Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,920
- 30,263
SOKO LA KARIAKOO KUANZIA UPYA WAKE MWANZONI MWA MIAKA YA 1900
Sisi tuliozaliwa miaka ya 1950 tumelikuta Soko la Kariakoo kama linavyoonekana katika picha ya tatu na ya nne.
Nikiangalia picha ya mwanzo ya Kariakoo akili yangu inanipeleka katika nyumba ambazo nyingine mimi zinanihusu na nyingine nawafahamu wenyewe najiuliza kama kipindi hicho zilikuwa zipo zimekwishajengwa?
Jibu ni kuwa nyumba hizo zilikuwapo kabla ya soko na sababu ni kuwa baadhi ya baba na shangazi zangu mathalan wamezaliwa katika nyumba yetu ya Swahili miaka ya 1920.
Hawa wameliona soko katika upya wake na wakalishuhudia soko likivunjwa na kujengwa soko jipya la Kariakoo hili lililopo hivi sasa kabla halijaungua.
Nyumba za jirani sana na Kariakoo ambazo mimi nazikumbuka ingawa zilikuwapo nyingi ya kwanza kabisa ni nyumba ya bibi yangu Bi. Deborah Mgone (1890 - 1995) ambayo iko Mtaa wa Swahili.
Bi. Deborah ni mtoto wa bibi yetu mkuu Bi. Catherine Hamadi ambae sisi tumezaliwa tumemkuta hapo kwenye nyumba ya Mtaa wa Swahili.
Yeye kafariki 1969 akiwa na umri kwa kukisia labda miaka 90.
Nina kumbukumbu nyingi na Soko la Kariakoo lile ambalo mimi nililikuta wakati nazaliwa.
Ilikuwa mwaka wa 1956 au 1957 nikipelekwa kushinda kwa mama yangu mkubwa Bi. Mwanaisha Bint Mohamed Mtaa wa Nyamwezi na Narung'ombe.
Nyumba hii ilikuwa ya Mzee Kasembe ikatazamana na nyumba ya akina Hariz ambako kulikuwa na mnada maarufu katika mji wa Dar es Salaam - Hariz Auction.
Mnada huu bado upo hadi hivi sasa.
Nyumba ya Mzee Kasembe haipo.
Leo hapo ndipo lilipo lango kuu la kuingilia Shimoni Kariakoo.
Kulikuwa na mwendawazimu jina lake Boimanda na watoto tukimuogopa sana.
Matembezi ya Boimanda siku zote yalikuwa pale sokoni na watu wakimtisha Boimanda kwa kumwambia kuwa askari wa kodi wanakuja na yeye atatoka mbio kukimbia ovyo.
Ilikuwa katika kutishwa kama hivi ndipo alipovamia meza ya biashara ya mtu mmoja anaitwa Manyanga na yeye kwa hasira ya kumwagiwa vitu vyake akampiga kichwa Boimanda akafa palepale.
Kisa hiki kikawa maarufu hadi zikatoka khanga na jina la Boimanda.
Kumbukumbu yangu nuyingine ni ya Ayubu Kiguru shabiki mkubwa sana wa Sunderland (sasa Simba).
Ayubu mguu wake mmoja ulikuwa na athari na hii ndiyo sababu ya yeye kuitwa jina hilo "Ayubu Kiguru."
Nikimjua Ayubu kwa karibu sana na sababu ni kuwa alikuwa na ubao wa biashara pale sokoni jirani na ubao wa mjomba wangu Bwana Khamis Salum.
Soko la Kariakoo enzi hizo lilikuwa moja ya vituo vya ushabiki mkubwa wa mpira Dar es Salaam kati ya Sunderland na Yanga.
Sijui kama hali hii iliendelea hadi miaka hii.
Yanga na Sunderland walitawala soko na Yanga washabiki wao wengi walikuwa na biashara ya kuuza samaki kiasi ikawa watani wao wakiwaita Yanga, ''Wauza Samaki.''
Siku ya mechi ya Sunderland na Yanga moto ulikuwa unawaka sokoni pale toka mapema asubuhi.
Ushabiki huo utaendelea kwa juma zima takriban baada ya mechi.
Sasa ikitokea kuwa Yanga imefungwa na Sunderland washabiki wa Yanga walikuwa tabuni kwa juma zima pale sokoni wakipigwa makombora na Ayubu Kiguru.
Namfananisha Ayubu na Haji Manara na kwa kweli siwezi kuamua nani amemshinda mwenzie kwa kipaji cha kupanga maneno.
Ayubu alikuwa na uwezo wa yeye peke yake kuwanyamazisha Yanga wote pale sokoni.
Ayubu alikuwa bingwa wa maneno ya kejeli na kebehi lakini katika namna ambayo mtu hawezi kughadhibika bali atakuwa yeye anacheka tu.
Ilikuwa Sunderland ikiwafunga Yanga na kuchukua kikombe Ayubu atakuja sokoni na kikombe kile na kukiweka mbele yake anauza nyanya zake huku amevaa jezi no 6 ya Hamisi Kilomoni.
Hapo siku hiyo kutwa nzima washabiki wa Sunderland watapita kwa Ayubu kuja kutunza.
Lakini kubwa kabisa linalostahili kuhifadhiwa katika historia ya Soko la Kariakoo ni historia yake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Wakati huo Market Master alikuwa Abdul Sykes na Nyerere alikuwa hapungui hapa khasa baada ya kuacha kazi ya ualimu na kuja kuishi na Abdul Sykes nyumbani kwake Mtaa wa Stanley na Sikukuu.
Huu ulikuwa mwaka wa 1955.
Hapo sokoni ndipo Nyerere alipofahamiana na Shariff Abdallah Omar Attas na Mshume Kiyate pamoja na wazalendo wengine waliokuwa mstari wa mbele katika TANU.