Chadema Bukombe Yazidi Kupukutika.Viongozi Wake Wa Wilaya 3 Watimkia CCM.Wapokelewa na NWM Dotto Biteko.

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,042
49,727
Baada ya kuripotiwa Kwa habari za mvurugano huko Chadema ambapo Lisu anataka Kumpindua Mwenyekiti Mbowe huku Mbowe akitaka Sugu agombee Urasi Hali ya sintofahamu imezidi kushika Kasi.

Huko Geita, Chadema Wilaya ya Bukombe imeanza kupukutika Kwa Viongozi na Wanachama wake kutimkia Chama pendwa Cha CCM kilichobeba matumaini ya Watanzania chini ya Mwenyekiti wake Shupavu Dr.Samia.

Hii Leo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dotto Biteko amepokea Wanachama 3 kutoka Chadema kama ishara ya mamia waliomiminika chama Cha Mapinduzi.

=====

Wananchama watatu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bukombe mkoani Geita, wamehamia Chama cha Mapindizi (CCM) na kupokewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko.

Wanachama hao wamejiunga CCM leo Jumamosi Desemba 30, 2023 na kupokewa kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Bukombe wakati wa ziara yake mkoani Geita, ambapo wameeleza kuwa wamefanya uamuzi huo kutokana na kujionea jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo wilayani Bukombe ikiwemo ujenzi wa barabara, shule, umeme.

Baada ya kupokea Wanachama hao, Biteko amewakaribisha CCM na kueleza kuwa, chama hicho ni cha watu wote, kinachowaangalia Watanzania na kuwaza maendeleo yao, hivyo amewaasa kuwa wakiwa ndani ya CCM, wajifunze mila na desturi ikiwemo, kusikilizana, kuvumiliana, kuheshimiana na kupendana huku wakati wote mawazo yao yakiwa ni kuwapelekea wananchi maendeleo.

(Imeandaliwa na Elizabeth Joachim)

My Take
Chadema ni Saccos ya waganga njaa na matapeli ,kimbieni mapema rudinj nyumbani kumenoga.

Kazi iendelee
 
Mmeanza Tena Mambo Ya Kufika Bei Mkiwalipa Cash Ndefu Sana
Ila Siasa Inalipa Sana Yaani Chap Wanachota Wanaingia 2024 Na Vyeo Serikalini
 
Ukitaka future ya siasa hamia CCM,huko kwingine ni wahuni tuu.

Samia hahitaji kununua watu wenyewe watakuja Kwa sababu wanaona kinachofanyika kwenye maeneo Yao hususani maendeleo.
 
Attachments

  • 20231215_140742.jpg
    20231215_140742.jpg
    31.3 KB · Views: 1
Baada ya kuripotiwa Kwa habari za mvurugano huko Chadema ambapo Lisu anataka Kumpindua Mwenyekiti Mbowe huku Mbowe akitaka Sugu agombee Urasi Hali ya sintofahamu imezidi kushika Kasi.

Huko Geita, Chadema Wilaya ya Bukombe imeanza kupukutika Kwa Viongozi na Wanachama wake kutimkia Chama pendwa Cha CCM kilichobeba matumaini ya Watanzania chini ya Mwenyekiti wake Shupavu Dr.Samia.

Hii Leo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dotto Biteko amepokea Wanachama 3 kutoka Chadema kama ishara ya mamia waliomiminika chama Cha Mapinduzi.

View: https://www.instagram.com/p/C1eyxEdt1fr/?igsh=NmJiYWZiY2E0Mg==

My Take
Chadema ni Saccos ya waganga njaa na matapeli ,kimbieni mapema rudinj nyumbani kumenoga.

Mbona unadanganya? Mara viongozi wa wilaya tatu huku taarifa inasema wanachama watatu.
 
Naona mmeingia kwenye mtego wa CHADEMA vizuri Sana. Mnaitangaza Sana kwa hizi siku mbili tatu. Endeleeni waenezi wetu.
 
📌📌🔨

Punguza uongo. Leta taarifa sahihi. Wanachama watatu Tena kwenye mkutano wa Naibu Waziri Mkuu, baada ya Mwenezi na Makamu mwenyekiti wa ccm kufanya mikutano Geita, ni aibu. Jamaa wenyewe hata t-shirt zimechanika, Wana njaa tu.
 
Bora wameondoka tu kwenye chama kilichokosa Dira na muelekeo. chama kimebakia kama mradi binafsi wa familia .yaani mbowe tangia arithishwe chama na mkwe wake amekifanya kama Sacco's au kikoba.
 
Elewa ulichoelewa dunia ipo kasi sana!

Hakuna kuelewa kwenye uongo. Taarifa anayo rejea inasema ni wanachama watatu, ingawa wanamuonesha mmoja tu. Ila huyu mleta mada anadai ni viongozi wa wilaya tatu tofauti. Sasa hapo utaelewa uongo?.
 
Baada ya kuripotiwa Kwa habari za mvurugano huko Chadema ambapo Lisu anataka Kumpindua Mwenyekiti Mbowe huku Mbowe akitaka Sugu agombee Urasi Hali ya sintofahamu imezidi kushika Kasi.

Huko Geita, Chadema Wilaya ya Bukombe imeanza kupukutika Kwa Viongozi na Wanachama wake kutimkia Chama pendwa Cha CCM kilichobeba matumaini ya Watanzania chini ya Mwenyekiti wake Shupavu Dr.Samia.

Hii Leo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dotto Biteko amepokea Wanachama 3 kutoka Chadema kama ishara ya mamia waliomiminika chama Cha Mapinduzi.

View: https://www.instagram.com/p/C1eyxEdt1fr/?igsh=NmJiYWZiY2E0Mg==

My Take
Chadema ni Saccos ya waganga njaa na matapeli ,kimbieni mapema rudinj nyumbani kumenoga.

Kazi iendelee 👇

View: https://twitter.com/Juma__Mariam/status/1741040617843818605?t=epz_4uzUyiGeiLfnenGV0Q&s=19

Chadema ni imani... Ukitaka kujua nguvu ya CDM subiri uchaguzi wa serikali za mitaa
 
Hakuna kuelewa kwenye uongo. Taarifa anayo rejea inasema ni wanachama watatu, ingawa wanamuonesha mmoja tu. Ila huyu mleta mada anadai ni viongozi wa wilaya tatu tofauti. Sasa hapo utaelewa uongo?.
Habari ni kuwa mwanachama wa chadema kahamia ccm ila naye habari kaletewa!
 
Back
Top Bottom