Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 8,848
- 15,252
Soko la Mitumba aina zote maarufu kama Memorial, lililopo katika manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro lipo katika hali ya kusitikitisha kutokana na kuwa limejengwa katika mfumo wa vibanda vya miti.
Soko hilo pia limekuwa maarufu kutokana na kuwa na wateja wa mataifa mbalimbali wanaokuja kununua bidhaa zao na baadhi ya watalii wanaokuja kutalii soko hilo la kimataifa.
Wafanyabiashara wa soko hilo wamekuwa wakilipa ushuru miaka yote lakini hakuna uboreshaji wowote ndani ya Soko hilo licha ya kuwa na wateja kutoka pande zote za mikoa ya kanda ya kaskazini, kama vile Manyara. Arusha. Na hata nchi jirani ya kenya.
Kila mfanyabiasha anajenga kibanda chake cha miti kwa jinsi anavyojua yeye na wengine kuweka bidhaa zao chini wakati huo huo wakilipia ushuru kila siku ya Soko.
Soko hilo limekuwa ni katika moja ya masoko yanayoleta aibu katika manispaa ya Moshi kutokana na kuwa katika mfumo wa vibanda vidogo vya miti na mabati chakavu.
Miundombinu ya maji.,choo, na barabara ndani ya Soko ni ya hovyo
Na endapo basi Moto ukitokea katika soko hilo kila kitu kitateketea kulingana na mfumo wa soko zima lilivyo.