kwenda! Songea i miss you mamaland
 
Ha ha haaa!nimesoma comment za wana JF wote nimecheka sana.binafsi nimeishi songea,watu wengi ni wachawi,hawataki kufanya kazi na ukijaribu jambo la maendeleo basi bundi wote wanahamia nyumbani kwako.

Mademu wa huko ni wepesi sana kutongozwa kazi hawafanyi muda wote ni kujiremba na jioni kwenda kutafuta 'mabuzi' kwa wale wafanyabiashara watakubaliana na mimi kuwa watu wa songea wengi wana tabia za kukopa chochote iwe dukani,bar, sokoni,buchani na ulipaji wake ni 20%.

Ukienda kwenye bar huwezi kunywa bia moja ikaisha bila ya aliekaa jirani yako hajakuomba bia,ukimnyima visa.ukiacha hayo wenyeji wa songea ni wakarimu ukiwatembelea hutoki bila kula ugali! Kwa upande wa kiuchumi mzunguko wa pesa ni mdogo sana kwani kama mdau mmoja alivyosema hapo juu hakuna kiwanda hata kimoja kinachoto ajiza za uhakika ukiacha viwanda vidogovidogo kama SIDO.

Mzunguko wa pesa unategemea sana sana wageni,makampuni yanayojenga barabara,madiniyanayochimbwa huko msumbiji na pindi wakulima wakivuna mazao yao kuanzia mwezi may. Nawapa hi wazee wote wa mtini pub,kalali pub,delux one&two.
 
Songea ndio kwenyewe bhana mji una hali ya hewa nzuri kabisa.......haina haja ya madala dala kwenda mahali ni kwa mguu tu unafika bila jasho fresh kabisa nipo MOONLIGHT,KATIKATI YA BOMBA MBILI NA MSAMALA KARIBUNI
 
Songea karibu kila nyumba uwani wanafuga mkuu wa meza aka kitimoto! Songea ni tajiri kwa madini kuna wakati mtu alikuwa anafua akaokota kipande kidogo cha gold pale chini ya daraja mto matalawe, raia nusura wachimbue daraja lote, bombambili nako nyumba ya mtu ilitaka kwenda! Songea i miss you mamaland
Bana, hapo pa kufuga kuku uwani hapana... Mi pale Lizaboni wala hatufugi kuku uwani....
 
Chimunguru yaani mkuu nimekusoma vilivyo we inaelekea ni wa miaka ya 198.... maana hiyo mechezo ya dombi dombi mmmh! nakumbuka sana hasa nikiwa shule ya msingi Majimaji
 
Last edited by a moderator:
Fruit Kama ulikwepo mkuu! Ila kuna huyo memba anadai songea kuna wahavi sana yaani wachawi ni muongo km uchawi upo tz yote! Wala tusichafuane kule sumbawanga kunakopiga radi mchana hakun mvua je, acha majungu mwana jf
 
Last edited by a moderator:
kelao Mkuu veve u mdesi(kwa kihehe uwongo) Songea gani hiyo? Uchawi kila sehemu ukienda utapewa story za wanga so usiseme uwongo
 
Last edited by a moderator:
Fruit ukosiwi mbelele na mbasa na ugali wa mayau au wachimela
 
Last edited by a moderator:
Mleta mada,upo maeneo gani saa hizi? Lizaboni,Matarawe,Ruvuma,Mahenge,Manzese,Msamala au Mfaranyaki?
Au upo Peramiho,Namabengo,Hanga,Matimira au Chipole...?

Huyu yuko Nanguruwe na anaelekea Nakapanya........
 
Wakazi wake wengi wanaendekeza ushirikina na majungu. Kazi kudanganywa tu na kina Nchimbi. Eti nao wanajifanya kulalamika kwa kupandishiwa nauli wakati hata sukari inauzwa bei ya anasa tu.Wameletewa vyuo lakini hawataki kusoma kubwa kupiga ramli tu maeneo ya Ruvuma huko na Namabengo kwa binti Ndembo.

....kwani Binti Ndembo anamzidi Kalembwani?...chezea Ruvuma nyie....
 
Back
Top Bottom