Sababu za wanafunzi wa kizazi hiki kufeli masomo ni hizi hapa

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,859
18,277
Habari zenu wadau wa elimu? Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Awali ya yote napenda ku declare interest kuwa mimi ni mwanafunzi wa zamani na mshauri wa masuala ya elimu ninayefanya kazi na kampuni ya Shuledirect. Kwa hiyo, ushauri ninaotoa hapa ni wa kitaalamu na kitafiti.

Kiwango cha elimu na ufaulu wa wanafunzi kimekuwa kikishuka kwa kasi ya kutisha. Hata ukilinganisha uwezo wa wahitimu wa zamani na wa kizazi cha sasa, utagundua tofauti kubwa sana. Ukimlinganisha kijana wa kitanzania aliyehitimu Kidato cha Nne hana tofauti na yule aliyeishia Darasa la Saba na wakati mwingine mhitimu wa Kidato cha Nne anaonekana bomu kuliko yule wa Darasa la Saba. Hili ni tatizo kubwa sana la kielimu ambalo limepaliliwa kwa muda mrefu na sasa limefikia pabaya kiasi hiki.

Tofauti na miaka ya 1980 kurudi nyuma hadi nchi hii ilipopata uhuru, kiwango cha elimu pamoja na ufaulu wa wanafunzi vimeporomoka kwa kasi kubwa. Baada ya kufanya utafiti wa muda mrefu nimegundua sababu zifuatazo ndizo chanzo ya kuporomoka huku:

1. Mrundikano wa wanafunzi
Zamani darasa moja lilikuwa likichukua wanafunzi 45 tu. Sasa hivi sio ajabu kukuta darasa moja lina wanafunzi zaidi ya 200! Kwa idadi hii ya wanafunzi unategemea mwalimu ataweza kumfikia mwanafunzi mmoja mmoja na kugundua uwezo wake wa kujifunza ili amsaidie kwa undani? Haiwezekani.

2. Mitihani ya kubet
Naishangaa mno serikali kwa kulazimisha kutunga mitihani ya kubahatisha (kubet) inayowawezesha wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kupenya kwenda sekondari. Hii hupelekea idadi kubwa ya wanafunzi wasiokuwa na uwezo kuingia sekondari, hivyo kushindwa kumudu masomo. Na hawa ndio huongeza idadi ya wanaofeli katika mitihani ya kuhitimu sekondari (CSE).



3. Umri mdogo wa kuanza shule
Kwa makusudi kabisa, serikali imekuwa ikipunguza umri wa watoto kuanza shule kadri miaka inavyoenda mbele. Wanafunzi wa zamani tulianza darasa la kwanza tukiwa na umri wa miaka 9–13. Sasa hivi serikali inashauri watoto kuaanza darasa la kwanza wakiwa na miaka 5! Madhara ya kuanza shule katika umri mdogo ni makubwa kuliko tunavyodhani. Nitajaribu kuyaeleza kwa ufupi.

Kwanza, mtoto humaliza shule akiwa bado hajitambui na hajui umuhimu wa kutia bidii masomoni yeye binafsi bila kuhimizwa na wazazi. Na kwa kuwa hatii bidii kwenye masomo, ana uwezekano mkubwa wa kutofaulu mitihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE), hivyo kuongeza idadi ya wanafunzi wanaofeli.

Pili, watoto wanaobahatika kwenda sekondari kupitia mitahi ya kubet, wakifika huko hukutana na masomo magumu na yanayofundishwa kwa lugha wasiyoielewa barabara. Hili nalo hupelekea kufeli wanafunzi wengi katika mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari (CSE). Mtiririko huu wa kufeli na kushuka kwa kiwango cha elimu huendelea hadi wanafunzi wanapohitimu kidato cha sita na kuingia vyuo vikuu.

4. Mtindo wa maisha
Mtindo wa maisha tunaoishi haujawaacha wanafunzi salama. Watoto wa siku hizi wanalelewa kwa mtindo wa kudekezwa ukilinganisha na mtindo wa maisha wa zamani ambao watoto waliishi kingangari bila kuwategemea wazazi wao kwa asilimia kubwa. Watoto wa sasa hivi bila kuwapa ahadi ya kuwanunulia zawadi kama vile simu, baiskeli na zawadi nyingine kedekede ikiwa watafaulu, hawatii bidii kwenye masomo ng’o. Na tatizo hili huanza tangu wakiwa wadogo kwa kudekezwa na kufanyiwa homeworks na wazazi.

5. Kukua kwa sayansi na teknolojia
Zamani hakukuwa na TV, movies, games, internet na mambo mengine kama hayo. Tulitarajia kwamba kukua kwa sayansi na teknolojia kungewasaidia wanafunzi kujifunza lakini hali imekuwa tofauti. Wanafunzi wengi wanaomiliki simu badala ya kuzitumia kujisomea huzitumia kutongozana, kuimba singeli, kuangalia video za utupu na kutukana walimu. Hivyo, hujikuta wanapoteza muda mwingi kwenye mtandao kufuatilia mambo ya kijinga na hatimaye kufeli mitihani.

6. Upatikanaji rahisi wa mahitaji ya shule
Kama ilivyo kazi ngumu kutafuta na kuchimba madini, vivyo hivyo thamni yake iko juu. Ingekuwa dhahabu inapatikana bwerere wala isingekuwa na thamani kubwa sana.

Sawa na madini, zamani haikuwa rahisi mwanafunzi kupata notisi kibwerere. Ilikulazimu kutembea mamia ya kilometa hadi kijiji cha mbali kuwahi notisi kwa mwanafunzi aliyehitimu masomo kabla wanafunzi wengine hawajakuwahi. Hata walimu walipata notisi kwa shida sana kwa kuwa vitabu vilikuwa vichache. Uchache huu ndio uliwafanya wanafunzi wa zamani kutumia notisi hizi kikamilifu na kuafaulu masomo kwa ufaulu mkubwa.

7. Serikali kuingiza siasa kwenye elimu

Kama ilivyo kwenye mitihani ya kubet serikali pia ina mkono wake kwenye kutunga mitihani rahisi na kuisahihisha kwa urahisi (simple exams and lenient marking of papers).

Siku moja niliongea na mwalimu wa sekondari anayeteuliwa kusahihisha mitihani kila mwaka akaniambia serikali huwapa maelekezo ya kusahihisha mitihani kwa urahisi na endapo mwalimu atakiuka anaweza kushushwa cheo kazini na hatateuliwa kwenda kusahihisha mitihani kamwe!

Yaani serikali inawaelekeza walimu watunge mitihani rahisi ya kubet na inaenda mbali zaidi kuwalazimisha walimu kuisahihisha kwa ulaini, na bado wanafunzi wanafeli. Kama serikali ingekuwa haiingilii kati, basi idadi ya wanafunzi wanaofeli ingekuwa ya kutisha zaidi ya hii tunayoshuhudia

Mjadala
Je, unadhani nini kifanyike ili kuepuka au kupunguza ukubwa wa tatizo hili? Karibu tujadiliane.

Nawasilisha

 
Mitihani ya kubet
Naishangaa mno serikali kwa kulazimisha kutunga mitihani ya kubahatisha (kubet) inayowawezesha wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kupenya kwenda sekondari. Hii hupelekea idadi kubwa ya wanafunzi wasiokuwa na uwezo kuingia sekondari, hivyo kushindwa kumudu masomo. Na hawa ndio huongeza idadi ya wanaofeli katika mitihani ya kuhitimu sekondari (CSE).

Tatizo kubwa sana hii, na chini ya kapeti "Mtihani ya kubet" wanataka kuleta mpka O-level
 
Mitihani ya kubet
Naishangaa mno serikali kwa kulazimisha kutunga mitihani ya kubahatisha (kubet) inayowawezesha wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kupenya kwenda sekondari. Hii hupelekea idadi kubwa ya wanafunzi wasiokuwa na uwezo kuingia sekondari, hivyo kushindwa kumudu masomo. Na hawa ndio huongeza idadi ya wanaofeli katika mitihani ya kuhitimu sekondari (CSE).

Tatizo kubwa sana hii, na chini ya kapeti "Mtihani ya kubet" wanataka kuleta mpka O-level
kwa kweli kama mitihani ya KUBET itapenya hadi kidato cha sita basi tutarajie elimu ya nchi hii kufa kabsa.
 
Inatakiwa Elimu ipandishwe thamani kwa kuhakikisha Kama ni darasa la saba basi mwanafunzi afaulu kweli kwa kujari viwango vyenye ubora kwenda kidato cha kwanza, vivyo hivyo kwa kidato cha nne kwenda Kidato cha tano nk.

Yaani Kuna muda fulani unakutana na mwanafunzi wa sekondari ukijaribu kumpima uwezo wake wa kutathmini mambo unakuta ni mdogo sana.

Nimalize kwa kusema Elimu inatakiwa ikazwe vizuri ili kuwa na wasomi wazuri.
 
Kabla ya kukujibu naomba kukuuliza "kwanini shule za private zinaongoza kuwa na ufaulu mkubwa tofauti na shule zetu hizi za kata...??????
Kwanza zile shule hazina mrundikano mkubwa wa wanafunzi na pia wana mitihani yao kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga pale......hawatungi mitihani ya ajabu kama hii ya NECTA.
 
Kabla ya kukujibu naomba kukuuliza "kwanini shule za private zinaongoza kuwa na ufaulu mkubwa tofauti na shule zetu hizi za kata...??????
Aina ya wanafunzi na michujo ya shule ndio inayo saidia ila kuna private ni majanga makubwa
 
Mkuu mbona sasa ndo wanafaulu rahisi sisi ilikuwa kwenda sekondari tu ni kasheshe.
Wanafuluje wakati unakuta darasa ina wanafunzi 800; divisheni wani zero divisheni 2 watatu, divishen three 17, divishen four 33 na wengine wote waliosalia wanapata zero. Ufaulu uko wapi hapo mkuu. Na kumbuka mitihani ni ya kubet na inasahihishwa kwa urahisi.
 
Nini kifanyike ili tutoke kwenye mkwamo huu mkuu?
Kuhusu namba 1, ni kuweka sera ya elimu iwe ya uhalisia kuachana na siasa. Changamoto zinazotokana na maendeleo ya teknolojia hususan katika hoja namba 5 na 7 ni ngumu kuyaepuka kama taifa.

Wazazi wana nafasi kubwa sana kuwalewa wayoto katika njia ambazo zitawasaidia kutumia teknolojia vizuri.
Kwa sasa wazazi wamewaachia waalimu watoto wawasaidie kulea.
 
Kwanza zile shule hazina mrundikano mkubwa wa wanafunzi na pia wana mitihani yao kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga pale......hawatungi mitihani ya ajabu kama hii ya NECTA.
Umejibu vyema mkuu,,vipi kuhusu mfumo mzima wa elimu kwa shule izi za kata,,,sizani kama inapendeza mwanafunzi kutumia lugha mbili tofauti katika elimu ya primary na secondary.
 
Back
Top Bottom