Utapeli mpya wa mtandao

Zogoo da khama

JF-Expert Member
May 20, 2013
622
582
Wakuu ninaomba kushare nanyi suala hili...

Ilikuwa siku ya Jumamosi ya tarehe 23/05/2020 nilipokea taarifa kutoka kwa wife akinitaarifu kuwa ametapeliwa na wakala wa mitandao ya simu aliyekuwa amevalia mavazi na kitambulisho cha kampuni ya TIGO.

Wakala huyo alifika dukani kwake na kumwambia kuwa anaunganisha vifurushi vya chuo, hapo dukani palikuwa na wateja wawili ambao nao waliomba kupatiwa hiyo huduma kutoka kwa wakala huyo na walionesha kuridhika na huduma yake.

Wife alivyoona wateja hao wamepatiwa huduma na wameprove inafanya kazi vizuri naye aliomba aunganishwe. Alimpatia simu wakala huyo na, kutokana na maelezo yake, alikuwa anashuhudia kila kitu alichokuwa anafanya. Kwa maelezo yake ni kwamba alitumia muda mwingi katika eneo la APN.

Baada ya dakika kadhaa alimaliza shughuli yake na kumrudishia wife simu yake na alimtaka ajaribu kama mtandao unafanya kazi ambapo mwanzoni uligoma, akamrudishia simu akaenda tena kwenye APN akarekebisha akamwambia ajaribu ndipo mtandao ukarudi.

Alimuaga na kumuhakikishia kwamba kila kitu kipo vizuri na atarudi baadae ili kupata mrejesho. Katika mchakato wote huo, wakala hakuomba wala kuonesha dalili yoyote ya kutaka kufahamu Namba za Siri (Passwords) za TigoPesa wala SimBanking katika mazungumzo yake.

Baada ya wakala huyo kuondoka wife alipata hitaji la kuhamisha fedha kutoka CRDB SimBanking kwenda kwa mtu aliyemuagiza mzigo. Tatizo lilianza kila anapoingiza menu ya SimBanking (*150*03#) anapata error inayoleta ujumbe 'Try Again....'

Baada ya kujaribu muda mrefu bila mafanikio alinipigia na kuniuliza endapo SimBanking yangu, nilimwambia ipo poa. Aliconfirm pia na watu wengine na kuambiwa kuwa hakuna tatizo lolote. Ndipo alianza kuhisi hali ya hatari kwamba kuna kitu kimefanywa na yule wakala katika simu yake.

Alipiga simu Huduma kwa Wateja @CRDBBankPlc akataarifiwa kuwa muda mfupi uliopita ametoa fedha (kiasi kimehifadhiwa) kutoka katika akaunti kwenda kwenye namba ya @VodacomTanzania 0743938273 iliyosajiliwa kwa jina la NYAMIZI MASANJA.

Pamoja na wife kuwataarifu Bank situation nzima iliyotokea still Bank walisisitiza kwamba fedha hizo amezihamisha yeye! Kitu pekee ambacho walishindwa kukitolea maelezo hadi sasa ni error ya 'Try Again'.... ambayo ni kama vile amekuwa blocked asiaccess menu ya SimBanking totally!

Alipiga simu @VodacomTanzania na kutaarifiwa kwamba fedha hiyo imeshatolewa kwa wakala na hivyo hawana cha kusaidia. Tuliwarudia tena @Tigo_TZ nao walilisitiza kwamba kwakuwa transaction hiyo haijahusisha TIGOPESA basi wao hawahusiki kwa lolote, hivyo tufuatilie @CRDBBankPlc.

Pia namba hiyo ya wife imeunganishwa na NMB Mobile Banking, tulipoangalia salio huko napo (via ATM) tulikuta pesa yote iliyokuwepo imechukuliwa. Na kila tukiingiza menu ya Mobile Banking ya @NMBTanzania (*150*66#) inaleta same error ya 'Try Again...'!!

Kiufupi ni kwamba wakala huyo ameweza kubreak accounts zote ambazo zimekuwa linked na hiyo namba ya @Tigo_TZ na kuziblock zisiweze kutumika kupitia namba hiyo hadi sasa. Namba za siri zote zinatofautiana hivyo ni ngumu kufanya guesswork katika muda mfupi kiasi kile na kufanikiwa.

To cut the long story short, ni kwamba tangu siku hiyo ya Jumamosi, wife hawezi tena kuaccess CRDB SimBanking wala NMB Mobile Banking, hapati meseji za TIGOPESA, vifurushi na meseji zozote zinazohusiana na huduma za @Tigo_TZ.

Even Internet imekuwa superslow, app karibu zote katika simu yake hazifunguki except WhatsApp only! Meaning kwamba Google, Facebook, n.k. hazifanyi kazi tangu siku hiyo ya Jumamosi. Na wife hutumia Traditional USSD Codes kuaccess Mobile Banking Accounts zake na hatumii Apps zao.

Wakuu, ninaomba msaada wenu wa kimawazo, inawezekanaje a person kubreach systems za Bank kirahisi na ndani ya muda mfupi kiasi hicho? Is it possible mhusika wa hiyo crime akawa ni mmoja au ni organized crime?

Au kuna uwezekano wa 'Wakala' (criminal) kutumia Hacking Device/Software/App ambayo ina uwezo wa kuscan log files/strokes za password zote zilizokuwa typed kwenye simu pamoja na kulock/kublock kila kitu kinachohusiana na namba/device husika?

Wasiwasi wangu unazidi kuongezeka pale ninapofikiria uwezo wa huyu criminal (s) kudeny access ya accounts zako via Sim/Mobile Banking bila hata ya Taasisi husika kung'amua hilo. Je, itakuwaje endapo mtu akipoteza/akiibiwa simu, akiwa anachajisha kwa malipo or whatsoever!?

Je, kutokana na aina hii ya uhalifu, fedha zetu zipo salama? Mifumo ya Benki zetu ipo strong enough kuzuia aina hii ya uhalifu? Jumamosi, mshahara wote wa wife pamoja na hela yote ya biashara imepotea ndani ya nusu saa, na hajaweza kuaccess Mobile Banking zake hadi sasa.

Nani atakayegharamia damages zote zilizotokea tangu Jumamosi? Ninaamini hii itakuwa eyeopener kwa taasisi zote za fedha husika zikiwezo taasisi za kichunguzi @tanpol, @TzPccb, wadau na wananchi wote kwa ujumla!

Ninatanguliza shukrani na mniwie radhi kwa andiko refu.
 
Ni ajabu kwangu kuhamisha pesa bila password!

Je kama mke wako ameamua kutuma hiyo pesa kwa mchepuko wake ili wajenge kwa siri, baada ya mwaka akutoroke? akaishi nae
NB : polLE SANA BRO
 
Poleni sana cheapest always is expensive, pesa ni salama sana shida ni uzembe wake amempa simu amehack simu card na kuwa yy ndo controller wa hiyo no kwa mda.
 
There is absolutely no way ya kuweza ku hack kupata password tena inayoingizwa kwa njia ya USSD kwa kushika simu tu. Kama hii story sio chai basi mkeo anajua alipopeleka hela na iyo kufail kwa line Ni trick ya kujilinda. Imeandikwa tuishi nao kwa akili ... Over
 
Shemeji yetu amekosea sana, kwa kifupi huyo tapeli angefanya Dizain ya Idris Sultan kwa sasa mkeo angekuwa nyuma ya Nondo za Segerea kusubiri mashtaka. Kumpa mtu mwingine simu iliyosajiliwa kwa jina lako siyo busara hata kidogo.
 
Huu ni ushahidi tosha kuwa zoezi la usajili wa SIM cards kwa vitambulisho vya taifa lilikuwa upotevu wa muda tu.

Toka hii taarifa ianze kusambaa huyo NYAMIZI MASANJA angeshapatikana.
 
Ina maana uzi huu sio halisi, ni fake, ni CTRL-C + CTRL V. Stori hii imeshaletwa wiki iliyopita na watu wameijadili sana hapa hapa JF.

Kwa kuwa wewe umeshaiona hivyo stori ni fake..?

Sio wote tulipata kuiona, binafsi nimejifunza kitu japo kwa maswali bila majibu... naomba tuwekee huo uzi hapa au ‘nitag’ huko unasema watu wameijadili sana nikapate elimu.
 
Hakuna cha utapeli mpya hapo bali ni uzembe wauyo mwanamke wako.Unaaminije mtu kirahisi rahisi nakumpa simu yako wakati dunia yenyewe ina mambo mengi hivi.Kutapeliwa siku zote ni ujinga na uzembe wa mtapeliwa.
 
Ncha Kali nimeshakupeleka kwenye uzi urijino. Hapa inawezekana tunajadili kitu halisi lakini tunachanganyikiwa kwa sababu kilishaletwa na mtu mwingine wiki iliyopita.
 
Back
Top Bottom