Somo la Katiba ya CCM kwa Nape & Co

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,919
19,627
Nichukue fursa hii kumfunza kijana Nape katiba ya chama kilichomlea tangu azaliwe na kinachomuweka mjini leo hii:

Bahati mbaya sana kwa ccm, siku ya kufa nyani miti yote huteleza,

CCM ipo HOI bin Taabani na inahitaji msaada wa hali na mali kuurejelea uzima.

Lakini nani wa kuleta tumaini la uhai wa ccm? Hili ndilo swali kuu walilojiuliza mwezi jana walipokutana pale Dodoma wahafidhina wa chama hiki mufilisi.
Ilikuwa ni kazi ngumu hasa kumpata msemaji wao kwani ilihitaji mtu makini na mwenye weledi si wa makengeza.

Hili linatokana na uwazi kuwa mtu huyo ndie atakuwa msemaji pia kwenye mitandao ya kijamii inayoaminika kuwa vijana wengi wazalendo na wasomi wa elimu za juu wameweka vituo vya ukombozi wa nchi yao dhidi ya mkoloni mweusi ccm kwenye mitandao hii.

Ajabu na nikweli, nafasi hiyo ilirejea kwa yuleyule ambae siku za nyuma alikimbia vita ya kisiasa mitandaoni na si mwingine ni NAPE NNAUYE

Kijana huyu aliye mjuvi wa siasa angavu ilihali anaombwe kichwani, amekuja na staili mpya ambayo inamfanya awe kituko mbele ya tuzijuazo siasa za kisasa na siasa za maji taka.

Kwa hoja na matamko yake anayo iwakilisha ccm, Niseme wazi Nape Haijui Katiba ya CCM.

Najiuliza huyu kweli kama haijui katiba ya Chama chake je, ataijua ILANI ya chama hicho? Je ataijua Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Nimeonelea busara nianze kwa kumfunza kitu kimoja kimoja, na nimeanza na vifungu vichache muhimu vya katiba ya CCM ambavyo ndivyo vilivyosababisha nitambue kuwa kijana huyu hajui chochote ndani ya chama chake, si katiba wala ilani za chama hicho.

Naaaam naanza hivi:


Soma Katiba ya CCM toleo la mwaka 2010. Ibara ya 13. kifungu (1).

Inahusu WANACHAMA NA VIONGOZI.

Uanachama utakwisha kwa:
(a) Kufariki.
(b) Kujiuzulu mwenyewe.
(c) Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(d) Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(e) Kutotimiza masharti ya uanachama.
(f) Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.
(2) Mwanachama ambaye uanachama wake unakwisha kwa sababu yoyote ile hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa.


Sasa nikufahamishe kuwa, Dr Slaa alijiunga na chama kingine cha siasa zaidi ya miaka 15 iliyopita (Nape ulikuwa hujamaliza hata darasa la saba)

Amekuwa mbunge wa kuchaguliwa kupitia chama kingine cha siasa (CHADEMA) kwa miongo kadhaa.

Leo hii Nape & co mnauliza kadi yake ya CCM?


1. Nape na wenzake mnaijua vema katiba ya CCM? wanaelewa masharti ya uanachama?

2. Ni kifungu gani cha katiba ya CCM kinachosema kuwa ili uanachama wa CCM ukome sharti mhusika arudishe kadi?

NB

Shukrani kwa FJM
 

nya2nya2

Senior Member
Apr 1, 2012
113
10
asikuumize kichwa kila mtu siku hizi anajua wameandaa utaratibu wakuropoka kila siku lengo tusahau shida zetu tujadili upuuzi usiokuwa na tija kwa taifa letu ,maisha bado magumu huku uswahilini ye anatuletea mambo yasiyokuwa na msingi wowote
 

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,919
19,627
asikuumize kichwa kila mtu siku hizi anajua wameandaa utaratibu wakuropoka kila siku lengo tusahau shida zetu tujadili upuuzi usiokuwa na tija kwa taifa letu ,maisha bado magumu huku uswahilini ye anatuletea mambo yasiyokuwa na msingi wowote

Inasikitsha sana, badala ya kuja hapa nakuwaambia watu kucha chama kimefanya hili na lile kuleta maendeleo yeye anakuja na ngonjera za kipupwe
 

Ditto

Member
Aug 30, 2010
56
41
Yericko Nyerere Well, hata mie nimesikitika sana kwa hili alilolianzisha ndugu yetu msemaji wa chama tawala.. Nahisi sasa chama tawala kinapoteza focus na kujiendesha kama chama cha upinzani.. Kuna mengi sana wananchi wanatamani kuyasikia kuhusu maendeleo kuliko hili suala la Dr. Slaa na kadi ya CCM.
 
Last edited by a moderator:

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,919
19,627
Yericko Nyerere Well, hata mie nimesikitika sana kwa hili alilolianzisha ndugu yetu msemaji wa chama tawala.. Nahisi sasa chama tawala kinapoteza focus na kujiendesha kama chama cha upinzani.. Kuna mengi sana wananchi wanatamani kuyasikia kuhusu maendeleo kuliko hili suala la Dr. Slaa na kadi ya CCM.

Huyu ndie msemaji wa chama, chama kimempa dhamana ya kukihubiria mbele ya uso wa watanzani, lakini naamini chama kililenga ahubiri sera na mafanikio ya chama katika kuwaletea maendeleo watanzania!

Sijui hiyo kadi ikirudi itawasadieje watanzania na wana ccm?
 
Last edited by a moderator:

Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,553
2,330
Hivi hizi hoja zipo sawa?
1) Bwana Nyerere ana kadi ya TLP
2) Bwana Nyerere ni mwanachama wa TLP

Nadhani umekimbia hadi umepitiliza kwenu.
 

bluetooth

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
4,403
2,520
Hivi hizi hoja zipo sawa?
1) Bwana Nyerere ana kadi ya TLP
2) Bwana Nyerere ni mwanachama wa TLP

Nadhani umekimbia hadi umepitiliza kwenu.

wewe kilaza .... kuna watu wanazo toilet paper nyumbani lakini wanatumia maji kujitawaza ....

think ... think again ... think more and more
 

sifongo

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,896
5,295
Mkuu Yericko sio kwamba Nape hajui hayo uliyoandika hapo, anajua sana ila ataongea nini ambacho hajaongea huko nyuma? wanachofanya CCM ya sasa ni kutafuta utumbo wowote ule waumwage mtaani waungwani mshangae, mhoji, magazaeti yaandike ionekane CCM mpya inafanya kazi, kumbe waongee nini zaidi ya uzushi?

Wameshindwa kujibu hoja za msingi wanarukia vitu sio vya msingi

CCM kimechoka, niliwahi kuandika humu jf kama CCM ingekuwa timu ya mpira basi wachezaji wake wote ni majeruhi na wengine wana kadi nyekundu, kwa ufupi CCM ya sasa haina first eleven, sasa kumbe wafanyeje na dakika zinayoyoma? lazima wabutue bora liende mbele mpira uishe, wenyewe wanaamini refa (tume ya uchaguzi) ni wao atawapendelea 2015, kosa kubwa.

Umefanya vyema kutuelimisha kwa maandiko yako binafsi sikuwa nayafahamu hayo.
 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
15,159
19,149
yericko hilo swali la katiba nape hawezi kulijibu sababu hajui!!!yeye ni mwanachama wa ccj,katiba ya ccm wapi na wapi?
 

Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,553
2,330
wewe kilaza .... kuna watu wanazo toilet paper nyumbani lakini wanatumia maji kujitawaza ....

think ... think again ... think more and more

Hilo ndilo jibu analostahili kujibiwa Yericko, hicho kipande cha katiba alichokinukuu hakina kabisa uhusiano na kuwa au kutokuwa na kadi. Kinaongelea uanachama, hiii ni hoja tofauti kabisa na kuwa mwanachama au la, na iwapo Nape alisema Dr bado ni mwanachama anastahili hilo darasa lakini kama aliongelea kadi kitu ambacho hata Dr mwenye amekili, basi Yericko ndiye anapaswa kujifundisha kiswahili upya.
 

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,478
Wanabodi,
Kuna msemo unaosema kuwa, ukijibishana na kichaa na wewe unakuwa ni kichaa. Kwa maana nyingine, ukijibishana na "mpiga porojo" na wewe unakuwa ni "mpiga porojo".


Kwa viongozi wa CHADEMA kama wanavyopenda wananchi waamini, Nape Nnauye ni "mpiga porojo" lakini katika "porojo hizo", wanatumia nguvu kubwa katika kuzijibu. Kwa sisi tunaoangalia kwa mbali tunaachwa na maswali mengi yasiyokuwa na majibu zaidi ya kurudi kwenye usemi wa mwanzo na kuwa na hitimisho kuwa basi hata viongozi wa CHADEMA nao ni "wapiga porojo" (manzi ga nyanza) na kama sivyo, basi inawezekana maneno ya Nape Nnauye yakawa yamebeba ukweli ndani yake mpaka kufikia kujibiwa kwa nguvu na viongozi wengi wa chama kinachotaka watu wakiamini kama ni makini katika utendaji wake (damage limitation).

Watanzania kwa sasa hatuutumikishi ubongo wetu katika kujenga hoja na maswali magumu na kuyatafutia majibu na suruhisho mbadala badala yake tunaridhika kuwa kwenye "comfort zone" za kimaskini katika mawazo na fikra kuimba nyimbo zilezile ambazo wanasiasa wanaziimba.

Ndiyo maana hata wanasiasa wetu wako kwenye "comfort zone" za kimaskini katika mawazo na fikra. Kwa mawazo haya, Siyo kitu cha kushangaza pale wanasiasa wa vyama vyetu vikuu nchini wanapoanza kujadili kwa wiki nzima achilia mbali sekunde tano kuhusu kadi ya chama ( unayo, sina, mwanachama, siyo mwanachama ). Silly politics.

Nchi inahitaji jamii yenye mawazo na fikra pevu katika kupambana na changamoto za karne ya 21 na hii itatokea kama Wananchi wataondokana na hizi siasa za matukio na mufilisi.

Kama hivyo vyote vipo, basi siasa za Tanzania zina kansa ambayo inatakiwa "amputation" ndani ya fikra za wananchi kwa sababu nchi haiwezi kujengwa kwa porojo za kisiasa kama hizi bali kwa fikra malidhawa na zenye maono ya kukabiliana na changamoto za karne hii ya sayansi na tekinologia.
 

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,395
Katika matatizo makubwa tulionayo kwa VIONGOZI wa NCHI hii ni kuzisoma na kuzielewa KATIBA za vyama vyao na katiba ya JMT. Sijui ni kwa vile wanaapishwa kwa kutumia MISAHAFU?! Yericko mhurumie Nape bure. Yeye sio kada wa CCM. Ameanza SIASA wakati vyuo vyote vya makada wa CCM vimeshafungwa na kufa. Nimesikia wamempa kazi Wilson Mukama kuanzisha chuo kingine cha aina ile ya chuo cha CCM Kivukoni, Hombolo, Murutunguru,.... Nape awe wa kwanza kuhudhuria mafunzo haya. Akitoka huko apelekwe JKT. Sidhani kama alipitia huko.
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,655
938
Leo hii Nape & co mnauliza kadi yake ya CCM?


1. Nape na wenzake mnaijua vema katiba ya CCM? wanaelewa masharti ya uanachama?

2. Ni kifungu gani cha katiba ya CCM kinachosema kuwa ili uanachama wa CCM ukome sharti mhusika arudishe kadi?

NB

Shukrani kwa FJM


- Huwezi kumtumikia Mungu huku umemficha Shetani nyumbani uvunguni mwa kitanda chako, unatakiwa kumchukia shetiani kwa akili zako zote na uwezo wako wote, Slaa anapopewa kadi za wasioitaka CCM na huku yeye binafsi anajua anayo vipi akili au nafsi yake haimsuti?

- I mean kama Slaa ana kadi ya CCM airudshe now, kuendelea kuwa nayo ni dalili kwamba ahana uhakika na anachokifanya huko kwenu, hawezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja!! mbona ni simple common sense tu!

Es!
 

Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,659
2,233
Tuwashangae waandishi wa habari ambao waliona hii kuwa habari kwa sababu imenenwa na Nape. Ikumbukwe kuwa Slaa hajaweka kufanya ni Siri yeye kuwa na kadi ya CCM. Hata wakati wa kampeni 2010 aliweka wazi na kusisitiza kuwa mtu si lazima kurejesha kadi ya Chama kukoma kuwa mwanachama. Katiba za vyama vingi vya siasa haviweki hili Kama sharti. Waandishi wa habari walipaswa kumkumbusha/kumuuliza hili alipolitoa.
 

Limbani

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
1,439
440
- Huwezi kumtumikia Mungu huku umemficha Shetani nyumbani uvunguni mwa kitanda chako, unatakiwa kumchukia shetiani kwa akili zako zote na uwezo wako wote, Slaa anapopewa kadi za wasioitaka CCM na huku yeye binafsi anajua anayo vipi akili au nafsi yake haimsuti?

- I mean kama Slaa ana kadi ya CCM airudshe now, kuendelea kuwa nayo ni dalili kwamba ahana uhakika na anachokifanya huko kwenu, hawezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja!! mbona ni simple common sense tu!

Es!

Ile kadi ni karatasi (document) ya kuonesha alama ya kuwa yeye ni Mwanachama wa CCM. Lakini pia Yericko Nyerere amekuwekea masharti ya ukomo wa uanachama kulingana na Katiba ya CCM zikiwemo KUTOLIPIA kadi yako ya uanachama na KUJIUNGA na chama kingine cha siasa kitu ambacho Dr Slaa amefanya hivyo. Kulingana na katiba ya CCM, Nape, Dr Slaa, wewe mwenyewe Malecella na hata Wassira si wanachama wa CCM maana mlishajiunga na vyama vingine!!
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,655
938
Ile kadi ni karatasi (document) ya kuonesha alama ya kuwa yeye ni Mwanachama wa CCM. Lakini pia Yericko Nyerere amekuwekea masharti ya ukomo wa uanachama kulingana na Katiba ya CCM zikiwemo KUTOLIPIA kadi yako ya uanachama na KUJIUNGA na chama kingine cha siasa kitu ambacho Dr Slaa amefanya hivyo. Kulingana na katiba ya CCM, Nape, Dr Slaa, wewe mwenyewe Malecella na hata Wassira si wanachama wa CCM maana mlishajiunga na vyama vingine!!

- Hoja ni batili cause mimi sio Malecella, sorry! ha! ha! ha! halafu next time kabla hujarusha majina ya watu wasiokuwepo kwa nini suitaje lako kwanza? ha! ha! ha! si nilisema hoja zinzwapa taabu sana bila matusi na kurusha rusha majina ya watu hamuwezi kujadili anything chellenging, mkishakuwa challenged mnaanza kurusha rusha majina ya watu vipi bro simamia hoja hapa! ha! ha1

- Hoja yangu ni kwamba huwezi kumtumikia shetani na Mungu kwa wakati mmoja, so Slaa kama anayo kadi kama dalili zote zinavyoonyesha arudishe kadi, wala hakuhitaji mjdala on that ni waste of time!!

Es!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

20 Reactions
Reply
Top Bottom