Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,845
- Thread starter
- #41
Masikini.
Mi hii biashara ya watu kubadili status kila siku ndio inanichosha. Leo "in a relationship". . . baada ya muda "its complicated". . . kidogo kidogo huyo kawa "single". , who needs to know? Mpaka kila mtu ajue mkiwa na matatizo?Ndio mwanzo wa waliokua wanamvizia mtu wako kujaribu bahati.
Mi tangu nimejiunga nimeweka "married" sibadili hata nikifa, maana haileti usumbufu wala maswali na comment za ajabu ajabu.
...hahaha, wewe ni miongoni mwa wale msovua pete ya ndoa hata kama kuti lishadondoka...
nice one, ushajichongea kuweka status yako hadharani, endelea nayo tu...wengine tupo tupo kwanza,
hatuna status japo nililazimishwa niweke eti married to, ebo?!...lol
....Njemba ilikuwa tayari kumpiga chini mkewe lakini mke baada ya kuona hali ile imezua kasheshe kubwa ndani ya nyumba na hali kuzidi kutishia future ya ndoa yao siku moja akaomba kuongea na mumewe na kujitetea kwamba hakukuwa na lolote njemba ikagoma, mamsap akaanza kulia vilio vya kwikwi na kudai kwamba ndoa yao ilikuwa haina tatizo ila amefanya makosa na kama ndoa ikivunjika basi watachekwa sana na mahasidi wao. Njemba akadai hiyo ilimgusa mno na hivyo kuamua kubadilisha maamuzi yake lakini anadai alikuwa amefikia hitimisho la kuivunja ndoa...kisa njemba imejaa tele linkedIn.
...aisee kama ni sukari basi ishaingia sumu,...sawa na kufunga upepo 'Dengu Beach' pale Ocean Road na lile shombo la mwani.