Sokoine was not a hero, Salim was...

Sokoine was not a hero, Salim was...

Nikiri toka mwanzo mimi ni mshabiki mkubwa wa Sokoine. I have very fond memories. Sitapenda kufanya comparison na watu wengine au mawaziri wakuu wengine. Lakini nikiangalia anecdotes fulani, ninashuhudia kwamba Sokoine alikuwa mfano bora wa kiongozi. Si lazima watu wahusike na mambo yale yale ili tukubali nafasi zao katika historia.

Wakati wa Nyerere huo, usafiri Dar es Salaam ulikuwa umehodhiwa na serikali hasa kwa kutumia UDA, na pengine kidogo COCABS. Kama mleta uzi alivyosema, biashara kubwa za binafsi na hata ndogo sehemu nyingine zilipigwa vita. Jiji la Dar liliendelea kupanuka wakati mabasi ya UDA yakipungua. Sokoine, Waziri Mkuu wakati huo, alishuhudia hilo siku moja alipenda Ubungo pale Maji wakati huo ndiyo kituo, akaona saa 4 asubuhi pamesheheni watu wakisubiri UDA zinazokuja zimeshajaa toka Magomeni. Pale zinageuza tu.

Kwa mbali kule watu walikuwa wanakimbilia mabasi ya watu binafsi yaliyokuwa yakisomba watu kuwapeleka makazini kinyume cha sheria kwa nauli ghali sana wakati huo ya Dala (lile gwala la Sh. 5 lilivyoitwa wakati huo). Ndivyo zilivyoanza daladala. Nauli ya UDA wakati huo ilikuwa Sh 1.50. Alipouliza kilichokuwa kinaendelea, akapata stori kamili. Haraka sana kwa maagizo ya Sokoine ukaundwa utaratibu wa kuhalalisha daladala, ambazo wakati huo walipaswa kuilipa UDA. Nafikiri alifanya kitu kikubwa ambacho siamini kama kilikuwa katika ratiba za Mwalimu.

Nilikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam wakati huo. Maji yalikuwa yanakatika ovyo kwa wiki kadha pale. Na tulikuwa na viongozi wa serikali ya wanafunzi ambao wengine sasa hivi wana nyadhifa za juu sana hapa TZ. Viongozi hao hawakushinikiza utawala wa chuo kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo. Utawala wa chuo, nadiriki kusema, haukuwa na interest yoyote ya kulitatua pia. Maghorofani kule, hebu fikiria hakuna maji kwa mwezi.

Sokoine alianza masomo ya uzamili pale chuoni. Siku moja akaomba aoneshwe maliwato. Ilikuwa kasheshe. Hatimaye akaoneshwa hali halisi. Akawaita wahusika wa chuo, wizara ya elimu na wizara ya maji. Mara moja tukaona matanki ya maji yamemwagwa pale mlimani. Haraka sana kazi ikaanza ya kujenga tanki lile lililo nyuma ya Hall 4. Mabomba yakajengwa kuunganisha na Ruvu Chini.

Ukweli ni kwamba alikuwa mtu ambaye alikuwa tayari kufanya kazi kutatua matatizo ya wananchi. Wengine tuliguswa moja kwa moja na utendaji wake. Doa katika utendaji wake hasa linatokana na kampeni ya wahujumu uchumi ambayo kwa maoni yangu ni kwamba iliendeshwa vibaya na watu nchini kote na pia hakupata kuungwa mkono ipasavyo katika serikali ya Mwalimu. He was like a lone ranger. There were other people whose performance in that office was mediocre, but most certainly Sokoine was not one of them.

Sasa hapo alitatuwa matatizo ya wananchi au yake?

Asingeenda yeye huko chooni ina maana maji yasingekuwepo.
 
Vipindi tofauti kila mmoja alikutana na changamoto zake kwangu wote walikuwa bora.
 
Je kamata kamata ya wazururaji ya Sokoine mwaka 1983 ( almaarufu kama sheria ya nguvu kazi) ilikuwa ina tija kwa Tanzania?
 
Nimejikuta namkumbuka Sokoine na siasa za Tanzania miaka ile na kwa jinsi ambavyo watu huwa wanam refer kama 'a big hero' au best PM ever..

Tanzania yetu hii ni nadra sana watu hajadiliwa katika 'fairness inayostahili'wapo ambao wanakuzwa kupita hali halisi na wapo ambao wanapondwa kuliko hali halisi..

Mmoja wa watu ambae mimi binafsi nimefuatilia kidogo tu siasa zake za enzi hizo ni Edward Sokoine aliwahi kuwa waziri mkuu mara mbili....wakati wa Nyerere....kiukweli tukiwa kama watu ambao tunataka kujifunza from our past ni sahihi sana tuwe tunajadili vitu kama why Sokoine alioneka 'a hero' kwa baadhi ya watu? Na nini hasa alikifanya kustahili sifa hiyo? Na kama aliyoyafanya yanastahili kumuita shujaa na mfano wa viongozi wengine wa baadae wa Taifa hili.. na kama hakuwa a big a hero then.. je wanaojaribu kumfuata wana kipi cha kujifunza?

Kuna vitu viwili vilijitokeza ambavyo binafsi naona ni mfano tosha wa kwa nini Sokoine hakuwa 'role model ya viongozi bora' Tanzania.....na Salim A Salim kwangu namuona a hero sababu alifanya yale ambayo Sokoine alishindwa kwa muda mfupi tu....bila kutafuta sana ujiko wala kujipa credit ...ilikuwa kimya kimya lakini wanaojua historia wanakiri....

La kwanza ni lazima pia kujua mazingira ya Tanzania kipindi kile;

Kufuatia vita ya Iddi Amini na Nyerere kukataa masharti mbalimbali ya World Bank na IMF nchi iliingia kwenye shida kubwa mno ya bidhaa za msingi za matumizi vitu kama sigara,sukari,unga mchele vilikuwa adimu kupatkana, watu walikuwa wanapanga foleni hasa mijini kama Dar kwa ajili ya kupata tu sukari au sigara.....sasa wafanyabiashara wengi wakawa wana take advantages kwa kulangua bidhaa na wengine kuzificha ili zizidi kupanda bei..

Hapa ndo umaarufu wa Sokoine ulipojitokeza.... Sokoine aliiongoza kamata kamata ya 'walanguzi' na 'wahujumu wa uchumi' na aliifanya hiyo kazi na kusaidia 'kupunguza' hiyo shida ya bidhaa madukani..

Alionekana shujaa wakati ule lakini kiukweli tatizo halikuisha.....lakini alikuwa anaogopwa kupita maelezo 'alionekana mzalendo na anaejali' kwa kuwakamata 'walanguzi' lakini mwisho wake tatizo liliendelea.

Nchi ilikuwa na matatizo tele mfano nguo za kuvaa tu ilikuwa hakuna.... usafiri wa mijini kampuni kama KAMATA ilishakufa na kadhalika...matatizo haya yaliendelea kuwepo moja ya sababu ilikuwa KUKOSA ' mtu wa kumwambia Nyerere UKWELI wa hali halisi na makosa ya sera na mbinu mpya inahitajika kuondoka na matatizo hayo na sio kuendelea kukamata kamata tu watu...

Baada ya Sokoine kufariki kwa ajali mwaka 1984 Nyerere alimteua Salim kuwa Waziri mkuu na Salim bila woga alienda kum face Nyerere na kumwambia lazima baadhi ya sera zibadilishwe hata kwa dharura tu, baada ya tukio maarufu Mtwara ambapo wananchi walijifunga viroba kumkaribisha waziri mkuu na wengine wanasema 'walivua nguo' kuonesha kero yao ya kukosa nguo za kuvaa.

Salim alim face Nyerere na ndio 'mitumba ikaruhusiwa Tanzania' kama 'sera ya dharura' baada ya viwanda vyote kufa.....Salim alipoona watu wanahangaika na kusubiri mabasi ya KAMATA kwa masaa kadhaa akaja tena kuruhusu 'daladala' kama mbinu ya dharura kutatua tatizo hilo.

Nyerere alikuwa hataki kabisa hizi sera za kuruhusu watu binafsi wafanye biashara hata kama wananchi wanateseka, 'ujasiri wa Salim' kumface na kumshawishi Nyerere akubali japo kwa 'dharura' ili wananchi wasiteseke hadi hapo nchi uchumi utakapotengemaa..

Nyerere alikuwa anaogopwa... Ndio maana Mtei alijiuzulu alikuwa hashauriki.......lakini Salim mbele ya mateso ya wananchi aliweza kum face na kumbadili msimamo.

Sokoine kwangu naona alikuwa 'mtiifu' na waziri mzalendo na mchapakazi akitekeleza 'vizuri' maagizo ya Nyerere lakini kama 'ushujaa' mimi namuona Salim alikuwa 'shujaa mkubwa'.

Aliweka maslahi ya wananchi mbele, sera za kukamata kamata na kufukuza fukuza zinaweza mfanya kiongozi awe maarufu sana na avuume mno lakini je zinatatua tatizo kiasi gani? Je, sera zinabadilishwa? Je, unafuu unaohitajika unapatikana?

Kiongozi anaweza kupata 'cult followers' huku 'matatizo' yale yale bado yapo vilevile unafuu wa msimu tu lakini sio kuondoka kabisa...

Salim alifanya kile Sokoine alipaswa kukifanya siku nyingi....lakini hakukifanya ingawa Sokoine ana 'cult followers' na Salim hana mashabiki die hard...lakini still ukitazama historia unbiased..utakubaliana na mimi.

Nakaribisha mjadala, ambao mnaamini Sokoine was a hero nini mnaamini alikifanya cha kustahili kuitwa a hero?

Kumbuka ninachokisema, Sokoine alikuwa mzalendo na mchapakazi lakini siamini kama alikuwa mfano bora wa viongozi... Salim was better......
after 5 years of sack this one, appoint that one, terminate that, demote this bado tupo pale pale...........

The Boss bado andiko lako linaishi, 'cult followers and cult figures'
 
after 5 years of sack this one, appoint that one, terminate that, demote this bado tupo pale pale...........

The Boss bado andiko lako linaishi, 'cult followers and cult figures'

The Boss.

Tumemiss mada zako zenye calibre hii.

Wakongwe msiache kuleta mada mkaishia kucomment nyingine tu
 
Nikiri toka mwanzo mimi ni mshabiki mkubwa wa Sokoine. I have very fond memories. Sitapenda kufanya comparison na watu wengine au mawaziri wakuu wengine. Lakini nikiangalia anecdotes fulani, ninashuhudia kwamba Sokoine alikuwa mfano bora wa kiongozi. Si lazima watu wahusike na mambo yale yale ili tukubali nafasi zao katika historia.

Wakati wa Nyerere huo, usafiri Dar es Salaam ulikuwa umehodhiwa na serikali hasa kwa kutumia UDA, na pengine kidogo COCABS. Kama mleta uzi alivyosema, biashara kubwa za binafsi na hata ndogo sehemu nyingine zilipigwa vita. Jiji la Dar liliendelea kupanuka wakati mabasi ya UDA yakipungua. Sokoine, Waziri Mkuu wakati huo, alishuhudia hilo siku moja alipenda Ubungo pale Maji wakati huo ndiyo kituo, akaona saa 4 asubuhi pamesheheni watu wakisubiri UDA zinazokuja zimeshajaa toka Magomeni. Pale zinageuza tu.

Kwa mbali kule watu walikuwa wanakimbilia mabasi ya watu binafsi yaliyokuwa yakisomba watu kuwapeleka makazini kinyume cha sheria kwa nauli ghali sana wakati huo ya Dala (lile gwala la Sh. 5 lilivyoitwa wakati huo). Ndivyo zilivyoanza daladala. Nauli ya UDA wakati huo ilikuwa Sh 1.50. Alipouliza kilichokuwa kinaendelea, akapata stori kamili. Haraka sana kwa maagizo ya Sokoine ukaundwa utaratibu wa kuhalalisha daladala, ambazo wakati huo walipaswa kuilipa UDA. Nafikiri alifanya kitu kikubwa ambacho siamini kama kilikuwa katika ratiba za Mwalimu.

Nilikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam wakati huo. Maji yalikuwa yanakatika ovyo kwa wiki kadha pale. Na tulikuwa na viongozi wa serikali ya wanafunzi ambao wengine sasa hivi wana nyadhifa za juu sana hapa TZ. Viongozi hao hawakushinikiza utawala wa chuo kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo. Utawala wa chuo, nadiriki kusema, haukuwa na interest yoyote ya kulitatua pia. Maghorofani kule, hebu fikiria hakuna maji kwa mwezi.

Sokoine alianza masomo ya uzamili pale chuoni. Siku moja akaomba aoneshwe maliwato. Ilikuwa kasheshe. Hatimaye akaoneshwa hali halisi. Akawaita wahusika wa chuo, wizara ya elimu na wizara ya maji. Mara moja tukaona matanki ya maji yamemwagwa pale mlimani. Haraka sana kazi ikaanza ya kujenga tanki lile lililo nyuma ya Hall 4. Mabomba yakajengwa kuunganisha na Ruvu Chini.

Ukweli ni kwamba alikuwa mtu ambaye alikuwa tayari kufanya kazi kutatua matatizo ya wananchi. Wengine tuliguswa moja kwa moja na utendaji wake. Doa katika utendaji wake hasa linatokana na kampeni ya wahujumu uchumi ambayo kwa maoni yangu ni kwamba iliendeshwa vibaya na watu nchini kote na pia hakupata kuungwa mkono ipasavyo katika seriikali ya Mwalimu. He was like a lone ranger. There were other people whose performance in that office was mediocre, but most certainly Sokoine was not one of them.
Mengine uliyosema hapa si kweli. Tanki kubwa la maji Chuo Kikuu cha DSM lilijengwa kwa mradi wa 'Waswiss' miaka ya 90 baada ya kifo cha Sokoine, na wala maji hayakuunganishwa Ruvu moja kwa moja
 
Back
Top Bottom