Tishio la walio na madaraka

mabutu1835

JF-Expert Member
Nov 25, 2018
439
729
Hivi ni vitu vitatu vinavyotafuna viongozi wote duniani katika ngazi na maeneo mbalimbali. Vitu hivyo ni:

1: MAMLAKA: Viongozi wengi wanashindwa kutumia vyema nguvu na uhalali wa kuamrisha au kuagiza kutokana na nafasi walizo nazo kiasi cha kutumia isivyo sawa. Mfano mzuri utaona pale ambapo kiongozi anatoa maagizo ambayo mwisho wa siku wahusika au mhusika anaumia kiakili, kiafya na hata kiuchumi. Ukiwa kiongozi mahala popote kuwa makini na mamlaka yako, tumia busara na hekima sana katika kuamua au kuagiza. Rejea mfalme Daudi na mke wa kamanda wake.

2: UCHU WA FEDHA: Viongozi wengi katika nafasi walizo nazo kiu ya fedha kwao huwa kubwa kiasi cha kutokuwa na utu. Matukio ya rushwa na dhuluma ni matokeo ya Uchu wa kutaka kujilimbikizia fedha huku wakiwakandamiza walio chini yao. Pamoja na mishahara minono na marupuru waliyo nayo bado hudiriki hata kuchukua au kuminya haki za wengine.Viongozi wa ngazi mbalimbali katika maeneo mbalimbali ndio wanaoongoza kwa kupokea na kutoa rushwa.Rejea Yuda Iskarioti.

3: NGONO: Ulevi mkubwa wa viongozi wote ni mademu kwa wanaume na kwa wanawake ni vijana wadogo. Huu ni miongoni mwa mitihani ambayo viongozi wameonekana kushindwa. Baadhi ya matukio ya viongozi kufia guest ni ushuhuda tosha. Rejea mfalme/nabii Suleimani.

Ongeza vingine kama unavyo huku ukitoa ushauri au namna ya kushinda mitihani hii.
 
Hiyo namba 3 naweza kukubaliana nawe. Rejea kitabu cha marquis de sade. Cha 120 days of sodomy.
 
Back
Top Bottom