Ipi ni falsafa ya CCM kwa sasa?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
948
2,857
Enzi za Mwalimu katika mikutano ya CCM walichezesha nyimbo za akina Mbaraka Mwinshehe (nyimbo bila jasho) ulionekana Uzalendo hata unapocheza nyimbo hizo,juzi katika mikutano yetu ya Uchaguzi zilichezeshwa nyimbo na mtindo wanaocheza.

Basi mtu utagundua tupo ki-hip hop singeli na rusha roho tofauti kabisa na wazee wetu tulivyowazoea kuvaa kinadhifu na kucheza taratibu nyuzi zetu zilipendwa zenye Uzalendo wa ki-Tanzania, kwa lugha ya picha utagundua tumesahau tulipotoka na hatujui tunapokwenda.

Hatuhijui falsafa yetu ya Chama, je ni 'Uvuguvugu, moto au baridi au zote kwa pamoja' tumepoteza dira, wenye dhamana wanasema vijana wajiajiri, lakini hakuna mazingira wezeshi ya kujiajiri, hakika dereva asipojua njia anakoenda, mafuta akanyagayo kwenye gari lake ni kazi bure sawa na kuzunguka tu mbuyu pale barabara ya Ali Hassan Mwinyi Road - Masaki.

Tunaishia kusema Taifa hujengwa na wenye moyo, hutafunwa na wenye meno' Enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, CCM ilikuwa na falsafa ya ujamaa na kujitegemea, CCM ilikuwa na mipango iliyotokana na falsafa kama maadili ya uongozi, mapambano dhidi ya rushwa, umoja wa Afrika n.k.

Ila Azimio la Zanzibar lililoleta wafanyabiashara liliua ideolody na hapo ndipo Chama kikavurugwa hadi leo hatuna ideology hatuna falsafa, Wana CCM wenzangu ebu niambieni ideology yetu leo ni ipi? Ipi ni falsafa yetu leo!?

CCM ni chama cha kijamaa, misingi na falsafa ya CCM ni Ujamaa, Chama cha kijamaa kama CCM ni chombo cha kuongoza mapambano ya ujamaa nchini. Ni kweli kuwa Ujamaa kimsingi ni siasa ya Wakulima na Wafanyakazi na kwamba utajengwa na wafanyakazi katika umoja wao wa kitabaka.

Lakini ni kweli pia kwamba bila ya wapiganaji ujamaa wa mstari wa mbele,bila kikosi cha askari wa mstari wa mbele kujenga ujamaa haliwezi kufikiwa, kikosi hicho cha wapiganiaji ujamaa wa mstari wa mbele ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.

Chama chetu cha CCM ni miongoni mwa vyama vichache katika bara la Afrika ambavyo vilifaulu kubuni nadharia yake ya ujamaa iliyo sahihi, iliyo wazi na ya kiwango cha juu. Nadharia hiyo ya CCM inajidhihirisha yenyewe katika Katiba ya CCM yaani Azimio la Arusha.

Nadharia hii ya siasa yetu ya Ujamaa na Kujitegemea ilitujengea msingi wa uelewano, umoja na ushirikiano wa aina mpya katika ujenzi wa taifa na kutufanya tueleweke na wengi kimataifa, jambo ambalo limetupa sifa na heshima duniani kote.

Ujenzi wa ujamaa si lelemama bali ni mapambano, mapambano ya kudumu dhidi ya ubepari na unyonyaji, dhidi ya wapinga maendeleo na wababaishaji wa kisiasa, dhidi ya wahujumu uchumi, majambazi, wezi, wazururaji na wazembe. Msimamo sahihi wa mapambano unaotokana na nadharia sahihi ya ujamaa ungelituepusha na maamuzi na vitendo ambavyo vimerahisisha kuoteshwa kwa mizizi ya ubepari.

Kinyume cha msimao wa mapambano dhidi ya ubepari,leo ubepari, una vishawishi vingi zaidi nchini kuliko ulivyokuwa kabla ya Azimio la Arusha kwa sababu pamoja na kwamba sasa tuna sekta kubwa ya umma lakini kutokana na udhaifu wa kutopambana nao, ubepari umefaulu kujipanua na kujipenyeza hata ndani ya sekta yenyewe ya Umma.

Na ndiyo maana ubepari sasa unathubutu kujitokeza hadharani kuukashifu ujamaa, kubabaisha baadhi ya viongozi na kututaka tubadilishe siasa yetu.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwaambia "mnaondoa Azimio la Arusha na mambo yake yote, mnaweka nini badala yake", nadhani hawakumwelewa kabisa "kwamba wametema falsafa na wanahitaji mbadala".

Aliwaambia chukueni mazuri muache mabaya, tena akawaambia ninyi mnachukua mabaya na kuacha mazuri.Siku hizi Waandishi wa habari wakiwa kazini nao wanagombea Uongozi ndani ya CCM,kama haitoshi wafanyabiashara nao wanagombea Uongozi ndani ya CCM,utasikia wajumbe wakisema "hatutaki vipeperushi" jibu unalo wanataka "vipepe-rushwa". Kama hauna ukwasi basi sahau Uongozi.

Nimalizie kwa kuwakumbusha,Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika "Nguvu na Mamlaka ya Umma" (The People's Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao,aidha falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi.

Na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni,Uchaguzi wa ndani wa CCM umeisha,Swali tumewachagua Wajamaa au Mabepari? Wakulima na Wafanyakazi (Maofisa waandamizi) wanaruhusiwa kugombea (Nyundo na Jembe)?

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
ccm ilikosa dira na mwelekeo tangu alipojiuzulu Mwl. Nyerere. Na ndo maana alikuwa anapambana dhidi ya ccm.
Horace Kolimba aliyaweka haya bayana.
Ile Jembe na nyundo kwenye nembo yao ni ulaghai!
Sema nchi hii elimu ndo tatizo la msingi. Wengi wana elimu ya kutafuta chakula na mavazi!
 
Chakubanga hongera san kwa contact zako, mchango wako tunauona tutafanya namna yoyote ila tafadhali ambatanisha email address!!
 
January makamba utamwambia hata socio-democratic ideology hataelewa. Ameshabaki kwenye unyonyoji
 
Falsafa ya CCM ni CHUKUA CHAKO MAPEMA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom