WANDUGU LEO ASUBUI NIMEPATA SMS TOKA +358897578, ZINZOMKASHIFU DR. SLAA, ZIMEANDIKWA HIVI; slaa ni mropokaji na mgomvianayelumbana na vyombo vya ulinzina usalama wa nchi, anataka damu imwagike ili mradi ashinde. tusikubali nchi yetu iwe kama burundi....
sasa ninajaribu kujua namba hii ni ya mtandao gani, kwa sasa nipo moshi , najua na wengi mmepata sms hizi. naomba mwenye kuelewa huu ni mtandao gani na uko nchi gani tujue.
isije ikawa kuna nchi zimeamua kuingilia uchaguzi wetu
pili, huwa napata sms za kuisifu ccm toka mitandao yote ya voda na tigo, naomba wanasheria wanisaidie kwani nataka kuwashtaki tigo na voda kwa kutoa namba yangu ya simu bila ridhaa yangu, pengine nitawaunganisha na TCRA kwa kuwa zoezi la kusajili namba za simu halikuwa na maana ya kuanza kutoa namba za watu ili waanze kupelekewa sms za matusi kama hayo juu. naomba kama kuna wanasheria makini huku wani sms nianze mapema mchakacho wa kuwashtaki hawa
That code is from finland. CCM sasa inatapatapa. wanajaribu kufanya kila njia kujiokoa but it's too late. Pia nasikia mtoto wa makampa yuko voda uenda hao ndo wanatoa namba za watu.naomaba mod nirekebishie hapo juu, ni dr.slaa siyo slamm nimeandika kwa hasira
Ndugu zangu Ile timu ya kijana Miraji Kikwete na wa IT wake wameibuka na mbinu ya kutuma SMS kwa kila mtu anayemiliki simu ya mkononi ili kumfanya Mh Slaa asikubalike kwa wananchi, Moja ya sms hizo ambazo zipo njiani zinakuja ni nii..
Sms kutoka No. +3588976578
Slaa ni mropokaji na mgomvi anayelumbana na vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi. Anataka damu imwagike ili mradi ashinde. Tusikubali nchi yetu iwe kama Burundi, Congo au Somalia. Hana uwezo wala sifa ya kuwa Rais. Tumuepuke Slaa kama ukoma, Tusidanganyike.
Kwa muono wangu huu ni uchochezi, na tusikubali kuingizwa katika chuki zidi ya mgombea wetu
dawa ni kuiripoti hiyo number kwenye tume lakini pia kwenye international forum ili mwenyewe ajulikane... Ni lazima iwe registered somewhere
alternatively, ni chadema/kafu nao kufungua like kama hizo na kusambaza ujumbe wenye mantiki hiyohiyo ili ku-neutralize the effects
Mwaka huu kazi kweli kweli, hadi ifike 31 Oktoba 2010 tutaona na kusikia mengi tu!! Hii namba iliyotuma ujumbe yaonekana si ya hapa nchini, ina maana mtumaji message anaishi huko nje au yuko hapa nchini kwenye roaming akaunt? Hivi +358 ni suffix ya nchi gani?