Ama kweli UALIMU kazi ya wito
MWANAFUNZI mmoja hajui kujumlisha wala kutoa. Mwalimu katumia njia zote kumuelimisha lakini wapi ikabidi ajaribu njia hii.
Mwalimu: Kwenu mnafuga nini?
Mwanafunzi: Kuku na mbuzi
Mwalimu: Mbuzi mnao wangapi?
Mwanafunzi: 25
Mwalimu: Mbuzi 25 toa mbuzi 5 watabaki wangapi?
Mwanafunzi: Unawajua mbuzi wetu au unawasikia? Ukimtoa mmoja tu nje wote wanatoka!
Mwalimu: Mmh! Naacha kazi mimi kama mambo yenyewe ni hivi, basi tena.
*************************************
Mrembo alipokea simu ngeni na mambo yalikuwa kama hivi:
Simu: Hellow una boy friend?
Mrembo: Ndio nine. Kwani we nani?
Simu: Mimi baba yako. Kumbe una boy friend ukirudi utanitambua. Simu ikakatika akiwa na mawazo nini afanye. Simu ikaita tena kwa namba ngeni.
Simu: Hello una boy friend?
Mrembo: Hapana sina!
Simu: Vipi mpenzi ina maana unanisaliti?
Mrembo: Hapana BABY nilijua baba!
Simu: Ni mimi baba yako nilitaka kuhakikisha tu kama kweli una boy friend. UTANIKOMA LEO!
*********************************
Fikiria ingemuwa baba yako ni Remmy Ongala, na mama yako Anne Makinda. Mjomba wako ni Mizengo Pinda na shangazi yako ni Anna Mkapa. Babu yako ni Stephen Wasira na bibi yako ni Bi. Kidude. Je sura yako ingekuwaje?
***********************************
Mwanasheria alimuuliza Lulu, Mbona wewe malaya sana? Lulu akajibu, Rose Muhando ndio malaya kwani Ameonja hadi Utamu wa Yesu. Mwanasheria akaguna!!
************************************
Jamaa alikuwa anasumbuliwa na panya akaamua kuwategea sumu kwenye nyama ya nguruwe. Kesho yake akakuta karatasi imeandikwa 'TUWEKEE KWENYE SAMAKI SISI WENGINE NI WAISLAM'