ACCOUNT FULL
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 1,984
- 360
Wakuu habari,
Jana nilikuwa nahitaji kumtumia Mtu Account namba yangu ili anitumie pesa nikatoe, hii yote ni katika kupunguza gharama ya Makato.
Nikamuandikia SMS, mimi natumia mtandao wa Tigo, niliandika Majina kamili, jina la bank husika na namba ya Account cha ajabu kila nikituma ile SMS, SMS inakataa kwenda, nikituma sms ya kawaida inaenda, nikajaribu kuandika sms ndefu zaidi bado ikaenda, nikirudia kuituma ile sms ya Account namba ikawa bado inakataa!
Cha kushangaza nilipoamua kuzituma zile namba za Account kwa mafungu, SMS ilikubali kwenda nikajaribu pia kuituma ile Account namba tupu (bila majina yangu wala jina la bank, yani ikaonekana kama Vocha tu) SMS ilikubali kwenda!
Leo pia nimejaribu, matokeo ni yale yale.
Je, kuna uwezekano Tigo wamezuia watu kutumiana Account namba ili tutumie tigo pesa yao kwa sisi wateja wa Tigo?