Nikiri toka mwanzo mimi ni mshabiki mkubwa wa Sokoine. I have very fond memories. Sitapenda kufanya comparison na watu wengine au mawaziri wakuu wengine. Lakini nikiangalia anecdotes fulani, ninashuhudia kwamba Sokoine alikuwa mfano bora wa kiongozi. Si lazima watu wahusike na mambo yale yale ili tukubali nafasi zao katika historia.
Wakati wa Nyerere huo, usafiri Dar es Salaam ulikuwa umehodhiwa na serikali hasa kwa kutumia UDA, na pengine kidogo COCABS. Kama mleta uzi alivyosema, biashara kubwa za binafsi na hata ndogo sehemu nyingine zilipigwa vita. Jiji la Dar liliendelea kupanuka wakati mabasi ya UDA yakipungua. Sokoine, Waziri Mkuu wakati huo, alishuhudia hilo siku moja alipenda Ubungo pale Maji wakati huo ndiyo kituo, akaona saa 4 asubuhi pamesheheni watu wakisubiri UDA zinazokuja zimeshajaa toka Magomeni. Pale zinageuza tu. Kwa mbali kule watu walikuwa wanakimbilia mabasi ya watu binafsi yaliyokuwa yakisomba watu kuwapeleka makazini kinyume cha sheria kwa nauli ghali sana wakati huo ya Dala (lile gwala la Sh. 5 lilivyoitwa wakati huo). Ndivyo zilivyoanza daladala. Nauli ya UDA wakati huo ilikuwa Sh 1.50. Alipouliza kilichokuwa kinaendelea, akapata stori kamili. Haraka sana kwa maagizo ya Sokoine ukaundwa utaratibu wa kuhalalisha daladala, ambazo wakati huo walipaswa kuilipa UDA. Nafikiri alifanya kitu kikubwa ambacho siamini kama kilikuwa katika ratiba za Mwalimu.
Nilikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam wakati huo. Maji yalikuwa yanakatika ovyo kwa wiki kadha pale. Na tulikuwa na viongozi wa serikali ya wanafunzi ambao wengine sasa hivi wana nyadhifa za juu sana hapa TZ. Viongozi hao hawakushinikiza utawala wa chuo kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo. Utawala wa chuo, nadiriki kusema, haukuwa na interest yoyote ya kulitatua pia. Maghorofani kule, hebu fikiria hakuna maji kwa mwezi. Sokoine alianza masomo ya uzamili pale chuoni. Siku moja akaomba aoneshwe maliwato. Ilikuwa kasheshe. Hatimaye akaoneshwa hali halisi. Akawaita wahusika wa chuo, wizara ya elimu na wizara ya maji. Mara moja tukaona matanki ya maji yamemwagwa pale mlimani. Haraka sana kazi ikaanza ya kujenga tanki lile lililo nyuma ya Hall 4. Mabomba yakajengwa kuunganisha na Ruvu Chini.
Ukweli ni kwamba alikuwa mtu ambaye alikuwa tayari kufanya kazi kutatua matatizo ya wananchi. Wengine tuliguswa moja kwa moja na utendaji wake. Doa katika utendaji wake hasa linatokana na kampeni ya wahujumu uchumi ambayo kwa maoni yangu ni kwamba iliendeshwa vibaya na watu nchini kote na pia hakupata kuungwa mkono ipasavyo katika serikali ya Mwalimu. He was like a lone ranger. There were other people whose performance in that office was mediocre, but most certainly Sokoine was not one of them.