SKONGA: Kipindi 'kinachovua nguo' wanafunzi

Kuna mwanafunzi wa kidato cha tatu,aliulizwa binadamu ana figo ngapi??
Akasita kwanza (akionyesha hajui figo ni nini)......kisha akajibu MOJA...
Ilivyofika Wakati wa kuimba sasa...nilichoka...

so sad
 
Umesaema atlas nimekumbuka, tulikuwa tunapenda kucheza michezo wa kutafuta miji kwente atlas.
Anayeona, anachagua yeye mji mtafute.

Ilikuwa inasaidia sana kujua ramani, it was fun.
Hivi tuna ramani ya mikoa mipya kweli? Uoto wa asili sijui na ma nini nini?

mkuu umenikumbusha mbali kweli. Ule mchezo ulisaidia sana kupanua ufahamu wa jiografia ya dunia. Sasa kila somo lingekuwa na vichemsha bongo ambavyo wanafunzi kwa wakati wao wangekuwa wanapashana ingesaidia sana.
Kwanza pangekuwa na siku nzima katika wiki ambayo wanafunzi wangeongozwa na mwalimu husika katika kuchemshana juu ya ufahamu wa kiujumla wa masomo wanayofundishwa. Hii ingesaidia sana wanafunzi kukumbuka na kuondoa hofu juu ya maarifa ya kiujumla
 
Elimu iliyokufa imekuja kufufuliwa na Kikwete na imeanza kupanda kuliko wakati wowote ule. Kwa mtu mwenye macho lakini asiye na muono kama wewe, huwezi kuyaona hayo.

Hivi hawa watoto wasiojua binadamu ana figo ngapi wako katika utawala wa Rais yupi? Hivi katika historia ya elimu nchi hii na duniani ulishaona wapi Baraza la Elimu likirisiti kama sio Tanzania chini ya JK? Tukirudi kwenye hoja ya msingi, nini cha ziada kifanyike ili hawa watoto chini ya utawala huu wawe na uelewa wa masomo na mazingira yanayowazunguka? Ni sahihii kwa leo mwalimu kuingia darasani na gazeti mathalan uhuru na kuwapa wanafuzi waanze kulichambua? Them days were superb!
 
kwa elimu kama ile bado tutakuwa palepale kama hatutaboresha mazingira ya utoaji waelimu yenyewe,kipindi hicho wanafunzi wachache walipata nafasi ya kwenda sekondari na pia shule zilikuwa chache,tukbali hii ni changamoto kwetu sote wazazi,wadau waelimu,wanasiasa,serikali..nilichogundua wengi tunaopiga kelele na kuilaumu mojamoja serikali,kwanza kabisa watoto au wadogo zetu hawasomi hizi shule za watoto wa makabwela,naona kelele za lawama nikama kuwacheka waliokasa nafasi ya kuwapeleka watoto wao shule za gharama juu..Elimu yetu ndio msingi imara wa ukombozi wa Tanzania

Mimi sio mtaalamu sana wa mambo hayo so naomba nikae pembeni!!! Ila nilipenda sana mfumo ule...
 
Leo lunch nilikuwa naongea na mama mtu mzima kabisa mid 60s anasema anapenda kuangalia hicho kipindi kwa sababu kinaonyesha jinsi wanafunzi wa shule za Tanzania hawajui kitu. Amesikitishwa sana. ameseama wakati wakiwa shuleni wanafunzi walikuwa wanajiamini na hata maswali mengine wanayouliza yeye anayajua.

Anachosema elimu ya siku zile ilikuwa bora kwa mbali sana.
 
Ni kweli hii?
Mimi ni msikilizaji mzuri wa Skonga kwani kila nikiangalia kipindi hiki siachi kucheka kwa jinsi wanetu wanavyotoa majibu ya utumbo,hii niliisikia live laini haikuwa hivyo.Binti mmoja wa kidato cha nne aliyedai kuwa anaweza sana somo la historia aliulizwa wewe unatoka mkoa gani?,akajibu mkoa wa tabora,akaulizwa tena ni mtemi gani mashuhuri kutoka mkoa wa Tabora?akajibu mimi nina siku nyingi sana sijaenda Tabora hivyo watemi wa sasa hivi siwafahamu,kwa mshangao mtangazaji akamuuliza kwani wewe neno mtemi unalielewaje?binti akajibu mtemi ni mtu mbabe anayefanya fujo kwenye madisco!

Hivi hawa watoto wasiojua binadamu ana figo ngapi wako katika utawala wa Rais yupi? Hivi katika historia ya elimu nchi hii na duniani ulishaona wapi Baraza la Elimu likirisiti kama sio Tanzania chini ya JK? Tukirudi kwenye hoja ya msingi, nini cha ziada kifanyike ili hawa watoto chini ya utawala huu wawe na uelewa wa masomo na mazingira yanayowazunguka? Ni sahihii kwa leo mwalimu kuingia darasani na gazeti mathalan uhuru na kuwapa wanafuzi waanze kulichambua? Them days were superb!

Hao wamefundishwa na Waalim waliotokea tawala zilizopita, au hujuwi hilo? Unanchekesha.

Sasa tazama waalimu wanaokuja kutolewa na utawala huu halafu uwaone wanafunzi wao miaka si mingi ijayo.
 
sio wanafunzi tuu wanaohitaji kupaongeza maarifa yao..hata wazazi na wanajamii kwa ujumla...swali ni kua......na sisi kama wazazi, tunafanya hayo mambo?
au tatizo ni kwa wote,wazazi na watoto
 
Umesaema atlas nimekumbuka, tulikuwa tunapenda kucheza michezo wa kutafuta miji kwente atlas.
Anayeona, anachagua yeye mji mtafute.

Ilikuwa inasaidia sana kujua ramani, it was fun.
Hivi tuna ramani ya mikoa mipya kweli? Uoto wa asili sijui na ma nini nini?

Kusema kweli tulikuwa tunapata uelewa mpana wa Jiografia. Darasa la nne Jiografia ya Tanzania, la tano Jiografia ya Africa, darasa la sita ya Ulimwengu na Darasa la saba Jiografia ya Afrika Mashariki.

Humo utajua mazao gani yanalimwa wapi na yanakuzwa vipi, unajua tofauti ya hali ya hewa toka sehemu moja mpaka nyingine. Utafahamu mito mikubwa, maziwa, majangwa nk nk. Utajua hesabu za longitudo na latitudo.

Na kuna zile hadithi tamu na zenye mafunzo bila kusahau kitabu cha Kiingereza na mtoto Musa na familia yao, na shule anayosoma ya Mtakuja Primary school.

Hivi hata somo la sanaa lipo kweli?
 
Hao wamefundishwa na Waalim waliotokea tawala zilizopita, au hujuwi hilo? Unanchekesha.

Sasa tazama waalimu wanaokuja kutolewa na utawala huu halafu uwaone wanafunzi wao miaka si mingi ijayo.

Imebidi nicheke. Unazungumzia hawa Walimu wa toleo la kipindi hiki!! Nina bahati ya kuishi nao ama kukutana nao..Ni msiba! Tena ukiongezea na ugumu wa maisha "product" zitakazotoka baada ya miaka 5 ni balaa mara mbili ya hili tulilonalo.
 
Labda hujuwi mipango na mikakati ya elimu inavyokwenda sasa hivi. Big Results.
 
Nawashauri wenye vijana jitahidini sana uweke DSTV premium,,kuna channels kama history,discovery world,national geographic,crime and investigation,,,,hapa kijana wako atajifunza mengi kuanzia history,people who are shaping our world through various achievements,,,ila pia kila wiki asome vitabu vya biography,psychological,inspirational i tell the sky will be his/her limits,,hii ni kwa wazazi pia
 
Labda hujuwi mipango na mikati ya elimu inavyokwenda sasa hivi. Big Results.

Hakuna mipango ya Elimu iliyo siri. Na kwa bahati nzuri ni rahisi kuona matokeo yake. Hao wanafunzi unaowaona hawajui hata Mtemi Mirambo ni mtu gani ama mto Rufiji uko Tanzania ama Malawi ndiyo Walimu wa baadaye!

Hata wale wachache walio afadhali hutawaona wakishika chaki, na hata kama wakishika ni kwa mpito tu! Labda kama unaamini katika miujiza.
 
Vipindi vya burudani na miziki kwenye TV za Taifa ziwe baada ya saa tatu usiku. Masaa yaliyobaki viwe vipindi vya shule na dokyumentari zinazofundisha.
Mimi nilikuwa naamka usiku kutazama music ,saa 6 usiku .enzi hizo ni Itv tu.So hata hawa wataamuka tu aisee
 
Hakuna mipango ya Elimu iliyo siri. Na kwa bahati nzuri ni rahisi kuona matokeo yake. Hao wanafunzi unaowaona hawajui hata Mtemi Mirambo ni mtu gani ama mto Rufiji uko Tanzania ama Malawi ndiyo Walimu wa baadaye!

Hata wale wachache walio afadhali hutawaona wakishika chaki, na hata kama wakishika ni kwa mpito tu! Labda kama unaamini katika miujiza.

Mazao ya kuporomoka kwa elimu chanzo chake ni Nyerere na vibaraka wake, nani alifuta masomo ya History na Geography mashuleni? na nani kayarudisha?
 
Mimi nakushauri wewe ukitaka watoto wako wawe na upeo
leta magazeti ya maana nyumbani
why unafikiri watoto wa kihindi wana general knowledge zaidi kuliko wa kiswahili?
wahindi karibu kila familia wanasoma Daily News nyumbani
sababu ndo Bussiness zao nyingi hata matangazo yao ya vifo na ndoa yapo humu
sasa linganisha Daily News na magazeti ya udaku tunayoyajaza majumbani?
bado ukute mna mikanda ya Kanumba tele
watoto watapata wapi general knowledge??
kuna familia hata taarifa ya habari ya saa mbili usiku hawatazami
mwendo ni mikanda ya Kanumba tu

Umeongea kitu cha muhimu na kweli kabisa.. Magazeti serious yanaongeza general knowledge. Kila mzazi ajitahidi kuleta nyumbani magazeti ya maana na vitabu na si magazeti pendwa na bongo movies!
 
Mazao ya kuporomoka kwa elimu chanzo chake ni Nyerere na vibaraka wake, nani alifuta masomo ya History na Geography mashuleni? na nani kayarudisha?
Umeshavimbiwa futari sasa unatuletea mashuzi tu hapa, wewe kwa Nyerere ni sisimizi tu na wala hapatakuwa na FaizaFox day wala Mwinyi day wala Kikwete day, ila ipo Nyerere day na itaendelea kuwepo, na Nyerere ndio symbol ya Tanganyika & Tanzania, huu ndio ukweli ambao hutoweza kuubadili kwa post zako uchwara hapa JF.
 
This is not random selection. Ulitegemea Rais akafungue kimeo? Hata kati ya vipofu mwenye chongo mfalme. Elimu yetu dada Faiza imedidimia hasa miaka ya karibuni

Mkuu umenigusa sana jinsi unavyojaribu kuwa objective kwenye hii topic muhimu,
Kwa kuwa vijana wetu wako kidigital zaidi, tubadili mfumo wa utoaji wa elimu nao uwe kidijital zaidi?

Mimi binafsi redio BBC, DW na sauti ya america zimenisaidia sana nilianza kusikiliza tangu shule ya msingi, general knowledge inapatikana kwenye vyanzo vingi sana. tungeangalia hata jinsi vyombo vyetu vya habari vina endeshwaje (Biashara huria) kama asilimia kubwa ni miziki na burudani, unategemea nini, achilia mbali mambo ya Fiesta na Big brother.

Hii ni changamoto kwa kweli.
 
Mazao ya kuporomoka kwa elimu chanzo chake ni Nyerere na vibaraka wake, nani alifuta masomo ya History na Geography mashuleni? na nani kayarudisha?

Huenda ukawa sahihi kwamba tulianguka wapi, kosa letu tumeshindwa kutengeneza na hali inazidi kuwa mbaya!
 
Back
Top Bottom