Soma hapa baadhi ya maswali muhimu ya kujiuliza kwenye maisha

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,239
22,318
TUJIKUMBUSHE baadhi ya maswali ya kujiuliza hasa kwa vijana;

1. Unaishi kwenye maadili mema au tabia zako una mashaka nazo?

2. Mpenzi/mchumba uliye naye utafika naye kwenye ndoa au mnakulana tu? Utamuoa huyo binti/utaolewa na huyo kijana?

3. Wewe kama mtumishi wa Mungu unatenda yale unayohubiri au tusikilize unachosema na sio unachotenda?

4. Mavazi yako kwenye nyumba za ibada yanaonyesha utukufu wa Mungu au tukuache kwa sababu imani iko moyoni na sio mavazi?

5. Wewe ni mwislamu kweli au ukienda kwa SHIRIMA Kitimoto unaitwa Aloyce badala ya Juma?

6. Akiba uliyo nayo inaweza kukufikisha siku au miezi mingapi ikitokea ghafla huwezi kuingiza kipato?

7. Kazi unayofanya unaipenda?

8. Kweli wewe unakipenda chama chako cha siasa toka moyoni au upo hapo kimaslahi au kutega mitego yako?

9. Unafahamu hata ibara moja ya katiba ya jamhuri? Ungependa kitu gani kiondolewe au kiongezwe kwenye katiba?

10. Unakubalia kwa dhati kuwa CCM imebeba matumaini ya watanzania wote ukiwemo wewe?

11. Una uhakika watoto ulio nao ni damu yako? Wewe mama una uhakika hujambambikizia jamaa watoto?

12. Kwa imani yako unadhani ikitokea umekufa ghafla utaenda mbinguni au ni direct motoni?

13. Wewe mwalimu wa sekondari hasa wa Sayansi ukipewa ghafla mtihani wa somo unalofundisha utapiga A?

14. UNAUCHUKIA UFISADI AU ROHO INAKUUMA HAUPO KWENYE KITENGO CHOCHOTE CHA UPIGAJI?

15. Kwa hizi tuhuma wanazopewa wabunge kwamba wamehongwa mamilioni, wewe ungeweza kuyakataa kama ni kweli?

16. Unadhani ukibarikiwa kuwa tajiri hutabadilika kitabia na kuanza kuwa mshenzi kwenye jamii?

17. Unavyowaita kina Uwoya, wema na madada wengine kuwa ni wadangaji sio kwamba hadhi yako hairuhusu kuwapata?

Ongezea mengine....
 
TUJIKUMBUSHE baadhi ya maswali ya kujiuliza hasa kwa vijana;

1. Unaishi kwenye maadili mema au tabia zako una mashaka nazo?

2. Mpenzi/mchumba uliye naye utafika naye kwenye ndoa au mnakulana tu? Utamuoa huyo binti/utaolewa na huyo kija
Tafuta hela ndugu. Majungu hayaleti chakula.
 
Hayo maswali Ni magumu kupitiliza sidhani Kama Kuna mtu anaweza kuyapatia kwa asilimia 💯
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom