Songea yetu, karibuni mji uliobarikiwa

Songea yetu, karibuni mji uliobarikiwa

Mleta mada,upo maeneo gani saa hizi? Lizaboni,Matarawe,Ruvuma,Mahenge,Manzese,Msamala au Mfaranyaki?
Au upo Peramiho,Namabengo,Hanga,Matimira au Chipole...?

Au Ngwinde,mpitimbi,litola,mandepwende,mgombasi,kitanda,mchomoro,ngemba mbili,mtonya au nandungutu...
 
mimi nipo ligera naelekea lusewa kwa mzee wangu wa siku nyingi Ali Chitenje. nikirudi nafikia mgombasi na mtimbati maji kula mandondo

Mkuu kuna kinjonga...bwana wewe!!..ukigonga hiyo hutoondoka namtumbo.
 
Posta na gereza bado zipo pale2......had mpambalyoto kuna rami siku hizi....karibu tena Songea uone mabadiliko

....Dah! Kweli Songea sasa kumeendelea! Huu mtaa wa Mpambalyoto si ndio unashuka chini na kwenda kukutana na mtaa wa Songea Girls? Nakumbuka hapo katikati palikuwa na nyumba kama tano hivi, mojawapo ikiwa ndio tuliyokuwa tukiishi!
 
Hali ya songea kimaendeleo na unafuu wa maisha ni bora zaidi ukilinganisha na miji mingi hapa nchini (ukiondoa miji ya dsm, mbeya, arusha, moro na mwanza).

Ishu ya tabia za wenyeji wa songea ni ya mtazamo binafsi wa mtu lakini navojua kila mkoa una watu wake na tabia zao.
 
daah umenikumbusha mbali sana..nimekumbuka Mayao..aka mihogo
 
Mji ambao nilibahatika kukutana na wachawi usiku na kuwaona kwa macho mara mbili tofauti, bila kufanyiwa dawa yoyote. Maeneo ya Hospitali ya Mji Mwema.
 
Back
Top Bottom