Songea yetu, karibuni mji uliobarikiwa

Songea yetu, karibuni mji uliobarikiwa

Fruit

Senior Member
Joined
Jan 1, 2013
Posts
193
Reaction score
54
Karibuni Songea Mji wa kitalii:

1. Kuna matuta makubwa ya barabarani Tanzania nzima (bumps) yapo bombambili ambapo kabla ya
kufika Songea mjini lazima ukutane nayo.

2. Kuna pikipiki nyingi kuliko watu.

3. Kuna matunda mengi ya kipekee kama madonga, masuku, mfudu, mbula, mamvubula na mengine mengi.

4. Kuna mboga nyingi za kipekee kama Mangaukau, linamfusulela, chikandi, likungu, kipele,
mangatungu n.k.

5. Majina mengi ya watu wake ni ya wanyama mfano Komba, Mapunda, Mbawala, Tembo,
simba (Kahimba), Nungu, Nyoka, Matembo, Ngonyani, Nyati, Kobe n.k.

6. Pia kuna ngoma nyingi mf. Madogoli, beta, zilanga, ligambusa, kihoda, mganda, lindeku,
Mandilo, Chomanga, Tumba, Puyanga.

7. Bila kusahau Dagaa watamu sana (Nyasa) na viazi vitamu kuliko vyote vinavyojulikana kwa jina
la makaba.

Hiyo ndiyo SONGEA yetu, Mji uliobarikiwa, Chezea Songea yetu weye.
 
......lakini pia ni wilaya pekee iliyopakana na Mkoa wa Morogoro lakini tokea uhuru hakuna barabara ya kuunganisha Ruvuma (Songea) na Morogoro japo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma (Said Mwambungu) ni mwenyeje wa Mkoa wa Morogoro hususani Kijiji cha Misegesi (Malinyi) ambapo daraja la kuunganisha mikoa hiyo limekwisha jengwa.
 
SONGEA mji uco nakiwanda hata kimoja,mahindi,tumbaku,korosho,kahawa,mazao yasiyoleta tija kwawananch wa mkoa wa RUVUMA
 
mji ambao wakazi wake hawapo aware kabisa na haki zao za msingi. wanaamini uongo kuliko ukweli...
 
Mji ambao unaongoza kwa kuhongwa na wana ccm siku za uchaguzi buku 2,5 ,kanga,vilemba,t,shirt na kofia halafu wa kwanza kulalamika kama serikali haiwajali
 
Mleta mada,upo maeneo gani saa hizi? Lizaboni,Matarawe,Ruvuma,Mahenge,Manzese,Msamala au Mfaranyaki?
Au upo Peramiho,Namabengo,Hanga,Matimira au Chipole...?
 
Wakazi wake wengi wanaendekeza ushirikina na majungu. Kazi kudanganywa tu na kina Nchimbi. Eti nao wanajifanya kulalamika kwa kupandishiwa nauli wakati hata sukari inauzwa bei ya anasa tu.Wameletewa vyuo lakini hawataki kusoma kubwa kupiga ramli tu maeneo ya Ruvuma huko na Namabengo kwa binti Ndembo.
 
lakini pia ni mji unaoamini zaidi ktk ushirikina...(binti ndembo)akiwa ni mganga wao maarufu huko namabengo.
 
Wakazi wake wengi wanaendekeza ushirikina na majungu. Kazi kudanganywa tu na kina Nchimbi. Eti nao wanajifanya kulalamika kwa kupandishiwa nauli wakati hata sukari inauzwa bei ya anasa tu.Wameletewa vyuo lakini hawataki kusoma kubwa kupiga ramli tu maeneo ya Ruvuma huko na Namabengo kwa binti Ndembo.

Hakika Mkuu, hata geshi la polishi likitaka kukamata wahalifu lazima liwasiliane na BintiNdembi!
 
Mleta mada,upo maeneo gani saa hizi? Lizaboni,Matarawe,Ruvuma,Mahenge,Manzese,Msamala au Mfaranyaki?
Au upo Peramiho,Namabengo,Hanga,Matimira au Chipole...?
Nahisi atakuwa Litapwasi
 
lakini pia ni mji unaoamini zaidi ktk ushirikina...(binti ndembo)akiwa ni mganga wao maarufu huko namabengo.
Ukitaka kujuwa wapi kuna ushirikina sana angalia matangazo ya waganga wa jadi, utawasikia mganga toka Tanga, Sumbawanga, Naijeria, Tabora etc etc
 
hayo
nayatambua,kuwa waganga wengi wanatoka ktk hyo miji unayoizungumzia,ila
kwa sasa tunaizungumzia songea,kwani ishu ya matuta makubwa ya
barabarani yanayoongoza duniani ina uhakika kwa asilimia ngapi?HAPA
TUNAIZUNGUMZIA SONGEA,NA REFFERENCE ZOTE ZTOKE HUKO,SIO NIGERIA. Ngalikihinja
 
Last edited by a moderator:
mji ambao ukiwa na not ya sh.10000 ukaenda sokoni kununua kitu, change itatafutwa saa nzima. yaani ukiwa na sh.elfu kumi wewe ndio tajiri. ukienda kusalimia wazee lazima uende na sukari usipobeba sukari ww huna maana tena utasikia wakilalamika "yaani anakuja bila hata kilo ya sukari, amekuja kufanya nini sasa" yaani kule kwetu sukari ni anasa.
 
Kinachonikera Songea ni Wanasongea kutokuwa waelewa yaani kofia tu ya njano basi. Halafu mashabiki wa CCM wooote choka Mambo mengine acha wafanye
 
Watu bana, wao wanajua kubeza tu, mara ooh washirikina oohh sijui mji usiokuw na kiwanda hata kimoja, mara sijui nini! na wengi wanaponda kwa kusikia story za kwenye kahawa, hata kufika hawajahi!! inamaana hakuna mambo mazur huko?
 
Yaani wana JF mlio comment hapo juu kama ni watu wa songea au mmesikia tu kijiweni mmechemsha, mimi kwa sasa nipo mjini (DSM) nilikuwa huko likizo tena maeneo ya Misufini yaani kama mmetoka huko miaka mingi iliyopita nawaomba mrudi mkakuangalie vizuri then mje muedit comment zenu.

Kuhusu chakula kwa taarifa tu songea ipo katika big 5 ya mikoa inayoongoza kwa kulima mahindi na maharage na mazao mengi yanayopelekwa mikoa mingine ya msaada yanatoka songea
(hata mwaka mmoja songea haijawahi kupelekewa chakula cha msaada na haitatokea) kuhusu suala la Binti Ndembo kweli yupo.

Lakini sidhani kama kuna mkoa ambao hauna waganga wa aina hiyo kwa hapa DAR wenyewe ni mashahidi, na kuhusu kofia na tisheti za rangi ya kijani na njano hivi ni wapi ambapo hakuna vitu kama hivyo, au mnaropoka tu, tatizo lenu story za vijiweni ndio zinawakomaza
.
 
Back
Top Bottom