Sokoine was not a hero, Salim was...

Sokoine was not a hero, Salim was...

KVM hata mitumba huko inakotoka inashonwa, lakini inashonwa kwenye viwanda bora mashine za kisasa na ubora wa vitambaa vinavyotumika unakuwa wa hali ya juu sana. Tanzania tulikuwa na kiwanda cha kushona Jeans kilikuwa kinaitwa Ubungo Garments kilikuwa kinauza nguo zake mpaka Marekani, sasa hivi kimegeuzwa kuwa Ofisi za wanaharakati wa kupigania haki za kijinsia!

Vile vimashine vinavyoitwa Butterfly ambavyo vimeenea kwa washonaji wetu Bongo vinatia kinyaa kabisa. Hizo mashine tunazoita za kisasa kama Juki n.k. hazina bei za ajabu hata kidogo. Tanzania imejaa vitu vingi sana vya gharama kuliko hata hizo cherehani za bei ya juu.

Kile kiwanda cha Ubungo Garments kama nakumbuka vyema kilikuwa ni SU. Kilikuwa kinachukua hata vijana waliokuwa wanamaliza JKT. Walikuwa na tenda ya kupeleka nguo Marekani - Jeans na Makaptula. Lakini kama zilivyo SU zote kikajifia kwa vile walikuwa wanashindwa kulinda Standards.

Jiulize kiwanda cha maturubai Morogor kimeishia wapi? Kile kiwanda kilipewa mpaka tenda ya ku-supply maturubai kwenye jeshi la Marekani. Wakafilisika bila sababu ya maana.

Nimebahatika kutemblea Bangkok mara kadhaa. Hizo nguo tunazokwenda kununua kule Thailand hazishonwi na viwanda vikubwa bali na viduka vidogo vidogo kama vile vilivyopo Mwenge. Hapa nazungumzia masoko kama Indra Market pale Bangkok. Wao wameweza sisi tunashindwa nini?

Kwa maoni yangu narudia tena ni bora kabisa kupiga marufuku uuingizaji wa mitumba Tanzania. Na tukipandisha kidogo kodi ya nguo zilizoshonwa watu wataweza kuanza kushona nguo kwa ushindani. Watu binafsi siyo mashirika.

Ni aibu kuona mpaka leo hii tuanaagiza nje mashati ya watoto wa shule. Kweli yanatushinda kushona? Mbona zamani zile tulikuwa na kiwanda cha Gossage kule Tanga amabcho kilikuwa kinavuma Afrika Mashariki nzima?
 
usikurupuke hovyo kama Pombe.
hebu fanya research kazi ya kutengeneza sera ni ya nani?
mmesoma shule gani nyie watu??

[h=1]NHS London chairman quits over government policy change

The chairman of NHS London has resigned after stating his vision of healthcare delivery had "little in common" with that of the new government.
[/h]In a letter to the health secretary Andrew Lansley, Sir Richard Sykes said he thought his work had made real improvements for Londoners.
Other NHS London board members may also leave, Sir Richard also claimed.
Mr Lansley said he was sorry that Sir Richard did not wish to lead NHS London in developing improvements.
The news follows the government's announcement last week that it was ordering NHS London to scrap its plans for changing the way hospitals and GPs worked in the future.
[h=2]Healthcare vision[/h]However, the new government says it wants the plans re-drawn - with more input from patients and doctors.
In his letter, Sir Richard said: "I have reflected on what you said and concluded that our visions of healthcare delivery bear so little in common that it would make no sense for me to continue in this role.
"I am, therefore, writing to give notice of my resignation from this office, with effect from 7 July."
Sir Richard, who was appointed to the role in 2008, also said that he had "relished" the task of delivering change as outlined by the Healthcare for London report.
Responding, Mr Lansley said that the Healthcare for London approach should be to set out a range of innovative and challenging solutions for how to improve quality of care.
He said: "Neither the government nor NHS London should dictate decisions made. The decisions that patients make through choice, and which GPs make through commissioning, should not be pre-empted from on high."


Link: NHS London chairman quits over government policy ... - BBC

Wewe unadhania kazi ya kutengeneza sera niya mtu mmoja au wawili? Unadhania kama ni waziri ni yeye anakaa na familia yake na kuunda sera?!
 
kazi ya kuwatimua watendaji na kuacha sera mbovu ziendelee kutamalaki ni kazi ya mfalme juha.
Pombe atafukuza wakurugenzi wote kila kukicha na hakuna marekebisho yoyote yatakayopatikana kwakuwa tatizo ni sera na sio watendaji.

Bohari kuna dawa lakini wagonjwa wanaambiwa wakanunue dawa hizo hizo walizoandikiwa.
Mnasema ni sera, sera ya kuwanyima dawa wagonjwa? Au alitakiwa afanye nini na kuna wagonjwa likuki wakisubiria matibabu?
Mlicheka na JK ila zama hizo sasa zimepita, bora mfanye kazi tu!!
 
Kwangu mimi ushauri wa Dk. Salim kwa Nyerere haukuwa mzuri, na ndio uliotufikisha hapa-viwanda vya ndani vimekufa. Lkn kama tungekomaa hivohivo na sisi tungetoka kwani tungelazimika kuendelea kuzalisha Zaidi kupitia viwanda vyetu mwishowe tungeweza ku compete ktk soko la Dunia. Mfano wa nchi iliyokomaa ni India
 
Kwangu mimi ushauri wa Dk. Salim kwa Nyerere haukuwa mzuri, na ndio uliotufikisha hapa-viwanda vya ndani vimekufa. Lkn kama tungekomaa hivohivo na sisi tungetoka kwani tungelazimika kuendelea kuzalisha Zaidi kupitia viwanda vyetu mwishowe tungeweza ku compete ktk soko la Dunia. Mfano wa nchi iliyokomaa ni India

Umeongea.. Umeongea vema sana, SAS alitupoteza, ila Mwalimu Na Moringe Na Sera ya dhati ya ujamaa walikua wanatupeleka hatua ya juu kama tu, tungekomaa.

M.A.P Jkn Na Ems
 
Nchi ya wakatoliki hii .... Mfumo huu unajali zaidi maslahi ya Vatican zaidi ya wananchi wa Tanzania ... Jiulize nani ni beneficiaries wa madini yetu ? kwanini walioingia huo mkataba ni wakatoliki pekee ?... So far katika uteuzi AG na Moi ... wote wamechukua wakatoliki na mafungu yametolewa ... Ndo maana Kimei ameoona upuuzi tu ngoja na yeye achangie kanisa lake ...
 
mie napita tu ndio kwanza nilikuwa primari nikivaa nguo za kumzika idd amini dada , asante kwa kumbukumbu lakini kulinganisha marehemu na aliye hali haijakaa sawa.
 
The Boss, nenda tu moja kwa moja kwenye hoja yako," Magufuli ni Sokoine, hatatoa suluhu ya matatizo ya Tz".Sikutegemea tu hizi propaganda kwa mtu kama wewe, it's too low kwako. TISS ongezeni tu ulinzi wa Magufuli, waswahili washaanza uchuro wao na hawachelewi kweli kumuua, wa Tz ni watu wa ajabu sana.



Kidoogo nimepata mwanga,kumbe inawezekana thread haina nia ya kuwazungumzia hao watajwa.ngoja niendelee kufuatilia.
 
Last edited by a moderator:
Sokoine will always be a good and TRUE leader. Namkubali EL lakini haingii hata 0.5. Magufuli akae mbali kabisa
 
Watu wa Dar bwana mnazungumza matatizo ya Dar as if Dar zama hizo ilikua tanzania pekee.... mimi si msomi kabisa ila nilibahatika kuwa katika zama hizo japo nilikua bado kinda kama la miaka 9 kumi hivi.... nayakumbuka maduka ya kaya, bado nazikumbuka katambuga na viloba ya sandarusi baadhi ya watu wakijisitiri navyo..... nakumbuka suruari za kodrai toka kenya zikiuzwa kwa magendo... nakumbuka sana tukiogea sabuni ilula na kujipaka pia kama lotion na kuna wakati hata sabuni hiyo ilikosekana...nazikumbuka foleni za sukari na bidhaa nyingine muhimu.....bado naikumbuka misemo ya '' shati la mikono mirefu, propoza, mwendo wa kuruka nk. nakumbuka nikiwa shule na baada ya SAS kuingia ndio walau tukavaa viatu toka bora enzi hizo zikiitwa asante salimu.... nakumbuka mengi sana ila sina wa kumlaumu zilikua zama zile na leo tuna vitu chekwaaaaa Alhamdulillah
 
Historia Ya NCHI hii Sio ile tulioisoma na tunayoendelea Kuisoma kwenye Vitabu.

Historia ya Tanzania Haipo na Haitakuwepo Milele Kwa kuwa tuna Uficha Ukweli wa Historia Yetu Iliyotukuka na Kushabikia Ile Iliyoandikwa na Kuchapishwa kwenye Vitabu.

Daima Mungu ndio Ataujua Ukweli Kwa Wote kwamba ni nani Ambaye Alikuwa bora na Shujaa Wa Kweli lakini Kwa Ukweli Wa Historia Yetu...

SITAKI KUA MNAFIKI NAIPINGA NA NITAIPINGA MILELE. UHALISIA HAUKUWA HUU TUNAO USOMA

BRING BACK OUR TANGANYIKA
 
Sokoine zaidi, hao walioruhusu mitumba ndo wamefanya uchumi wetu ufe, utaruhusu vipi vitu vya nje ile hali hamna uwezo wa kushindana.Ndo tunayoyaona sasa, hata chop stick inabidi tuagize china, maana tumekuwa tegemezi na maarifa ya kuendesha viwanda yalikufa.
 
I beg to differ, Sokoine alikuwa na courage ya kum face Nyerere, ni kiongozi pekee wakati ule ambaye angerudi kwa Mwalimu hata mara tatu hadi Mwl amwelewe.
 
Watu wa Dar bwana mnazungumza matatizo ya Dar as if Dar zama hizo ilikua tanzania pekee.... mimi si msomi kabisa ila nilibahatika kuwa katika zama hizo japo nilikua bado kinda kama la miaka 9 kumi hivi.... nayakumbuka maduka ya kaya, bado nazikumbuka katambuga na viloba ya sandarusi baadhi ya watu wakijisitiri navyo..... nakumbuka suruari za kodrai toka kenya zikiuzwa kwa magendo... nakumbuka sana tukiogea sabuni ilula na kujipaka pia kama lotion na kuna wakati hata sabuni hiyo ilikosekana...nazikumbuka foleni za sukari na bidhaa nyingine muhimu.....bado naikumbuka misemo ya '' shati la mikono mirefu, propoza, mwendo wa kuruka nk. nakumbuka nikiwa shule na baada ya SAS kuingia ndio walau tukavaa viatu toka bora enzi hizo zikiitwa asante salimu.... nakumbuka mengi sana ila sina wa kumlaumu zilikua zama zile na leo tuna vitu chekwaaaaa Alhamdulillah

Katika hivyo vitu chekwa Kiasi gani tunatengeneza wenyewe
 
The Boss

Salim alikataa kuwa Rais akaona bora kuwa katibu mkuu wa umoja wa afrika, hilo tu lilimchafua.

Salim hajawahi kukataa kuwa rais wa Tanzania isipokuwa alikubali kugombea mwaka 1985 ndani ya chama akiwepo Kawawa na Mwinyi. wakati huo chaguo na kipenzi cha Nyerere alikuwa Salim hivyo ili kurahisisha mchakato na ili kufanikisha adhma hiyo ukatengenezwa mpango Kawawa na Mwinyi wajitoe ili kumpisha Salim aonekane amepita bila kupingwa mpango ambao ulifanikiwa nusu kwa Kawawa kuondoa jina lake na baadae akawa anasubiriwa Mwinyi naye afanye hivyo. kutokana na minyukano ya kisiasa iliyokuwepo bara na visiwani ndipo walipotokea watu na kumtonya Mwinyi asijitoe kwani wao wamepanga kumwadhibu Mkuu wa nchi hivyo watamchagua yeye awe rais. mpaka inafika asubuhi wakati wa maandalizi ya vikao vya uteuzi ndani ya chama bado Mwinyi sio tu kwamba hakuwa amejitoa bali hakuonyesha dalili ya kutaka kuliondoa jina lake katika kinyang'anyiro hicho na ndipo ilipoamriwa demokrasia iamue mgombea wa urais kati ya Mwinyi na Salim. Inasemekana kama sio kina Getrude Mongela na wenzie leo hii rais wa awamu ya pili angekuwa anatajwa kama Salim Ahmed Salim. Hii ndio fimbo aliyowahi kuchapwa Mwl Nyerere na CCM na hakika ilimuuma. Sokoine is my favourate.
 
Wengi hawakuwepo wakati huo wanafata wanayoyasoma au kuyasikia ambayo mengi yamebadilishwa uhalisia wake.

A question to you, why now?

Sifa/maelezo aliyotoa mtoa mada kuhusu Sokoine zinafanana na za kiongozi wetu wa sasa: mtiifu, implementer as opposed to a strategic thinker, nyapara etc. On timing: labda mtoa mada anataka contextualise sifa za kiongozi mkuu wa sasa aliyeanza kazi yake hapo majuzi.
 
Mimi wote nimesoma kwenye vitabu na kusimuliwa na watu mbalimbali waliokuwepo enzi hizo...hakika sokoine ni MZALENDO NAMBA MBILI BAADA YA NYERERE..
 
Back
Top Bottom