Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwa makini na kuchukua hatua za haraka kurejesha amani kabla Watanzania hawajaishiwa uvumilivu na utawala wa serikali yake.

Dk. Slaa amesema kuongezeka kwa matukio ya matumizi ya nguvu ya dola katika kulinda uhalali wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiasi cha kufikia hatua ya kuua watu wasiokuwa na hatia, yanadhihirisha kuwa muda si mrefu ujao nchi itakuwa haitawaliki tena ikiwa Kikwete ataendelea kufumbia macho mauaji hayo.

Akifungua Ofisi ya Baraza la Vijana wa chama hicho (Bavicha) Mtaa wa Togo, Dar es Salaam jana, Dk. Slaa alisema kuwa mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola chini ya serikali ya CCM kupitia kwa viongozi wake hususan Jeshi la Polisi, hayawezi kuvumilika tena na yanawasukuma wananchi kufikia mwisho wa uvumilivu.

Alisema sasa kuna dalili zote za wazi zinazotishia amani na mustakabali wa nchi na watu wake, zikiifanya nchi isitawalike, na wala serikali haiwezi tena kukwepa lawama za kuhusika na mauaji ya wananchi, na kutolea mfano wa tukio la kutwangwa risasi kwa watu wanne wasiokuwa na hatia waliokuwa wakiandamana kudai haki ya kulindwa na serikali yao mkoani Ruvuma mapema wiki hii.

Dk. Slaa akizungumza kwa uchungu alisema mauaji ya Songea yalitokana na uzembe wa hali ya juu wa viongozi wa serikali na vyombo vya dola ngazi ya wilaya na Mkoa wa Ruvuma.

“Napenda kutoa kauli juu ya mauaji dhidi ya raia yaliyofanywa na Jeshi la Polisi huko Songea. Kwa taarifa nilizonazo, mauaji yale yametokea kwa sababu ya uzembe wa hali ya juu na ufinyu tu wa akili ya viongozi, akiwamo mkuu wa Mkoa na polisi wale. Hivi unawaambiaje raia wenye uchungu na vifo vya wananchi wenzao, waliojikusanya na kuamua kuandamana kudai haki, eti wachague kiongozi wa kuonana na mkuu wa mkoa,” alisema.

Aliitaka serikali kuunda tume huru ya kuchunguza mauaji hayo ya Songea na kudai kuwa hakuna uhalali wowote wa viongozi wa serikali wa mkoa ambao ni watuhumiwa wa mauaji hayo kuunda chombo cha kuchunguza.

“Tunawapongeza wananchi na hasa vijana wa Songea kwa kuandamana kudai haki. Tunataka ufanyike uchunguzi huru juu ya mauaji hayo, yatakayoihusisha mahakama (Korona) na mkuu wa mkoa na polisi hawana uhalali wa kuunda tume za kuchunguza kwani wao pia ni watuhumiwa katika tukio hilo,” alisema.

Katibu mkuu huyo wa CHADEMA alilaani tukio la juzi usiku, ambapo polisi katika mji wa Tunduma wanadaiwa kushusha bendera za chama hicho katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

Alisema kitendo hicho ni uchokozi tosha kwa CHADEMA na kimelenga kuleta fujo nyingine zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani.

“Niliwasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, pia mkuu wa mkoa, niliwaambia mimi sipendi kugombana nao kwa masuala ya hovyo kama hayo, tupo kwa mujibu wa sheria, bendera zetu zinatokana na kodi za Watanzania, wakasema eti zingine ziko sokoni, nikawauliza za CCM huwa zinawekwa wapi?

“Watu hawana maji, hawana zahanati, elimu inashuka, mkuu wa wilaya hajawahi kuamuka usiku, lakini kwenye kushusha bendera za CHADEMA wanaamka usiku wa manane,” alisema.

Alitumia wasaa huo kuwataka vijana wa CHADEMA wasimamie haki na kupinga dhuluma na uonevu popote pale wanapofanyiwa Watanzania na wahakikishe wanajua kinachoendelea katika maeneo ya Songea na Tunduma ili chama hicho kijue hatua za kuchukua.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche, mbali ya kumshukuru Dk. Slaa na makao makuu ya chama hicho kwa kuwawezesha kuwa na ofisi yao, alisema kuwa watakuwa mstari wa mbele kusimamia malengo ya chama hicho hasa katika kutetea haki za Watanzania, kudai uwajibikaji wa viongozi na serikali kwa wananchi, pia kulinda rasilimali za taifa.

Alisema kuwa vijana watakuwa mstari wa mbele katika vuguvugu la mageuzi yanayoendelea nchini, akisema kuwa ofisi hiyo itakuwa sehemu sahihi ya kuendeshea mipango ya ukombozi wa taifa ambalo pamoja na utajiri wa rasilimali za kila aina, bado wananchi wake wanaishi katika umaskini wa kupindukia.

Dr. Slaa nataka nione akifuatilia na kutupa majibu yaliyo sahihi ktk hili suala la kushusha bendera za cdm ili tujue kama kiongozi mkubwa akienda shm bendera za upinzani zinatakiwa ziondolewe, basi nasi tutamwalika kiongozi wa cdm huku kwetu ili tuondoe nasi uchafu wa bendera za ccm huku kwetu ambapo zimekuwa kero
 
Cha msingi tuendelee kuwakataa viongozi hawa na serikali yao na chama chao,na tujitokeze waziwazi kukataa kila tunapoona wanakiuka haki za binadamu hasa wanapozidi kuendeleza mauaji ya wananchi,na siku hizi mauaji ya raia ni jambo la kawaida sana kufanywa na polisisiemu na serikali yake na wala hakuna anayehoji wala kuchukua hatua ndani ya serikali na wala CCM magamba hawajawahi kukemea mauaji na uonevu wote unaofanywa na serikali ya CCM-magamba

Watakemea je wakati wao ndo wamewatuma?
 
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba kiongozi wa nchi ambaye anatakiwa kuhakikisha usalama wa Watanzania hatatia neno kufuatia kuuawa kinyama kwa Watanzania hawa. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi~AMEN

Na walioaga dunia wakawaandalie hawa wote wanaosababisha yote haya kuni za kutosha ili pindi watakapokwenda huko wasicheleweshewe kwa kukosekana kuni
 
CCM=CHAMA CHA MASHETANI, CHAMA CHA MAJAMBAZI, CHAMA CHA MAUAJI, CHAMA CHA MAJONZI, CHAMA CHA MAFISADI, CHAMA CHA MATAJIRI, CHAMA CHA MAOVU,CHAMA CHA MAKAFIRI, CHAMA CHA MAJERAHA, CHAMA CHA......1 day 2tawasahau hawa jamaa!WIMBI LA MABADILIKO LIMESOGEA!
 
Tanzania ni nyepesi sana na wananchi wake tupo tupo tu ndiyo mana ccm inafanya lolote wawezalo wakijua na kuamin kuwa hatuna lolote la kuwafanya.

zaidi ya yote wanafurahia sana huu ulofa wa kuchekelea hata maovu yanapofanywa na ccm mlangoni mwa majumba yetu. Kila uchao wanaimba amani na utulivu, ili waendelee kututwanga risasi kwa kuhofia nguvu ya umma.

Kwanza hata sielewi hao ndugu wa Generali Kombe wanasubiri nini kuwasafirisha ahera hao polisi walioachwa huru kwa mauaji ya ndugu yao. Wawamalize tu kwa risasi, mbona warundi na wasomali wako wa kutosha kabisa kuwakodisha wawamalize wale polisi.
 
CCM=CHAMA CHA MASHETANI, CHAMA CHA MAJAMBAZI, CHAMA CHA MAUAJI, CHAMA CHA MAJONZI, CHAMA CHA MAFISADI, CHAMA CHA MATAJIRI, CHAMA CHA MAOVU,CHAMA CHA MAKAFIRI, CHAMA CHA MAJERAHA, CHAMA CHA......1 day 2tawasahau hawa jamaa!WIMBI LA MABADILIKO LIMESOGEA!

Mbona mkuu unakua na jazba mpaka unasahau sifa yao nyingine?CHAMA CHA MACAMEROON
 
a. Wanaharakati mko wapi au mnasubiri tu kuja kuandika mi-ripoti ndefu mara baada ya familia kadhaa nchini kupoteza zaidi y nusu ya ukoo wao?

b.
UDASA huu ukimya wenu tafsiri yake ni kujiunga na mdhulumishi au tuwaelewe vipi?

c.
Tangnyika Law Society ndio tuseme mpaka O'Campo awe ametoa neno ndio mtiririko wote huu wa mauaji katika mkoa mmoja baada ya nyingine ipate kuwagusa?

d.
Akina Mama kwenye taasisi zenu zote kama vile UWT inamaana uchungu wa mtoto wa mke mwenzio wala haukuhusu kitu isipokua ni jukumu la Mama Nkya na Kijo Bisimba peke yao sio?

e.
Enyi wanafunzi wa vyo vikuu nchini mliopata kua VIWAKILISHI VYA SAUTI YA HAKI KATIKA JAMII, mnaona ni vema hadi afe mtu wa ngapi tangu Mauaji ya raia Mwembechai, Pemba, Arusha, Igunga, Musoma, Uyole-Mbeya, na sasa Songea, ndio mpate hata kuguna tu juu ya mwenendo wote huu wa mambo?

f.
Kamisheni na taasisi zote za haki za binadamu nchini, inamaana hata kukemea tu muaji haya yote ni mpaka kupatikane mfadhili kutoka nje ya nchi ndio akawape fedha ndio mpate kutekeleza majukumu yenu?

g.
Vyombo vya maamuzi ya Juu nchini kama vile NEC-CHADEMA, NEC-CCM, Baraza la Mawaziri na Taasisi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivi kweli vikao vya dharura mtaweza kuviitisha tu pindi mambo ya kisiasa yanapowaendeeni vibaya kwa njia moja au nyingine na wala si kule KUTOLEWA ROHO Mtanzania mwenzetu??

h. Hivi kweli Tanzania tumefika mahala ambapo uhai wa raia ni sawa tu na uhai wa inzi na wala halichukuliwi kwa uzito wake kama ambavyo tumewahi kusikia enzi hizo Mzee Mwinyi alipokua Waziri wa Mambo ya Ndani?

i.
Wazee wetu tunaowaheshimu saaana katika taifa hili; Joseph Sinde Warioba, Salim Ahmed Salim, Benjamin Mkapa, Edwin Mtei, Bob Makani, Mufti Mkuu Sheikh Simba, Mwashamu Askofu Polycarp Pengo, Jenerali Ulimwengu, Rejnald Mengi, Mzee Bahresa ...

!!
Umewasahau BAKWATA
 
Ni ajabu na kweli; yaani vifo vya raia Songea lakini Rais Kikwete yeye anaendelea kujisherehesha na Makirikiri Botswana.

Safari ya nyuma kidogo ilikua ni vifo hospitali zote nchini kufuatia mgomo wa Madaktari (ambao kuna kila dalili kujirudia tena kwa kuwa siku 30 za ahadi ya serikali kwao ndio hizo zinayoyoma bila mabadiliko yoyote), huku yeye akiwa anakula good time mawinguni kuelekea Davoa Uswisi.

Ndio sasa mtu amkumbushe kutuma salamu za rambirambi hivi sasa wakati wale wanaouuwa ni sawa tu na inzi tena waliobandikwa jina WAHUNI na kiongozi mwandamizi mojawapo huko serikalini??????
 
Chanzo cha mapinduzi ya Libya had nothing to do na Uislam na 'kupinga katuni ya udhalilishaji wa mtume.'

Beginnings of protests

Between 13 and 16 January, upset at delays in the building of housing units and over political corruption, protesters in Bayda, Derna, Benghazi, Bani Walid and other cities broke into, and occupied, housing that the government had been building. Protesters also clashed with police in Bayda and attacked government offices. By 27 January, the government had responded to the housing unrest with a €20 billion investment fund to provide housing and development.

"In late January, Jamal al-Hajji, a writer, political commentator and accountant, "call[ed] on the Internet for demonstrations to be held in support of greater freedoms in Libya" inspired by the Tunisia and Egytian revolutions. He was arrested on 1 February by plain-clothes police officers, and charged on 3 February with injuring someone with his car. Amnesty International claimed that because al-Hajji had previously been imprisoned for his non-violent political opinions, the real reason for the present arrest appeared to be his call for demonstrations. In early February, Gaddafi, on behalf of the Jamahiriya, met with political activists, journalists and media figures and warned them that they would be held responsible if they disturbed the peace or created chaos in Libya."
Wikipedia.

Kwa hiyo usituambie eti walikuwa wanapinga katuni ya Mtume, wamedhalilishwa, wanapinga katuni ya Mtume kwani Libyan government ndio ilichora katuni ya Mtume?
Fwatilia, kule Benghazi, wanafamilia wa waandamanaji waliouwawa pale walipoandamana kulaani ile katuni iliyochorwa yenye kumdepict mtume wao, waliuwawa na serikali ya Gadaffi, na aliwachukulia kwamba ni mujahedeen, hata alipoohojiwa alisema hao ni alkaeda, mwanaharakati aliyekuwa akiwatetea alikamatwa na kupelekwa makao makuu ya polisi Benghazi kuhojiwa na Al Senusi mwenyewe ambaye ni chief of intelligence, akimmuliza kuwa nia yake haswa ni nini? na kumtaka aachane na hayo mambo ya kampeni ya kuanzisha mapinduzi kwa kupitia mtandao,(this is due to the so called Arab Spring), wananchi walipopata taarifa, kwa wingi wao wakakusanyika nje ya polisi kudemand aachiwe, na ikabidi aachiwe, kuanzia hapo moto haukuzimwa, hilo lilikuwa ni tukio la kwanza hapo february kuelekea mapinduzi, wananchi waliamuwa kupambana na hao polisi wenye kuwanyima haki.

Usipende kukurupuka na wikipedia, siyo kila kitu kinaweza kuwa backed up na wikipedia, hapo ni pa kuanzia tu kuelekea kwenye ukweli wenyewe wakati unafanya research, wikipedia haikubaliki hata kwenye academics.
 
...wikipedia haikubaliki hata kwenye academics.
haya, mimi nimetoa changu na wewe tupe chanzo chako kinachokubalika kwenye 'academics' kinachosema mapinduzi ya Libya chanzo chake ni maandamano ya kupinga katuni ya Mtume!
 
KATIKA KUJENGA KATIBA SLAA ALIKUWA MNYONGE KAMA MBWA MFYATA MKIA. lEO ETI ANATAKA KUMHADHALIHA KIKWETE. Slaa ni hatari kudanganya watu kupita Kar Max na Angels walioleta ukomunisti duniani/
 
Back
Top Bottom