Soko kuu la dhahabu lazinduliwa Chato, Waziri Biteko atoa maagizo

Naunga mkono maendeleo yote ya Chato

P
Pasco nimegundua kitu kimoja, huyo muzee mnampoteza kwa ushauri wenu wa mafuta ya mgongo wa chupa.
Haiwezekani hadi Leo hii asisikie aibu hata kidogo kuwa speed hii ya 120 kwenye kona kusifiwa ni kujipeleka kuzimu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani, tatizo liko wapi?? Mlitaka hizi rasilimali zetu ziendelee kuibwa kila siku?? Huku walijaa wakutoka nje tu. Wakaja na vifedha vyao wakavibadili mpakani kwa njia mbaya. Wakaingia humu nchini na kutunyonya. Leo mmejengewa mahali sahihi pa kuiuza dhahabu yenu wenyewe mnabeza?? Hapana, hii nasema sio vyema. Jengo la dhahabu mnataka liwe la udongo?? Tuleteeni basi michoro
Mkuu shida ni jengo soko la dhahabu kujengwa Chato au jina la Chato?
Kuna maeneo mengi inapatikana dhahabu katika wilaya ya Chato.
Walitaka lijengwe wapi.Basi vumilieni hadi 2040 likapohamishiwa eneo jipya.
 
Hongera JPM jengo zuri sana bila shaka ni fedha zetu za ndani na wachimbaji wadogowadogo sasa mambo yataenda vizuri maana walilaliwa sana zama zile..

Maendeleo Tanzania yanakuja kwa kasi sana chini ya jemedari JPM na uchumi unakimbia kwa kasi ya zaidi ya 7% heko JPM 2020 kura zote kwako ushindi 99.9%..
 
Leo katika viunga vya Chato kumezinduliwa soko kuu la dhahabu. Hivi kumbe haya masoko ni kwa kila wilaya? Maana makao makuu pale Geita napo pana mjengo wa soko la dhahabu.

Hongera Chato kwa kuyafikia maendeleo ya kweli. Unapaa kwa kasi kweli kweli.

View attachment 1304965
Swali LA kujiuliza mhe akimaliza muda wake kuna mtu atayaendeleza hayo ya chato? Simple answer is no
 
Gbadolite yetu lazima iwe na kila kitu.
Kitajengwa kiwanda kikubwa cha kubangua korosho. Shida iko wapi? Zitatoka Mtwara.
Long live the Fuehrer
Soon wapeleke na dada zetu wale wa mitaa ya kona ili wachangamshe jiji
 
Sijawahi kuona kiongozi mwenye uoendeleo kama tuliye naye sasa.


Hajaanza leo, kumbuka alipo kuwa waziri wa ujenzi aliwahi kupeleka taa za kuongozea magari sehemu ambayo ina magari hata 100 hayazidi.


Ni ubinafsi mkubwa , hata jengo lake ambalo ameweka tausi toka ikulu ni uhinafsi mkubwa kwa sababu ukisha chaguliwa kuwa Rais tunakupa nyumba ambayo ni ikulu na baada ya kutoka kuna utaratibu wa kujengewa nyumba , sasa yeye amejibegea jengo kama hoteli .


Tusipo angalia tutapata shida sana kwa huu utawala.

Mungu mlinde JK na mkapa na warioba , maana hawa ndio pekee wameshikilia msimamo wa katiba.

Mwinyi sijui kapewa nini katiba kesha ikanyaga, pinda ndio kabisa.. wengine hawaeleweki msimako wao.


Tunahitaji katiba mpya itakayo zuia mambo mambo kama haya.

Atatokea mtu siku moja akaingiza kwenye chama kabila lake tuu na viongozi kabila lake tuu kisha akapata urahisi wa kuikanyaga katiba kwa kigezo cha watu wanamtaka aendelee.

Sent using Jamii Forums mobile app

..hukumsikia Waziri Prof.Kabudi akidai kura za kanda ya ziwa zinatosha kumpa ushindi Jpm?

..kama siyo mwenyeji wa huko tafuta chama kingine tu. Hata mikutano ya hadhara kidogo kidogo hotuba zimeanza kuwa za kilugha.
 
Hilo jengo siku moja miaka sita ijayo litakuwa maskani ya mapopo, mijusi na hata mapepo tu. Time will bear me witness.
 
Leo katika viunga vya Chato kumezinduliwa soko kuu la dhahabu. Hivi kumbe haya masoko ni kwa kila wilaya? Maana makao makuu pale Geita napo pana mjengo wa soko la dhahabu.

Hongera Chato kwa kuyafikia maendeleo ya kweli. Unapaa kwa kasi kweli kweli.

View attachment 1304965
Unashangaa wilaya ya chato kuwa na soko la dhahabu wakati kjj cha Nyamongo kina soko la dhahabu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono maendeleo yote ya Chato

P

Una Ujinga mwingi
 
Back
Top Bottom