Maswali 20 ya kujiuliza kuhusu mwenzi wako

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
The Seven Principles For Making Marriage Work

Hapo awali nilijiuliza sana ni kwanini kitabu cha 'The Seven principles for making marriage work' kilikuwa kwenye list ya vitabu bora sana vya mahusiano na ndoa lakini baadae taratibu baada ya kuanza kukisoma nilielewa ni kwanini.

Professor John Mordechai Gottman, mwandishi wa kitabu hiko anatoa muelelezo wa maswali 20 ya kujipima kama kwenye mahusiano yenu mnathaminiana, kuheshimiana na kupendana sana kiasi kwamba mnaweza kudumu Kwa muda mrefu.

Jibu linatakiwa liwe ndio au hapana.

1. Je, unaweza kuorodhesha kwa urahisi sana mambo matatu unayoyapenda sana kutoka kwa mpenzi wako?
2. Je, unapokuwa mbali naye huwa unamfikiria sana mpenzi wako?
3. Je, mara nyingi huwa unamwambia mpenzi wako kuwa unampenda?
4. Je, mara nyingi huwa unamgusa au kumbusu mpenzi wako kwa upendo?
5. Mpenzi wako anakuheshimu sana?
6. Je, unahisi kupendwa na kujaliwa katika mahusiano yenu?
7. Je, wewe mwenyewe unahisi kukubalika na kupendwa na mwenzi wako?
8. Je, mwenzi wako anakuona mrembo na mwenye kuvutia?
9.Je, mpenzi wako anaona fahari kuwa na wewe?
10. Unaona shauku yoyote katika mahusiano yenu?
11. Je, katika mahusiano yenu bado kuna hisia za dhati na mapenzi ya kweli?
12. Unajivunia sana kuhusu mpenzi wako?
13. Mwenzi wako anafurahia na kuvutiwa na mafanikio au maendeleo yako?
14. Je, unaweza kutoa sababu za msingi ni kwanini upo kwenye mahusiano na mpenzi wako huyo?
15. Je, upo tayari kudumu na mwenzi wako huyo kwa muda mrefu?
16. Je, kuna baadhi ya siku huwa mnalala bila kuongea nae?
17. Je, mwenzi wako anafurahi kukuona hasa pale mnapokutana?
18. Mpenzi wako anafurahia juhudi zako au mambo unayoyafanya kwenye mahusiano yenu?
19. Je, mpenzi wako anapenda jinsi ulivyo?
20. Je, unamuamini saa mpenzi wako, na unaweza kumuambia jambo lolote, wakati wowote kuhusu hisia zozote juu yake?

NDIO KUMI KWENDA JUU:
Baada ya kujiuliza maswali hayo, hesabu majibu ya Ndio, kama ni kuanzia 10 kwenda juu basi hongera sana. Hiki n kipindi maalumu sana Cha mahusiano yenu, mna ngao inayoweza kuwasaidia kudumu kwenye mahusiano yenu muda mrefu zaidi. Basi jitahidi sana kujilinda, kila mtu amheshimu na kumthamini sana mwenzake, hakikisheni kumbukumbu njema ndio zitawale mahusiano yenu na wala si kingine.
(Ameandika J. M. Gottman, katika ukurasa wa 66)

NDIO KWANZIA 10 KUSHUKA CHINI:
Ikiwa majibu yako ya ndio yapo chini ya Kumi basi pole sana. Mahusiano yako yanahitaji baadhi ya maboresho, mnatakiwa kujilinda mno maana la sivyo mtaishia kwenye shimo la lawama tu kwa kila mtu. Msingi wenu wa mahusiano wa Heshima na Kuthaminiana umelegea sana, hakikisheni mnasimama imara kujua jinsi ya kutetea mahusiano yenu. Msipokuwa makini basi mbegu ya dharau itaota kwenye mahusiano yenu, na matokeo ya dharau ni utengano tu.
(Ameandika J. M. Gottman, katika ukurasa nambari 67)

Ahsante kwa kunisikiliza naitwa Amani Dimile

Screenshot 2023-07-26 113005.png

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom