Ushauri wa Wasomi: Mabadiliko ya mitaala hayahitaji hisia; kurugenzi ya Mafunzo ya Wizara ya Afya ifuate kanuni.

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Sep 28, 2010
851
1,216
Mkufunzi Mstaafu na Mbobezi wa Mitaala.

Siku chache zilizopita niliona andiko katika mitandao ya kijamii lenye kichwa cha habari, “BILA ‘D’ TANO HAUSOMI FAMASIA” na katika andiko hilo kulikuwa na picha ya Mfamasia Mkuu wa Serikali. Nimejaribu kufuatilia kwa ukaribu habari ile nikagundua kuwa kumbe kuna vuguvugu kubwa la mitaala ya vyuo vya kati hapa nchini.

Baada ya kufuatilia kwa wadau na wengine ni wanafunzi wangu, nimejiridhisha kuwa Mfamasia mkuu wa Serikali na Kurugenzi ya mafunzo wizara ya afya ni ama uwezo wao katika kuendesha mambo ya kitaaluma hasa yanayohusiana na mitaala ni mdogo sana. Na kama wanaelewa kanuni za mitaala basi ni kudhalilisha utaalamu na ni dharau kwa taaluma.

Nasikia Mfamasia Mkuu wa Serikali Ndg. Daudi Msasi anazungumza juu ya kuwa na wataalamu wenye ubora, nasikia mabaraza ya famasia na uuguzi na ukunga yanazungumza hicho hicho. Ni sawa, pamoja na kwamba kwa kuwasahihisha kidogo, hapa tunazungumzia umahiri. Sasa inavyoonekana wanataka ubora wa wanafunzi wanaomaliza kozi za afya utokane na vigezo vya kujiunga. Hapa ndio changamoto ilipo. Yaani hawaelewi kanuni za mitaala kabisa.

Huwezi kupata ubora wa muhitimu au umahiri wa muhitimu yeyote yule kutoka wenye vigezo vya kujiunga na kozi yoyote. Ubora au umahiri unapatikana kwenye maudhui ya mtaala na utekelezaji wake. Vigezo vya kujiunga lengo lake ni kumwezesha atakayejiunga aweze kumudu mafunzo, kama yanavyotakiwa na mtaala husika.

Kitaalamu kanuni za kuandaa mitaala zipo na ni lazima zifuatwe ili kupata mitaala bora. Vigezo vya kujiunga katika programu yoyote vinawekwa mwishoni, kwa kuangalia maudhui ya mtaala ambayo mwanafunzi mtarajiwa atapaswa kufunzwa. Hapa ndio utaona sasa kwa maudhui haya ili anayetaka kusoma aweze kumudu maudhui ya mtaala anatakiwa awe na uelewa upi. Ni jamo la kitaalamu kabisa.

Kwa mtaala uliotengenezwa vizuri na kuangalia uhusiano uliopo kati ya maudhui na vigezo vya kujiunga, ukimchukua mtu asiye na vigezo hivyo ukamuweka katika mafunzo hayo, atashindwa kumudu mafunzo hayo, atafeli, wanaita ku-disco. Hawezi kuyamudu. Kwa mfano uchukue kijana aliyemaliza kidato cha nne, aliyefaulu somo la historia, biolojia na kiingera kwa ufaulu hata wa alama A, halafu mengine yote amefeli, ukasema asome usanifu majengo (Architect), hataweza kumaliza masomo, yatamshinda. Kwa sababu ufahamu wa hesabu na fizikia ni muhimu sana.

Lakini ukiona ameyamudu mafunzo na amefaulu, amemaliza halafu ukasema sio msanifu majengo mahiri, hapo shida haipo kwenye vigezo alivyoingilia katika kozi, shida ipo kwenye maudhui ya mtaala. Anafundishwa kitu gani na anapimwaje? Na kama akiudu mafunzo na akawa mahiri basi, pengine changamoto ipo kwenye maudhui ya elimu yake ya kidato cha nne. Kwa mfano huo maana yake, kuna shida kwenye upimaji huko kidato cha nne, ka maana anaoneka amefeli hesabu na fizikia lakini anaufahamu wa kutosha kuwemzesha kumudu maudhui ya mtaala wa usanifu majengo.

Mitaala ya kozi za afya, mitihani ya kuwapima inatungwa na wizara ya afya, mitihani hiyo inasimamiwa na wizara ya afya tena siku hizi na polisi na vyombo vya usalama wapo, tofauti na huku kwenye uhandisi. Inasahihishwa na Wizara ya afya, na vijana wanafaulu. Halafu anapokuja kwenye utendaji mabara ya kitaaluma nayo yanawapa mtihani halafu eti wanafeli. Maswali ni mengi sana hapa, sijui nani anam-fool mwingine.

Halafu badala ya kuangalia maudhui ya mitaala na utekelezaji wake, wasomi hawa kama wanavyojiita, wanakimbilia vigezo. Nimefuatilia wadau wanasema mitaala mingi iliyofanyiwa mabadiliko haina tofauti kubwa. Na mingine ni ku-copy na ku-paste, hii ni dhahama kubwa katika nchi.

Wasomi hawa hawatumii takwimu za kitafiti, hawafuati kanuni za kitaaluma za uandaaji mitaala, wamekuwa watu wa mihemko tu na propaganda ambazo kama msomi ukizisikia zinakatisha tamaa. Wasomi wanaotumia mihemko na propaganda katika masuala ya taaluma, katika weledi waangaliwe vizuri, hawafai, watatulete majanga makubwa.

Nadhani ni wakati wa serikali kupitia Waziri wa Afya, kuangalia vizuri. Pengine wasomi hawa waliopewa dhamana wanampima Waziri wa Afya, kwa sababu ya profession yake. Wanakiuka kanuni za uandaaji mitaala, hawana takwimu na zilizopo hawazitumii vema.

Wizara ya afya inatumia mabilioni ya fedha kutunga, kusafirisha, kusimamia na kusahihisha mitihani. Mabaraza nayo yanatumia fedha nyingi kutunga, kusafirisha, kusimamia na kusahihisha mitihani. Na fedha hizi ni za watanzania, vijana wanalipa fedha nyingi za mitihani. Swali ni Je, mitihani hii inaendana na mitaala iliyopo? Mitihani hii inapima umahiri. Tena nimesikia mitihani ya baraza la uuguzi na ukunga na baraza la famasia imefutwa, imevuja. Na imekuwa kama kitu cha kawaida kuvuja na kufutwa kila uchao.

Sasa, wizara, au mabaraza yenye wataalamu wasomi wanaojinadi kuwa walikuwa na vigezo vya juu vya kujiunga (japo tunajua wengine hawakuwa navyo) mbona wanashindwa kusimamaia mitihani na inavuja hovyo?

Naomba nishauri mambo kadhaa;
  • Mosi, nashauri, kurugenzi ya mafunzo wizara ya afya iangaliwe vizuri mwenendo wake, ili isije kuleta madhara kwa taifa.​
  • Pili, Mfamasia mkuu wa serikali naye aangaliwe vizuri, ajue namna ya kuwa rational na sio emotional kama anavyo-comment kwenye makundi yetu ya WhatsApp.​
  • Tatu, kanunzi za ku-set vigezo zifuatwe kikamilifu kwa kuangalia maudhui ya mtaala, si jambo la kubishana ni jambo la kitaalamu hili.​
  • Nne, jukumu la kupitia mitaala liendeshwe na wataalamu wenye weledi kwa kuzingatia, soko la ajira, sera na hali halisi ya nchi yetu.​
  • Tano, Waziri wa Afya na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia mkae pamoja na vyombo vyenu vya utendaji kwa kuzingatia maoni ya wadau wote na matakwa ya miongozo ya uandaaji wa mitaala, mpate uelewa mpana wa jambo hili kabla ya kulitekeleza.​
Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.​
 
Wewe uko sahihi na yeye(mfamasia) yuko sahihi pia. Mimi kama mfamasia naunga mkono hoja ya mfamasia mkuu. Uthibitisho ni matokeo ya mtihani wa leseni uliofanyika October 2023 ambapo ufaulu wa pharmaceutical technicians ulikua 15.6%. Tena hapo wengine wamepass kwenye second attempt baada ya kufeli mtihani wa kwanza.

Nadhani katika kuyachanganua matokeo hayo mabaya ndio wakafikia conclusion kwamba kuna shida kwenye admission. Vijana wengi wana uwezo mdogo kuweza kuelewa wanachofundishwa.

Hoja yako ipo sawa kabisa lakini matokeo yanaonyesha hao wanafunzi hawaelewi. Je tatizo ni mtaala au ni wanafunzi wabovu?. Unahitajika utafiti wa kina kujibu hili swali
 

Attachments

  • NOTES FOR EXAM-RESULTS-OCTOBER-2023-AND-SCHEDULE-FOR-UPCOMING-EXAMS.pdf
    2.4 MB · Views: 1
Back
Top Bottom