Somo kwa wanaume

Uko sawa Ligogoma, tafiti zinaonesha sisi wanaume tunakufa haraka kwa sababu ya kubeba ma-stress, sasa hivi wanaume wengi wanatafuta namna ya kuzikwepa stress hizo ili kuongeza walau siku za kuishi, maisha yenyewe magumu ukiongezewa na stress za wanawake basi inakuwa shida, wakati huo huo wanawake wana enjoy life ambayo wewe mwanaume una struggle kila siku
 
mbona umewasilisha kwa hasiera na jazba sana, pengine labda ungekuwa wazi na specific zaidi maana kwa andiko lako hilo labda imekutokea mwenyewe but all in all mwanaume harekebishwi kwa kauli kama hizo, mwanamke ana nguvu na ushawishi mkubwa sana juu ya mwanaume bali ila tatizo linakuja kwenye namna ya kuutumia ushawishi wenu, nyumbani panaweza kugeuka jehanamu kwa mwanaume au pakawa paradiso, yote yako kwenye uwezo wa mwanamke ndo maana hata maandiko yakasema mwanamke mpumbavu ataivunja ndoa yake kwa mikono/ulimi wake mwenyewe!!!
 

Na nyie mpunguze gubu.maana wanawake wengine hawatoi hata nafasi ya mwanaume kupata utulivu.ni mikelele mwanzo mwisho

so kuepuka usumbufu na kukuzaba kibao bora nipotezee nirudi ukiwa una usingizi
 
Kaa na mumeo myazungumze, usituletee stress zako wenzio leo tunarudi saa nane na lazima tukague gymkhana unaweza ukamkuta MOO anaomba lifti
 
Pole kwa mumeo kama balaa kalipata tena balaa haswa.
Kama somo kwa mwanaume ndio huwa linatolewa kwa namna hiyo, kuna haja ya kukagua vyeti vya waliokufunda kabla hujaolewa.
 
Ashinde nyumbani wakati kutwa nzima umegeuka vuvu zela unampigia kelele zisizo na msingi ndo maana anakuwa wa Kwanza kuondoka na wa mwisho kurudi,ndo maana wengi wetu hatuoi siku hizi kuepusha kero Kama hizo
 
Pole sana kama vipi achana naye.
 
Tunakimbia minuno yenu na kuchoka kila siku. Msosi aniandalie HG wewe kucha ndefu unashinda na insta whatsup facebook na tamthilia tuu. Sie wazee wa kambi popote hatupendi kupigwa mswaki siku tatu nne, hata sie twachoka lkn linapofika suala la tendo na mpira uchovu huisha km povu la Kilimanjaro lager! Hatuna mambo mengi hiyo tuu mnashindwa kutusoma?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…