Sokoine was not a hero, Salim was...

Sokoine was not a hero, Salim was...

Mkuu, kuna facts inabidi tuziweke sawa. Nahisi wengine wameshagusia. Nakumbuka nikiwa mwanafunzi tulichukuliwa na kusambazwa jiji zima kukusanya data za mienendo (modus operandi) ya daladala wakati ule zikifanya kazi kiwizi. Tulipouliza tukaambiwa Waziri Mkuu (Sokoine) ametoa agizo apewe ripoti si zaidi ya wiki kuhusu athari ya dala dala kwenye soko la UDA. Hakuelewa kwa nini zinakamatwa wakati wananchi wanazikimbilia wenyewe. Waziri wa Uchukuzi alikuwa Malecela. Tulipomaliza mara moja daladala zikaanza kazi kwa masharti ya kulipa pasenti UDA kitu tulichoona mzaha kwani daladala zilikuwa zinachukua ziada ya abiria ilioshindwa UDA.

Kingine, kuna wakati unga wa njano (yanga) nao uliadimika sana ikawa taabu madukani. Sokoine alitembelea NMC na kukuta mahindi ya njano yamerundikwa milima. Alipouliza kwa nini hakuna unga akaambiwa mashine nyingi za kusagisha zimekufa (no vipuri). Akauliza (kwa lafudhi yake ya kimasai) kama wananchi hawana mashine huko mitaani. Jibu alilopewa ni kuwa hawaruhusiwi kuuza mahindi bali unga tu. Alitoa amri palepale mahindi yote yatolewe na kuuziwa wananchi. Tulikuwa tumezoea unga mchafu wa NMC lakini baada ya kuanza kusaga kwenye mashine mitaani mtazamo wa yanga uliboreka sana.

Huyo ndiye Sokoine. Inadaiwa Mwalimu hakuwa comfortable naye sana (kama alivyozoea kwa Kawawa) kwa jinsi alivyokuwa akitoa maamuzi magumu bila simile. Ndio maana conspiracy theories bado zimeweka kivuli kwenye ajali iliyomfisha!
 
Asante mkuu The Boss kwa thread hii kuna kitu nimejifunza
 
The Boss

Candidly umeongea ....

KATIKA Watu wawili waliokubalika zaidi kwenye Jeshi la nchi hii Ni Nyerere ....wa pili wanayemuheshimu ni ....Salim AhMed Salim......., Kama alivyowasaidia wananchi walikuwa uchi ndio hivyo anatambulika jeshini ....Baada ya kutoka vitani ...magari mengi yalifia huko ....mengine yakawa grounded kwa kuwa serikali haikuwa na pesa ya vipuri.

Salim alienda Japan akiwa Prime Minister ....na akaomba msaada kwa kutumia influence yake kupitia rafiki yake ...ambaye walikuwa naye UN ...alipewa magari landcruizer left hand karibu 400 ..mpya ....akaja akagawa kwenye vikosi vyote jeshini .....akawa amewasitiri.

Kuna wakati Hali ilikuwa ngumu sana ...wakati huo tayari mwinyi ameingia na yeye akawa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa ulinzi .....kulitokea mushkel kidogo Kambi kubwa ya Tabora ...sasa kwa kuwa Hali ilikuwa ngumu viongozi wote wakuu wa nchi walijiuma umma kwenda kuongea na Askari ..kuwaeleza Hali halisi Ili wawe wavumilivu ....Ni Salim alienda kule akaongea na vijana wakamuelewa......, ukizingatia Askari wengi wakitaka yeye awe Rais na hakuwa ....angekuwa Sio mzalendo ....angeweza kuasi na akaongwa mkono ...

Kwa kifupi hata kitendo cha salim kupigiwa chapuo ..kwenda OAU ...KUNA msukumo mkubwa wa wahafidhina ambao walihakikisha hawi Rais ..1985 ...wakiamini kwa u maarufu aliokuwa nao Ndani ya jeshi na system nzima .....na kukubalika kwake na wananchi alikuwa na nafasi kubwa ya kuweza hata kumuondoa Mzee mwinyi 1990 au kuwa candidate alipomaliza muda wake 1995.

Kama mpango wa Mwalimu kumuachia Salim nchi 1985 ungefaulu alikuwa Ni the right person kufanya mabadiliko ya sera ...kutokna na kuwa na elimu mzuri ..exposure ...na kukubalika sana kimataifa.

Ijulikane kuwa Nyerere alitaka mtu wa kufanya reforms mbali ya yeye ....na aliamini kwa salim na Sio mtu mwingine ...., makosa aliyofanya Mzee mwinyi kwenye reforms ...Sio ya makusudi ...Bali alijitahidi kadiri ya uwezo wake ..

Hazikuwa landcruiser bali ni Nissan single na double cabin
 
Kwangu mimi ushauri wa Dk. Salim kwa Nyerere haukuwa mzuri, na ndio uliotufikisha hapa-viwanda vya ndani vimekufa. Lkn kama tungekomaa hivohivo na sisi tungetoka kwani tungelazimika kuendelea kuzalisha Zaidi kupitia viwanda vyetu mwishowe tungeweza ku compete ktk soko la Dunia. Mfano wa nchi iliyokomaa ni India

Viwanda gani tena wakati waambiwa vilikuwa vimekufa?
 
Kwa Sikoine hata Mwl Nyerere anasubiri! Hakuwa na chembe ya unafiki hata kidogo.Lowassa anafanana na Sokoine vitu vitatu tu, Urefu, ubunge wa monduli na wote waliwahi kuwa Mawaziri wakuu.Kwny Uadilifu ni kama Mbingu na Ardhi au Magharibi na Mashariki

Haha Umesemaje?
 
Nimejikuta namkumbuka Sokoine na siasa za Tanzania miaka ile na kwa jinsi ambavyo watu huwa wanam refer kama 'a big hero' au best PM ever..

Tanzania yetu hii ni nadra sana watu hajadiliwa katika 'fairness inayostahili'wapo ambao wanakuzwa kupita hali halisi na wapo ambao wanapondwa kuliko hali halisi..

Mmoja wa watu ambae mimi binafsi nimefuatilia kidogo tu siasa zake za enzi hizo ni Edward Sokoine aliwahi kuwa waziri mkuu mara mbili....wakati wa Nyerere....kiukweli tukiwa kama watu ambao tunataka kujifunza from our past ni sahihi sana tuwe tunajadili vitu kama why Sokoine alioneka 'a hero' kwa baadhi ya watu? Na nini hasa alikifanya kustahili sifa hiyo? Na kama aliyoyafanya yanastahili kumuita shujaa na mfano wa viongozi wengine wa baadae wa Taifa hili.. na kama hakuwa a big a hero then.. je wanaojaribu kumfuata wana kipi cha kujifunza?

Kuna vitu viwili vilijitokeza ambavyo binafsi naona ni mfano tosha wa kwa nini Sokoine hakuwa 'role model ya viongozi bora' Tanzania.....na Salim A Salim kwangu namuona a hero sababu alifanya yale ambayo Sokoine alishindwa kwa muda mfupi tu....bila kutafuta sana ujiko wala kujipa credit ...ilikuwa kimya kimya lakini wanaojua historia wanakiri....

La kwanza ni lazima pia kujua mazingira ya Tanzania kipindi kile;

Kufuatia vita ya Iddi Amini na Nyerere kukataa masharti mbalimbali ya World Bank na IMF nchi iliingia kwenye shida kubwa mno ya bidhaa za msingi za matumizi vitu kama sigara,sukari,unga mchele vilikuwa adimu kupatkana, watu walikuwa wanapanga foleni hasa mijini kama Dar kwa ajili ya kupata tu sukari au sigara.....sasa wafanyabiashara wengi wakawa wana take advantages kwa kulangua bidhaa na wengine kuzificha ili zizidi kupanda bei..

Hapa ndo umaarufu wa Sokoine ulipojitokeza.... Sokoine aliiongoza kamata kamata ya 'walanguzi' na 'wahujumu wa uchumi' na aliifanya hiyo kazi na kusaidia 'kupunguza' hiyo shida ya bidhaa madukani..

Alionekana shujaa wakati ule lakini kiukweli tatizo halikuisha.....lakini alikuwa anaogopwa kupita maelezo 'alionekana mzalendo na anaejali' kwa kuwakamata 'walanguzi' lakini mwisho wake tatizo liliendelea.

Nchi ilikuwa na matatizo tele mfano nguo za kuvaa tu ilikuwa hakuna.... usafiri wa mijini kampuni kama KAMATA ilishakufa na kadhalika...matatizo haya yaliendelea kuwepo moja ya sababu ilikuwa KUKOSA ' mtu wa kumwambia Nyerere UKWELI wa hali halisi na makosa ya sera na mbinu mpya inahitajika kuondoka na matatizo hayo na sio kuendelea kukamata kamata tu watu...

Baada ya Sokoine kufariki kwa ajali mwaka 1984 Nyerere alimteua Salim kuwa Waziri mkuu na Salim bila woga alienda kum face Nyerere na kumwambia lazima baadhi ya sera zibadilishwe hata kwa dharura tu, baada ya tukio maarufu Mtwara ambapo wananchi walijifunga viroba kumkaribisha waziri mkuu na wengine wanasema 'walivua nguo' kuonesha kero yao ya kukosa nguo za kuvaa.

Salim alim face Nyerere na ndio 'mitumba ikaruhusiwa Tanzania' kama 'sera ya dharura' baada ya viwanda vyote kufa.....Salim alipoona watu wanahangaika na kusubiri mabasi ya KAMATA kwa masaa kadhaa akaja tena kuruhusu 'daladala' kama mbinu ya dharura kutatua tatizo hilo.

Nyerere alikuwa hataki kabisa hizi sera za kuruhusu watu binafsi wafanye biashara hata kama wananchi wanateseka, 'ujasiri wa Salim' kumface na kumshawishi Nyerere akubali japo kwa 'dharura' ili wananchi wasiteseke hadi hapo nchi uchumi utakapotengemaa..

Nyerere alikuwa anaogopwa... Ndio maana Mtei alijiuzulu alikuwa hashauriki.......lakini Salim mbele ya mateso ya wananchi aliweza kum face na kumbadili msimamo.

Sokoine kwangu naona alikuwa 'mtiifu' na waziri mzalendo na mchapakazi akitekeleza 'vizuri' maagizo ya Nyerere lakini kama 'ushujaa' mimi namuona Salim alikuwa 'shujaa mkubwa'.

Aliweka maslahi ya wananchi mbele, sera za kukamata kamata na kufukuza fukuza zinaweza mfanya kiongozi awe maarufu sana na avuume mno lakini je zinatatua tatizo kiasi gani? Je, sera zinabadilishwa? Je, unafuu unaohitajika unapatikana?

Kiongozi anaweza kupata 'cult followers' huku 'matatizo' yale yale bado yapo vilevile unafuu wa msimu tu lakini sio kuondoka kabisa...

Salim alifanya kile Sokoine alipaswa kukifanya siku nyingi....lakini hakukifanya ingawa Sokoine ana 'cult followers' na Salim hana mashabiki die hard...lakini still ukitazama historia unbiased..utakubaliana na mimi.

Nakaribisha mjadala, ambao mnaamini Sokoine was a hero nini mnaamini alikifanya cha kustahili kuitwa a hero?

Kumbuka ninachokisema, Sokoine alikuwa mzalendo na mchapakazi lakini siamini kama alikuwa mfano bora wa viongozi... Salim was better......

Third world country waziri mkuu anasifiwa kwa kuleta mitumba baada ya viwanda kufa na kuruhusu daladala keny wanasema matatuu we still have long way to go na wewe umekaaa ukaona umeandika kweli kweli urojo huu
 
Kuna mtu kasema hilo mahali. Langu lipo tofauti. Hahaha

Mkuu Sibonike nikushukuru sana kwa kusaidia thread isiharibike

tunaweza tusikubaliane kila kitu lakini angalau nikiri umesaidia watu kuona angle

siku zote tunapowasifia viongozi wa zamani tukumbuke 'wataigwa' na viongozi wa sasa
na kama kuna makosa 'yataigwa pia'

hivyo mijadala kama hii ni muhimu sana sana kuliko tunavyo fikiri
 
Last edited by a moderator:
Niwashukuru wakuu wote mliochangia hii thread
imetufundisha mengi sana

Nikiri kuna 'some factual errors' katika mifano niliyotumia hasa ule wa Daladala

na nikiri pia masahihisho ya baadhi ya members yamenisaidia pia kujifunza na mimi


naweza kusema nakubaliana na members wengi now waliosema Sokoine na Salim walikuwa
ni watu wawili tofauti sana.....na wote walikuwa 'very good' katika waliyoyafanya....
sasa nikiri kuwa 'umuhimu wa threads' kama hizi ni mkubwa now
kama alivyosema member mmoja kuwa historia iliyopo kwenye vitabu haiko complete

Kwa ujumla michango ya members wote hasa wale walioweza kuiona 'angle'
ya thread vizuri bila kuwa biased wala kuhisi 'wanakuwa attacked' imenisisimua na
naamini hii thread imetusaidia wote...
 
Wengi hawakuwepo wakati huo wanafata wanayoyasoma au kuyasikia ambayo mengi yamebadilishwa uhalisia wake.

A question to you, why now?

Sasa wewe uliyekuwepo wakati huo ungetuambia basi kwamba hayo yaliyobadilishwa uhalisia wake je ni nani alifanya hivyo na kwa sababu ipi na kwa manufaa ya nani??
 
Sasa wewe uliyekuwepo wakati huo ungetuambia basi kwamba hayo yaliyobadilishwa uhalisia wake je ni nani alifanya hivyo na kwa sababu ipi na kwa manufaa ya nani??

Kwanza nimeuliza swali hapo, juu. Wacha mleta mada alijibu kama yu mkweli.
 
Kwanza nimeuliza swali hapo, juu. Wacha mleta mada alijibu kama yu mkweli.

Swali la why now?

huoni Sokoine ana fananishwa na kila anae onekana ni 'kiongozi bora'?
au anaetaka kuonekana 'kiongozi bora'?

Kama kuna watu walikuwa au still wanamfananisha Lowassa na Sokoine basi ni muhimu Sokoine ajadiliwe
na kama kuna watu wanamfananisha JPM na Sokoine pia ni muhimu Sokoine ajadiliwe

Na kama kati yao au wote Lowassa na JPM wangependa kufananishwa na kumuiga Sokoine
basi ni muhimu zaidi Sokoine ajadiliwe in 'fairness'
ili kama kuna makosa ya Sokoine ya kuyaepuka yaepukwe....na kama Sokoine was 100 percent a good example
wamuige tu hakuna shida...time will tell.....
 
Swali la why now?

huoni Sokoine ana fananishwa na kila anae onekana ni 'kiongozi bora'?
au anaetaka kuonekana 'kiongozi bora'?

Kama kuna watu walikuwa au still wanamfananisha Lowassa na Sokoine basi ni muhimu Sokoine ajadiliwe
na kama kuna watu wanamfananisha JPM na Sokoine pia ni muhimu Sokoine ajadiliwe

Na kama kati yao au wote Lowassa na JPM wangependa kufananishwa na kumuiga Sokoine
basi ni muhimu zaidi Sokoine ajadiliwe in 'fairness'
ili kama kuna makosa ya Sokoine ya kuyaepuka yaepukwe....na kama Sokoine was 100 percent a good example
wamuige tu hakuna shida...time will tell.....

Utaja ishia kuambiwa humpendi Magufuli na unampinga kwenye kila kitu.

We subiri tu....
 
Utaja ishia kuambiwa humpendi Magufuli na unampinga kwenye kila kitu.

We subiri tu....

Ngabu kuna siku niliwahi kusoma Ujerumani wamei introduce chess ichezwe shule ya msingi
ili watoto waweze kuwa na akili zaidi na kutazama mambo na kujiuliza

huwa kila siku najiuliza why watanzania wengi tuko 'one dimensional'?
 
Swali la why now?

huoni Sokoine ana fananishwa na kila anae onekana ni 'kiongozi bora'?
au anaetaka kuonekana 'kiongozi bora'?

Kama kuna watu walikuwa au still wanamfananisha Lowassa na Sokoine basi ni muhimu Sokoine ajadiliwe
na kama kuna watu wanamfananisha JPM na Sokoine pia ni muhimu Sokoine ajadiliwe

Na kama kati yao au wote Lowassa na JPM wangependa kufananishwa na kumuiga Sokoine
basi ni muhimu zaidi Sokoine ajadiliwe in 'fairness'
ili kama kuna makosa ya Sokoine ya kuyaepuka yaepukwe....na kama Sokoine was 100 percent a good example
wamuige tu hakuna shida...time will tell.....

Kwa hiyo wewe unamfananisha na nani?

Mimi nnaona hafanani na yeyote kwa utendaji kati ya uliowataja.
 
Back
Top Bottom