Somo la Katiba ya CCM kwa Nape & Co

Mkuu hizo ni prpaganda uchwara ndiyo maana jambo la maana kama kuikwa kwa katiba ya CCM hakuna hata mwana CCM yeyote anayehoji. Hakuna asiyejua kuwa wanaousema ni uongo, na mbinu wanazodhani wataidhoofisha CDM. Watanzania wa leo sio wa jana, CCM watatumia pesa nyingi kuwatumia vijana ndani ya CDM kuendeleza ajenda hii lakini hatudanganyiki.
 
Inawezekana Nape hajui hata katiba ya chama chake inasemaje! Niwa kuonewa huruma yule kijana maana anayofanya ni aibu kwa vijana wenzake.

Hivi?
1. Dr slaa alipo wataja mafisadi wa list of shame pale mwembe yanga ambao wengi ni viongozi waandamizi wa ccm alikuwa akisema kama mwana ccm au chadema?

2. Hoja zilizoibua mambo mazito bungeni kuhusu ufisadi hadi wakaamua kumuwekea mtego wa vinasa sauti chini ya kitanda ina maana walikuwa wanataka kumuuwa mwana ccm mwenzao?

3. Walihangaika nini kuchakachua kura za uraisi ambazo hadi leo mpaka tume inagwaya kuweka kwenye tovuti kama Dr Slaa ni mwana ccm mwenzao?

Lakini kubwa linalo acha midomo wazi ni ibara ya 13(1) ya katiba ya ccm ya mwaka 2010. Inasema hivi... Uanachama wa mtu katika ccm unakwisha kutokana na sababu moja wapo kati ya sababu zifuatazo:
kufariki, kujiuzulu,kuachishwa kwa mujibu wa katiba, kufukuzwa kwa mujibu wa katiba, kutotimiza masharti ya katiba au kujiunga na chama chochote cha siasa.

Tujiulize.
1. Je, kwa kipindi cha miaka 15 ambacho Dr Slaa amekuwa mbunge wa chadema hakuvunja moja ya masharti ya ibara hiyo hapo juu?
2.Je, Dr Slaa ameshawahi kuomba upya uwanachama mara baada ya kuachia kugombea ubunge na kuchakachuliwa kura zake za uraisi?
3. Je, ada ya uwanachama wa ccm inaweza kulipwa na mtu ambaye si mwanachama wa ccm?

Hitimisho.
Unahitaji kuwa na akili za maiti kukubaliana na hoja za Nape juu ya umiliki wa kadi ya ccm wakati kimantiki na kisheria mtu anapo nunua kadi inakuwa mali yake na si mali ya chama kama jinsi zilivyo kadi za kibenk (kadi ya benki ni mali ya bank). Ukimiliki kadi ya chama na baadae kuamua kujiunga na chama kingine una hiari ya kuichana kadi uliyonunua kwa pesa zako, kuihifadhi, au hata kuichoma.

Vijana wenye mawazo aina ya Nape ambao hawawazi wala kufikiria mkwamo wa nchi yetu kwenye kila sekta na kuwaza vitu vidogo kama kadi nachelea kusema wana ukame wa fikra na kiangazi cha maono.

Kwa nini?
1. Amesha tuambia kuwa Dr Slaa ana kadi ya ccm, fine. Je ndio pesa zetu zitarudi kutoka Uswis?
2. Tumeshajua kuwa Dr Slaa ana kadi ya ccm, je wale vinara wa ufisadi alio wataja pale mwembeyanga ndio watashughulikiwa au wataachwe waendelee kudunda huku wezi wa kuku na vibaka wakiuwawa?
3. Dr slaa kama katibu wa chadema tumeshajua kuwa ana kadi mfu ya ccm, je, ndio kampuni ya katibu wa ccm iliyokamatwa na meno ya tembo kule china itataifishwa na yeye kuamriwa ajiuzulu?

Kama haya hayawezekani basi Nape ni mwenda wazimu na ni aibu kwa vijana wa rika lake.

NB. Uwendawazimu ni kutojua unazungumza nini kwa kina nani na wakati gani, na useme nini, kinacho gusa nini.
 
Ukiona Nape ambaye ni ***** na Mchumi (Mzinzi wa wake za watu) mkali duniani wakipokea maelezo ya ujenzi wa barabara pasipo na utaalamu basi hapo unaona kuna tatizo. Sijui hata neno VISCOSITY wanafahamu ni kitu gani kwenye ujenzi wa barabara.

Yale yale ya AFANDE ninaumwa Photosynthesis......

6.JPG
 
Sikonge,umenifurahisha sana uliposema nape mzinzi,hebu walingenishe kwanza na mzinzi mwenzie padri slaa alafu nipe jibu nani zaidi.
 
Tanzania ya mwaka 1980s c ya leo NAPE,unaleta uanalog kwenye digital, unaleta misifa wait za day come TIME FOR REVOLUTION choshwa na magamba.
 
Hahahahahaha Hili la Slaa nadhani limewashika pabaya, mnatafuta kila njia ya kutokea! RIP CHADEMA! Laana ya ubaguzi dhidi ya vyama vingine kuviita CCM B haiwezi kuwaacha!
mkuu hili linakula zaidi kwa magamba,unaongozaje chama bila kufuata katiba? Lakini pia ni kweli mkuu kuna ccm B,we huifahamu? Si wazee wa Uamsho?
 
Ukiona Nape ambaye ni ***** na Mchumi (Mzinzi wa wake za watu) mkali duniani wakipokea maelezo ya ujenzi wa barabara pasipo na utaalamu basi hapo unaona kuna tatizo. Sijui hata neno VISCOSITY wanafahamu ni kitu gani kwenye ujenzi wa barabara.

Yale yale ya AFANDE ninaumwa Photosynthesis......

6.JPG
mkuu hapo kwenye uzinzi umenifurahisha mkuu, nasikia aliwahi kugongana na mhindi koko kwa girl!
 
Nape inabidi aachie ngazi,maana mwenyewe anamiliki kadi ya ccj na ccm. Amevunja makusudi katiba ya chama chake. Lakini ccm kuvunja katiba ndo zao hizo!
 
du hata sielewi nani mkubwa kati ya mwenyekit wa ccm mkoa na mkuu wa wilaya maanake kuna mahali mkuu wa wilaya anasema hapa ni bara barani hapafai kuwa soko,,,,,,,pana weka fence lakini anakuja mkiti mkoa anasema ngoa fence
 
Sikonge,umenifurahisha sana uliposema nape mzinzi,hebu walingenishe kwanza na mzinzi mwenzie padri slaa alafu nipe jibu nani zaidi.

Dr. hawezi kurudisha kadi maana anajua hatima ya cdm si mbali harafu atatangaza kurudi katika chama makini-CCM
 
Ni jambo linalosikitisha sana kuona chama kikongwe kama hiki kukosa kumbukumbu sahihi za kiutendaji, ni hii ndo kansa iliyokuwa kwa kasi katika hadi kwenye asasi za kiserikali, ni vigumu sana kuamini ila huu ndo ukweli,

Kumekuwepo na uvumi mwingi sana kuwa Dr Slaa anamiliki kadi ya ccm, lakini mimi hapa nina maswali mengi sana kwa KATIBU MWENEZI bwana Nape Nnauye,

1. Naomba utoke uueleze uma, je Dr Slaa aliajiuzulu uanachama wa ccm mwaka gani?
2. Ni kifungu kipi au utaratibu upi ulio rasimi unaotumika kuhusu kadi iwapo mwanachama anaamua kuasi chama chake
3.Je ni lini Dr Slaa kalipIa ada ya uanachama kwa mara ya mwisho?au hakuna ada ya uanachama?
4.Je mtu anahesabika si mwanachama baada ya kushindwa kulipa ada ya uanachama wake baada ya muda gani?

Ukinijibu hapa nadhani tutakuwa na mjadala mzuri wenye tija kwa taifa juu ya PROPAGANDA zinazoonezwa na watu wenye hila na fitina kwa vyama vya upinzani! najua hiyo ndo siasa ila lazima siasa ilenge ukweli na si kupotosha uma.
 
- Wewe badala ya kumuuliza Slaa kama ni kweli anailipia kadi yake ya CCM kila mwezi maana so far ahajajibu hilo, la kwamba ana kadi ya CCM Slaa amekubali kwamba ni kweli sasa anatakiwa akanushe kuwa hajalipia kadi yake ya CCM awekewe ushahidi wa risiti zake hapa, hivi kwa nini mnamuogopa sana Slaa nyie Chadema?

Yaaani uko radhi umuulize Nape hizi nonsense, kuliko kumuuliza Slaa kama analipia kadi yake ya CCM which he does!!

Es!!
 
Wananchi watanzania wengi tunahitaji mabadiliko, hatuhitaji propaganda zisizokuwa na msingi nape pamoja na wewe wote hamuijui katiba ya chama cha mapinduzi sasa soma hapa.
13. (1) Uanachama wa mwanachama
utakwisha kwa:-
(a) Kufariki.
(b) Kujiuzulu mwenyewe.
(c) Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(d) Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(e) Kutotimiza masharti ya uanachama.
(f) Kujiunga na kingine chochote cha siasa
 
Wananchi watanzania wengi tunahitaji mabadiliko, hatuhitaji propaganda zisizokuwa na msingi nape pamoja na wewe wote hamuijui katiba ya chama cha mapinduzi sasa soma hapa.
13. (1) Uanachama wa mwanachama
utakwisha kwa:-
(a) Kufariki.
(b) Kujiuzulu mwenyewe.
(c) Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(d) Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(e) Kutotimiza masharti ya uanachama.
(f) Kujiunga na kingine chochote cha siasa........

Hainiingii akilini kujadili propaganda za kitoto kama hizi badala ya kufanya mambo yenye tija kwa taifa. Nani asiyefahamu Dr. ni mwanachama wa CHADEMA.

Hilo halitoshi kuweka wazi kwamba amekosa kwa 100% hadhi ya kuwa mwanachama wa CCM? Je, ina mantiki gani CCM kuanza kumfuata Dr. Slaa? Wana upungufu wa wanachama? Mbona mitaani wako watu wengi hawana vyama, si wawafuate kuwashawishi wajiunge nao?
 
Hainiingii akilini kujadili propaganda za kitoto kama hizi badala ya kufanya mambo yenye tija kwa taifa. Nani asiyefahamu Dr. ni mwanachama wa CHADEMA. Hilo halitoshi kuweka wazi kwamba amekosa kwa 100% hadhi ya kuwa mwanachama wa CCM? Je, ina mantiki gani CCM kuanza kumfuata Dr. Slaa? Wana upungufu wa wanachama? Mbona mitaani wako watu wengi hawana vyama, si wawafuate kuwashawishi wajiunge nao?........

Huo ni mpango wao ndugu,coz wametambua (kimakosa) kuwa Dr.Slaa ndo hasa mwiba kwao nA tena wanaamini(kimakosa) ya kuwa CDM bila Slaa haiwezi kusimama.

Wanasahau ya kuwa CDM ina watu makini wengi tena wenye uwezo mkubwa huenda kumzidi Slaa, hivyo wakaamua waje na mbinu hiyo ya kipuuzi wakiamini wataweza kuisambaratisha CDM, kama mbavyo wamekuwa wakitamba ya kuwa haitafika 2015.

Kwangu mimi chama tawala kubuni mbinu za kipuuzi namna hii,inanifanya sasa niamini kuwa tunaongozwa na watu wa hovyo, wenye uelewa finyu wa mambo ambao mwisho wa siku wanakuja na mikakati ya hovyo wakiamini itaweza kutatua matatizo ya taifa hili.
Laiti kama tungekuwa naviongozi makini kutoka chama makini,wenye kutumia akili na hekima zao sawasawa:

  • Wasingekurupuka kuja na kaulimbiu ya kilimo kwanza nakulazimisha kila halmashauri iagize power tillers kama ndo suluhu ya matatzo ya sekta ya kilimo.
  • Wasingekurupuka na kulazimisha wananchi kuhangaika kujenga shule za sekondari kila kata na kuamini kuwa hilo ndo suluhisho la matatizo ya sekta ya elimu nchini.
  • Wasingekurupuka na kutoa majibu ya hovyo na ya vitisho kwa wafanyakazi (rejea sakata la TUCTA,madaktari na walimu), wakiamini kuwa hiyo ndo njia muafaka ya kumaliza migogoro.
  • Wasingekurupuka na kupeleka bajaj kwenye vituo vya tiba ili ndo uwe usafiri wa kuwawahisha wajawazito hospitali wakiamini huo ndo muarobaini wa kupunguza vifo na adha ya usafiri waipatayo wajawazito huko vijijini.

Hili la kung'ang'ania kuidhoofisha CDM kwa hoja ya Dr Slaa kuwa na kadi ya CCM(ambayo aliinunua mwenyewe,mali yake), na kusahau katiba yao inaeleza nini juu ya kukoma kwa uanachama wa ccm, pamoja na hayo niliyoyaorodhesha hapo juu ni dhahiri kuwa wanazidi kujivua nguo hadharani na huku wakiendelea kusimama( muungwana akivuliwa nguo uchuchumaa).

CHADEMA HAITASAMBARATISHWA NA MBINU HII YA KITOTO NA KIPUUZI, IKIWA ZILE ZA UKABILA, UKANDA NA UDINI ZIMESHINDWA.
PEOPLES.......
 
Hili swala la kadi mbona lipo wazi hasa kisheria? Kadi za vyama vya siasa sio sawa na kadi za bank au mifuko ya jamii... Ni mali ya mwanachama na si chama. Ndio maana wengine huzichoma pasipo kushtakiwa. Nape alikurupuka kama kawaida yake. Si mnakumbuka pia alikurupuka na hoja ya kujivua gamba?
 
Back
Top Bottom