Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

- Irrelevant, wapi hoja za masilahi ya taifa mzee wa malezi bora? This is too low for me kujibu mkuu!

Respect.


FMEs!
Na bora unyamaze Mnyanda za juu ww,huna stara hapa...thanks for your fonts again...nazipenda sana.
 


Mkuu vipi wewe mbona bado unaendeleza mipasho?Wewe mtoto wa kiume hiyo habari ya mama Sofia kuzaa na wanaume wa watu inakuhusu nini?Na una uthibitisho gani kama hao watoto ni wa wanaume za watu?Ulishawafanyia DNA testing mkuu au basi tu ni mipasho kama ya Bi Khadija Kopa?
Halafu kwanini ujifanye unamjua kila anayechangia hapa?Unasema Jeetu hakuhusika na harusi wala kumchangia Malecela 200M,wewe kama nani wa kukanusha hayo madai?Are u John Samuel Malecelaa?
Majibu ya Malecela kwamba Sofia kichaa hayatoshi kumsafisha.Huo ukichaa umeanza juzi aliposema kuwa kampeni yake ilikula 200M za Jeetu?Kwanini kama alimjua ni kichaa asingemjulisha Mwenyekiti wake wa CCM siku hizo kuwa uteuzi wa Sofia haufai kwa vile ni kichaa?
Mkuu mtawazuga haohao,sisi wengine hatuzugiki.Huyu mama siyo kichaa,isipokuwa kamwaga radhi sasa watu mmebaki kupagawa.
 

- Irrelevant!


- mkuu soma hapa chini kutoka forums ya wanabidii hii sio mimi mkuu, ila soma chini hapa wanaomjua kuliko mimi:-

 

- Irrelevant!


- mkuu soma hapa chini kutoka forums ya wanabidii hii sio mimi mkuu, ila soma chini hapa wanaomjua kuliko mimi:-


duh kaazi kwelikweli
hii mipasho haina issue mkuu.Leta hoja hii mipasho waachie kinamama!
 
Mimi naomba majina ya hao watot angalau tuwe na ushahidi mkuu kama hutajali .
 
Field Maeshal aka Hadija Omari Kopa
Siku folder la Mama Malecela litakapo kuwa unfold utasemaje?na sijui utakmblia blog gani Mkuu? me naona CCM hamna wakumdefend.
Huyu mama Sophia pamoja na uchangudoa wake katupa kakj data ambacho katatusaida watanzania kuwajua na kuwachunguza wapiganaji. Nyamaza na acha kuwatetea mafisadi.
 


Naomba mwongozo.
Ili kuweka mambo sawia nikiwa na mlengo wa kati.
kama Malecela anavyotakiwa kuonyesha wafadhili wake ili kujisafisha naonelea vivyo hivyo na mama simba atuletee DNA ya watoto wake na wanaume aliozaa nao.

Kweli kabisa kunamisingi ya uadirifu ktk uongozi hii inaenda sambamba na wafadhili wako ndivto vivyo umalaya.

kuzaa na wanaume zaidi ya wawili ni umalaya na hafahi kuwa hata katibu kata
 
 
mkuu FMES

TUACHANE NAO WAMECHOKA HAO...NDIO WANAOFADHILIWA NA VIJI BUKU VYA MAMA SIMBA WANALETA NJAA ZAO JF...DEMN
 

- Huwezi kuninyamazisha bila facts wala ukweli, labda uanze kunyamaza wewe, Mama kilango hana tatizo lolote ni kiongozi imara na shupavu, mwenye matatizo ni Sophia, tena ana kichaa cha ajabu sana ndio maana kila mwisho wa mwezi lazima akatibiwe SA.

- Anyways, naomba kupumzika sasa maana nimesema sana leo sasa inatosha.

Respect.

FMEs!
 
feld marshall
mbona unaonekana unamtetea sana mama ana klango?mtoto acha kupga mayowe.


aendekezi umbea na unafiki ndio maana anawaelekeza na wala amtetei...mama yenu sophia simba mnafiki mama kilango kamuuliza ulikuwa wapi miaka ote toka 2005 anakumbuka leo alifadhiliwa na jeetu...shame on her...mbona ile mijibaba aliyozaa nayo imeoa na ikachangiwa sana na matapeli na mafisadi wa ccm...shame kuliko zote yeye anaenda kuomba michango ya harusi ya bwana anaemchapa huku mwanamke mwingine akila koni....shame simba....nimeweka wazi jamani mwambieni huyo mama asiguse ndoa ya malecela kilango kasema atafia nae kidondani...kama mabuzi awachezee hao aliozaa nao....
 

Hoja yako ya kijinga.kwanini?
Kwanza hoja ya mama Sofia kuzaa na waume za watu haikuletwa na Malecela mwenyewe.
Pili yani wewe mtu aliyetafuna 200M za kifisadi katika kampeni yake ni kiongozi bora kwako lakini mwanamke aliyezaa na wanaume zaidi ya wawili hafai kuwa kiongozi.Hivi vigezo vya wapi mkuu?Mimi nilidhani ungezungumzia uchapakazi na kujali maslahi ya taifa kwanza hapo labda ningekuelewa.
 


mkuu p53

lipi bora

kutumia million 200 kwenye harusi

kutumia billion 2 za mafisadi kwenye kampeni za uwt

yupi kiongozi bora kwako???
 
mkuu p53

lipi bora

kutumia million 200 kwenye harusi

kutumia billion 2 za mafisadi kwenye kampeni za uwt

yupi kiongozi bora kwako???


Now ur talking na haya ndiyo kina Malecela ilibidi wayasimamie ili tujue mkweli nani na siyo kutuletea bla bla sijui Sofia kichaa au mipasho ya kuzaa na waume za watu.
BTW sikusema kuwa Sofia ni kiongozi bora.Nilipinga hoja ya jamaa eti mtu akizaa na wanaume wawili tofauti hafai kuwa hata katibu kata.Huu ni ujinga.
 
ooooooooooooooh junius na wewe upo???haya tusaidie kumfikishia mama ujumbe....mpate hata vijisent vya gahawa vijiweni
Unajuwa nakushangaa wapi,ww unashabikia usilolijuwa...ukitafari na kuacha haya maneno ya "wavuta bangi" humu JF,utagundua ukweli ninaokwambia...kuwa alichokimaanisha Mama Simba,kwa ufupi tu kuwa,Chama chao cha Mapinduzi (CCM), chote kichafu,manake ni Mafisadi, hakuna yeyote katika wao, as long as yumo katika CCM,atakaejifanya,atakaejitenga na ufisadi huo...sasa kuna watu humo humo wanajida wao siwo,hawamo katika vice hiyo. Wanajidai wao ni "majamadari", "wapiganaji" na "wapambanaji" wa ufisadi...kitu ambacho mimi sitaki kuamini na wala sitaaamini...kwa dalili kabisa nikupe mfano...Mwakyembe kahusika ktika mambo ya maamuzi ya sakata la umeme wakati yeye mwenyewe ni mdau binafsi na mjasiria mali wa sekta hiyo hiyo ya umeme (kumbuka ana kampuni yake ya umeme wa upepo) mfukoni na vita vyake na Rostam Aziz,havikuwa vya kupinga ufisadi...vilitokana na mgongano wa kimaslahi kwa kampuni ya Mwakyembe...sasa huyu huu ujemdari wa kupinga ufisadi kaupata wapi wakati yeye mwenyewe fisadi?
Ndo Mama Simba, akasema kuna watu hawastahiki kuwanyooshea wenzao vidole kwa kuwa wao wenyewe walakini mtupu.
Nyie mmebaki, oooooh changudoa, mwendawazimu...n.k
Hamtazami nini kinaendelea ndani ya chama mnachokisubri kikuleteeni maisha bora...huku viongozi wake wakinyosheana vidole vya uchafu.
WATANZANIA MMESHAPEWA SOMO KUWA CCM YOTE HAIFAWI HAKUNA JEMEDARI WA KUPIGANA NA UFISADI HUMO,WOTE WEZI
WW endelea kucheza mdundiko wenzako wanapiga charanga
 
HAYA WALE WA VIDOLE JUU MNAYAJUA HAYA????

Jeetu Patel akana madai ya Waziri Sophia Simba kuhusu mgao wa fedha

Na Sadick Mtulya

MFANYABIASHARA nchini Jeetu Patel amesema asihusishwe katika malumbano ya kisiasa yanayoendelea baina ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba na mbunge Mama Kilango na mumewe Malecela.

Kauli ya Patel inafuatia baada ya hivi karibuni waziri Simba kupitia kikao cha kamati maalumu inayoongozwa na rais mstaafu, Ali Hassani Mwinyi kutoa tuhuma za kuwa wawili hao walipewa Sh 200 milioni na mfanyabiashara huyo kwa ajili ya kufanyia kampeni na pia kufadhili harusi yao.

Patel ambaye kwa sasa ana kesi katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kuchota fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Sh11 bilioni, alisema malumbano hayo hayamhusu.

"Mimi sio mwanasiasa mimi ni mfanyabiashara siwezi kuingilia masuala ya siasa, kwa kweli mimi simo na wala siwezi kusema lolote kwa kuwa wanayoongea hayanihusu," alisema Patel alipozungumza na Mwananchi Jumapili jana.


Akijieleza kwenye kamati hiyo, Simba alimtuhumu Malecela, ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu katika serikali ya awamu ya kwanza, kuwa wakati akiwania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005, Jeetu Patel alimpa Sh200 milioni kwa ajili ya kampeni zake.

Malecela, ambaye wakati huo alikuwa makamu mwenyekiti wa CCM, aliondolewa mapema kwenye mbio za urais, ikiwa ni mara ya pili baada ya kuenguliwa tena mapema mwaka 1995.

Hata hivyo, akijibu mapigo hayo juzi Malecela alisema tuhuma hizo zinatokana na waziri Simba kuwa mgonjwa wa akili, huku mkewe Anne Kilango, akimshangaa kwa kukalia tuhuma hizo kwa kipindi kirefu.

Waziri huyo mwenye dhamana ya utawala bora akiwa na taasisi nyeti kama Takukuru na Idara ya Usalama wa Taifa, alisema Mama Kilango ni mnafiki na sio msafi kiasi cha kuwanyooshea wengine vidole wakati harusi na kampeni zake za ubunge zilifadhiliwa na mtuhumiwa huyo wa ufisadi. Alhamisi Patel, alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo za waziri Simba kwamba alifadhili harusi ya Malecela na kampeni zake za urais, alionekana kustuka na kusema: "Haa...we nani kakwambia... Bwana ehee, mimi sijui lolote kuhusu hayo. pamoja na hayo alishauri asiusishwe na mipasho yoyote inayoendelea juu ya ccm...mi sijazoe mipasho nanukuu....
 
Unatakiwa ujue JF kuna watu wa aina gani! Kuna wengine hapo juu wametoa piacha ya mzee Mengi na mwanamke fulani, wengine wakamuita Sofia malaya nk, wapo pia waliotukanana. Unaweza ukaona watu wanafanya vitu kwa makusudi kabisa kudivert attention ya hoja. Hii ni tabia mbaya na haina tofauti na ufisadi. Tuzungumze issue siyo mambo ambayo hayana maana. So km Mengi ana mwanamke??? au Sofia anawanaume sita ya nini???
 
Srce mwananchi
Soma kwa makini hiyo info maana ipo kwenye vyombo vya habari toka jana. Huyo Patel ni mjanja saana hiyo issue kaiacha inahang generally hajakubali wala kukataa.
 

teh teh
Mbona cliton walimweka kati kwa kula uroda tu na kimwana mpaka akaomba msamaha, ndio nje kukwapua waume za watu na kuzaa nao.

Hayo si maadili na kigezo cha maadili mtu wa namna hii haiwezi kuongoza hata familia yake, fuatilia tu watu wa namna hii na historiaa zao majumbani.

tuhuma ni tuhuma sio lazima zitolewe na mwibiwa ,aje clean na DNA.

Pia Malecela nae aje clean na mchanganuo wake kuhusu wafadhili wake ktk kampeni zake.
huo ndio msimamo wa kati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…