Sizipendi mbichi hizi! CCM 'asili' ni ipi? Ya akina nani? Je, ni CCM hiyohiyo inayotabiriwa kupasuka kama katuni ya Kipanya?

SYLLOGIST!

JF-Expert Member
Dec 28, 2007
7,101
6,708
Kiukweli sipendi kulishwa maneno, sipendi kulishwa taarifa, na sipendi Kukashifu. Sipendi kauli mbichi [Generalities] kwani huwa zinapotosha au kupotosha maana halisi iliyomo kwenye maudhui. Nimekutana na mijadala mitatu tofauti, ikimaanisha maudhui matatu tofauti, lakini kwa kauli na misemo ya mara kwa mara. misemo na mawazo ya mara kwa mara. imejumuishwa kati.

Mfano:
Mada moja inaomba Viongozi wa Vyama mbadala kuacha kuharibu sifa na kujaribu kumfanya mtu aonekane ni muovu.

Wanasema, katika moja ya hoja zao -Ni muovu kwa sababu alitaka kuua "Private Sector". Ukiuliza ni maovu gani wanadai 'Alipora' ' Ni mnyama' n.k kweli hayo? Hizo ni Mbichi!
"Sukuma gang" imo humo

Mada nyingine, inayohusu maridhiano yanayoendelea nchini, ikiwa na maono kwamba maridhiano yanaweza kuwa batili kisheria, wanasema katika hoja zao kuwa siyo ! haiwezi kuwa batili per se CCM ni tofauti sasa, kwa sababu CCM ya sasa ni ya asili, CCM nyingine haikuwa ya asili.

Ilikuwa mali ya Warundi! hivyo hakuna ubatili unaoweza kutokea hata kama vyama vingine havihusiki na mustakabali wa Taifa! Hizo ni mbichi, ni inference isiyoweza kurekebishika, ni wazi, hakuna ukweli. Kumbuka marehemu Raisi ni Msukuma[ati Sukuma gang] lakini anatuhumiwa kuwa Mrundi, maneno haya yanajirudia,yana uKashifu. Ina maana CCM ilitekwa kimzabezabe na watu wasio CCM? na Warundi?

Mada ya kudaavua katuni;picha ya mkatunisti Kipanya nako vivyohivyo. Kiunagaubaga-Sukuma huyu, sio CCM yenu ile, oh nyie misukule, maneno yanayojirudia rudia

Hali yote ni kuwa CCM ilipoteza uasilia wake?? Upi? wa kuwatetea [wasiokuwa na sauti] au kwa lugha nyingine 'Wanyonge'
Asili ya CCM ni upi?

Kuwatetea makaburu, kuwakumbatia mabepari wa mabeberu? Kuna mpasuko CCM unaoashirika na katuni ya kipanya?

Nashindwa kupata jibu bila kujua CCM asili ndio nani? Ndio akina nani?

Yote hayo mbali, CCM asili ndio ipi?

Watetezi, wakumbatiaji, nisaidieni kuelewa.
 
Sizitaki mbichi hizi Sungura akagumia

Naona nafanya Kazi Bila faida kujua

Katika tena karuka matunda akarukia
Mwishoe akachokea
Kachoka hata mkia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom