Mgogoro wa soko la CCM Katoro Geita na wafanyabiashara wa soko hilo

Mkurya mweupe

JF-Expert Member
Aug 10, 2023
218
740
Kutokana na mgogoro ulioibuka wa wafanyabiashara wadogo wa soko la CCM Katoro Geita , takribani wajasiriamali 300 ,wanatakiwa kumpisha mwekezaji mpya wa kujenga soko hilo na kumpisha mwekezaji mpya katika hilo soko .Leo tarehe 11, September ,machinga wa soko hilo wakishirikiana na wajasiriamali wengine wadogo wadogo wa soko hilo kama mama Ntilie wamekaa kikao na kuridhia mambo yafuatayo;

1. Wamekubaliana kuwa wamepewa notisi kinyemela na kinyume na mjibu wa sheria ,kwa kuwa wameamuliwa kutoka ndani ya eneo la hilo soko ,hivo hawatakuwa tayari kutoka kumpisha mwekezaji mpya huyo.

2.Wamehoji kwa kuwa huwa wanakilipa chama kupitia control number ,inakuwaje wenyewe watolewe na kumpisha mtu mpya anayekuja kuwekeza katika soko hilo ,bila kupewa maeneo mengine ya kufanyia kazi ,hvo hawatakubali kumpisha mwekezaji huyo.

3. Wamehoji kwa kuwa ,Chama Cha Mapinduzi ni kwa ajili ya kutetea watu wakipato kidogo na kuwainua zaidi ,ukizingatia hasa ,ahadi ya Chama Cha Mapinduzi ,ambayo ni kuondosha umaskini ,ujinga na dhuluma ,wanahoji ni kwanini chama Cha Mapinduzi kinaenda kuwatia umaskini ,ukizingatia hilo soko ni la watu wa kipato cha chini tu ? Iweje mtu mmoja awanyime ulaji watu 1000, na maendelo ni kwa ajili ya watu.

4. Wameazimia kuandika barua kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuanzia ngazi ya kata ,mpaka mkoa,pamoja na Mkuu wa wilaya na Mkuu wa mkoa kukitaka Chama Cha Mapinduzi, kuwatendea haki wajasiriamali wadogo kuendelea kufanya kazi katika eneo hilo ,wakitaka Mwekezaji huyo atafutiwe eneo jingine ambalo ataona linafaa zaidi atengeneze soko lake ,kuliko kuleta athari kwa mamia ya watu.

5 Wamemtaka Mkuu wa mkoa wa Geita ,Ndugu Martin Shigela kuingilia suala hilo ,maana ni suala linalogusa maisha ya Watanzania wa kipato cha chini.

6.Wamehoji kuwepo na harufu ya rushwa ,kwani mwekezaji aliyepatikana kujenga hilo soko alisaini tender ya kujenga ,wakati tenda ya kujenga haijatangazwa ,hivyo wameomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kuingilia suala hilo.

7.Baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo wamesema wameahidi kurudisha kadi za Chama Cha Mapinduzi kutokana na chama hicho kushindwa kujali maisha ya maskini wenye kipato kidogo na kutaka kurudisha kadi hzo kwenye ofisi za Chama kama matatizo yao hayatatatuliwa kufikia tarehe 15 September

8.Wameviomba vyombo vya habari vifike katika eneo la soko hilo hili kuweza kuwapazia sauti , ikiwezekana Mh Raisi aweze kuingilia kati suala lao ,kwani hili suala linakihusu Chama Cha Mapinduzi na Serikali pia.

9. Mwisho wamehoji kwa kuwa na wao walikuwa wamewekeza kwenye hilo soko na wao ndo chanzo cha hilo soko kuwa hvo lilivyo , inakuwaje leo wanatolewa kinyemela kisa kaja mtu mmoja kuwekeza katika hilo soko.

NB: Hizo chini ni baadhi ya picha za machinga na wajasiriamali wadogo wadogo wengine wakati wakisaini kukubaliana kwa pamoja kuwa hawatakuwa tayari kutoka katika eneo hilo la soko kinyemela bila hatua nzuri na za kisheria kufuatwa

IMG_20230911_160502_601.jpg

View attachment 2746354View attachment 2746355
 
Mkuu tuachie wawekezaji.
Maisha ni mabadiliko ya kila sijui.
 
Mkuu tuachie wawekezaji.
Maisha ni mabadiliko ya kila sijui.
Katika kitabu Cha My life,My purpose Benjamin Mkapa ,ameelezea madhara ya uwekezaji ulio mbovu na umuhimu wa uwekezaji wenye manufaa ,Ila alisema uwekezaji mzuri ni ule unaozingatia maisha ya watu ,akijutia baadhi ya maamuzi yake.
 
Katika kitabu Cha My life,My purpose Benjamin Mkapa ,ameelezea madhara ya uwekezaji ulio mbovu na umuhimu wa uwekezaji wenye manufaa ,Ila alisema uwekezaji mzuri ni ule unaozingatia maisha ya watu ,akijutia baadhi ya maamuzi yake.
ULIWAHI KUJIUULIZA HILI SWALI.

NANI ANAJALI?
 
Update: Wana ccm wamedai viongozi wa CCM wamepewa Rushwa kumpa mwekezaji wa ccm ,TAKUKURU TZ fuatilie uwekezaji huu ,mwekezaji katoa rushwa kwa viongozi wa chama ili aweze kumiliki soko hilo kwa miaka 7 ,kwahyo TAKUKURU TZ fatilien kwa makini hii tenda kuanzia ngazi zote mpaka mkoa waliohusika katika tenda hii wawajibishwe
 
Back
Top Bottom