Ni kweli kwamba hakuna sharti sehemu yoyote linalosema kwamba ili kuwa mwanachama wa chama kingine, ni lazima urudishe kazi ya chama chako cha awali; Lakini tatizo linakuja pale inaposemekana kwamba Dr. Slaa ni mwanachama hai na amekuwa analipia ada ya kadi yake ya CCM wakati wote, Je hii ni taarifa sahihi? Iwapo sio sahihi na kwamba tu ana kadi ya CCM katika makabrasha yake, suala hili linakuzwa bila sababu kwani hakuna cha ajabu hapo, lakini iwapo ni kweli mbali y akuwa na kadi, pia analipia ada yake kila mwaka, hapa kuna tatizo - kwani ina maana Dr Slaa ni mwanachama hai wa vyama CCM na Chadema - kwani uhai wa uanachama unapimwa kwa kigezo cha malipo yako ya ada kila mwaka;
Swali linalofuatia ni je, mtu anaweza kuwa mwanachama wa vyama viwili? Kwa uelewa wangu, it is not illegal lakini kuna justifications to expel mhusika from one or both parties, ikigundulika kwamba anatumikia vyama vyote viwili; je kutumikia maana yake nini - kupiga kura, kuhudhuria vikao vya wanachama? kulipia ada ya uanachama? kuwa kiongozi kupitia chama husika? Vyote manne kwa pamoja? Sina uhakika, kwani yote haya yap open to debate; Lakini suala muhimu na la msingi hapa ni kwamba Dr. Slaa kwa hili ameyumba, hasa iwapo taarifa kwamba amekuwa analipia kadi yake miaka yote ni za kweli, kwani nje ya suala hili la kuwa mwanachama hai badala ya mfu, he can easily get away na sakata hili;