Inachukua muda gani kupata namba ya NIDA?

vert boy

Member
Nov 29, 2023
18
23
Habari za wakati huu wana jamii.

Hivi inachukua muda gani kupata namba ya NIDA baada ya kujiandikisha katika ofisi zao? Nakumbuka ilikuwa tarehe 9 October 2023 nilienda kujaza taarifa zangu katika ofisi za NIDA (wilaya ya Siha Kilimanjaro) nilikamilisha kila kitu hadi picha.

Niliambiwa nirudi baada ya wiki mbili ili kwenda kuchukua namba yangu ya NIDA. Wiki mbili zilipoisha nilienda lakini wahudumu wa pale wakaniambia hakuna mtandao na tatizo hilo lipo nchi nzima, wakaniambia nirudi baada ya siku tatu au nifuatilie online, nimejaribu kila njia lakini sijafanikiwa chochote mpaka leo.

Ukizingatia mimi ni mwanafunzi nilipaswa kwenda chuo mwaka jana ila nimeshindwa kutokana na kukosa namba ya NIDA. Nahitaji kufahamu itanichukua muda gani kupata namba ya NIDA?

Naomba kuwasilisha
 
Wiki 3 tu, ilivyo kosa katika hizo wiki mbili ulizo ambiwa ulirudi kuuliza nini tatizo?
 
Nida wanajikuta sana..mashine za Nida na zile zavitambulisho vya kura hazina tofauti sana ..lakini wanavyo kuzungusha sasa unafikiri unawaomba ajira wao..yamejaa majinga majinga ofsini kupoteza mda tu kupokea mshahara..kazi 0.0
 
Habari za wakati huu wana jamii.

Hivi inachukua muda gani kupata namba ya NIDA baada ya kujiandikisha katika ofisi zao? Nakumbuka ilikuwa tarehe 9 October 2023 nilienda kujaza taarifa zangu katika ofisi za NIDA (wilaya ya Siha Kilimanjaro) nilikamilisha kila kitu hadi picha.

Niliambiwa nirudi baada ya wiki mbili ili kwenda kuchukua namba yangu ya NIDA. Wiki mbili zilipoisha nilienda lakini wahudumu wa pale wakaniambia hakuna mtandao na tatizo hilo lipo nchi nzima, wakaniambia nirudi baada ya siku tatu au nifuatilie online, nimejaribu kila njia lakini sijafanikiwa chochote mpaka leo.

Ukizingatia mimi ni mwanafunzi nilipaswa kwenda chuo mwaka jana ila nimeshindwa kutokana na kukosa namba ya NIDA. Nahitaji kufahamu itanichukua muda gani kupata namba ya NIDA?

Naomba kuwasilisha
INATEGEMEA NTU NA NTU.
 
Back
Top Bottom