Taifa Digital Forum
Member
- Jun 4, 2022
- 68
- 184
Mwaka huu 2023 Mwezi Machi 05, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alikabidhi hati ya kiwanja chenye ukubwa wa hekari 125 kilichopo eneo la Kisongo Arusha kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwajili ya ujenzi wa Kituo kikubwa cha Diplomasia Afrika.
Hii inaishara kwamba Tanzania inakuwa kitovu cha diplomasia Afrika kwani nchi mbalimbali hasa za Jumuiya ya Afrika Mashariki zitakuwa zikifanya mikutano yao hapo, mafunzo kwa wanadiplomasia mbalimbali na pia kukalibisha wawekezaji mbalimbali nchini kwasababu ya utulivu wa kisiasa.
Tanzania inakuwa mwenyeji wa kikao cha 23 cha Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo kinafanyika Jijini Arusha kwanzia tarehe leo 23 hadi 24 Novemba 2023.