DC Chato: Wanaosema mbuga ya Burigi - Chato imekufa ni wapuuzi

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,738
15,211
Mkuu wa wilaya ya Chato mkoani Geita amekanusha uvumi wa kwamba mbuga ya wanyama ya Burigi Chato imefungwa na wanyama wamekufa au wamekimbilia kwingine.

Mkuu huyo wa wilaya amesema mbuga hiyo ya Burigi Chato ipo imara na wanyama wanaendelea kuzaliana kwa kasi na mwaka huu mwezi wa 12 wameandaa tamasha kubwa la utalii Chato festival ili kuifungulia dunia uzuri wa mbuga hiyo.

View: https://youtu.be/h_Z4O_OrEBk?si=Qijd7E4TGvPZ72Bq
 
Watu wanachanganya mambo iliyokufa ni ile Bustani ya Dikteta kama unatokea Buzirayombo kwenda Chato.

Burigi ilikuwepo kabla hata ya hao kuhamia hapo kutokea Burundi.
 
Kweli wanyama wanazaliana, Kuna mapanya mengi sana, na ukitaka kujua, yanagongwa sana na magari, mizoga mingi barabarani
 
Mkuu wa wilaya ya Chato mkoani Geita amekanusha uvumi wa kwamba mbuga ya wanyama ya Burigi Chato imefungwa na wanyama wamekufa au wamekimbilia kwingine.

Mkuu huyo wa wilaya amesema mbuga hiyo ya Burigi Chato ipo imara na wanyama wanaendelea kuzaliana kwa kasi na mwaka huu mwezi wa 12 wameandaa tamasha kubwa la utalii Chato festival ili kuifungulia dunia uzuri wa mbuga hiyo.

View: https://youtu.be/h_Z4O_OrEBk?si=Qijd7E4TGvPZ72Bq

Mbuga Iko chato au Iko kagera?
 
Atuambie imeingiza shs ngapi na watalii wangapi wametembelea?
Safari ni hatua. Tupende au tuchukie, mbuga ipo na haitandoka kwa urongo wetu mitandaoni. Kukua kwa biashara ya utalii, ni mipango mkakati.
Kama hatuna mipango ya watu kujua Burigi kuna nini, nani atakwenda? Kigoma na Katavi mbona watu hawaongeli kuna nini wakati kuna mbuga zenye wanyama wa kutosha
 
Angeutumia muda huo kutueleza wanyama wameongezeka kwa kiasi gani na nchi inanufaika vipi badala ya kujibu kwa hasira
 
Kwanini ameamua Kutugombeza na kututusi??kwani Bwana mdogo Mteuliwa Mkuu wa wilaya,,meshindwa kabisa kujibu Kwa hoja zenye mashiko na kama Kiongozi mwenye uadilifu ndani yake,, busara na vijihekima ndani yake??Tuna kazi sana watz na viongozi wetu
 
Back
Top Bottom