Soko la Hisa la Dar es Salaam na orodha ya makampuni yaliyosajiliwa

KeyserSoze

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Messages
2,962
Points
2,000

KeyserSoze

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2014
2,962 2,000
1. Hisa ni nini?

Hisa ni sehemu ya umiliki wa kampuni. Hivyo hisa moja inawakilisha asilimia ndogo ya umiliki katika kampuni. Kama kampuni ina hisa milioni moja na mwekezaji anamiliki hisa 10,000, mwekezaji huyu anamiliki 1% ya kampuni. Mwekezaji anayenunua hisa basi ananunua haki ya kumiliki kampuni. Stahili za mwenye hisa ni pamoja na kushiriki katika kutoa maamuzi ya kampuni katika mkutano mkuu wa wanahisa na kupata gawio litokanalo na faida. Ana haki pia ya kuuza hisa zake kwa faida pale ambapo kuna ongezeko la thamani ya hisa.

2. Gawio ni nini?

Gawio ni malipo yanayofanywa na kampuni kwa wanahisa kutokana na faida ya kampuni. Malipo haya yanapendekezwa na wakurugenzi na kuidhinishwa na mkutano mkuu wa wanahisa. Gawio linaweza kulipwa kutokana na faida ya mwaka husika au malimbikizo ya faida za nyuma. Gawio linaweza kulipwa kwa fedha taslim au kwa kuwaongezea hisa wanahisa.

3. Hatifungani ni nini?

Hatifungani ni hati ya deni ambalo kampuni au serikali huwakopa wawekezaji kwa makubaliano maalumu na kuwalipa riba na marejesho baada ya kupevuka kwa hatifungani hiyo. Mwenye hatifungani anastahili kulipwa riba (kwa kawaida ni kila miezi sita) na kurudishiwa mtaji wake hatifungani ikishapevuka. Pale ambapo kampuni inafilisika, wanaomiliki hatifungani wana haki ya kulipwa pesa zao kabla ya wale wanaomiliki hisa.

4. Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ni nini?

Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) ni taasisi ya serikali iliyo chini ya Wizara ya Fedha na Uchumi iliyoanzishwa na Sheria namba 5 ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ya mwaka 1994 ili kusimamia na kuendeleza masoko ya mitaji hapa Tanzania.

Majukumu makubwa ya Mamlaka yameainishwa kwenye kifungu namba 10 cha Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana. Majukumu hayo ni pamoja na:

a) Kuanzisha na kuendeleza masoko ya mitaji Tanzania;
b) kuidhinisha uanzishwaji wa masoko ya hisa na mifuko ya uwekezaji wa pamoja, na kutoa leseni kwa wataalamu wa masoko ikiwa ni pamoja na madalali, wachuuzi, wawakilishi wao, washauri wa uwekezaji, n.k.
c) Kusimamia masoko ya mitaji pamoja na wataalamu wote wanaohusika na utendaji wa masoko hayo; na
d) Kuishauri Serikali kwenye masuala yote yahusuyo masoko ya mitaji na dhamana.

5. Soko la hisa la Dar-es-Salaam ni nini?

Soko la Hisa ni soko ambalo huwezesha hisa, hatifungani na dhamana zingine zilizoorodheshwa katika soko hilo kuuzwa na kununuliwa. Bidhaa hizi huitwa dhamana au kwa lugha ya kigeni (securities). Soko la hisa hapa Tanzania limeanzishwa mwaka 1996 kama kampuni binafsi yenye dhima (limited by guarantee); kwa maana ya kwamba wanachama wa soko hawatakiwi kuweka mtaji wowote. Mwanzoni kulikuwa na wanachama 11 ambao ni madalali wa soko la hisa pamoja na wawekezaji wakubwa (Institutional investors). Soko la hisa lilianza kazi zake rasmi mwezi April mwaka 1998 wakati hisa za TOL Ltd zilipoorodheshwa na kuanza kuuzwa na kununuliwa. Soko la hisa ni soko ambalo linajiendesha lenyewe likisimamiwa na Baraza la Wadhamini (DSE Council). Kwa sasa lina wanachama 27.

6. Kuna tofauti gani kati ya Soko la Hisa la Dar-es-Salaam (DSE) na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)?

Mamlaka (CMSA) ni taasisi ya serikali, ambayo ilianzishwa na Sheria ya Bunge ili kusimamia masoko ya mitaji na dhamana. Mamlaka imepewa jukumu la kuanzisha na kusimamia masoko haya nchini. Katika kutekeleza wajibu wake, Mamlaka ilianzisha Soko la Hisa la Dar es salaam mwaka 1996 na kusimamia uendeshaji wa soko hilo kwa mujibu wa sheria.

Pia Mamlaka ndiyo inayotoa leseni kwa washiriki wa soko la hisa kama vile madalali, washauri wa uwekezaji na kuidhinisha uanzishwaji wa masoko ya hisa. Mamlaka pia ina mamlaka kwa mujibu wa Sheria kusimamia utendaji wa soko la hisa kwa kutoa maelekezo pale inapobidi kwa Baraza la Wadhamini la DSE.


Wajumbe wa Bodi ya CMSA huteuliwa chini ya kifungu cha 6 kifungu kidogo cha 3 cha sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhaman Tanzania. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania humteua mwenyekiti na wajumbe wengine 5 huteuliwa kutokana na nyadhifa zao kama Gavana wa Benki Kuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Msajili wa Makampuni na afisa Mtendaji wa Mamlaka.

Wajumbe wengine 4 waliobaki huteuliwa na Waziri wa Fedha kwa kuzingatia utaalamu wao kwenye fani ya sheria, uhasibu, fedha na uchumi. DSE inaongozwa na Baraza la Wadhamini (Wakurugenzi) ambao wako 10. Wadhamini hawa wanawakilisha taasisi za fedha kama mifuko ya pensheni, madalali wa soko la hisa, kampuni zilizoorodheshwa katika soko, mwakilishi wa umma wa wawekezaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE.

7. Ni nini faida ya kuwekeza kwenye hisa, hatifungani na vipande?

Kwa ujumla dhamana za fedha (hisa, hatifungani, vipande) ni rasilimali ambazo zinagawanyika na ni rahisi kuziuza kwa kiurahisi. Kutokana na urahisi huo, dhamana zinaweza kuwekwa rehani kwa ajili ya kupata mkopo kutoka taasisi za fedha.

Wawekezaji kwenye hisa wanapata gawio ikiwa kampuni itakuwa imepata faida. Wanahisa pia huweza kupata faida itokanayo na ongezeko la thamani iwapo bei ya hisa itaongezeka kwenye soko la hisa. Ongezeko la thamani ni tofauti ya bei ya kununulia hisa na bei ya kuuzia. Ikiwa bei ya kuuza ni ndogo kuliko bei ya kununulia, mwanahisa anapata hasara. Uwekezaji kwenye hisa hauna uhakika wa gawio kwa sababu gawio linategemea faida ya kampuni.

Kwa upande wa hatifungani, riba inayolipwa inajulikana tangu mwanzo kwa sababu ni asilimia ya deni lote. Riba inayolipwa inaweza kuwa ya kubadilikabadilika au isiyobadilika. Wawekezaji kwenye hatifungani wanaoamua kukaa nazo hadi zitakapopevuka wanajua kiwango cha faida yao tangu wanapowekeza. Hatifungani pia zina ongezeko la thamani.

Kwa upande wa vipande, faida inategemea aina ya mpango. Vipande ni sehemu ya umiliki kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja. Tofauti na hisa vipande vinajumuisha mseto wa uwekezaji wa vitega uchumi mbali mbali ambavyo fedha zilikusanywa kwa ajili ya uwekezaji wa pamoja zinawekezwa. Kama ni mapango wa kukua, mwekezaji anategemea kufaidika kutokana na kukua kwa thamani ya vipande. Wawekezaji wanatakiwa kujua kuwa bei ya vipande inabadilika mara mwa mara. Kama mpango wa uwekezaji wa pamoja ni wa mapato, mwekezaji anafaidika kutokana na mgao wa mapato ya mpango huu.

8. Ni zipi haki na wajibu wa wanahisa, wenye hatifungani na wenye vipande?

Mwanahisa Mwenye Hatifungani Mwenye Vipande
HAKI HAKI HAKI
Kuhudhuria na kupiga kura kwenye mikutano ya kampuni Ana haki ya kupokea mapato yake kama riba kulingana na mkataba Anamiliki mali za mpango na mapato yake
Anashiriki kwenye mgao wa faida ya kampuni Kampuni ikiwa na mapato ya kifedha, mwenye hatifungani ana kipaumbele kwenye madai kuliko wanahisa Ana haki ya kupata mgao wa faida ya mpango kutoka kwa meneja wa mpango
Ana haki ya kupata tarifa zote za kampuni kutoka kwa wakurugenzi wa kampuni Ana haki ya kupata tarifa zote za kampuni kutoka kwa wakurugenzi wa kampuni Ana haki ya kupata taarifa zote mpango kutoka kwa meneja wa mpango na haki za kukagua nyaraka zote za mpango
Ana haki ya kuuziwa hisa mpya kabla ya wawekezaji wengine ambao hawana hisa kwenye kampuni Hana haki ya upendeleo ya kuuziwa hisa mpya za kampuni Ana haki ya kuuziwa vipande vipya vya mpango kabla ya wawekezaji wengine ambao hawamiliki vipande vya mpango
Ana haki ya kuuza hisa zake kwenye soko la hisa kama kampuni imeorodheshwa Ana haki ya kuuza hatifungani zake kwenye soko la hisa kama hatifungani zimeorodheshwa Kwa mpango wa vipande uliofungwa ana haki ya kuuza wakati wowote katika soko la hisa. Ila kwa mpango wa vipande uliowazi ana khaki ya kuuza kupitia mdhamini au meneja wa mfuko, mfano CRDB na UTT Kwa vipnde vya Umoja.
MAJUKUMU MAJUKUMU MAJUKUMU
Ana kila sababu ya kujua uwekezaji wake unavyoendelea kwenye kampuni Ana kila sababu ya kujua uwekezaji wake unavyoendelea kwenye kampuni Ana kila sababu ya kujua uwekezaji wake unavyoendelea kwenye kampuni
Ana haki ya kupiga kura Hana haki ya kupiga kura Ana haki ya kupiga kura
Madeni ya kampuni yana ukomo kulingana na mtaji wake kwenye kampuni Madai yake yana ukomo kulingana na uwekezaji wake kwenye kampuni Madai yake yana ukomo kulingana na uwekezaji wake kwenye mpango

9. Toleo la awali lina maana gani?

Toleo la awali ni mauzo ya hisa na dhamana kwa umma kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kukusanya mtaji. Kwa lugha nyingine inajulikana kama IPO (Initial Public Offer) Mauzo hayo yana kipindi chenye ukomo. Baada ya hapo, kama mwekezaji anataka kuwekeza kwenye kampuni hiyo atatakiwa kwenda kwenye soko la pili kupitia madalali wa soko la hisa.

10. Kama mimi sio Mtanzania, ninaruhusiwa kununua hisa kwenye toleo la awali?

Kwa toleo la awali la ubinafsishaji wa hisa za Serikali kwenye mashirika ya umma kuna vivutio maalum kwa Watanzania. Wasio Watanzania hawaruhusiwi kununua hisa hizo. Kama ilivyo sera ya ubinafsishaji, Serikali imekuwa inatenga kiasi cha hisa kwa Watanzania wakati inapouza hisa kwa wawekezaji wa nje kupitia Tume ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC).

Kwa matoleo mengine ya awali Watanzania wanapewa kupaumbele wakifuatiwa na raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na hatimaye raia wengine. Kwa mujibu wa Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana kikomo cha wawekezaji wa nje kwenye masoko ya mitaji sii zaidi ya 60% ya hisa za kampuni. Katika kiwango hiki wawekezaji wa nje na wa ndani wanaruhusiwa kuwekeza. Kiasi cha 40% kinachobakia ni ajili ya wawekezaji Watanzania pekee. Uwekezaji kwenye dhamana za Serikali ni kwa ajili ya Watanzania pekee.

11. Je kama nitanunua hisa ya kampuni halafu kampuni ikafilisika nitapataje fedha zangu?

Siku zote uwezekano wa kupata hasara au hatari za uwekezaji zinaendana na umiliki wa uwekezaji huo. Wamiliki wa hisa wanategemea kupata gawio pamoja na kupanda kwa bei ya hisa zao. Vivyo hivyo, kama kampuni itapata hasara basi idadi ya hisa zako zitabaki vilevile ila thamani itapungua. Na iwapo ikitokea kampuni ikafilisika kabisa basi sheria inaelekeza kuwa kutakuwa na mfilisi. Mfilisi kwanza kabisa anapaswa kulipa madeni kwa kutumia fedha za mauzo ya mali za kampuni, na kama fedha hizo zitabaki, watalipwa wanahisa wa kampuni hiyo. Endapo fedha hazitabaki, ni hasara kwa wenye hisa.

12. Je ninapataje gawio langu?

Gawio ni faida ambayo analipwa mwanahisa iwapo kampuni imepata faida na kuamua tulipa sehemu ya faida kama gawiwo. Njia itumikayo kulipa inategemea na kampuni. Kampuni nyingi zinatumia Shirika la Posta pamoja na mabenki. Ni juu ya mwekezaji kuwasiliana na kampuni aliyowekeza na kutoa habari muhimu kama vile anwani ya posta pamoja na akaunti ya benki.

Kama malipo yatalipwa kwa kupitia njia ya posta basi utapata Hawala ya Posta kupitia anwani yako, na kama malipo yanafanyika kupitia kwenye akaunti ya benki basi utapata hundi au pesa zitaingizwa kwenye akaunti yako. Ni muhimu kutoa taarifa iwapo anwani au akaunti yako itabadilika. Kampuni nyingi zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa zinatoa gawio mara mbili kwa mwaka.

13. Je ninaweza kuhamisha miliki ya hisa zangu kwa mke au mume wangu?

Ndiyo, hisa zinahamishika. Hisa zilizoorodheshwa Soko la Hisa la Dar-es-Salaam zimehifadhiwa katika Hifadhi ya Dhamana, hivyo uhamishaji wa umiliki ni rahisi kuliko uhamishaji wa kutumia makaratasi na hati. Kwa kanuni za Soko la Hisa la Dar es Salaam, uhamishaji binafsi wa umiliki wa hisa huwezekana wakati dhamana haziko katika mnada. Hivyo uhamishaji wa umiliki wa hisa kutoka kwa mume kwenda kwa mke ni uhamishaji binafsi unaoruhusiwa.

14. Ninawezaje kununua au kuuza hisa zangu?

Kama unataka kununua hisa ambazo zinauzwa kwa mara ya kwanza (IPO) kuna mawakala maalum ambao huwa wamepewa wajibu wa kuuza hisa kwenye soko la awali. Mwekezaji anatakiwa kujaza fomu ya maombi na kukabidhi pesa kwa wakala kulingana na idadi ya hisa anazotaka kununua na atapewa stakabadhi pamoja na kikonyo cha fomu yako kama uthibitisho.

Kama mwekezaji anataka kunuua hisa kutoka katika soko la pili (DSE), basi itabidi awaone madalali wa soko la hisa. Atawaeleza mahitaji yake. Dalali atatoa ushauri lakini uamuzi ni wake.
Ufuatao ni utaratibu wa kuuza na kununua hisa kaitka soko la pili (DSE):-

Ununuzi

Mwekezaji anayetaka kununua hisa atafuata taratibu zifuatazo:
a) Wasiliana na dalali wa soko la hisa na kumweleza kusudio lako la kununua hisa
b) Jaza fomu maalum za kununua hisa na kulipia hisa unazotaka kununua
c) Dalali ataweka fedha kwenye akaunti maalum ya benki kwa ajili ya kununua na kuuza hisa za wateja
d) Dalali ataweka oda yako ya kununua hisa kwenye mfumo wa kompyuta wa soko la hisa akitumia namba maalum ya mteja.
e) Iwapo bei unayotaka kununulia hisa itafanana na bei ya mwekezaji mwingine anayetaka kuuza, basi atakuwa amekununulia hisa hizo. Mwekezaji atapokea cheti cha kuthibitisha kuwa ni mwekezaji kwenye kampuni hiyo.

Uuzaji

Mwekezaji anayetaka kuuza hisa atafuata taratibu zifuatazo:
a) Wasiliana na dalali wa soko la hisa na kumweleza kusudio lako la kuuza hisa
b) Kabidhi hati yako ya umiliki wa hisa kwa dalali
c) Dalali atahakiki umiliki wa hisa hizo kabla ya kuuza. Kama hisa haziko kwenye hifadhi ya hisa, dalali ataziweka kwenye hifadhi kabla ya kuuza
d) Dalali ataweka oda yako ya kuuza hisa kwenye mfumo wa kompyuta wa soko la hisa akitumia namba maalum ya mteja. Iwapo bei unayotaka kuuzia hisa itafanana na bei ya mwekezaji mwingine anayetaka kununua, basi atakuwa amekuuzia hisa hizo na mwekezaji atalipwa.

Kuna gharama za kushiriki kwenye soko la pili la hisa. Ushuru unaotozwa ni 2% kwa hisa zinazouzwa kwenye soko la hisa la DSM. Vilevile kuna gharama ya kushiriki kwenye soko la pili la vipande vya Mfuko wa Umoja ambavyo vinauzwa kupitia benki ya CRDB na Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT). Wanunuzi na wauzaji kwenye masoko ya pili hulipa ushuru huu. Kwa upande wa vipande, mwekezaji anatakiwa kulipa 1%. Vipande vya Umoja havijaorodheshwa kwenye soko la hisa la DSM kwa sasa. Mauzo na manunuzi kwa upande wa makampuni ambayo hayajaorodheshwa yana taratibu tofauti za mauzo ya hisa zao.

15. Nikiwa nje ya Tanzania nitanunuaje hisa?

Watanzania wanaoishi nje ya nchi wana fursa ya kuwekeza kwenye masoko ya mitaji hapa nchini kwenye masoko ya awali na pia kwenye masoko ya pili. Wanaweza kushiriki kwa kumchagua dalali wake ambaye atakuwa anamsaidia kuwekeza. Mwekezaji anatakiwa kuwa na mkataba na dalali wa kumsaidia kuwekeza akiwa nje ya nchi. Mkataba huo utabainisha jinsi ya kupokea fedha na namna ya kuidhinisha manunuzi au uuzaji wa hisa.

16. Madalali wa soko la hisa wanapatikana wapi?

Madalali wa soko la hisa kwa sasa idadi yao ni 6 na wote wapo Dar es Salaam. Lakini, kutokana na kukua kwa teknologia na utumiaji wa mawakala, wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali za nchi wanaweza kupata huduma ya madalali bila kulazimika kuja Dar es Salaam.

Ni kweli wawekezaji walio nje ya Dar es Salaam wanawekeza kwa gharama kubwa zaidi ukilinganisha na wenzao walio Dar es Salaam kutokana na muda, gharama za posta, gharama za kutuma au kutumiwa fedha n.k. Juhudi zinafanyika ili kuweza kuwafikishia Watanzania huduma hii kulingana na upatikanaji wa biashara na kukua kwa teknolojia kwa sababu kampuni za udalali zinaendeshwa kwa misingi ya kibiashara.

17. Kwa nini tunahitaji madalali ili kununua au kuuza hisa?

Kila soko lina taratibu zake, masoko ya mitaji yanahusisha fedha nyingi hivyo ni vyema kuweka taratibu zinazohakikisha uwazi na haki. Madalali hawa ni wataalam katika masoko haya. Wanasaidia kuuza na kununua hisa pamoja na kutoa elimu kwa wawekezaji. Kwa ufupi kuwepo kwa madalali kunawezesha kuwepo na utaratibu na mpangilio mzuri wa mnada na kunapunguza uwezekano wa vitendo vya udanganyifu ambavyo vingeweza kufanywa na wajanja wachache kama kila mtu angeruhusiwa kwenda moja kwa moja kwenye soko la hisa.

18. Kwa nini tulipe ada ya udalali?

Madalali wanatoa huduma kwa wateja wao kwa kuwasaidia kununua na kuuza hisa zao. Na zaidi ya hapo wanatoa ushauri wa ununuzi na uuzaji wa hisa na mambo mengine yahusuyo soko la hisa. Kutokana na huduma hiyo madalali wanaruhusiwa kwa mujibu wa sheria kutoza ada (Brokerage commission) ambayo ikichanganywa na ada ya Soko la Hisa (DSE) na Mamlaka (CMSA) haitakiwi kuzidi 2% ya thamani ya mauzo au manunuzi husika.

Mgawanyo wa ada ya manunuzi na mauzo ya hisa unakua kama ifuatavyo

Thamani ya Hisa (mauzo au manunuzi) Mgawanyo wa Dalali Mgawanyo wa CMSA Mgawanyo wa DSE Mfuko wa Fidia Jumla ya Ada Inayotozwa Ada ya Hifadhi ya hati ya hisa (CDS)
Kiasi kisichozidi TZS. 10 Milioni 1.7% 0.14% 0.14% 0.02% 2.00%
TZS. 100
Kiasi kisichozidi 40 Milioni 1.5% 0.14% 0.14% 0.02% 1.80% TZS. 100
Kiasi kinachozidi TZS. 50 Milioni 0.8% 0.14% 0.14% 0.02% 1.10% TZS. 100

19. Nini tofauti kati ya Dalali na Mchuuzi (broker and dealer)?

Mchuuzi (dealer) anaruhusiwa kununua hisa au dhamana nyinginezo kwa niaba yake mweneyewe (principal) na vile vile kwa ajili ya wateja. Dalali (broker) kwa upande mwingine haruhusiwi kununua hisa/dhamana kwa ajili yake. Yeye anafanya kazi kama wakala (agent) kwa niaba ya wanunuzi na wauzaji tu. Dalali anatakiwa kuwa na mtaji usiopungua milioni 10 na 30% kati ya hizo ikiwa ni fedha taslim au aina ya uwekezaji ambao unaweza kugeuzwa kuwa fedha kwa haraka. Mchuuzi anatakiwa kuwa na mtaji isiopungua milioni 20, 30% unatakiwa kuwa fedha taslim au aina ya uwekezaji ambao unaweza kugeuzwa kuwa fedha taslimu kwa haraka. Madalali na wachuuzi wanapewa leseni na kusimamiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) .

20. Nini umuhimu wa kuwa na Soko la Hisa nchini?

Soko la Hisa lina nafasi kubwa katika kukuza uchumi wa nchi kama vile:
Kusaidia makampuni kupata mitaji
Kusaidia wananchi kuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba
Kuongeza maeneo ambayo wawekezaji wanaweza kuwekeza
Ni kipimo cha hali ya uchumi wa nchi
Kusaidia kuongeza utawala bora na uwazi kwenye kampuni zilizoorodheshwa.
Kusaidia kubinafsisha mashirika ya umma.
· Kusaidia utambuzi wa bei halisi ya hisa
· Huwezesha umilikishaji wa hisa za kampuni kwa umma
· Kuwezesha uuzaji kwa urahisi wa hisa

21. Kwa nini linaitwa soko la hisa la Dar es salaam na sio soko la hisa la Tanzania?

Ni jina tu limechaguliwa kuonyesha kuwa soko hilo liko kwenye jiji la Dar es Salaam. Ingewezekana likaitwa soko la hisa la Tanzania bila kuathiri kitu chochote. Mfano soko la hisa lililoko Kampala Uganda linaitwa Soko la Hisa la Uganda na sio Soko la Hisa la Kampala.

22. Je, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana inashauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pia?

Ndiyo, Mamlaka inashauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

23. Kuna tofauti gani kati ya Hisa na Kipande?

Hisa ni sehemu ya umiliki katika kampuni. Na kipande ni sehemu ya umiliki katika mfuko wa uwekezaji wa pamoja kwa maana ya Amana ya Kikundi (Unit Trust Scheme). Hisa ni sehemu ya umiliki wa kampuni Fulani wakati kipande kinajumuisha mseto wa uwekezaji katika vitega uchumi mbali mbali.

24. Kuna tofauti gani kati ya kampuni na Mfuko wa Umoja?

Mpango wa uwekezaji wa pamoja kwa muundo wa kampuni ni mpango uliofungwa ambapo hauna fursa kwa mpango kununua vipande kutoka kwa wawekezaji mara baada ya toleo la awali kukamilika. Mpango huu una idadi maalumu ya hisa na vipande kwenye mpango.

Hisa na vipande vya mipango hii huuzwa kwenye masoko ya pili ya mitaji (huorodheshwa soko la hisa). Kama mpango haujaorodheshwa vipande vyake vianuzwa na kununuliwa kwenye soko lisilo rasmi (OTC). Mfano wa mpango uliofungwa ni kampuni ya NICOL.

Mpango wa uwekezaji wa pamoja kwa mfumo ulio wazi au amana ya kikundi ni mpango ulio wazi ambao unawezesha mipango hiyo kununua hisa au vipande wakati wowote mwekezaji akihitaji kuuza vipande. Mpango huu sio kampuni kwani huundwa kwa njia ya Hati ya Amana (Trust Deed) kati ya wadhamini wa mpango na mameneja wa mpango huo. Mfano wa mpango huu ni Mfuko wa Umoja.

Mpango wa uwekezaji wa pamoja kwa mfumo ulio wazi au amana ya kikundi una tofauti kubwa na mfuko wa uwekezaji uliofungwa ama muundo wa kampuni. Tofauti ya kwanza ipo kwenye sheria. Kampuni inaundwa kwa kufuata sheria ya kampuni wakati mfuko wa Amana ya Kikundi unaundwa kwa sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana. Kampuni ikishauza hisa zake haiwezi tena kuzinunua, wenye hisa wanaweza kupata pesa zao kwa kuuza hisa zao kwa watu wengine kupitia soko la hisa kama hisa zimeorodheshwa.

Lakini Mfuko wa Umoja, kama mpango wa wazi unaweza kununua vipande kutoka kwa wawekezaji wake. Tofauti nyingine ni kwenye uwekezaji, kwa mpango ulio wazi uwekezaji hufanywa katika rasilimali za fedha kama hisa, hatifungani na amana za benki tofauti na mpango uliofungwa ambao unawekeza pia katika uzalishaji wa bidhaa na huduma.

25. Je thamani ya kipande inatafutwaje?

Thamani ya kipande (NAV) inatafutwa kwa kuchukua thamani ya mali zote za mfuko (rasilimali kwa maana ya kilichopo na kinachotegemewa kupokelewa) na kutoa madeni yanayotegemewa kulipwa, na gharama za uendeshaji na kugawanya kwa idadi ya vipande vyote vya mfuko.

26. Kuna kiwango maalum cha gawio ambacho mwekezaji anatakiwa kutegemea kama atakuwa amenunua hisa au vipande?

Hisa za kawaida hazina mapato ya uhakika kwani mapato ya hisa hutokana na vitu viwili muhimu hali ya utendaji wa kampuni na sera ya kampuni kuhusu gawio la faida. Upatikanaji wa faida hutegemea ufanisi wa kampuni, kitu ambacho hakitabiriki kwa 100%. Vivyohivyo, mapato ya vipande vya mipango ya uwekezaji wa pamoja havina uhakika kwani hutegemea ufanisi wa mfuko/mpango.

27. Je ni kiwango gani cha chini ambacho ninaweza kuwekeza katika hisa?

Kima cha chini cha uwekezaji katika soko la awali inategemea na toleo lenyewe. Katika soko la pili kiasi cha chini cha uwekezaji ni walau hisa 10. Bei ya hisa inatofautiana kutoka kampuni unayotaka kuwekeza. Ili kuleta maana ya uwekezaji ni vema kiasi au thamani ya kuwekeza ikawa kikubwa kuliko ada / garama ya uwekezaji. Kiwango cha chini kinachotozwa na dalali wa soko la hisa ni shilingi 1,000.

28. Mwekezaji akifariki nini kitatokea kwenye dhamana zake?

Hisa na dhamana nyingine ni mali kama zilivyo mali nyingine kama vile nyumba na magari. Mwekezaji akifariki, dhamana zake zinachukuliwa kama mali nyingine za marehemu kwenye mchakato mzima wa mirathi. Kama marehemu alikuwa ameacha wosia, basi dhamana hizo zitarithiwa na aliyeachiwa urithi. Kama hakuacha wosia, dhamana hizo zitagawanywa kama sheria ya mirathi inavyobainisha.

29. Kwa nini kampuni huwa hazigharamii gharama za usafiri, malazi, chakula na gharama nyinginezo kwa wanahisa pale wanaposafiri kwenda kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa au mkutano maalum.

Huu ni utaratibu unaotumika kimataifa. Thamani ya wanahisa inaonyeshwa au kubebwa na thamani ya hisa. Kwa hiyo, wanahisa wanapohudhuria mkutano mkuu wa mwaka au mkutano mkuu maalum wanakuwa wanatumia moja ya haki zao kuisimamia Bodi ya Wakurugenzi kwa kupitisha au kutopitisha mapendekezo mbalimbali ya Bodi.

Kwa hiyo wanahisa wanapohudhuria mikutano kama hiyo hufanya hivyo kwa ajili ya kusimamia/kutetea maslahi yao kwenye kampuni. Kama kampuni ikilipa gharama za wanahisa wanapohudhuria mikutano mikuu au mikutano maalum (AGMs/ EGMs) itakuwa imeongeza gharama za uendeshaji, hali itakayo punguza faida wanayotakiwa kupata wanahisa. Huenda ikawa ni vizuri kueleza hapa kuwa baadhi ya kampuni zinaweza kuwa na utaratibu tofauti ambao unaweza kuwa wa ki-pekee.

Kwa mfano, benki ya CRDB ina muundo wa aina yake ambapo kila tawi la benki linateua wawakilishi kuhudhuria mkutano mkuu wa mwaka na gharama zote zinalipwa na benki.

30. Je kuna uwezekano kwa mwana hisa kusimamia moja kwa moja uendeshaji wa kampuni ambayo yeye ni mwanahisa kama vile rasilimali na madeni?

Mwanahisa hana usimamizi wa moja kwa moja katika uendeshaji au usimamizi wa mali za kampuni kama vile rasilimali na madeni. Uendeshaji wa shughuli za kampuni ni jukumu la Menejimenti ikisimamiwa na Bodi ya Wakurugenzi. Haki za mwanahisa katika kufanya maamuzi kuhusiana na uendeshaji wa kampuni zinaishia kwenye kupiga kura katika mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa au mkutano maalum kuwachagua Wakurugenzi kulingana na katiba ya kampuni (MEMART).

Mwanahisa ana haki ya kushiriki maamuzi ya kuteua kampuni ya kukagua mahesabu (auditors), kupitisha taarifa ya mwaka, na kupitisha mapendekezo mengine yanayohitaji kupitishwa na mkutano mkuu kulingana na katiba ya kampuni. Rasilimali za kampuni zinamilikiwa na kampuni wakati wawekezaji/wanahisa wanamiliki hisa za kampuni. Hali kadhalika, madeni ya kampuni iliyoanzishwa kwa mtaji wa hisa yana ukomo kwa kiasi mwanahisa alichowekeza na hayawezi kugusa mali binafsi za wanahisa kama kampuni ikifilisika.

31. Ninaweza kutumia hisa zangu kama rehani ya kupata mkopo wa benki?

Ndiyo, kumekuwa na ongezeko la taasisi za fedha kukubali hisa hasa za kampuni zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa kama rehani kwa ajili ya kutoa mikopo. Utaratibu wa kuweka hisa au vipande kuwa rehani umedhihirisha kuwa ni wenye manufaa na rahisi kwa mkopaji na mkopeshaji kwa sababu inachukua muda mfupi, uko wazi, hakuna gharama za kuthaminisha na kuna uwezekano mdogo wa kufanya udanganyifu. Hatifungani za serikali, hawala za serikali na hatifungani za makampuni zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa zinakubaliwa na taasisi nyingi zinazokopesha kama rehani ya mikopo.

32. Kama kitu kibaya kikitokea kwa hisa zangu nitapatiwa fidia?

Hapana, uwezekano wa hasara zinaenda pamoja na umiliki. Bei ya hisa inaweza kupanda (ambapo ni jambo jema kwako kama mwekezaji) na inaweza kushuka (ambapo ni jambo baya kwako kama mwekezaji). Mashaka ya namna hii (uwezekano wa hasara) yapo tangu siku unapoamua kuwekeza kwenye hisa. Iwapo utapoteza hati yako ya hisa (kwa wale ambao bado wanamiliki / wanazo hati za hisa kwenye baadhi ya makampuni yaliyoorodheshwa kwenye soko la hisa) unashauriwa kutoa taarifa ya upotevu huo kwenye kituo cha polisi kilicho karibu ili upewe taarifa ya polisi na kuiwasilisha mara moja kwa katibu wa kampuni.

33. Kama sifahamu cha kufanya kuhusiana na kuwekeza kwenye dhamana, au kama nataka kutoa taarifa kuhusiana na mwenendo wa kutiliwa mashaka wa mauzo fulani ya hisa/ dhamana, je, ninaweza kutoa taarifa kama hiyo wapi?

Mahali hasa pa wewe kuwasiliana unapotaka kuwekeza katika dhamana ni dalali yeyote wa soko la hisa. Madalali wa soko la hisa watakushauri na iwapo utaamua kuwekeza, watafanya hivyo kwa niaba yako. Kundi jingine unaloweza kuwasiliana nalo kwa msaada na ushauri ni washauri wa uwekezaji waliopewa leseni na Mamlaka. Washauri wa uwekezaji ambao si madalali wa soko la hisa wanaweza tu kutoa ushauri lakini hawaruhusiwi kununua hisa kwa niaba yako.

Endapo unahitaji kutambua orodha ya madalali wa soko la hisa unaweza kuangalia orodha yao kwenye swali la 15 hapo juu. Aidha unaweza pia kuwasiliana na Soko la hisa au Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ili kupata orodha ya washauri wa uwekezaji.

Kwa upande wa mauzo au manunuzi ya hisa yenye kutiliwa mashaka sehemu muafaka hasa ya kutoa taarifa ni Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) au Soko la Hisa (DSE). CMSA inao wajibu wa kusimamia masoko ya mitaji na kuona kuwa biashara hii inafanyika katika utaratibu unaozingatia sheria na taratibu halali zilizopo.

Vilevile mienendo yenye kutiliwa mashaka katika kuuza na kununua hisa inaweza kutolewa taarifa katika Soko la hisa la Dar-es-Salaam. Soko la hisa kama taasisi yenye kujisimamia inazo kanuni mbalimbali na utaratibu wa kuwaadhibu wanachama wake.

34. Kampuni ambayo ninamiliki hisa zake inaweza kunipa mkopo kwa kushikilia hisa zangu kama rehani?

Hapana, kwa kawaida kampuni zilizoorodheshwa huwa hazina utaratibu wa kutoa mikopo kwa wanahisa wake kwa kushikilia hisa zao kama rehani. Wewe kama mwanahisa iwapo unataka fedha taslim kutokana na hisa zako kuna njia mbili. Njia moja ni kuiendea taasisi yenye kutoa mikopo na kuiomba mkopo kwa kuweka hisa zako kama rehani (hii inategemea kama unatimiza vigezo vingine vya kupewa mkopo kulingana na masharti ya benki husika). Njia ya pili ni kuuza hisa zako kwenye soko la hisa kupitia kwa dalali wa soko la hisa.

35. Ni utaratibu upi ninaotakiwa kufuata ili kuorodhesha hisa za kampuni yangu DSE?

Mchakato wa kuorodhesha hisa huhitaji mwongozo wa kitaalam. Kanuni za Mamlaka (CMSA) na Soko la Hisa la Dar-es-Salaam (DSE) zinaelekeza kuwa kila anayetaka kutoa hisa au hatifungani kwa umma inabidi ateue dalali mdhamini au mshauri mteule kwa ajili ya kudhamini toleo hilo jipya au kuorodheshwa. Dalali mdhamini au mshauri mteule ataisaidia kampuni katika kutimiza masharti yanayotakiwa kwa kuzingatia mambo mbalimbali kama vile iwapo hisa za kampuni husika tayari ziko kwenye mikono ya umma (mfano hisa za TCCIA Investment Company Ltd) au ni hisa mpya.

Dalali mdhamini ataiongoza kampuni inayotaka kuuza hisa kwa umma na kuorodheshwa kwenye safu kuu ya soko la hisa (MIMS); na mshauri mteule ataiongoza kampuni inayotaka kuuza hisa kwa umma na kuorodheshwa kwenye safu ya soko la kukuza kampuni na ujasiriamali ya soko la hisa. Aidha kampuni zinazotaka kuuza hisa kwa umma na hatimaye kuorodheshwa katika safu hizi mbili, zinatakiwa kuwa na sifa fulani na kutimiza masharti yaliyoainishwa na Sheria ya Masoko ya Mitaji na dhamana na taratibu za Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Imenukuliwa kutoka www.cmsa.go.tz (Hii Site haifanyi tena kazi) ila habari hii inapatikana pia hapa http://mybusinessmanual.blogspot.com/2012/07/unajua-nini-kuhusu-soko-la-hisa.html


Company
ISIN
Date ListedNumber of Listed Shares
Nature of Business
TOL Gases Ltd. (TOL)TZ199610000815th April, 199837,223,686Production and distribution of industrial gases,welding equipments, medical gases, etc.
Tanzania Breweries Ltd.(TBL)TZ19961000169th September, 1998294,928,463Tanzania Breweries Limited (TBL) manufactures, sells and distributes clear beer, alcoholic fruit beverages (AFB's) and non-alcoholic beverages within Tanzania. TBL has controlling interests in Tanzania Distilleries Limited (TDL) and Darbrew Limited.
Tatepa Company Ltd.(TATEPA)TZ199610006517th December, 199917,857,165Growing,processing,blending, marketing and distribution of tea and instant.
Tanzania Cigarette Company.(TCC)TZ199610003216thNovember,2000100,000,000Manufacturing,marketing,distribution and sale of cigarettes.
Tanga Cement Public Ltd Co.(SIMBA)TZ199610005726thSeptember,200263,671,045Production, sale and marketing of cement.
Swissport Tanzania Ltd.
(SWISSPORT)
TZ199610004026th September,200636,000,000Airports handling of passengers and cargo.
Tanzania Portland Cement Co. Ltd. (TWIGA)TZ199610002429th September,2006179,923,100Production, sale and marketing of cement.
DCB Commercial Bank (DCB)TZ199610021416thSeptember,200867,827,897Commercial bank
National Microfinance
Bank (NMB)
TZ19961002226thNovember 2008500,000,000Commercial bank
CRDB Bank(CRDB)TZ199610030517thJune 20092,176,532,160Commercial bank
Precision Air Services Plc
(PAL)
TZ199610104821stDecember 2011193,856,750Air transport services
Maendeleo Bank Plc
(Maendeleo)
TZ19961016834thNovember 20139,066,701Commercial bank
Swala Gas and OilTZ199610186511[SUP]th [/SUP]August 201499,954,467Mineral Exploration
Mkombozi Commercial BankTZ199610197229th December 201420,615,272Commercial bank
CROSS-LISTED COMPANIES
COMPANYISINDate listedNumber of Issued SharesNature of Business
Kenya Airways Ltd. (KA)KE00000003071[SUP]st[/SUP] October 2004461,615,484Passengers and cargo transportation to different destinations in the world
East African Breweries Ltd (EABL)KE000000021629[SUP]th[/SUP] June 2005658,978,630Holding company of various companies involved in production, marketing and distribution of balt beer in Kenya, Uganda, Tanzania and Mauritius
Jubilee Holdings Ltd (JHL)KE000000027320[SUP]th[/SUP] December 200636,000,000Holding company of many companies involved in insurance business in Kenya, Uganda and Tanzania
Kenya Commercial Bank (KCB)KE000000031517[SUP]th[/SUP] December 20082,217,777,777Commercial Bank
National Media Group (NMG)KE000000038021[SUP]st[/SUP] February 2011157,118,572News media group
Acacia Mining PLCGB00B61D2N637[SUP]th[/SUP] December 2011410,085,499Mining and production of gold
Uchumi Supermarket LtdKE000000048915[SUP]th [/SUP]August 2014265,426,614Supermarket

 

mmakonde

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2009
Messages
968
Points
0

mmakonde

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2009
968 0
Vodacom wako radhi kujifanya wanatoa misaada kila siku,angalia bolg ya michuzi.
ukiangali a shareholders wao,kama VODACOM group(65%) na Mirambo(35%),kama mtanzania wa kawaida anatakiwa ajue ni nani hawa,kiasi gani cha tax kimelipwa etc.
Je ni nani ana audit hawa,kiasi gani waremit kweny parent company etc,ambayo haya
lazima yawe kwenye published accounts.

sector ya communication katika nchi yoyote ni muhimu sana maana ni chanzo kikubwa
cha income.I guess VODACOM ni kampuni ya kigeni,kwa nini isiwe na dual listing?

Hawa akina Mirambo ni nani?

Nchi za Ulaya/Marekani zimeweza kuendelea kwa sababu la soko la mitaji.
 

Prodigal Son

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2009
Messages
990
Points
250

Prodigal Son

JF-Expert Member
Joined Dec 9, 2009
990 250
Vodacom wako radhi kujifanya wanatoa misaada kila siku,angalia bolg ya michuzi.
ukiangali a shareholders wao,kama VODACOM group(65%) na Mirambo(35%),kama mtanzania wa kawaida anatakiwa ajue ni nani hawa,kiasi gani cha tax kimelipwa etc.
Je ni nani ana audit hawa,kiasi gani waremit kweny parent company etc,ambayo haya
lazima yawe kwenye published accounts.

sector ya communication katika nchi yoyote ni muhimu sana maana ni chanzo kikubwa
cha income.I guess VODACOM ni kampuni ya kigeni,kwa nini isiwe na dual listing?

Hawa akina Mirambo ni nani?

Nchi za Ulaya/Marekani zimeweza kuendelea kwa sababu la soko la mitaji.
MIRAMBO AKINA NANI halihitaji kufikiri saaaaana ni akina Edward Ngoyayi & R:Azizi na genge lao
 

Nsemwas Junior

Senior Member
Joined
Oct 23, 2009
Messages
165
Points
225

Nsemwas Junior

Senior Member
Joined Oct 23, 2009
165 225
we dont even know how much these telecommunication companies are making as a profit monthly,nadhani financial statements zao zinafichwa,NADHANI kuna ka mchezo hapa between govt(TRA) na hizi kampuni.Kuna umuhimu wa kutungwa sheria inayobana kama banks,kutoa audited financial statements quartely hii itasaidia wananchi kujua how much they are making and how much they pay as TAX to the govt.Tutawabana vizuri tu,au mwalionaje hili wadau?
 

Nanu

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2009
Messages
1,224
Points
1,195

Nanu

JF-Expert Member
Joined May 29, 2009
1,224 1,195
Vodacom wako radhi kujifanya wanatoa misaada kila siku,angalia bolg ya michuzi.
ukiangali a shareholders wao,kama VODACOM group(65%) na Mirambo(35%),kama mtanzania wa kawaida anatakiwa ajue ni nani hawa,kiasi gani cha tax kimelipwa etc.
Je ni nani ana audit hawa,kiasi gani waremit kweny parent company etc,ambayo haya
lazima yawe kwenye published accounts.

sector ya communication katika nchi yoyote ni muhimu sana maana ni chanzo kikubwa
cha income.I guess VODACOM ni kampuni ya kigeni,kwa nini isiwe na dual listing?

Hawa akina Mirambo ni nani?

Nchi za Ulaya/Marekani zimeweza kuendelea kwa sababu la soko la mitaji.
Sheria imeshapitishwa na bunge inayolazimisha kampuni za mawasiliano ziuze hisa kwenye DSE, wamepewa 3 years za kujiandaa hivyo by 2013 all of them must be listed and sold some shares to the public. Sheria ilishapitishwa, "it is only execution which is required now"!!
 

Bulesi

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2008
Messages
7,554
Points
2,000

Bulesi

JF-Expert Member
Joined May 14, 2008
7,554 2,000
Sheria imeshapitishwa na bunge inayolazimisha kampuni za mawasiliano ziuze hisa kwenye DSE, wamepewa 3 years za kujiandaa hivyo by 2013 all of them must be listed and sold some shares to the public. Sheria ilishapitishwa, "it is only execution which is required now"!!

Mbona hiyo 2013 ni mbali sana kwanini isiwe 2011 kwani hawa jamaa wanajitayalisha kwa kufanya nini zaidi ya mikutano yao na kuanza utekelezaji wa sheria?Serikali yetu ni too timid!
 

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
18,107
Points
2,000

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
18,107 2,000
Wadau wa jukwaa hili najitokeza leo kwa mara ya kwanza kuomba msaada hasa kwa wale wana uchumi wenzetu juu ya somo la hisa. Ningependa kujua juu ya haya mambo kuhusiana na mada hii.

a) Hisa ni nini??
b) Naweza kuzimiliki kivipi?? ni kimaanisha umri, na kiasi na wapi?? kwa masharti gani??
c) Nitapata faida gani kwenye umiliki wa hizo hisa??
d) Je nitapataje gawiwo langu kwenye umiliki wa hisa?
e) Hasara zipatikanazo kwa ununuzi wa hisa.
f) Nitaijuaje bei ya hisa ama kuna hisa zinauzwa??
g) Kwa maisha ya kitanzania is this bussiness valid and does it pay??
 

Godwine

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2010
Messages
1,369
Points
1,225

Godwine

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2010
1,369 1,225
hisa ni mfumo wa umiliki wa biashara kwa pamoja. yani ni umiliki wa kipande au sehemu ya kampuni. jinsi ya kupata faida ni kutokana na gawio yani sehemu ya faida ya kampuni ugawanywa kwa wanahisa kulingana na idadi ya hisa na faida iliyopatikana.lakini pia kama ikitokea hasara imepatikana katika kampuni inamaana pia wanahisa watakuwa wanachangia mzigo unaotokana na hasara hii.pia unaweza kunufaika kwa upandaji wa thamani ya hisa katika soko kwani unaweza kuuza wakati ziko bei ya juu na kununua wakati wa bei ndogo. kwa hiyo ni vema kuzingatia kuwekeza kwenye kampuni zenye uhakika yani imara yani zenye historia na zinazopata faida. pia unaweza kupata faida kwa kuuza hisa katika soko la hisa yani stock exchange . kampuni nyingi zinatoa gawio mara moja au mbili kwa mwaka.
 

drphone

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2009
Messages
3,561
Points
1,250

drphone

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2009
3,561 1,250
hisa ni mfumo wa umiliki wa biashara kwa pamoja. yani ni umiliki wa kipande au sehemu ya kampuni. jinsi ya kupata faida ni kutokana na gawio yani sehemu ya faida ya kampuni ugawanywa kwa wanahisa kulingana na idadi ya hisa na faida iliyopatikana.lakini pia kama ikitokea hasara imepatikana katika kampuni inamaana pia wanahisa watakuwa wanachangia mzigo unaotokana na hasara hii.pia unaweza kunufaika kwa upandaji wa thamani ya hisa katika soko kwani unaweza kuuza wakati ziko bei ya juu na kununua wakati wa bei ndogo. kwa hiyo ni vema kuzingatia kuwekeza kwenye kampuni zenye uhakika yani imara yani zenye historia na zinazopata faida. pia unaweza kupata faida kwa kuuza hisa katika soko la hisa yani stock exchange . kampuni nyingi zinatoa gawio mara moja au mbili kwa mwaka.
asante kwa mwongozo mzuri mkuu
 

MaxShimba

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2008
Messages
35,814
Points
1,250

MaxShimba

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2008
35,814 1,250
I think they are 16
1. Tol Gases Limited TOL
42,472,537
2. Tanzania Breweries Limited TBL
294,928,463
3. Tanzania Tea Packers Limited TATEPA
17,857,165
4. Tanzania Cigarrete Company Limited TCC
100,000,000
5. Tanga Cement Company Limited SIMBA
63,671,045
6. Swissport Tanzania Limited SWISSPORT
36,000,000
7. Tanzania Portland Cement Company Limited TWIGA
179,923,100
8. National Investment Company Limited NICOL
69,178,134
9. Dar Es Salaam Community Bank DCB
32,393,236
10. National Microfinace Bank Plc NMB
500,000,000
11. Kenya Airways Limited KA
461,615,484
12. East African Breweries Limited EABL
658,978,630
13. Jubilee Holdings Limited JHL
36,000,000
14. Kenya Commercial Bank Limited KCB
2,950,169,143
15. CRDB Bank Public Limited Company CRDB
2,176,532,160
16. Nation Media Group Limited NMG
157,118,572
 

menny terry

Senior Member
Joined
Mar 18, 2011
Messages
187
Points
195

menny terry

Senior Member
Joined Mar 18, 2011
187 195
wakuu samahanini nimekuwa nikilisikia soko la hisa la Dar es salaam lakini sijui lipo wapi na je kama nikinuoua pengine hisa za milioni moja gawiwo huwa shilingi ngapi?Naombeni anaejua anisaidie.Nimefuatilia la soko la Hisa la Brazil nimeona watu wakitajirika sana sasa sijua hapa kwetu hali ikoje.
 

Kombo

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2010
Messages
1,819
Points
0

Kombo

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2010
1,819 0
Nenda Twiga House pale Samora Avenue.

Unaweza kupata taarifa zaidi kupitia website yao: www.dse.co.tz

Kwenye ununuzi wa Hisa hakuna lugha hiyo ya kutaka kununua hisa za Shilingi Milioni Moja na kufikiria faida utakayopata, jambo la msingi ni kujua hisa za kampuni/shirika lipi ziko juu kwa kipindi husika na zinapanda thamani kwa haraka na ndipo utaweza kufanya maamuzi ya kununua au la. Kwenye website yao kuna taarifa za soko za kila siku, anzia hapo.
 

Rich Dad

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Messages
737
Points
195

Rich Dad

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2010
737 195
Remember to invest the amount of money which you can afford to loose.
Bei ya hisa huwa dictated na forces of supply and demand. Kwa hivyo wauzaji wa hisa wakiwa wengi kuliko wanunuzi basi bei hushuka, and the vice versa is true.
Kwa sasa soko la hisa la dar es salaam investors ni wachache, na kinyume chake speculators ni wengi.
 

SUPERUSER

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Messages
962
Points
250

SUPERUSER

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2011
962 250
Also kama ni beginner jarib kunuua hisa kwenye mutual funds like umoja trust fund coz risk inakua ndogo..the most important thing ni kuona thamani au bei ya hisa za kampuni husika inapanda hapo ndo unaeza kuamua kuuza na kupata faida..eg nmb kipindi wanaissue share zao kwa mara ya kwanza(IPO) bei ilikua TZS 150 then kuna kipindi nikaskia imefika TZS 500....its a good business but risky..kama umefatilia news this week wanasema masoko ya hisa uko Asia yamedrop that means people getting loses..all the best!
 

Forum statistics

Threads 1,380,777
Members 525,872
Posts 33,779,353
Top