Soko la Hisa la Dar es Salaam na orodha ya makampuni yaliyosajiliwa

Ivi kwa nn? Makampuni ya simu kama tigo, vodacom, Airtel, zantel na ttcl
Yanapata faida kubwa lakini ayapo katika soko la hisa
TTCL tayari wapo DSE...hawa wengine nadhani bado wanajipanga, lakini pia inawezekana kuwa wamekiuka agizo la Raisi....
 
naomba kujua hivi hisa zinazo uzwa primary kama (IPO) huwa zinatangazwa wapi mana DSE mbona hawahusiki ?
Hisa za IPO zinatangazwa na CMSA ( Capital Market and Securities Authority) na baada ya hapo kampuni inakuwa listed kwenye stock market na DSE. na hisa hizi huuzwa katika stock brokerage firms zote zilizopo nchini.

Sasa zitakapotangazwa fika katika ofisi husika. Omba kitu kinaitwa prospectus itakupa mchanganuo mzima wa bei ya hisa, management ya kampuni, vitabu vya hesabu na wana plan kwenda ku invest hiyo pesa wapi.

Hii itakupa mwanga wa unapotaka kuweka fedha zako.
 
TTCL tayari wapo DSE...hawa wengine nadhani bado wanajipanga, lakini pia inawezekana kuwa wamekiuka agizo la Raisi....
Mkuu so far hakuna kampuni ya simu iliyokuwa listed na DSE mpaka sasa. Vodacom ndio wapo katika hatua ya mwisho kupata approval ya CMSA kuingia sokoni.
 
Wadau nataka kununua hisa, sina uzoefu sana Zaid ya elimu ninayo ipata kupitia hapa jamii forum, please mwenye uelewa anijuze

-kampuni gani ni zuri kununua hisa kwa sasa
-kwa pesa kama million 5(mfano) ni vzuri kununua hisa sehemu moja au zaidi ya moja
-kuna hatari kufanya manunuzi ya hisa kwa njia ya mtandao (*150*36#)
Naombeni msaada wenu wakuu
 

Faida ya soko la hisa ni kupata gawiwo na pia kuuza hisa zako pale zinapokuwa na thamani ya juu kuliko bei uliyonunulia.

Wafaidika wakuu wa uwekezaji katika soko la hisa ni wanne..

1. Kampuni husika,inapoingia sokoni kwa mara ya kwanza sababu inapata mtaji isillipia riba.
2'. Wamiliki wa kwanza ambao huuza hisa zao sokoni.
3. Wawekezaji wakubwa.
4.Madealer au mabroker kwenye soko la hisa.

Kusema mtu anaweza kukushauri kuwekeza fedha zako kwenye soko la hisa,tena milioni tano itabidi akuhoji ili akuelewe vizuri unachokitaka.
 
kwa mfano nimenumua hisa za voda leo kwa m pesa je nifanyeje kujua salio langu la hisa
 
Ivi katika awa mawakala wa mitaji na katika ishu ya kuifadhi pesa katika mtindo wa dhahabu wana husika
 
Bongo Kuna matapeli wa aina nyingi. Hawa DSE na CMSA hawataki kutoa taarifa za TCCIA na Vodacom share kuwa listed.
Ni jambo rahisi tu toa maelezo kwanini TCCIA na Vodacom ambazo tarehe zilizoainishwa kua zinakua listed hazijawa listed hadi sasa.


DSE na CMSA walitakiwa kuwa na Uzi humu special thread ila ni wavivu sana na kila ck zitaendelea kuporomoka kwa uchumi huu.


Same to BOT ni wavivu sana
 
CDS zinaweza kutumika zaidi ya Kampuni moja?
 
Nimeangalia hisa za Acacia hapa Dar es salaam stock exchange ni Tshs 7610 sasa hivi na nimeangalia London stock exchange ni 155.60 ni £1.5560 ( sina uhakika kama hapa nipo sawa, naomba kusahihishwa) kwa share.

Ukibadilisha hiyo £1.5560 Kwenye Tshs ni 4576.45. Hii ni tofauti ya Tshs zaidi ya 3000. Kwanini tofauti ni kubwa hivyo. Ni wapi sijaelewa?

Na ukinunua hisa za kampuni fulani DSE ni sawa na kununua hisa hizo hizo NYSE au LSE?
 
Ukitaka kununua hisa ni kitu gani hasa unatakiwa kuangalia, "volume", "volume average", "high and low", ............?
 
Ukitaka kununua hisa ni kitu gani hasa unatakiwa kuangalia, "volume", "volume average", "high and low", ............?

Ukitaka kununua angalia volume, volume ni inakuambia hizo hisa zinakuwa demanded kiasi gani,
High volume inamaanisha watu sokoni wanazinunua sana hivyo possibility ya kupanda bei ni kubwa.

Low volume inamaanisha hazinunuliwi sana, na zinaweza shuka bei soon
Pia volume ikiwa kubwa inamaanisha liquidity ya hisa hizo ni kubwa ambapo inakupa urahisi wa kuuza na kununua muda wowote

High volume pia inamaanisha bei yake haibadiliki ghafla ila steadily hii inakupunguzia shock.
 
Naomba kueleweshwa, unaweza kushindwa kuuza shares zako za kampuni ambayo gharama ya shares zake haijabadilika au inaongezeka?

Nimenunua shares kwenye LSE ni wonder kama baadae nitashindwa kuziuza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…