Nyikani, Mwanamke atainua mnyama kutoka majini atakayetupeleka Nchi ya ahadi

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,126
22,626
Salaam,Shalom!!

Leo twende Kona za kinabii, watakaodaka wadake, wasioelewa ndo basi tena, wale wasioamini kuwa Mungu husema na manabii, ndo kabisa, hawatodaka chochote.

MWANZO WA NDOTO.

Roho wa akanichukua Hadi Mahali palipokuwa na maji mengi, ufukweni mwa ziwa na tazama, mnyama mkubwa akazuka Kutoka ndani ya maji,

Kuonekana Kwa mnyama yule kulikuwa hivi, mnyama yule alikuwa na miguu ya mwanadamu, mwili wake ulikuwa kama wa mwanadamu, alikuwa na Vichwa Saba na pembe kumi.

Kisha nikaona pembeni ya mnyama yule akizuka JOKA kubwa lenye Vichwa Saba, JOKA lile lilitema maji yaliyoingia ndani ya Vichwa vya watu na kusababisha Giza kuu ndani Yao.

Kisha nikamwona mwanamke akiingia katika nyumba ya Ibada ameshika kitabu, na baada ya Kutoka nje ya nyumba hiyo ya Ibada, mwanamke huyo alirudi tena na kukabidhi kitabu hicho Kwa kiongozi aliyekuwa ndani ya nyumba hiyo ya Ibada.

.......Mwisho wa ndoto........


TAFSIRI YA NDOTO.

1. MAJI- Ni jamaa, Taifa, watu watokao Kanda zenye hizo location ya mwota ndoto alipoionea. Na maji aliyoyaona ni ya ukanda wa ziwa nyanza/ Victoria, Mwanza. ( Ufunuo:12:6, ufunuo 17:1.....).

2. MNYAMA- Tafsiri ya mnyama kibiblia ni utawala, uongozi.

3. MIGUU YA KIBINADAMU.
Miguu ya mnyama mwenye Vichwa Saba na pembe kumi kuwa ya kibinadamu, tafsiri yake ni kuwa, uongozi wa kiongozi huyo ajaye utakuwa na ubinafamu, ubinafamu ni huruma, kupenda HAKI,kulinda raslimali za nchi nk nk.

4. VICHWA SABA.

TAFSIRI ya KICHWA kibiblia ni Uongozi, viongozi, Watawala.

Mnyama mwenye miguu ya kibinadamu, mwenye ubinafamu, anao watu Saba ambao atasaidiana nao kufanya utawala wake kuwa Imara.

5. PEMBE KUMI .

PEMBE KUMI tafsiri yake kibiblia, ni Watawala, viongozi wa ndani ya utawala wa Vichwa Saba, PEMBE kumi, ni viongozi kumi ambao hawajapewa mamlaka Bado ambao baada ya mtawala huyo kusimama Kwa msaada wa viongozi Saba, watainuka viongozi wengine kumi ambao Kwa sasa hawajapewa kuongoza, watu hao au viongozi hao kumi, wataimarisha utawala wa kiongozi huyo mwenye miguu/ hatua/ utawala wa kibinadamu.

6. JOKA LENYE VICHWA SABA.

TAFSIRI ya JOKA kibiblia ni shetani,

JOKA kuwa na Vichwa Saba tafsiri ya KICHWA ni uongozi, au kiongozi.

JOKA/ kiongozi anayeongoza kupitia madhabahu ya shetani, ana Vichwa Saba/ viongozi waandamizi Saba. Viongozi hao waandamizi Saba wapo kuhakikisha JOKA anatawala watu, anahakikisha UOVU unatawala juu ya nchi.

7. JOKA KUTEMA MAJI KWENYE VICHWA VYA WATU, NA MAJI HAYO KUGEUKA GIZA.

TAFSIRI ya GIZA ni Ujinga/ UOVU/dhambi./ Machukizo/ Ibada ya sanamu.

Nyoka kutemea maji KWENYE VICHWA VYA WATU maana yake ni mtawala anayeongozwa na madhabahu ya Giza anatumia Vichwa 7/ waandamizi 7 kupeleka Giza Kwa wa Vichwa/ viongozi wa watu katika level za chini kuwajaza HOFU, Ujinga, Giza Ili washindwe kufanya maamuzi sahihi juu ya nchi Yao.

TAFSIRI YA JOKA KUWA KATIKA MAJI, NA MNYAMA KUWA KATIKA MAJI.

Maji ni watu, pia ni watu wa maeneo yenye maji au ukanda wa maji. Nchi yetu imebarikiwa maziwa na bahari zenye maji mengi.

JOKA lenye Vichwa Saba, ni mtawala mwenye waandamizi Saba ambao pia wanatokea maeneo yenye maji, ukanda wa maji, waliopata mamlaka kupitia madhabahu ya shetani/ JOKA

Mnyama kuonekana katika MAJI , ndotoni, location ni ukanda wa maji , nyanza Viktoria . TAFSIRI yake ni kiongozi Kutoka Kanda ya maeneo ya maji, na maji ni watu watakaompa nguvu mtawala, mnyama huyo.

8. MWANAMKE.

TAFSIRI ya mwanamke ni Kanisa. Si coincidence, Taifa kuongozwa na kiongozi mwanamke. Yapo mengi yanatokea Badala ya kuomba, watu wa Mungu wanalalamika. Uongozi kuwa chini ya mwanamke tafsiri yake ni Kanisa, watu wa Mungu wanaongoza, wanatakiwa kuomba, kumwombea, Kwa maana Mungu ndiye ameruhusu awe pale Ili kulifundisha na kuliadhibu Kanisa/ watu wa Mungu wamrudie Kwa mapigo mbalimbali kiuchumi, nk nk.

GENERAL TRANSLATION.

KANISA/ Watu wa Mungu ,ndio wenye turufu ya Kutoa kiongozi ajaye. Wawakatae viongozi wanaowalisha Ujinga( GIZA), wakatae kununuliwa Kwa RUSHWA, wajue umuhimu wa kuchagua viongozi Kwa HAKI na weledi na uwezo,

Na kiongozi huyo anatoka Kanda ya maji, na watu wanaotoka katika maji/ ukanda wa Maji, ndio watakaompa nguvu zaidi mnyama/ uongozi / kiongozi au mtawala huyo.

Na mwanamke kuingia nyumba ya Ibada ameshika kitabu na kurejea kukabidhi kitabu ndani ya nyumba ya Ibada, tafsiri yake, ni kuwa utatokea msuguano ambao mwishoni mtawala atasalimu na kukubaliana na Kanisa/ watu wa Mungu,

Na Kwa kuwa anakabidhi ndani ya nyumba ya Ibada, automatically, apokeaye mamlaka hiyo ni kiongozi wa Kanisa/ mtumishi. Kwa maana nyingine, Mwanamke/ Kanisa litatoa kiongozi wa Nchi ambaye ni mpakwa mafuta wa Mungu. Kwa wenye macho tayari wanaweza kupata picha ni nani huyo.

NYIKANI - Ni Mashariki, Nchi ya machweo ya jua, East Afrika. Tz ,Kenya na UG. Na Nchi iliyo salama, yenye Amani isiyomwaga Damu, iliyoshiriki kusaidia uhuru Kwa Nchi zingine Afrika, kisiwa Cha Amani, Bandari salama ni Tanga yika.

Nchi hii Ili matatizo yakome, ni Hadi mtawala aliyechaguliwa na Mungu akae kwenye KITI Cha mamlaka Ili aongoze sawasawa na maagizo ya Mungu na Sheria mama iliyo chanzo Cha Sheria na Katiba za Dunia.

2026, Inakuja njaa kubwa Dunia nzima, jua litasogezwa, litashushwa kidogo,ukame utakaoikumba Dunia Si wa kawaida, na ukame utadumu Kwa miaka 3 na nusu. Tulionya mvua za 2022 na kuendelea Kwa miaka 3 na nusu zitumike kukusanya na kutunza chakula ghalani, viongozi walisikia lakini nw wanapuuza tena, tunatakiwa tutunze chakula Kweli Kweli. Miaka Saba iliyobaki Hadi 2030 ni ya taabu kuu, lakini Nuru kuu itaonekana 2010 na kuendelea.

ITAENDELEA......... 1 June 2024.........
 
Hapo anaongelewa kahaba mkuu na mama wa makahaba katika ufunuo 17 na 18, aliyekuwa anamiliki biashara zote.
 
Hapo anaongelewa kahaba mkuu na mama wa makahaba katika ufunuo 17 na 18, aliyekuwa anamiliki biashara zote.
MWANAMKE WA KWANZA. ( Ufunuo wa Yohana 12:6-7).

Wanamke anayeongelewa aliyekimbulia Nyikani unaijua tafsiri yake?

Mwanamke wa Pili.(.Ufunuo 17:1....)anaongelewa Jezebel, mama wa makahaba, Roho ya Shetani, anaitwa pia malkia wa Baharini.

Unaelewa tafsiri ya ndoto hiyo?
 
Kwanza lazima ujue jambo hili
MWANAMKE WA KWANZA. ( Ufunuo wa Yohana 12:6-7).

Wanamke anayeongelewa aliyekimbulia Nyikani unaijua tafsiri yake?

Mwanamke wa Pili.(.Ufunuo 17:1....)anaongelewa Jezebel, mama wa makahaba, Roho ya Shetani, anaitwa pia malkia wa Baharini.

Unaelewa tafsiri ya ndoto hiyo?
Kwanza lazima ujue jambo hili

•Malkia wa mbinguni (yeremia 44:17-18)
•kahaba mkuu na mama wa makahaba (ufunuo 17&18)
•Mwanamke mchawi (kutoka 22:18)
•Yezebeli (1falme 19:1-2)
•Mama wa wote wenye uhai (mwanzo 3:20)
•ufunuo (ufunuo 12:1)
•wanawake saba (isaya 4:1)
• Nyoka (ufunuo 12:3)
• Vita (ufunuo 12:7)


Izo hapo juu ni nafsi za mvamizi zilizoangusha watakatifu wote (danieli 7:21,warumi 3:10) akiwemo kerubi (Ezekieli 28:13-16),aliyekuwa ameteka uumbaji kabla ya Muumba kuja mwenyewe (Mika 1:2-4, ufunuo 21:3, zekaria 14:9)

Na pia aliyepewa kusimamiwa uumbaji yaani moyo wa mwanzo (mwanzo 1:1) ilibidi ajibadili kwenye nafsi za miungu tisa mitakatifu kujinasua ila haikuwezekana ikiwemo

•Mwenyezi
•Yehova
•Mungu wa Majeshi
•Mungu wa Ibrahim,isaka na yakobo
•Mungu wa daudi
•Mungu wa roho za manabii
•Mungu wa danieli
•Mola
 
Kwanza lazima ujue jambo hili

Kwanza lazima ujue jambo hili

•Malkia wa mbinguni (yeremia 44:17-18)
•kahaba mkuu na mama wa makahaba (ufunuo 17&18)
•Mwanamke mchawi (kutoka 22:18)
•Yezebeli (1falme 19:1-2)
•Mama wa wote wenye uhai (mwanzo 3:20)
•ufunuo (ufunuo 12:1)
•wanawake saba (isaya 4:1)
• Nyoka (ufunuo 12:3)
• Vita (ufunuo 12:7)


Izo hapo juu ni nafsi za mvamizi zilizoangusha watakatifu wote (danieli 7:21,warumi 3:10) akiwemo kerubi (Ezekieli 28:13-16),aliyekuwa ameteka uumbaji kabla ya Muumba kuja mwenyewe (Mika 1:2-4, ufunuo 21:3, zekaria 14:9)

Na pia aliyepewa kusimamiwa uumbaji yaani moyo wa mwanzo (mwanzo 1:1) ilibidi ajibadili kwenye nafsi za miungu tisa mitakatifu kujinasua ila haikuwezekana ikiwemo

•Mwenyezi
•Yehova
•Mungu wa Majeshi
•Mungu wa Ibrahim,isaka na yakobo
•Mungu wa daudi
•Mungu wa roho za manabii
•Mungu wa danieli
•Mola
Usilazimishe kuelewa BIBLIA bila mafunuo na mwongozo wa Roho mtakatifu.
 
Usilazimishe kuelewa BIBLIA bila mafunuo na mwongozo wa Roho mtakatifu.
Sijalazimisha ndugu naelewesha kwa upendo (1korintho 13:13)maana hakuna aliyekuwa anayajua haya zaidi ya Muumba.

Maana dunia na ulimwengu waliificha kweli isijulikane ila sasa itajulikana maana Muumba ni mmoja na ni wa wote na anajitegemea yeye mwenyewe (warumi 11:36, 1korintho 15:24-28)

Yeye ni Moyo Halisi (Mithali 4:23, Mathayo 5:8) yaani mema na mazuri tu, sio roho wala nafsi au mwili.
 

Attachments

  • 4f3fff4a-1d8f-4784-861d-51862b8f8ffa.jpeg
    4f3fff4a-1d8f-4784-861d-51862b8f8ffa.jpeg
    119.1 KB · Views: 1
Watumishi wanashirikiana na viongozi wanaoongozwa na madhabahu ya Giza/ shetani wanakwiba pesa za miradi, pesa za mikopo,

Wanatumia pesa hizo hizo kuziba midomo ya wakaguzi Ili ionekane hakuna tatizo lolote.

Leo ni maandalizi ya sikukuu ya Pasaka Kwa wakristo, lakini pamepoa ni kama hakuna sikukuu,

Watu wa kipato Cha chini hawana pesa, pesa zinamilikiwa na kundi dogo.
 
Back
Top Bottom