Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

Unasema Dr slaa weka mbali na wanawake.Wewe Hammy-D kaa mbali na Juliana Shonza pia Kule İgunga mke wa mtu vipi? Nyani hacheck ......le
 
Sideeq,
Kwa bahati mbaya hata hujui mazingira yaliyomfanya Dr Slaa kusema, Kikwete kama hutarekebisha na na kuendelea kwa Hali hii nchi haitatawalika. Naomba niwaambie Watanzania, kuwa sijutii kutoa onyo Hilo, na Leo naomba kulirudia, tena kwa mdisitiso zaidi.

Ningependa Watanzania tufike mahali na kuacha ushabiki na itikadi kwenye mambo yasiyohitaji ushabiki na itikadi. Kwa Mara ya Kwanza kauli hiyo niliitoa kwenye Mkutano tarehe 5 January 2011 siku ambayo kwa Mara ya kwanza Polisi wametumia mabomu mengi ya Machozi na Risasi za Moto na kuua watu 3 ( kwa taarifa ya Serikali).

Leo miaka 3 baadaye, ninairudia kauli hiyo kwa ujasiri zaidi, baada ya kuisoma Taarifa ya Kamissioner wa Haki za Binadamu Mhe. De Mello ( ambaye sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu). Taarifa hiyo, haikuwekwa hadharani, kwa kuwa Serikali iliona inaidhalilisha.

Nilichokisema, kinathibitishwa na Taarifa hiyo,

(1) Wahalifu wa Siku hiyo wa kwanza ni Polisi kwa kufuta maandamano ya Chadema yaliyokuwa halali mpaka usiku yalipofutwa na polisi bila kufuata utaratibu wa Sheria. Taarifa inataja kabisa kuwa Sheria ya vyama vya siasa ilivunjwa na polisi.
2) haki za binadamu zilivunjwa na Polisi kwa kutumia nguvu kubwa kinyume na Sheria, na Taarifa iliwataka wahusika wote kuchukuliwa hatua.
3) IGP ndiye kinara wa kuvunja Sheria kwa kuingilia kuzuia maandamano kinyume na Sheria.

Baadhi ya Watanzania wakaendeleza ushabiki wa "Dr Slaa kachochea kwa kueleza nchi haitatawalika"..... Taarifa hiyo ya Arusha, inathibitishwa kwa mara ya pili na Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu ( ambayo ni chombo cha Serikali) ambayo nayo katika tukio la Mabomu lililosababisha kifo cha Mwandishi wa Habari Daudi Mwangosi, Polisi wakiongozwa na Kamanda Kamuhanda ndio wanaotuhumiwa kuvunja Sheria ya vyama vya siasa kwa kuingilia mikutano ya Chadema ten a ya ndani. Katika Tukio la Mwangosi, naye msajili wa vyama vya siasa anatuhumiwa kuvunja Sheria ya nchi kwa kuzuia mikutano ya Chadema wakati sheria ya Sensus haizuii shughuli.

Watanzania wenye kutafiti na kusoma Taarifa hizi badala ya kuandika kwa ushabiki. Kwa Taarifa yako ndio maana Dr. Slaa anaconda nje, kwa kuwa Serikali inajua onyo lilikuwa sahihi, kwa mujibu wa sheria, na lingetekelezwa maisha ya watanzania yasingeliangamia. Aidha, yote niliyoonya, mishahara, maisha magumu, ufisadi, ulinzi wa rasilimali za Taifa, tusingelifika tulipofika Leo. Serikali ijilaumu yenyewe, na mashabiki nanny mnasehemu yenu ya lawama.

noted, and well said Dr.
 
Baba V wewe ni mtu mzima, ningependa utoe mchango ambao ni constructive kwa ajili ya kukijenga chama chako. Bila upinzani imara na madhubuti, CCM italemaa.

Pumba tupu!! CCM bila upinzani italemaa halafu uko hapa kutwa kucha ukikusanya buku 7 kwa siku katika juhudi za kuisambaratisha chadema. Una upungufu wa akili wewe nenda kwa wataalamu wakakusaidie kabla hujaharibikiwa kabisa.
 
Vijana wa ccm msipoacha kutumia hayo madawa yanayouzwa na mabosi wenu mtawehuka siku si nyingi
 
Hii ni kauli mbiu ya Dr. Slaa. Kwani aliianza punde tu baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 na amekuwa akiirudia mara kwa mara kila anapopata nafasi kuongea na vyombo vya habari sema wananchi hawashawishiki kwa maneno tu.


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwa makini na kuchukua hatua za haraka kurejesha amani kabla Watanzania hawajaishiwa uvumilivu na utawala wa serikali yake.

Dk. Slaa amesema kuongezeka kwa matukio ya matumizi ya nguvu ya dola katika kulinda uhalali wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiasi cha kufikia hatua ya kuua watu wasiokuwa na hatia, yanadhihirisha kuwa muda si mrefu ujao nchi itakuwa haitawaliki tena ikiwa Kikwete ataendelea kufumbia macho mauaji hayo.

Akifungua Ofisi ya Baraza la Vijana wa chama hicho (Bavicha) Mtaa wa Togo, Dar es Salaam jana, Dk. Slaa alisema kuwa mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola chini ya serikali ya CCM kupitia kwa viongozi wake hususan Jeshi la Polisi, hayawezi kuvumilika tena na yanawasukuma wananchi kufikia mwisho wa uvumilivu.

Alisema sasa kuna dalili zote za wazi zinazotishia amani na mustakabali wa nchi na watu wake, zikiifanya nchi isitawalike, na wala serikali haiwezi tena kukwepa lawama za kuhusika na mauaji ya wananchi, na kutolea mfano wa tukio la kutwangwa risasi kwa watu wanne wasiokuwa na hatia waliokuwa wakiandamana kudai haki ya kulindwa na serikali yao mkoani Ruvuma mapema wiki hii.

Dk. Slaa akizungumza kwa uchungu alisema mauaji ya Songea yalitokana na uzembe wa hali ya juu wa viongozi wa serikali na vyombo vya dola ngazi ya wilaya na Mkoa wa Ruvuma.

“Napenda kutoa kauli juu ya mauaji dhidi ya raia yaliyofanywa na Jeshi la Polisi huko Songea. Kwa taarifa nilizonazo, mauaji yale yametokea kwa sababu ya uzembe wa hali ya juu na ufinyu tu wa akili ya viongozi, akiwamo mkuu wa Mkoa na polisi wale. Hivi unawaambiaje raia wenye uchungu na vifo vya wananchi wenzao, waliojikusanya na kuamua kuandamana kudai haki, eti wachague kiongozi wa kuonana na mkuu wa mkoa,” alisema.

Aliitaka serikali kuunda tume huru ya kuchunguza mauaji hayo ya Songea na kudai kuwa hakuna uhalali wowote wa viongozi wa serikali wa mkoa ambao ni watuhumiwa wa mauaji hayo kuunda chombo cha kuchunguza.

“Tunawapongeza wananchi na hasa vijana wa Songea kwa kuandamana kudai haki. Tunataka ufanyike uchunguzi huru juu ya mauaji hayo, yatakayoihusisha mahakama (Korona) na mkuu wa mkoa na polisi hawana uhalali wa kuunda tume za kuchunguza kwani wao pia ni watuhumiwa katika tukio hilo,” alisema.

Katibu mkuu huyo wa CHADEMA alilaani tukio la juzi usiku, ambapo polisi katika mji wa Tunduma wanadaiwa kushusha bendera za chama hicho katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

Alisema kitendo hicho ni uchokozi tosha kwa CHADEMA na kimelenga kuleta fujo nyingine zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani.

“Niliwasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, pia mkuu wa mkoa, niliwaambia mimi sipendi kugombana nao kwa masuala ya hovyo kama hayo, tupo kwa mujibu wa sheria, bendera zetu zinatokana na kodi za Watanzania, wakasema eti zingine ziko sokoni, nikawauliza za CCM huwa zinawekwa wapi?

“Watu hawana maji, hawana zahanati, elimu inashuka, mkuu wa wilaya hajawahi kuamuka usiku, lakini kwenye kushusha bendera za CHADEMA wanaamka usiku wa manane,” alisema.

Alitumia wasaa huo kuwataka vijana wa CHADEMA wasimamie haki na kupinga dhuluma na uonevu popote pale wanapofanyiwa Watanzania na wahakikishe wanajua kinachoendelea katika maeneo ya Songea na Tunduma ili chama hicho kijue hatua za kuchukua.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche, mbali ya kumshukuru Dk. Slaa na makao makuu ya chama hicho kwa kuwawezesha kuwa na ofisi yao, alisema kuwa watakuwa mstari wa mbele kusimamia malengo ya chama hicho hasa katika kutetea haki za Watanzania, kudai uwajibikaji wa viongozi na serikali kwa wananchi, pia kulinda rasilimali za taifa.

Alisema kuwa vijana watakuwa mstari wa mbele katika vuguvugu la mageuzi yanayoendelea nchini, akisema kuwa ofisi hiyo itakuwa sehemu sahihi ya kuendeshea mipango ya ukombozi wa taifa ambalo pamoja na utajiri wa rasilimali za kila aina, bado wananchi wake wanaishi katika umaskini wa kupindukia.
 
Mwaka 2010 baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania kumalizika na chama cha mapinduzi kushinda kupitia dr Jakaya Kikwete kwa takribani asilimia 61 na kufuatiwa na Dr slaa wa chadema aliyepata asilimia 26 ya kura zote za watanzania.
Dr Wilbroad Slaa alitoa kauli ambayo bado imeendelea kuleta tafsiri tofauti mpaka leo hii kwa watanzania wengi wapenda amani. Tafsiri hizo hutokea kwasababu ya matukio mbalimbali yanayoashiria uvunjifu wa amani kama Bomu la Olasiti, Kuuwawa kwa Mwangosi katika maandamano ya chadema, kumwagiwa tindikali viongozi mbalimbali wa dini, maandamano ya chadema yalio kinyume na sheria n.k
Katika gazeti la Rai la tarehe 20/1/2011 kupitia mwandishi wake Mayage s mayage ameandika barua kumsihi dr slaa kuachana na kauli yake ya kuwa 'NCHI HAITOTAWALIKA'. Pia mwandishi huyo alimpigia simu na kumuambia dr slaa 'najua umeniambia kuwa dhamira yako na chama chako ni nchi isitawalike ili serikali ishindwe kutimiza majukumu yake', na kumsihi aachane nayo.
Ukweli na kila mtanzania alikuwa anajua Chadema hakina uwezo wa kushinda uchaguzi ule, sasa ni kipi kilimpelekea dr Slaa kuhamaki kiasi kile baada ya matokeo na mpaka kufikia kutoa kauli ile? Nini khaswa agenda ya siri na 'NZITO' ilikuwa imejificha nyuma ya dr na chama chake? Je wanachadema mnaijua agenda hiyo ya siri au mnafuata upepo tu wa mambo.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA
NAMUOMBEA MUNGU RAISI JK AMALIZIE MIAKA YAKE MIWILI ILIYO BAKIA KWA AMANI NA KAULI YA DR ISHINDWE JAPO IMESABABISHA MENGI KATIKA KIPINDI HIKI CHA UONGOZI WA JK.
Nawasilisha.
 
Hivi karibuni Rais wetu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alifanya ziara katika mkoa wa Geita na katika ziara hiyo aliamuru wenye makarasha yao katika eneo la MAGEMA waondoke mara moja ili kupisha mradi wa maji safi kwa wakazi wa Geita mjini kukamilika kwa wakati uliopangwa. Rais alitoa agizo hilo baada ya kutaarifiwa kuwa mradi huo wa maji hautakamilika kwani wenye makarasha hayo wako karibu na hifadhi ya maji na wanachangia sana kuyachafua maji hayo na kuyafanya yasiwe salama kwani wanatumia kemikali aina ya mercury ambayo ni hatari. Cha ajabu ni kuwa tangu amri hiyo itolewe, hii ni wiki ya tatu na hakuna hatua yoyote ambayo imechukuliwa na jeshi la polisi ikizingatiwa kuwa agizo hilo lilitolewa na Amiri Jeshi mkuu.... Inasikitisha sana kuona kuwa nchi yangu imefikia kutotawalika sijui nikimbilie wapi. Isitoshe wenye makarasha husomba mawe kwa kutumia pikipiki ambazo hubeba viroba hivyo pamoja na abiria zaidi ya mmoja (mishkaki) na hupita mbele ya kituo cha polisi cha geita na hawachukuliwi hatua yoyote...sijui kama tutafika kweli. Naomba kuwasilisha.
 
Ungeandika kiswahili labda kwa mbaaali ungeeleweka hicho kisukuma wengi hatukijui.
 
Soma taarifa yangu hapo juu vizuri utapata jibu, Rais ni kiongozi wa juu kitaifa ametoa agizo lakini halitekelezwi, nani mwingine atatoa agizo zaidi yake ili litekelezwe, nadhani umeelewa
 
Poleni sana kwani sahiv polisi wamepelekwa Iringa kumdhibiti Dr. wa ukweli
 
Hizo ni sehemu za Ahadi za Kikwete tu... Nchi inatawalika ila Ahadi za Kikwete ndio hazitekelezeki...
 
NCCR NA CUF HII NI KWENU.

kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo chama cha CCM kilipata ushindi kwa mgombea wake ndugu Kikwete kuwa rais kwa kipindi cha pili,mara baada ya hapo kulitokea matamko mbalimbali kwa upinzani hasa CHADEMA kwa kutoa matamko ya kwamba nchi haitatawalika.

NCCR na CUF niwakumbushe kuwa mmeamua kuungana na CHADEMA na kujiita UKAWA na kukwamisha mchakato wa kupata katiba mpya.niwakumbushe NCCR na CUF kwamba CHADEMA wamekuwa watu wa vurugu sana na ninyi kujiunga nao nawaambia kuwa dhambi hiyo ya kukwamisha mchakato wa katiba mpya hamtasamehewa na vizazi vijavyo,mosi mnaendeleza nchi kutotawalika.

Muogopeni MUNGU na viongozi wanaoamini katika Mgomo haufai.

Nawasilisha
 
Mmaranguoriginal ulikuwa unataka kusemaje?issue ni nin hapa?
 
Jifunze hata kuandika kiswahili vizuri. Ok, hii hadithi yako inafundisha nini?
 
Back
Top Bottom