SMS zinatupunguzia wanaume pointi tatu muhimu

Wanawake wa sasa mbona pesa mnataka mtumiwe kwenye simu na si kuijia uso kwa uso?

Mbona watsap mnatuma sana sauti kuliko kuandika!?
 
Kama msikilizaji umekiri wao kukosa aibu kuzungumzia hizo story ndani ya daladala, Huyo mtongozaji atawezaje kumtongoza uso kwa uso?

Sitetei madomo zege ila stori yako inawapa lawama ya moja moja hao wanawake
Una akili sana....
 
Usiku kwenye daladala, saa ya simu yangu inaonyesha ni saa 4:47. Najilazamisha kuacha kusinzia, mara nasikia sauti za wanawake wawili wakizungumza viti vya nyuma yangu… stori zao zinanisaidia kukimbiza usingizi wangu.

Nasikia mmoja anamwambia mwenzake; “basi wakati namalizia kuosha vyombo akaja, eti ananiuliza vipi sasa? Nikajifanya sijui kinachoendelea, nikamuuliza vipi kuhusu nini? Akanambia nilichokuomba mchana, nikamuuliza kipi? Yaani nilikuwa najifanya kama vile nimesahau kila kitu, sikumbuki chochote.

“Basi akajizugisha zugisha pale ndio akanambia, nilikuomba namba yako. Nikamuuliza ya nini? Akanambia maswali gani hayo, nikamwambia si namba yangu, nitakupaje bila kujua ya nini. Akanambia kuna vitu nataka tuongee. Nikamwambia si uviongee hapa hapa. Akaniuliza kwani tukiongea kwenye simu kuna shida gani? Na mimi nikamuuliza kwani tukiongea hapa hapa huku tunaonana uso kwa macho kuna tatizo gani?

“Akaishiwa maneno, akanambia haya, nimeshindwa mimi, akaondoka.”
Nikiwa kwenye kiti changu nikajikuta natamani kugeuka kuwatazama hawa wanawake wawili angalau nijue wanaonekanaje, lakini tatizo ni kwamba, kama ningefanya hivyo ingeonekana wazi kwamba nawasikiliza na mimi nilikuwa sitaki tufikie huko nikaamua kujituliza, nikaishia kutengeneza picha ya namna walivyo nikitumia sauti zao na aina ya mazungumzo waliyokuwa wanayaongea kwa sauti bila soni kwenye usafiri wa umma.

Basi nikasikia yule mwanamke mwingine akicheka, yule msikilizaji; “He he heeee! Umemkomesha. Yaani hiyo ndio dawa ya vijanaume vya siku hizi. Vinapenda penda lakini havijui kutongoza, yaani tangu zimekuja simu na meseji wanaume hawajiamini kabisa kuongea mubashara. Wanakimbilia kuomba namba ya simu ili watume vimeseji vyao vya ajabu ajabu.”

Mwenzake akadakia; “Na emoji za kopa kopa.” kisha wote wakacheka kwa sauti utasema kwenye gari hakuna abiria wengine.

Ukiachana na kukosa aibu kiasi kwamba wanaweza kuongea mazungumzo ya aina hii kwenye usafiri wa umma, kitu walichokuwa wanakiongea huenda kina ukweli, wanaume siku hizi hatujiamini sana, hatujui kucheza na maneno kabisa, hususan uso kwa uso.
Ndiyo, tunajua vigori wenyewe siku hizi hawaelewi maneno makavu, kama ni mwanamume suruali utaimba mashairi yote, kuanzia ya hayati Sheikh Shaaban Robert mpaka ya William Shakespeare hutopata kitu, lakini hiyo haitunyimi uhuru wa kuonyesha makali yetu ya kusimama uso kwa uso na mrembo na kumuelezea yaliyojaa kwenye mtima wako.

Unajua uzuri wa kurusha makombora uso kwa uso ni kwamba ukikutana na kichwa ngumu anakuzodoa unaondoka umenywea, lakini bado ndani unajiona kidume. Na hiyo kuzodolewa ndio vijana siku hizi wanachoogopa, ndio maana wanakimbilia kuomba namba za simu, ili hata wakizodolewa iwe kwa njia ya meseji haiumizi kama ya ana kwa ana. Ebu tuache woga bwana.
sms-pc-data.jpg
 
Mimi ukiniona utadhani ni mtu smart sana. Ila kiufupi
1. Kutongoza siwezi
2. Kuomba namba siwezi
3. Kutongoza kwenye simu siwezi
4. Kuomba "koneksheni" siwezi
5. Hela sina

Kiufupi niponipo tu.
 
Mnatuchanganya!
 
Kwa mimi face to face inakuwaga nyepesi kuna muda unafika demu hana cha kukujibu anabaki kushangaashangaa tu na kubinya mikono, hapo unajua sound imekolea, ukiendelea kugonga msumari yeye mwenyewe anaomba kikao kiahirishwe mtapanga mengine siku nyingine, hapo nahakikisha natoka na nusu ya ushindi kwa gharama yoyote. Ila kwenye simu naonaga mizinguo coz ukimzidia na hakutaki anaweza asijibu txt au akakata simu na ukipiga hapokei.
 
Ukweli ni kwamba mishipa ya aibu za wanawake wengi imeshakatika unaongea na. Mtoto mzuri ana kwa ana anakukazia macho hawezi hata kuyalegeza anakuskiliza kwa makini mpaka mwamba unaanza kujistukia tayari uwoga unakuvamia mdogo unaisha maneno ukimya unakitawala na aibu juuu sasa mpira unakuwa umesogea kwake anaanza kukuzodowa na kukutolea kauli mbovu mnyamwezi unaamuwa kusepa hili ni moja.

Mbili ni hivi mazingira huwa yantufanya tukose kujiamini mtoto mzuri umekutana naye kwenye daladala au uchochoroni imagine umekuna na mtoto mzuri umetana naye lets say bar or lounge hivi kwa jinsi mvinyo na maneno matamu yanayotoka kinywani mwakao yatakunyima point.

Tatu sometime jaribu kutumia vitu kinachoweza kukutowa aibu story fupi kuna jamaa tulikuwa tumekaa naye jamaa ni mtumiaji wa marijuana mzuri kabisa ghafla akakipata katoto kazuri jamaa akakifuata na kuanza kuzoza mara wakaja pale tulipokuwa tumekaa jamaa aakaanza kushusha makombora yule jamaa nilimuona kma mchawi maana zilishuka kombora namuona binti akaanza kulegea taratibu.
 
Mimi siogopi kabisa na naenjoy kutongoza rekodi yangu ni kumtongoza koplo wa polisi aliekuja kusimamia mtihani wangu wa kidato cha sita nkisubiri kwenda kufanya dissection ya mende
Yes nlimtongoza akiwa amebeba sub machine gun yake half magazine..
Mara ya mwsho nlitongoza kiziwi kwenye basi ya abood nlikua nkiongea anasmile tu kumbe anisikiii
 
Usiku kwenye daladala, saa ya simu yangu inaonyesha ni saa 4:47. Najilazamisha kuacha kusinzia, mara nasikia sauti za wanawake wawili wakizungumza viti vya nyuma yangu… stori zao zinanisaidia kukimbiza usingizi wangu.

Nasikia mmoja anamwambia mwenzake; “basi wakati namalizia kuosha vyombo akaja, eti ananiuliza vipi sasa? Nikajifanya sijui kinachoendelea, nikamuuliza vipi kuhusu nini? Akanambia nilichokuomba mchana, nikamuuliza kipi? Yaani nilikuwa najifanya kama vile nimesahau kila kitu, sikumbuki chochote.

“Basi akajizugisha zugisha pale ndio akanambia, nilikuomba namba yako. Nikamuuliza ya nini? Akanambia maswali gani hayo, nikamwambia si namba yangu, nitakupaje bila kujua ya nini. Akanambia kuna vitu nataka tuongee. Nikamwambia si uviongee hapa hapa. Akaniuliza kwani tukiongea kwenye simu kuna shida gani? Na mimi nikamuuliza kwani tukiongea hapa hapa huku tunaonana uso kwa macho kuna tatizo gani?

“Akaishiwa maneno, akanambia haya, nimeshindwa mimi, akaondoka.”

Nikiwa kwenye kiti changu nikajikuta natamani kugeuka kuwatazama hawa wanawake wawili angalau nijue wanaonekanaje, lakini tatizo ni kwamba, kama ningefanya hivyo ingeonekana wazi kwamba nawasikiliza na mimi nilikuwa sitaki tufikie huko nikaamua kujituliza, nikaishia kutengeneza picha ya namna walivyo nikitumia sauti zao na aina ya mazungumzo waliyokuwa wanayaongea kwa sauti bila soni kwenye usafiri wa umma.

Basi nikasikia yule mwanamke mwingine akicheka, yule msikilizaji; “He he heeee! Umemkomesha. Yaani hiyo ndio dawa ya vijanaume vya siku hizi. Vinapenda penda lakini havijui kutongoza, yaani tangu zimekuja simu na meseji wanaume hawajiamini kabisa kuongea mubashara. Wanakimbilia kuomba namba ya simu ili watume vimeseji vyao vya ajabu ajabu.”

Mwenzake akadakia; “Na emoji za kopa kopa.” kisha wote wakacheka kwa sauti utasema kwenye gari hakuna abiria wengine.

Ukiachana na kukosa aibu kiasi kwamba wanaweza kuongea mazungumzo ya aina hii kwenye usafiri wa umma, kitu walichokuwa wanakiongea huenda kina ukweli, wanaume siku hizi hatujiamini sana, hatujui kucheza na maneno kabisa, hususan uso kwa uso.

Ndiyo, tunajua vigori wenyewe siku hizi hawaelewi maneno makavu, kama ni mwanamume suruali utaimba mashairi yote, kuanzia ya hayati Sheikh Shaaban Robert mpaka ya William Shakespeare hutopata kitu, lakini hiyo haitunyimi uhuru wa kuonyesha makali yetu ya kusimama uso kwa uso na mrembo na kumuelezea yaliyojaa kwenye mtima wako.

Unajua uzuri wa kurusha makombora uso kwa uso ni kwamba ukikutana na kichwa ngumu anakuzodoa unaondoka umenywea, lakini bado ndani unajiona kidume. Na hiyo kuzodolewa ndio vijana siku hizi wanachoogopa, ndio maana wanakimbilia kuomba namba za simu, ili hata wakizodolewa iwe kwa njia ya meseji haiumizi kama ya ana kwa ana. Ebu tuache woga bwana.

Mwananchi
sawa
 
Kaniuliza kama nina demu nikamwambia sina/
Anahisi ashaniona sehemu tatizo kanisahau jina/

Unaitwa nani? Ncha Kali
Unaishi wapi? Ghetto
Kazi yako nini? Mpishi

Domo linakuwa zito niongee kipi cha maana!
Kivipi nimkazie jicho wakati mtoto kasimama!
Au nijikombee maujiko kwamba sitaki kujuana?
hizi mistari naziimba ila nakosea yaani nimesahau huu wimbo wa nani!!hahhahah
 
shida unamuomba akusubiri halafu anakuuliza unasemaje??!!
unashusha mistari unamaliza anakwambia ndio ulichonisimamishia??!!
yaani nyie wanaume mkiona mtu tayari mnaanza usumbufu!!
unaona AIBU msela unajikataa huku unajifanya unapokea simu skioni kuua noma!!hahahha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom