Kwenye maisha usikubali yeyote akutishe kuwa hauwezi ingawa tahadhari ni muhimu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Uzoefu wangu unanionyesha kuwa yale yote niliyoambiwa na Watu siyawezi na ni magumu asilimia 99% nimeyaweza na nayaona ni mambo ya kawaida. Sio marahisi wala sio mambo magumu.

Jambo hilo naliona mpaka sasa, vijana wengi hutishiwa na kukatishwa tamaa na Watu katika safari yao ya maisha.

Moja ya mambo ambayo wakati nakua nilikuwa naambiwa na kuyasikia ni kuwa Kufaulu shule za Kata haiwezekani. Kisa na mkasa wanaofaulu ni wawili na wakizidi ni watano. Kumbe wapo wanaofaulu? Hata kama ni wachache.

Basi kati ya hao wachache jiwekee nawe utakuwa mmoja wao iwe jua iwe mvua. Yaani hakuna excuse hapo. Na Watu tulifaulu. Mpaka tukamaliza mwisho kabisa. Chuoni.

Oooh! Kitaa kigumu! Oooh! Kujitegemea ni kazi ngumu! Sijui kupanga chumba au nyumba ni kazi. Oooh! Kujiajiri ni kazi ngumu! Mara ooh! Hautaweza!

Ooh! Kuoa sijui kuwa na familia ni ngumu! Sijui kuishi na mke ni kazi ngumu. Sijui kulea mtoto ni kazi ngumu!

Hakuna ugumu wowote. Vijana hayo yote hakuna gumu hata moja. Siongei kwa kutaka kukufariji hapa. Naongea ukweli kwa sababu hayo maisha nimeyapitia na mengine ninayaishi hivi leo.

Kwenye maisha jambo gumu zaidi ni kutokuwa na Afya njema, kuumwa. Yaani hapo ndio unaweza kusema hilo ndio jambo gumu lakini ukishakuwa na afya njema hakuna jambo gumu hata moja.
Ni suala la mtazamo, utayari, imani na ujasiri(uthubutu) wa kufanya mambo yako yaende.

Oooh! Usiende kutafuta maisha Mjini au nje ya nchi kugumu. Hakuna sehemu ngumu wewee! Ngumu kwa wengine lakini sio kwako. Kwako jambo lolote lichukulie ni lakawaida. Sio rahisi wala sio gumu. Utashinda kama utakuwa makini kufuata kanuni za ushindi wa kulishinda jambo hilo.

Jiwekee kama kuna Watu wachache watakaofanikiwa kwenye jambo unalolifanya basi wewe ni sehemu ya Watu hao. Sio ufanye jambo huku moyoni unasema hili jambo ni gumu. Mtazamo wako ndio unafanya jambo hilo kuwa gumu na sio jambo lenyewe.

Kwa mfano kuanzisha Biashara au kampuni. Oooh! Biashara ngumu sijui ujasiriamali mgumu. Hakuna kitu kama hicho. Sijui TRA sijui serikali inahujumu sijui kodi kibao.

Sasa Kama TRA inahujumu na serikali inamakodi kibao mbona kuna wenzako wanafanikiwa kwenye hiyo biashara wakati hao kina TRA na serikali wapo? Acha visingizio vya Watu walioshindwa.

TRA na serikali inaongozwa na Watu kama wewe. Sawa vijana. Acheni woga wa kijinga. Kila jambo lina dawa yake. Jiwekee kuwa hata TRA iongozwe na Mashetani au serikali iwe ya kishetani wewe kufanikiwa ni lazima. Usikubali kutishwa.

Ingawaje tahadhari ni muhimu lakini tahadhari zisikufanye ukawa mwoga wa kuchukua hatua kwenye maisha yako.

Jambo lolote ambalo sio dhambi na sio uhalifu na sio kujitoa au kujidhalilisha utu wako haliwezi kuwa jambo gumu.

Kama walishindwa ni wao sio wewe. Kama yeye alishindwa biashara na kuiona ngumu mwambie ni yeye na mtazamo na uwezo wake.

Kama ndoa anaiona ngumu mwambie ni yeye. Mwambie wapo wanaoiona ndoa kama juisi ya embe, laini na tamu.

Mwambie kama alipata ugumu kujitegemea na kupanga chumba sijui kulipia Bills mwambie ni yeye na uwezo na mtazamo wake. Kwako wewe hayo ni mambo ya kawaida na ikiwezekana ni marahisi sana.

Kuna Watu wanatisha Watu kuwa kujenga nyumba ni kazi ngumu. Hiyo ni kwenu. Kama kwenye ilikuwa ngumu eleweni kuwa kwa sisi hilo ni jambo la kawaida. Ni suala la muda tuu.

Vijana, mambo yote mazuri ikiwemo uchumi mzuri, elimu nzuri, familia na ndoa bora, makazi mazuri ni mambo ya kawaida sana na hayapo kwenye orodha ya mambo magumu.

Imani thabiti!
Uwezo uliotukuka!
Ujuzi na maarifa Sahihi!
Malengo na mipango yenye Uhalisia.
Uthubutu wenye tahadhari!
Subira!

Haya ndio mambo ambayo kijana unatakiwa uwe nayo akilini mwako.

Watu wenye roho ya Korosho, roho za kishetani ndio hutishia na kukatisha tamaa. Kamwe usiwasikilize hata wakiongea mbele zako wachukulie kama Mbuzi mee anayepigapiga kelele tuu.

Nawatakia Ijumaa njema na maandalizi mema ya Sabato.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es salaam.
 
Oooh! Usiende kutafuta maisha Mjini au nje ya nchi kugumu. Hakuna sehemu ngumu wewee!

NAKAZIA.



Note:
Ila ndoa ni magumashi kweli wala sio utan

Mtazamo Mkuu.

Maisha yanakupa vile unavyoyachukulia.
Ndoa inakanuni zake.
Kanuni kuu ni upendo.
Ukishazingatia kanuni hiyo ndoa ni kama juisi ya embe.

Ishu inakuwa pale unapoingia kwenyw mahusiano na mtu ambaye unampenda alafu yeye hakupendi au yeye anakupenda alafu wewe humpendi alafu ukaiita NDOA. Hapo lazima ukwame
 
Mtazamo Mkuu.

Maisha yanakupa vile unavyoyachukulia.
Ndoa inakanuni zake.
Kanuni kuu ni upendo.
Ukishazingatia kanuni hiyo ndoa ni kama juisi ya embe.

Ishu inakuwa pale unapoingia kwenyw mahusiano na mtu ambaye unampenda alafu yeye hakupendi au yeye anakupenda alafu wewe humpendi alafu ukaiita NDOA. Hapo lazima ukwame
Surely
 
Ehĥhh bwana shukran sana kiongozi ...... ww ndoo kwanza kunitia moyo kwa mwaka huu 😊....... kila ninayefuata nipatee ushauri anikatisha taama kwanzia business ,marriage na hata kucomplete my university education .....
 
Umeacha chuo kisa safari ya nje.
Utarudi umeshindwa utatuomba msaada hapa, huna ujuzi nje unaenda kufanya nini, huna ndugu hata mmoja huko uendako utaishije, nauli hatutokusaidia sababu umekataa kusoma chuo.
Nashukuru mungu niliziba masikio nikatimka zangu, saivi simu zimekua nyingi kila mtu anataka attention yangu, bado wanataka tugawane hivi vidollar vya kubeba box.
wengine mpaka ugomvi, nakusema nina ringa.
mungu tusaidie waja wako.
 
well said binafsi niko hapa nilipo kwa sasa japo sio ninapo pataka ila ni afadhari zaidi hii yote ni kwasababu ya kurisk, always dare to do.
 
Success begins with someone's efforts, dicipline and hard work. If a person has a goal and does not try to fulfil his goal, then he can never achieve success. To be successful, a person needs to work hard, dicipline and put in a lot of effort. To achieve your goal, you need to chase after it, and you must be dedicated.
 
"kwasababu ya kurisk, always dare to do"
Your right b'se you can’t let people scare you.
You can’t go your whole life trying to please everyone. You can’t go through life worried about what everyone else is going to think.
Whether it’s your hair, clothes, what you have to say, how you feel, what you believe and what you have. You can’t let the judgment of others stop you from BEING YOU. Because if you do, you’re no longer you. You’re someone everyone wants you to be.
 
Ohopa Sana taarifa ya uwez huna mataji

Kataa kwa jina la yesu hicho kitu

Vyote vinawezekana duniaa hi mm kweli leo naandikiana msg na naibu waziri
 
Back
Top Bottom