So, unafikiri utakuwa kiongozi mzuri!...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,731
40,836
Uongozi ndilo tatizo kubwa kabisa linaloikabili nchi yetu sasa hivi na tunaweza kuona hilo CCM, serikalini, Chadema na kwenye taasisi mbalimbali. There is big vacuum of leadership. Tunao watawala na mameneja; tunao wenyeviti na makatibu, tunao wabunge na wanasiasa mahiri; tunao wasomi na watu waliobobea katika fani mbalimbali; hata hivyo tatizo kubwa tulilonalo na ambalo ni kiini cha mengine mengi liko kwenye Uongozi.

Kiongozi ni nani?
Tunaweza vipi kumtambua mtu kuwa ni kiongozi mzuri kabla hatujampa nafasi ya kuongoza?
Anatakiwa kuwa na sifa gani?
Je kiongozi anazaliwa hivyo au anapewa elimu ya uongozi na kuonesha cheti cha "kiongozi".
Je viongozi wanaweza kunolewa na kuwa viongozi bora hata kama hawapata elimu ya juu ya utawala?
Je watawala ni lazima wawe viongozi pia?
Ni kiongozi wa aina gani anahitajika katika nchi na ni wa aina gani wanahitajika katika vyama vya kisiasa?
Je wale wanaoongozwa wanatambua ni kiongozi gani wanayemtaka?
Je mtu maarufu anaweza kuwa kiongozi bora?

Haya ni baadhi ya maswali ambayo yanahitaji kujibiwa tunapotafakari kile tunachokiona dhahiri mbele ya macho yetu. Na kubwa zaidi tufanye nini kujipatia viongozi bora?

Jaribu kujibu angalau swali moja kati ya hayo hapo:
 
Uongozi ndilo tatizo kubwa kabisa linaloikabili nchi yetu sasa hivi na tunaweza kuona hilo CCM, serikalini, Chadema na kwenye taasisi mbalimbali. There is big vacuum of leadership. Tunao watawala na mameneja; tunao wenyeviti na makatibu, tunao wabunge na wanasiasa mahiri; tunao wasomi na watu waliobobea katika fani mbalimbali; hata hivyo tatizo kubwa tulilonalo na ambalo ni kiini cha mengine mengi liko kwenye Uongozi.

Kiongozi ni nani?
Tunaweza vipi kumtambua mtu kuwa ni kiongozi mzuri kabla hatujampa nafasi ya kuongoza?
Anatakiwa kuwa na sifa gani?
Je kiongozi anazaliwa hivyo au anapewa elimu ya uongozi na kuonesha cheti cha "kiongozi".
Je viongozi wanaweza kunolewa na kuwa viongozi bora hata kama hawapata elimu ya juu ya utawala?
Je watawala ni lazima wawe viongozi pia?
Ni kiongozi wa aina gani anahitajika katika nchi na ni wa aina gani wanahitajika katika vyama vya kisiasa?
Je wale wanaoongozwa wanatambua ni kiongozi gani wanayemtaka?
Je mtu maarufu anaweza kuwa kiongozi bora?

Haya ni baadhi ya maswali ambayo yanahitaji kujibiwa tunapotafakari kile tunachokiona dhahiri mbele ya macho yetu. Na kubwa zaidi tufanye nini kujipatia viongozi bora?

Jaribu kujibu angalau swali moja kati ya hayo hapo:

kiongozi annatakiwa awe na sifa zote hapo juu 1-3.
Si lazima watawala wawe viongozi.
viongozi wanaohitajika katika nchi ni wale wenye kukidhi matakwa ya wananchi wa nchi husika hata kama matakwa hayo hayana maslahi binafsi kwa kiongozi husika.
Wanaoongozwa inabidi wajue kiongozi wanaemtaka ili awatimizie matakwa yao, lazima watofautishe kiongozi bora na bora kiongozi.
Mtu maarufu anaweza kuwa kiongozi bora kama umaarufu utaambatana na sifa zingine za kiongozi bora.
 
Mada nzuri sana hii MKJJ na kama wana jf wakizingatia basi hii mada itatuletea sifa za kiongozi wetu ajaye ili wana jf kwa umoja tumpigie kampeni yule atakayeonekana kuendana na sifa zitakazotokana na mjadala huu kwa kuzingatia jamii tuliyonayo kwa wakati huu pia bila kusahau jamii ya kizazi kijacho.
Hivyo tunaomba watu wawe honest na kuchangia kwa nidhamu ili sifa halisi za kiongozi wetu ziainishwe na tujue pa kwenda 2010.
 
Je, mfumo uliopo unaruhusu kupata kiongozi bora mwenye sifa ambazo zimeainishwa kwenye maswali ya Mwanakijiji?

Kila mara chaguzi zinapokaribia huwa kuna mambo makubwa yanafanyika (rushwa, kupakana matope, na mengine machafu mengi tu) iwe kwenye chaguzi za vyama vya siasa ama uchaguzi wa rais na wabunge.

Nadhani kinachohitajika ni mfumo mzuri na wa uwazi unaotumika kuwapata wagombea nafasi za uongozi na mchakato mzima wa uchaguzi. Leo hii ukizihoji kamati kuu za vyama namna wanavyowapata wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi wa juu na kwamba wanatumia vigezo gani kuwafyeka wengine na wengine kuwapitisha unaweza kukosa jibu la kueleweka.

Kwanini kamati kuu yenye watu 20 au 30 ifanye uteuzi wa wagombea badala ya kuwashirikisha wananchi kwenye primaries ili angalau na wao washiriki kwenye hiyo process? Ni rahisi sana mgombea kuwahonga wajumbe 20 au 30 wa Kamati Kuu na wakampitisha kama mgombea. Bado hata kwenye Mkutano Mkuu ambao una wajumbe chini ya 2000 bado wanaweza kuhongwa na kumpigia kura mtu mwenye fedha badala ya kuangalia vigezo muhimu.

Pamoja na kuwa na mfumo wa uwazi, pia wananchi wa Tanzania wanahitaji kupata somo la uraia ili waweze kupata mwamko na kujua umuhimu wa kuchagua kiongozi bora/anayefaa na madhara ya kumpigia kura kiongozi ambaye ni bomu.

Wapiga kura wengi wa Tanzania hawana elimu hiyo na wengi wetu ambao tunajua umuhimu wa kuwa na kiongozi bora hatujajiandikisha kupiga kura na kama tumejiandikisha, siku ya uchaguzi ikifika hatuoni umuhimu wa kwenda kupiga kura kwa kuwa mfumo mzima wa kuwapata wagombea una kasoro nyingi na pia wagombea ambao tunaletewa kwa ajili ya kuwapigia kura tunaona kwamba walipatikana kwa mizengwe na hivyo mtu anaona bora aendelee kupumzika nyumbani kwake ama akafanye kazi nyingine badala ya kwenda kupiga kupanga foleni ya kupiga kura.

Walalahoi wengi ndiyo wamejiandikisha kupiga kura na siku hizi wamekuwa wakitumia shahada zao za kupigia kura kama mtaji wakati wa uchaguzi. Ikifika wakati wa uchaguzi wana uhakika wa kupata kapelo, khanga, t-shirt, shilingi 1000 ama 10,000. Kinachotakiwa kwa hawa watu ni kuwaelimisha kwamba kitendo chao cha kukubali kupokea shilingi 10,000 gharama yake ni kubwa kwa kuwa ataendelea kuwa na maisha magumu kwa miaka 5 ijayo kabla hajapokea 10,000 nyingine ama kapelo.
 
Mzee Mwanakijiji,

Nimeyasema haya kule kwenye waraka wa mchungaji kuhusiana na Uongozi. Naomba niyabandike.

Re: 'Marshall Plan' - Restoration and Recovery Plan for Tanzania
inaendelea....

Uongozi; Serikali, Utawala, Dola
Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) zimebahatika kuwa na awamu si chini ya nne za uongozi wa Serikali kuu, ingawa kwenye Bunge na Mahakama, watumishi wake wameendela kuwa ni wale wale kwa muda mrefu.

Tatizo kubwa tulilonalo kama Taifa ni ufinyu wa viongozi bora na utashi binafsi wa wachache walio katika nyanja za uongozi kwa kukosa sifa muhimu kwa viongozi. Mzee Mwinyi amesema majuzi kuwa Tanzania ina viongozi wasomi wasioelimika. Kauli hii ni ya kweli na ni ya msingi kutambua kuwa uongozi si lelemama, ni kipaji na ni kazi ngumu.

Uongozi ni kujitolea na kuweka matwakwa na maslahi ya wengine kuwa mstari wa mbele na si matakwa binafsi na kujinufaisha. Marehemu John Kennedy rais wa Marekani alitoa kauli moja maarufu iliyosema kuwa “kiongozi ajiulize ni vipi atalitumikia Taifa na si Taifa kumtumikia yeye Kiongozi” Umashuhuri na uzuri wa Kiongozi unatokana na hekima, busara, uchapakazi, ufanisi, ufuatiliaji, uimara, uungwana, uwajibikaji na unyenyekevu wake. Ama fikra endelevu na upeo wa kuongoza ni muhimu na si kauli tamu au uzuri wa sura.

Uwezo wa Tanzania kuwa na maendeleo ya kweli utaanza na Uongozi bora.

Uongozi bora ni ule;
· wenye mapenzi ya kweli na dhati na kujivunia Utaifa wake
· wenye kujali na kulinda maslahi ya Taifa lake na watu wake
· wenye uwezo wa kupanda mbegu imara ya Uzalendo kwa kila mwananchi bila kujali itikadi, rangi, kabila, dini, elimu, umri au jinsia
· wenye uwezo wa kuhamasisha na kuchochea juhudi za maendeleo ya jamii, umma na Taifa
· wenye nidhamu, watiifu, kuwajibika, tija, ufanisi, kujituma na ufuatiliaji wa hali ya juu
· wenye usikivu, uungwana na unyenyekevu kukiri makosa, kukubali kukosolewa na kupokea na kufanyia kazi maoni ya wengine
· wenye uwezo wa kufanya kazi, kufikiri, kuwa na upeo na wepesi wa kukabili na kufanya maamuzi magumu
· usiolea uzembe, ubaguzi, unyanyasaji, uhujumu, ubadhirifu, rushwa, kudharau, kudhalilisha, kujuana au kulinda maslahi ya wachache au kikundi Fulani

Wajibu wetu kama Taifa na haki yetu kama wapiga kura kuchagua viongozi kutuongoza unabidi uachane na mfumo duni tulioujenga wa kuangalia sura na chama na tuangalie wagombea wetu wa uongozi kwa vigezo hivyohapo juu ili kuunda tabaka jipya la viongozi ambao ni wachapakazi na watakuwa manahodha wazuri kutuongoza katika safari yetu ya kulijenga Taifa.

Tukilegalega katika hili na kupuuzia wajibu juu mkubwa na kuendelea kuchagua viongozi na wawakilishi wabovu, tutakuwa hatuna sababu yeyote kulia na kulalamika kuwa tu masikini au wanyonge kwa kuwa ni Ujinga na Upumbavu wetu kutumia akili na busara zetu tulizopewa Mungu tumekimbilia kurudia makosa ya kuwapa dhamana ya uongozi watu ambao hawafai kutuongoza.

Tuchague viongozi si kwa kuangalia vyama au sura, bali tuangalie uwezo wao wa kuongoza, kuhamasisha na kufanya kazi. Tupime kauli zao na matokeo ya kazi zao kama wanavyojinadi.
Serikali ni watu, inaundwa na watu tuliowachagua na tunawapa watu hawa na Serikali mamlaka makubwa ya kutuongoza, kupanga na kulinda Taifa na Katiba yetu. Dhamana hii imefanywa kwa kuaminiana kuwa Serikali itafanya kazi kwa manufaa ya Wananchi wake na kwa matakwa na utashi wa Wananchi wake.

Inapotokea kuwa Serikali inafanya kazi tofauti na dhamana iliyopewa, ni wajibu na haki ya kila Mwananchi kudai na kuhoji mapungufu yanayoonekana au kuzungumzwa. Ni wajibu wa Serikali na Uongozi kujibu na kuwajibika kwa Wananchi waliowapa dhamana ya kuongoza Taifa.
Ikiwa Serikali na watendaji wake na Viongozi wanashindwa kufanya kazi zao kama wanavyotegemewa kuzifanya na kushindwa kutimiza matarajio ya Wananchi na Taifa, ni wazi kuna umuhimu wa kupima uwezo wa viongozi na kuhoji Uzalendo wao na kama bado wanastahili kulitumikia Taifa.

Kuanzia Rais, Mawaziri, Majaji, Mahakimu, Wabunge, Wakuu wa Taasisi na Mashirika, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Polisi, Magereza,Jeshi na watendaji wengine wa Serikali, tumaini la Watanzania na Taifa ni kuwa watu hawa wamepewa nafasi hizo kwa kuwa wanauwezo wa kitaaluma na kiutendaji kuwa viongozi na walinzi wa nguzo za Taifa letu kupitia Katiba na Sheria zake.
Hivyo basi pamoja na kuwa ni jukumu la sisi kama Raia na Taifa kudai uwajibikaji, lakini uzito wa kuhakikisha ufanisi wa Uongozi na uwajibikaji wake utaanzia na Mkuu wa Nchi ambaye ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu.

Wasifu wa Uongozi bora nilioutaja hapo juu, si wa Rais pekee, ni wa kila mtu aliye kiongozi na ni shurti kila Mtanzania aishi kwa kuviangalia na kuvitumikia vipengele hivyo bila kujali yeye ni Kiongozi au la.

Serikali yetu ni kubwa sana na ina watendaji wengi ambao sitaficha kusema kuwa asilimia 55% hawastahili kuwa viongozi kutokana na kushindwa kuwa na sifa nilizozitaja hapo juu.

Hii ni hatari sana kwa Maendeleo na Usalama wa Taifa letu. Hatuwezi kuendelea kujiongoza kiholela huku zaidi ya nusu ya viongozi wetu hawana Uzalendo au uchungu na nchi yao. Swali kwako Mtanzania ni kwa nini basi ukubali kuendelea kujichagulia viongozi wabovu wasiofaa na kuwapa dhamana kubwa sawa na kumpa Simba jukumu la kulinda Mbuzi wako?

Kinachokosekana kutoka Uongozi Mkuu hasa Urais na hata Mawaziri ni uwezo wa kudai kwa nguvu uwajibikaji na uadilifu. Hadithi na tuhuma za ufisadi zilizotawala Taifa letu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 ni kutokana na kuwa na Uongozi dhaifu, usiojali maslahi ya Taifa, uongozi uliojaa woga na kulindana na kushindwa kusimama kidete kulinda rasilimali za Taifa letu.

Viongozi wakuu wa jamii kuanzia wakuu wa vijiji, kata, tarafa, wilaya, mikoa hata Taifa, wameendelea kufanya kazi bila kupimwa na waajiri wao wawe Wananchi au Serikali kuu kuhusiana na ufanisi na uwezo wao katika safari ya kulijenga Taifa na kuleta maendeleo.

Mapendekezo yangu ambayo yataanzia na wewe Mtanzania ni kuwapima viongozi wako kwa kutumia vipimo vyepesi sana. Vipimo hivi ni kama ifuatavyo;
· kupitia ripoti za kila mwezi, robo, nusu na mwaka mzima za maendeleo na kupima mafanikio na matatizo ya shughuli za maendeleo
· kuhoji na kuhakiki viwango vya kuongezeka vita dhidi ya ujinga katika wilaya au mikoa kupitia shule za msingi, sekondari, vyuo na elimu ya watu wazima
· kuhoji maendeleo ya afya kupiga vita maradhi, kuangalia takwimu za kupungua vifo vya Uzazi, vifo vya watoto, kupungua kwa uadimu wa lishe na magunjwa kama Kwashiakor, Utapiamlo, kupungua kwa magonjwa na vifo vya Malaria na Ukimwi
· ongezeko la nyumba bora, maji safi, barabara nzuri, shule, hospitali na zahanati, vyanzo vya ajira, viwanda na shughuli za kilimo
· hifadhi za chakula kukabiliana na njaa, mauzo ya mazao ya biashara na chakula
· matumizi bora ya fedha za bajeti ikiwa pamoja na kubana matumizi yasiyo ya muhimu, kudhibiti matumizi na mahesabu ya fedha za bajeti za matumizi na maendeleo
· kukagua na kuhakiki shughuli za maendeleo kuwa ni endelevu na kuhakikisha hazizoroti

Kwa kifupi ni kuhoji na kutathmini, ni shule ngapi tulizonazo, ni ngapi zimeongezeka, ni wanafunzi wangapi wamehitimu shule, ni hospitali ngapi tulizonazo zina uwezo gani, msisitizo wa kinga ni mkubwa kiasi gani kulingana na tiba, kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji mali na hifadhi za mazao, kubana matumizi na matumizi mazuri ya fedha.

Nimeweka wajibu huu kwako wewe mwananchi kwanza na si ile kasumba ya kusubiri Kiongozi Mkuu-Rais au Waziri Mkuu ndio wawe wenye jukumu na uhalali wa kuhoji haya.
Vipimo hivi haviishii kwa Mbunge, Mkuu wa Wilaya au Mkoa ni mpaka kwenye Serikali kuu na hata vigezo hivi vinaweza tumika katika mashirika na taasisi za umma na zile binafsi.

Kama vigezo hivi vya uongozi bora na kupima uwajibikaji vingekuwa vikifuatwa kwa makini, tungeweza kuona uwiano wa maendeleo wa Taifa letu. Lakini ni mpaka pale tutakaboshinikiza na kudai kwa nguvu Utawala na uongozi bora, ndipo tutakapoona mafanikio na hivyo kuanza kupata tumaini la maendeleo ya Taifa zima.

Uongozi na Utawala bora huendana sambamba na dola. Katika Utawala bora, Serikali na Viongozi ni wabunifu wa mipango mizuri ya maendeleo, ni wapimaji wa kasi ya maendeleo na hufuata kanuni na sheria katika kufanya kazi zao.

Panapokuwa na Uongozi na Utawala mzuri, kero za wananchi hupungua na hata matumizi ya dola na vyombo vyake huheshimika na huwa ni kwa ajili ya manufaa ya Taifa.
Hali halisi ya Tanzania imejenga mfumo wa utawala unaolinda utashi na maslahi ya chama tawala au kikundi chenye nguvu za madaraka nja mali. Hali hii imefikia hatua ya kikundi hiki cha watawala kutumia nguvu za dola kutawala kwa mabavu, kukiuka sheria na kanuni alimradi wanatumia kinga ya uongozi.

Utawala wa namna hii si mzuri na hauna manufaa hata kidogo kwa nchi yetu au Taifa lolote. Tunapaswa kukemea na kuondokana na mfumo huu mbovu wa Utawala ambao unatumia dola na kuweka wajibu wa kwanza wa Uongozi ni kulinda matakwa ya Chama au kikundi maalum.
Aidha matumizi mabovu ya dola na vyombo vyake, Bunge, Mahakama, Polisi, Jeshi na Usalama wa Taifa yamesababisha kwa kiwango kikubwa kuzorota kwa Uongozi, kuweko kwa utawala mbovu ambao umeishia kuangamiza uchumi na juhudi za maendeleo ya Taifa.

Wajibu wa vyombo kama Bunge na Mahakama ni kuwa mihimili mingine ya Serikali. Bunge likitunga Sheria, Mahakama ikitoa tafsiri za sheria na Serikali kuu kufanyia kazi sheria. Badala ya vyombo hivi kuwa huru na hata kuhakiksha vyombo visaidizi kama Polisi, Jeshi, Mahakama, Magereza, Usalama wa Taifa na ofisi ya Mwanasheria Mkuu vinabakia kuwa vyombu huru ndani ya mfumo wa kisiasa, vyombo hivi vimegeuzwa na kutumika kama silaha ya kulinda chama kinachotawala kwa kutoa vitisho kwa wananchi na vyama visivyo na madaraka.

Suluhisho la haya yote ni kuundwa kwa Katiba mpya na Sheria mpya ambazo zitalenga;
· kutoa haki sawa kwa kila mwananchi bila upendeleo
· kutofungamana na chama au kikundi cha siasa au watawala,
· kuwajibisha Watanzania wote bila kujali nafasi zao katika jamii na Taifa,
· kulinda maslahi, haki , uhuru na mali za Watanzania wote bila kujali itikadi, dini, elimu, jinsia, umri au kabila
· kutoa tafsiri na maelezo ya kisheria na kanuni ambayo hayana utata au kukosa nguvu kufanyiwa kazi na kufuatiliwa
· kumpa kila Mtanzania fursa na haki sawa katika kuchangia kwake ujenzi wa Taifa na hata kuongoza bila kuwa na vipingamizi vya kibaguzi ambavyo vimewekwa maksudi katika katiba ya sasa na Sheria kuzuia ushindani au kuwepo kwa uhuru kamili wa kujieleza na kufanya mambo ya siasa na uongozi
· kujenga miiko mikali na maadili kwa viongozi, utawala na wanachi kwa ujumla
· kuweka mfumo bora wa uteuzi au uchaguzi wa viongozi na wawakilishi

Penye nia pana njia, kama wote tutakaa mstari mmoja na kukubaliana kwa pamoja kuwa haya ndiyo tunayoyataka kutoka kwa viongozi wetu, mfumo wetu wa utawala na dola, nafasi ya kupata viongozi wazuri, kuwa na mipango mizuri itafanikiwa na hivyo kuruhusu wananchi na viongozi kuwajibika kwa dhati na kujituma ili kuhakikisha kuwa shughuli za Ujenzi wa Taifa kiuchumi unafanikiwa kukiwa na Amani, Mshikamano, Sheria na Uongozi Bora.
 
KIONGOZI ANAZALIWA. Mambo mengine yayofuata baada ya hapo yanamsaidia kuwa Kiongozi BORA, Kiongozi MZURI, Apambane na UDHAIFU na MAPUNGUFU aliyonayo. Mambo kama ELIMU ya darasani, VIKAO, USHAURI wa watu wenye NIA NJEMA, NDOA na mambo mengine ya kijamii vinasaidia sana kurutubisha UONGOZI ambao kimsingi ni KIPAJI adimu.
Tatizo tulilo nalo katika NCHI yetu kwa sasa ni namna ya KUWATAMBUA na KUWAPA NAFASI Viongozi wazuri tulio nao. HAWAFURUKUTI kwa kuwa uongozi umekuwa ni DILI. Kumekuwa na UWEKEZAJI mkubwa tu kwenye SIASA.
 
Uongozi ndilo tatizo kubwa kabisa linaloikabili nchi yetu sasa hivi na tunaweza kuona hilo CCM, serikalini, Chadema na kwenye taasisi mbalimbali. There is big vacuum of leadership. Tunao watawala na mameneja; tunao wenyeviti na makatibu, tunao wabunge na wanasiasa mahiri; tunao wasomi na watu waliobobea katika fani mbalimbali; hata hivyo tatizo kubwa tulilonalo na ambalo ni kiini cha mengine mengi liko kwenye Uongozi.

Kiongozi ni nani?
Tunaweza vipi kumtambua mtu kuwa ni kiongozi mzuri kabla hatujampa nafasi ya kuongoza?
Anatakiwa kuwa na sifa gani?
Je kiongozi anazaliwa hivyo au anapewa elimu ya uongozi na kuonesha cheti cha "kiongozi".
Je viongozi wanaweza kunolewa na kuwa viongozi bora hata kama hawapata elimu ya juu ya utawala?
Je watawala ni lazima wawe viongozi pia?
Ni kiongozi wa aina gani anahitajika katika nchi na ni wa aina gani wanahitajika katika vyama vya kisiasa?
Je wale wanaoongozwa wanatambua ni kiongozi gani wanayemtaka?
Je mtu maarufu anaweza kuwa kiongozi bora?

Haya ni baadhi ya maswali ambayo yanahitaji kujibiwa tunapotafakari kile tunachokiona dhahiri mbele ya macho yetu. Na kubwa zaidi tufanye nini kujipatia viongozi bora?

Jaribu kujibu angalau swali moja kati ya hayo hapo:

leadership is born, leadership is a talent, na kiongozi bora anaanza tangu utoto wake, experience makes it perfect; mtu hawezi on the edge of forty fifty hakuwahi hata kuwa monitor wa darasani ukampa aongoze mamailioni ya watu ukategemea atakua kiongozi bora, the leader who is born to be a leader akipata management courses, then unamsaidia zaidi, lakini bora kiongozi ukimpa kozi za utawala unamuharibu zaidi; kwani hana spirit hivyo you are teaching him/her politics........................................
 
Uongozi ndilo tatizo kubwa kabisa linaloikabili nchi yetu sasa hivi na tunaweza kuona hilo CCM, serikalini, Chadema na kwenye taasisi mbalimbali. There is big vacuum of leadership. Tunao watawala na mameneja; tunao wenyeviti na makatibu, tunao wabunge na wanasiasa mahiri; tunao wasomi na watu waliobobea katika fani mbalimbali; hata hivyo tatizo kubwa tulilonalo na ambalo ni kiini cha mengine mengi liko kwenye Uongozi.

Kiongozi ni nani?
Tunaweza vipi kumtambua mtu kuwa ni kiongozi mzuri kabla hatujampa nafasi ya kuongoza?
Anatakiwa kuwa na sifa gani?
Je kiongozi anazaliwa hivyo au anapewa elimu ya uongozi na kuonesha cheti cha "kiongozi".
Je viongozi wanaweza kunolewa na kuwa viongozi bora hata kama hawapata elimu ya juu ya utawala?
Je watawala ni lazima wawe viongozi pia?
Ni kiongozi wa aina gani anahitajika katika nchi na ni wa aina gani wanahitajika katika vyama vya kisiasa?
Je wale wanaoongozwa wanatambua ni kiongozi gani wanayemtaka?
Je mtu maarufu anaweza kuwa kiongozi bora?

Haya ni baadhi ya maswali ambayo yanahitaji kujibiwa tunapotafakari kile tunachokiona dhahiri mbele ya macho yetu. Na kubwa zaidi tufanye nini kujipatia viongozi bora?

Jaribu kujibu angalau swali moja kati ya hayo hapo:

Mzee Mwanakijiji,

Tunaweza kuandika vitabu kuhusu kiongozi mzuri lakini ukweli ni very simple. Kiongozi mzuri ni yule anaye deliver kwenye kazi zake au majukumu mengine aliyo nayo. Ni yule mwenye vision ya kuona nini hakiko sawa na uwezo wa kutatua hayo mambo ambayo hayako sawa.

Utamwona kiongozi mzuri kwa kuangalia performance yake kwenye kazi zozote alizowahi kufanya.

Angalia mafanikio ya mtu kwenye jamii anayoishi, kama hakuna cha maana alichowahi kufanya, hata umpe kuwa PM, jua hakuna kitu.

Uongozi ni kipaji ambacho sehemu kubwa watu wanazaliwa nacho lakini kinalelewa kuongezewa sifa na elimu ya darasani pamoja na elimu ya mitaani (kazi kwa vitendo). Elimu inasaidia kutoa tools ambazo kiongozi anaweza kuzitumia kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi na hivyo more delivery.

Siku hizi tofauti ya viongozi wa kwenye biashara na wale wa siasa ni ndogo sana. Wote wanatumia tools zile zile, wote wanapambana na matatizo yale ya change na mengineyo. Wote wanakabiliana na watu wasio na uwezo lakini pia wale ambao wanataka kuwang'oa kwenye vyeo vyao. Namna ya kushughulikia hayo matatizo ndio kuko tofauti kibao.

Ni muhimu kwa viongozi wa siasa kupitia maisha mengine katika maisha yao, kama wafanyakazi serikalini au kwenye private companies.

Kwa kujibu swali lako, ukishindwa kudeliver nyumbani kwako, most likely utashindwa kudeliver kwenye taifa.
 
If you are serious about understanding this subject and why are leadership is failing, you need to read this book, and it is very cheap! The title is " The powers to lead, the author is a renown Havard Professor Joseph Nye and the Amazon link is this one below:

0195335627
 
KIONGOZI ANAZALIWA. Mambo mengine yayofuata baada ya hapo yanamsaidia kuwa Kiongozi BORA, Kiongozi MZURI, Apambane na UDHAIFU na MAPUNGUFU aliyonayo. Mambo kama ELIMU ya darasani, VIKAO, USHAURI wa watu wenye NIA NJEMA, NDOA na mambo mengine ya kijamii vinasaidia sana kurutubisha UONGOZI ambao kimsingi ni KIPAJI adimu.
Tatizo tulilo nalo katika NCHI yetu kwa sasa ni namna ya KUWATAMBUA na KUWAPA NAFASI Viongozi wazuri tulio nao. HAWAFURUKUTI kwa kuwa uongozi umekuwa ni DILI. Kumekuwa na UWEKEZAJI mkubwa tu kwenye SIASA.

WildCard,
Umeongelea hasa nilichotaka kuandika. Kuna watu na BAHATI zao na KIPAJI cha uongozi. Mtu kama Billy Clinton, Obama, Nyerere, Tonny Blair, Putin*, Kikwete*, Kagame*, Museven*, Mao, JF Kenedy nk.
Hawa niliowekea nyota ninamaanisha wanakasoro fulani na zinajulikana.
Hawa wote ukiwachunguza sana wanakitu INCOMON. Ni watu wenye CONVISING LANGUAGE. Ingawa kwangu mie mzee wa wote alikuwa Adolf Hitler. Sasa katika hili nafikiri hao juu wamegawanyika. Kuna watu akisimama tu mbele za watu tayari KASHAWAMALIZA. Hawa ndiyo akina HANDSOME and smiling men au jamaa waliopanda JUU. Yaani hao ule mwili wake tu tayari akina mama wanamkubali na hii inatokana na HULKA alizoumbwa nazo Mwanamke kuwa "Mwanaume mwenye Afya ni Watoto wenye Afya.." Hii huwa inawasukuma kufanya mambo bila hata kujijua. Ila shida huanza pale akishafungua mdomo au akianza kuonyesha vitendo vyake. Kundi jingine ni lile ambalo akifika watu wanataka kuondoka ila akianza kuongea basi watu wanaanza kurudi na waliopo watakaa hadi mwisho na wakitoka hapo wapo tayari kuuwa FISADI yeyote. Hawa jamaa unakuta hata sura hawana ila WANACHONGA ni hatari.
Sasa hapa huwa ni wakati wa UCHAGUZI tu. Wakishinda na kuingia OFISINI huwa inaanza story nyingine. Hapa ndipo unaweza kukuta kuwa mtu asiye na sifa hapo juu ila anaFIT kabisa hapa. Hawa ni watu wazuri sana kuwa washauri kwani anamawazo mazuri na muono wa mbali ila HANA KIPAJI cha kufikisha hayo mawazo yake kwa watu wengine. Ndiyo maana Tanzania sasa tunalia kwani tulipata mtu mwenye sifa nzuri pale juu ila OFISINI kimewaka.
Nafikiri Kiongozi inabidi awe na sifa zote mbili. Awe na kipaji cha kuzaliwa (anavyoonekana na anavyosema) na pia cha kusomea na mwisho KIONGOZI KWA MATENDO. Ni shida sana kulifundisha TAIFA kumchagua Kiongozi kwa MATENDO na si KUCHONGA na KU-SMILE na jinsi ambavyo SUTI ZINAMKAA. Hili nafikiri hawana shida nalo Waingereza na Wajeruman maana huko WAZURI ni MINORITY. Urusi kwao Kiongozi lazima awe MBABE, ndiyo maana Putin alikuwa NYOTA yao. Sijui sisi Tanzania tunamisingi ipi. Kiongozi Mzuri ni yule FISADI atakeyekuja na KUTUHONGA Khanga, Nyama, Tshirt za NJANO, mashati ya Kijani na picha ukutani kila nyumba??? Kazi ipo!!
 
Wana JF,
Kwa wale wapenzi wa Mpira/michezo tangu miaka hizo yaani miaka ya 70, waatakumbuka nchi za Kikomunisti walikuwa wanmichezo wazuri saana. Ujeruman Mashariki, USSR, Rumunia, Checkslovakia, Yugoslavia, Poland, Rumunia, Hungary nk. Katika hizi nchi alikuwepo kocha mmoja ambaye kwa sasa ni Marehemu akiifundisha timu ya Poland. Huyu aliisaida sana Poland . Mwaka 1972 alishinda na kupata gold medal kwenye Olympic (akina Grzegorz Lato). Mwaka 1976 akapata medal ya fedha (kocha Henryk Kasperczak) na mwaka 1974 akawa wa tatu katika KOMBE LA DUNIA.
Nimetaka tu kuonyesha UMAHIRI wa huyu Mzee aitwaye Kazimierz Gorski. Huyu Mzee si tu kwamba alifanikiwa hivihivi tu bila ya kuwa na sifa NZURI KAMA KIONGOZI au KOCHA. Katika maisha yake alikuwa na VIMISEMO vingi sana ambavyo baadhi hadi leo ukivisoma unaona kuwa MZEE alikuwa na AKILI sana na kujua KUFIKISHA UJUMBE kwa vijana wake ingawa sasa nao ni Wazee kama huyu aliyekuwa kocha wa Senegal walipokuja Tanzania aitwaye Henryk Kasperczak. Nimeweka baadhi ya maneno yake na mtu ajaribu kusoma na kuangalia SISI waTanzania na JF yanawezaje kutusaidia. Samahani kwa kuweka Makala ndefu na isiyohusiana na UONGOZI hapo mwanzo.

1. To win, you must score one goal than your opponent.
2. Sometimes you win, sometimes you loose and sometimes you draw.
3. The longer we have the ball, the less they don't.
4. If the goodluck is repeating, it already not a luck.
5. A ball is round, and there are two goals, so either we win or they win.
6. A ball can go, not a player.
7. If football was rulled by money, UAE would win the World CUP.
8. As long as the ball is in play there's always a chance.
9. A FOOTBALL IS THE GAME, YOU PLAY AS THE OPPONENT ALLOWS.
10. MORE VALUABLE IS THE COACH WHO IS LUCK, THAN BEST UNLUCK COACH.
Hapo ndiyo utajua kuwa Mzee alikuwa MHAMASISHAJI si kawaida. Mwenye nimezipenda hizo mbili za mwisho. Nafikiri MAFISADI wanacheza na sisi kama SISI wenyewe Watanzania TUNAVYOWARUSU WACHEZE. Tukitumia PRESSING watabadili au hata hata KUPANIC na hapo tunaweza kufunga goli moja zaidi. Mungu Bariki Mechi haijaisha.
 
Mada hii ni nzuri kama tukiijadili kwa marefu na mapana yake.

Napingana na ile dhana eti viongozi huwa wanazaliwa, kwani naamini kuwa hakuna mtu aliyezaliwa eti kazi yake maalum ni kuongoza wengine,naamini kuwa kila mmoja anaweza kuwa kiongozi .

Ila kiongozi mzuri ni yule ambaye yupo tayari kujifunza kila mara,na kila wakati na awe tayari kupokea mawazo mapya na kuyafanyia kazi.

Kiongozi mzuri ni yule ambaye yupo tayari kupokea chanagamoto na kuzifanyia kazi.

Kiongozi ni lazima awe mtu mwenye kufanya maamuzi, awe tayari kuchukua hatua hata kama kufanya hivyo atakuwa anawaumiza baadhi kwa masilahi ya wengi, ila hapa sisemi kuwa minority waumizwe-hapa iwe haki bin haki.

Kiongozi ni yule ambaye yupo tayari kusikiliza .

Kiongozi awe tayari kufanya maamuzi na kuchukua hatua dhidi ya maamuzi yake-yaani kufuatilia kama maamuzi yake yanatekelezwa.

Kiongozi anatakiwa kuwa na ujuzi kama sio wa kusomea basi anaweza kuwa na ujuzi wa kimaarifa wa kuzaliwa.

Ila kwa zama hizi kiongozi lazima awe na elimu ili aweze kukabiliana na changamoto za sasa na zinazobadilika kila siku.


Haya ni mawazo yangu juu ya kiongozi.
 
Mwana Kijiji,
Hii heading yako kidogo ilinipa shida kujua nini unamaanisha. Hasa hili neno SO.
Nikakumbuka KAKA MKUU wetu nikiwa Mazengo alikuja na kutuambia umuhimu wa kumenya viazi kwani wapishi hawawezi kumenya kwa wanafunzi wote kama 800 hivi. Baada ya kuhamasisha akamalizia kwa kusema " So, wote tunakwenda kumenya viazi.." watu walianguka kicheko na hiyo ikawa story ya siku "So, wote tunakwenda ...."
 
Back
Top Bottom