Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,893
- 16,317
Hii hatari sana,lakini Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA)wanasema hawana taarifa yoyote rasmi ya kuwepo kwa mchele aina hiyo wa plastiki hapa nchini.
Lakini pia taasisi hiyo ya TFDA inawaasa wananchi watoe ushirikiano wa taarifa za mchele huo ili hatua za haraka zichukuliwe.
Kila siku TFDA wanasema huo mchele haupo. Mimi nmeshindwa kuelewa. Kama sio wa Plastic, ni mchele gani huu? Kama vipi tuwatumbue tuwaweke watakaoweza kutuambia ni mchele gani.
Kwanini video inapoanza anaanza kwa kufinyanga tonge la huo mchele anaosema ni fake? Kwanini asinze shooting kwa kuchota mchele kutoka sahani ya mama lishe ili tuamini ya kwamba hilo tonge la ubwabwa limetoka katika hiyo sahani?
Inaweza kuwa ni video ya propaganda ya kutia hofu watanzania.
Kwenye age ya technological advancements kama hii never trust virtual materials kabla ya ku prove wewe binafsi.